Notifications
  • THE NIGHTMARE (3)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TATUILIPOISHIA...Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Pia alijua kwanini mume wake alipendelea kufanya kazi uingereza na yeye kumfungulia ofisi huku huku Tanzania. Hakujua kuwa kazi anayoifanya mumewe ni ile ya kutembea na tajiri mkubwa…
  • THE NIGHTMARE (2)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA PILIILIPOISHIA...Khalidi alishangaa kuitwa na mtu asiyemfahamu. Alitoka na kwenda kumuangalia huyo mtu maana kiukweli hakua na ndugu aishie hapa Dar hata mmoja anayemfahamu..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Sabra pale.“ahsante mungu.” Aliongea Khalidi baada ya kumuona tu yule binti pale.“pole sasa kaka yangu, nisamahe mie.” Aliongea Sabra kwa…
  • THE NIGHTMARE (1)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA KWANZANi kipindi cha mvua za masika. Upepo mkali, na mvua kubwa iliendelea kunyesha kwa kasi kila kona ya nchi ya Tanzania.Ipo mikoa iliyofurahia mvua hizo kwa kuwa walikua wanaisubiria kwa hamu kwa ajili ya kilimo. Lakini ipo mikoa iliyokua inapata shida kwa uharabifu wa mazingira na mengineyo mengi.Moja ya miko hiyo ni Dar-es-salaam. Watu wanaoishi katika mkoa huo walichukia mvua mfululizo kutokana na sababu mbalimbali. Biashara nyingi…
  • MY DIARY (50)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA HAMSINITULIPOISHIA...Nilimnongo’oneza kuwa atumie kinga ili nisimwambukize ukimwi akanijibu kwa sauti ya mahaba nisiwe na hofu yeye yupo tayari kufa kwa ajili ya penzi langu hivyo hawezi kutumia kinga kwa mke wake aliyemoa tena siku muhimu kama hiyo.Sikutaka kumbishia yeye ndo muaamuzi wa mwisho kuhusu afya yake hivyo nilimuacha aendelee kufanya yake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kumbe na…
  • MY DIARY (49)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TISATULIPOISHIA...Baada ya maneno ya kusilimu ambayo waliambiwa wayatamke kiongozi huyo alisema neno ya mwisho kabla hajashuka.” Kila alie na akili timamu, mwenye busara naa anaetaka haki, na kusimama pamoja na haki, basi akiangalia dunia ilivyo na jinsi inavyokwenda basi lazima kutakuwa na nguvu kuuu nayo ni mwenyezi mungu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kuna vitu vingi sana…
  • MY DIARY (48)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NANETULIPOISHIA...Familia yangu haikukubali kabisa mimi kuolewa na rangi nyeusi hivyo walinitenga na kusema hawanitambui kuwa mimi ni ndugu yao.Lakini kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa baba yake na Leah nilijikuta nipo tayari kwa lolote hivyo nikahama na kwenda kuishi Tanzania.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Katika miaka hiyo tuliyokaa nilibahatika kupata mtoto huyu…
  • MY DIARY (47)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SABATULIPOISHIA...Lakini ilifikia mahali ndoto hiyo inanijia hata mchana nikiwa nimekaa mahali tulivu.Ilikuwa inanipa taswira nzuri ya sehemu ambayo madini yalikuwepo.Basi nilianza mikakati ya kulitafuta eneo hilo na hiyo ni mara baada ya ushauri wa mpenzi wangu Candy hapo akimaaanisha yule dada aliyekuwa naye pale jukwaaani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Candy alinisihii sana…
  • MY DIARY (46)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SITATULIPOISHIA...Nilikuwa kama niliyepigwa butwaa nisiamini nilichokuwa nakiona mbele yangu. Oooooh my God hold me on yalikuwa ni maneno yaliyonitoka kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu mara baada ya kumuona James kwa uzuri zaidi na kuamini kuwa yule kweli alikuwa ni kaka yangu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishindwa kuelewa nini kimetokea mpaka yeye kurudi katika hali yake ya…
  • MY DIARY (45)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TANOTULIPOISHIA...Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Sio kazi ya…
  • MY DIARY (44)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NNETULIPOISHIA...Yani alianza kutaka uhusiano na mimi tena uhusinao wa mapenzi.Mda wote alikuwa akiniganda kama luba.Na mimi nilikuwa mjanja sana maana nilijifanya sinywi pombe wala kuvuta sigara.Pia baada ya kugundua kuwa wahusika wengine walikuwa wanajiachia niliamua kujifanya mshauri wa mapenzi na mahusiano.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilikuwa nawasshauri sana mshiriki wa…

MUUZA CHIPS (43)

Sehemu ya Arobaini na Tatu, yake chidi huku, kwa ajili ya, mama yake chidi, mke wa ibrahim, baba yake chidi, kijana chidi huku, kutafuta na sio
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA AROBAINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Ibrahim toka aje mjini hajawahi kukanyaga kijijini hata siku moja, zaidi kurusha elfu 20 kwa miezi miwili au asirushe kabisa, kana kwamba kawasusa wazazi wake…….

Kwa niaba ya mke wa Ibrahim, Chidi alikubali kuja kumchukuwa mdogo wake ili akasome huko mjini…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Na leo kijana chidi yupo kijijini kwao akiwa tayari kwa kumchukuwa mdogo wake, lakini wazo hilo lilikuwa ni lakwake na shemeji yake kule mjini au pia na kaka yake, bali wazazi wao je wataafiki vipi kuhusiana na kijana chidi kumchukuwa halima akasome mjini,

Chidi kabla hajaongea kwanza alitoa zawadi kwa ajili ya wazazi wake kisha akaanza kuongea,…

"mama na baba…. Mimi nimekuja kumchukuwa halima akasome mjini"

Aliongea kijana chidi huku wazazi wake wakionekana kubadirikwa na sura,… Kana kwamba hawakutaka mtoto wao aondoke, chidi aliangalia chini kwa uoga wa wazazi wake, mana hashindwi kurushiwa mkibao wa shavu,… Wazazi wa chidi walinuna sana huku chidi akijiandaa kuomba msamaha kwa maneno hayo… Lakini kabla hajaanza kuwaomba msamaha ghafla wazazi wa chidi walianza kucheka huku wakisema kuwa

"heeeeee mwanagu kweli huko mjini umekwenda kutafuta na sio kutafutwa"

Aliongea baba yake chidi huku chidi akimuuliza baba yake

"hhhmmm baba kwani kuna mtafutaji na mtafutwaji"

"ndio mwanangu,.. Mtafutaji ni yule anaekwenda mjini na kufanikiwa, na mtafutwaji ni yule anaekwenda mjini na kupata maisha au hata kama hajapata, lakini kuna wanaomtafuta,… Nikimaanisha kuwa, yeye anatafuta pesa, lakini nyuma yake kuna mtu nae anatafuta pesa kupitia yeye… Nikilenga kwa wanawake, hivyo mtu anaetafutwa ni yule anaehonga wanawake na kusahau maisha yake binafsi… Hivyo kwa wewe mwanangu, naamini umekwenda kutafuta na sio kutafutwa,… Nakuombea sana mwanangu uzidi kufanikiwa katika mihangaiko yako"

Baba yake chidi aliongea kwa kirefu ili kumfafanulia maana ya kutafuta na kutafutwa,.. Hivyo nyie mnaehonga wanawake bila kujali maisha yenu ya mbele, basi mjue nyie ni wa kutafutwa na sio kutafuta… Sasa baba chidi alipomaliza kuongea maneno hayo, na mama nae kaja juu

"mbona unamuombea mwenyewe tu, kwani mimi sio mtoto wangu,….. Hata mimi baba nakuombea mwanangu ufanikiwe katika njia zako, mungu akuangazie kila njia unayopita"

Aliingea mama yake chidi…. Lakini jamani kumbuke kabisa dua za wazazi hua hazilali fofofo, yaani hapo inapoombwa, ndio hapo inapo pokelewa.. Dua za wazazi hazilali kamwe.. Hivyo tafadhalini jamani kwa wale vijana wenzangu mlio mijini, muwe mnakumbuka familia zenu nyumbani, hata kama umepata elfu kumi, wape elfu tano baki na elfu tano,.. Ivi kama wangekuuwa ukiwa mdogo, je hio elfu kumi ungeipata wapi wewe… Hivyo kuwa makini na familia yako hata kwa kiasi kidogo tu wataridhika, msiwasahau wazazi wenu kisa wanawake, na mkumbuke kuwa wasichana wa mjini nao wamekuja kutafuta, hivyo akipata bwege bwege kama Ibrahim, basi hapo ndipo tunapoita KUTAFUTWA yaani Ibrahim kutafutwa ila hatafuti kwa ajili ya maisha,… Unajali mwanamke wako na kumsahau mwanamke aliekuleta duniani, kweli unaaki za kizungu na sio za kiafrika.

Sasa wazazi wa kijana chidi walifurahi sana kuona maendeleo ya mtoto wao mpaka kufikia hatua ya kumchukuwa na mdogo wao wa mwisho kwenda mjini kusoma katika shule za pesa,…

"lakini mwanangu… Kweli tunashukuru kwa maendeleo yako, lakini halima kuna zile kazi anatuseidia baada ya mke wako kuondoka"

Aliongea mama yake chidi huku baba yake akiwa anasikiliza tu,

"mama, kwani hata kuosha vyombo huezi"

"sio vyombo mwanangu,… Mimi hata maji naweza kwenda kuchota korongoni ila kuhusu mambo ya shamba, na kwenda mjini kuleta mahitaji"

"aahhhhh mama, mi staki muende shamba tena"

Chidi aliongea hivyo na kumfanya baba yake akasirike huku akisema

"we mpuuzi nini wewe, yaani sisi tusiende shamba tutakula nini"

Aliongea baba yake chidi huku akiwa na hasira kwa chidi kusema kuwa wasiende shamba,…

"hapana baba yangu, sijamaanisha hivyo mzee,… Mimi najua tuna mashamba mengi sana kuliko hata familia zingine.. Maana yangu ni hivi mimi nitatuma pesa ya kulima mashamba kadha kwa ajili ya chakula, lakini sio nyie mkashike jembe, sasa maana ya mimi kuwa mjini ni ipi kama huku mtateseka wazee wangu"

"aahhh hapo sawa… Kwa hapo tutaelewaana"

"afu mzee nitakununulia baiskeli mpya ili uwe unaenda mjini wewe kwa vitu vidogo vidogo"

"mpuuzi wewe, yaani mi niende sokoni na wakati mama yako yupo"

"mzee wangu mambo ni kuseidiana mzee"

Mama chidi alikuwa akicheka tu kwa kijana chidi kumtania baba yake kuwa aende sokoni badala ya mama yake

"hapana mzee huo ni mtazamo wangu tu ila nyie wenyewe mtajua mahitaji madogo madogo mtayapataje,… Ila na mimi natakiwa nijue mwenyewe mnaipataje pesa"

Chidi alikuwa akiongea huku akitoa simu mpyaa, na kumkabizi baba yake

"mzee simu mpya hii hapa, nimesjili laini yako mpya, na nimeisajili na tigo pesa na na laini nyingine ya voda nimeisajili na m-pesa,. Ni nyie tu pale mnapoishiwa nipigieni simu"

"mwanagu, mpaka hapo tukushukuru tu,.. Wewe na mdogo wako Ondokeni hatutaki kuwaona tena"

"aahhhhh mzee ndio unatifukuza tena… Basi nilikuwa na pesa ya kuwapa sa siwapi tena"

"heeeeeee basi mwenetu kaaa mpaka keshokutwaa"

Basi ilikuwa ni utani katika familia hio iliokuwa na maisha magumu kiasi fulani, lakini baada ya mtoto wao kuingia mjini hali ya maisha huonekana kwa kiasi flani

Baada ya kijana chidi kukubaliwa kuondoka na mdogo wake halima ili aende nae mjini, chidi alichukuwa jukumu la kwenda shuleni kwa akina halima na kufanya utaratibu wa kumhamishia mjini, kweli na huko shuleni pia alifanikiwa kupata barua ya uhamisho juu ya mdogo wake,…

BAADA YA SIKU MBILI KUPITA

Na leo ni asubuhi mida ya saa mbili hivi, Kijana chidi bado alikuwa yupo kijijini lakini leo ndio siku aliokuwa akiondoka na kuelekea mjini,…

"heeeee mwanangu imependeza na hako kagauni"

Mama yake chidi alimsifia mtoto wake halima, kuwa alipendeza sana, mana chidi baada kumaliza ishu za shule, alienda mjini na halima ili kumnunulia mavazi mazuri,..

Kijana chidi alikuwa na pesa kiasi kidogo mana ulumbuke alipewa laki tano na mama sarah, afu akarushiwa laki tatu na kaka yake, bado ana marupu rupu ya hapa na pale…

Kwanza aliwachukuwa wazazi wake na kuwavuta ndani,… Chidi alitoa waleti yake iliokuwa imevimba kwa kitu kama laki 7 hivi, na hapo bado hajatoa ile laki tatu ya kaka yake, hivyo pesa alikuwa nayo..

"wazazi wangu, nashukuru sana kwa maombi yenu juu yangu, naami mwenyezi Mungu hatonitupa katika maisha yangu"

Aliongea hivyo kijana chidi huku wazazi wake nao wakimjibu kwa pamoja

"usijali mwenetu,.. Maisha ni kutafuta na sio kutafutwa kama baba yako alivyosema"

Chidi alitoa kiasi cha shilingi laki sita kamili na kuishikilia mkononi

"wazazi wangu nawapenda wote, sijui nimkabidhi nani hii pesa, mana staki upendeleo wowote ule"

Aliongea kijan chidi,.. Mana kuna wazazi wengine ukimpa mama kitu, baba atalalamika, MBONA MIMI SIPEWI… Au ukimpa baba mama pia atalalamika MBONA MIMI SIJAPEWA KAMA MAMA, hivyo chidi alitaka kujua amkabidhi nani

"mwanangu, mpe baba yako hio pesa"

Aliongea mama yake chidi huku chidi akimkabidhi baba yake shilingi laki sita

"mzee… Nawapatia hii pesa kwa ajili yenu, na najua zitawsukuma sana katika hali ya hapa na pale"

"haaaaaaaa rashidi mwanangu hii pesa ni nyingi sana, kwanini nisiirekebishe nyumba yetu hii"

Aliongea baba yake chidi kana kwamba alitaka kurekebisha nyumba kwa pesa hio aliipewa, ni pesa ndogo sana kwa maisha ya mjini, lakini kwa kijijini ni pesa moja kubwa sanaaaaaa

"mzeee swala la kujenga nyumba au kurekebisha naomba uniachie mimi,.. Hizi ni pesa za matumizi juu yenu"

Baba yake chidi alikuwa anatetemeka kwa uwingi wa pesa aliipewa na mtoto wake

"heeeee muone baba yako anatetemeka,.. Mimi nilijua tu"

Aliongea mama yake chidi huku akikaukiwa kwa kucheka, mana mzee kweli alikuwa akitetemeka,..

"nyie wapuuzi nini, mnanicheka pumbavu nyie, nilishawahi kuzishika hizi"

Baba yake chidi nae aliongea kiutani utani huki wakiingia ndani kabisa kwa ajili ya kuzificha.. Baada ya dakika kadhaa, wazazi waliwaaga watoto wao tena kwa furaha ya hali ya juu, huku wakitakiwa safari njema….

Tukija huku mjini, kwa Ibrahim na mke wake mida hio ya asubuhi wakiwa wanapata chai, Ibrahim alikuwa na wasiwasi juu ya wazazi wake kukubali kuondoka na halima, tena watakuwa na wasiwasi mwingi sana endapo atatajwa kuwa yeye ndie anaemuhitaji,..

"lakini mbona anachelewa hivyo"

Aliongea mke wa Ibrahim ambae ni jasmini,..

"kuna uwezekano wa wazazi kukataa"

"lakini Ibrahim, kwanini tusingelienda nyumbani, we mwenyewe ulisema una muda mrefu hujaenda nyumbani"

"ni kweli mke wangu, ila nafasi sipati mke wangu"

"hata kama,… Wale ni wazazi wetu eti"

"ok… Wacha chidi aje then tutapanga safari siku nyingine"

"Eti eee"

Ibrahim aliongea hivyo huku akijisemea kimoyomoyo kuwa

"kiukweli nyumbani siendi, yaani kulivyo kubaya vile, afu niende na mke wangu akantie aibu kuwa nina pesa huku afu kule kubaya,.. Hhhhmm siendi nitamdanganya kila siku lakini siendi"

Aliongea hivyo bwana Ibrahim huku wakiendelea kupata chai…

Ghafla simu ya mke wa chidi inaita, kuangalia jina aliandika shem, kana kwamba alikuwa ni chidi ndio anapiga

"huyu apa anapiga"

Aliongea mke wa Ibrahim kabla ya kupokea simu hio

"nani huyo"

"shemu wangu"

"anasemaje… Kafanikiwa kuja nae"

"subiri tupokee kwanza"

Ibrahim alikuwa haamini kama chidi angelipiga simu

"haloo shem mambo"

Alianza mke wa Ibrahim huku akiisikiliza kwa makini

"she…. She…. She.. Mmm. Shem kuna shida"

Jasmini alitoa macho huku akimuangalia mumewe

"nini shem, kuna shida gani"

"mmm… Md…. Md… Mdogo wangu ha.. Ha… Ha.. Hatu…. Hatu, aiiii"

"mdogo wako kafanyeje jamani chidi"

Ghafla mke wa Ibrahim akasikia sauti ya ving'ora vya zima moto…

"mungu wangu… Mume wangu naskia sauti ya ving'ora vya zima moto vikiwasili"

"ati unasemaje mke wangu???"

Ibrahim nae aliuliza huku akitoa macho..

Sasa tukija huku kwa chidi katika safari yao ya kuja mjini,… Laaaaaa Haulaaaaaaaaaaa,

Sasa tukija huku kwa chidi katika safari yao ya kuja mjini,… Aaasta Khafirulah Kumbe chidi alikuwa akimdanganya shemeji yake, ili ajue kama angejiskiaje kwa taarifa kama hizo,…

"haloo shem,… Mbona unalia sasa shem"

Aliongea kijana chidi huku akiwa na mdogo wake katika hoteli wakipata chai,.

"chidi, kuna nini lakini"

"nilikutania tu, wala hakuna lolote baya"

"mjinga wewe"

Basi chidi alikata simu kisha akakumbuka wazo hilo alilipataje na ni kwanini afanye hivyo….

ONA SASA ROBO SAA KABLA YA KUPIGA SIMU ILIKUWA HIVI KWA CHIDI

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
50 Muuza Chips Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni