SITOISAHAU FACEBOOK (4) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 30 Aprili 2024

SITOISAHAU FACEBOOK (4)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa


SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
MWANZA
Ulikuwa usiku wa kipekee sana kwangu, ndio kwanza nilikuwa nimerejea jijini Mwanza, kwa usafiri bora wa ndege. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Sijui niseme mara ya pili!! Maana mama alinihadithia kuwa nilipokuwa mtoto niliwahi kupanda ndege!!!Baada ya kushuka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere bila kuwa na wa kunipokea sasa hapa uwanja wa ndege wa Mwanza nilihitaji mtu fulani ajue kuwa nimekuja na ndege!! Huyo mtu ni nani kama sio John!!!

Nilimwomba John afike kunipokea. Nilifanya hayo makusudi ili kumkomoa kwa ubaya alionifanyia. Ubaya wa kuniacha na kuwa na mahusiano na msichana mwingine.Ni kweli John alikuwa amenitenda vile lakini John bado alikuwa moyoni mwangu. Nilikuwa nampenda sana John. Walikuwepo wanaume wengi lakini nafasi ya John bado nilikuwa sijaona wa kumrithisha.John aliposikia nakuja na ndege hakusita kunikubalia. Labda ili athibitishe kwamba kweli nimekuja na ndege ama la. John alinipokea huku akinipapatikia, niliifurahia hali hiyo. Tulichukua taksi iliyotufikisha katika hoteli yenye hadhi ya juu ya La kairo jijini Mwanza tukajipatia c

umba. Chumba cha bei ya juu kabisa!! Sikuwa na wasiwasi kuhusu pesa!!Wakati huo John tayari alikuwa amemdanganya mpenzi wake wa wakati huo Jesca kuwa hatarejea chuoni siku hiyo kwa kuwa kuna rafiki yake anaumwa. Ameenda kumsalimia.Usiku majira ya saa nne, tayari tulikuwa tumelia sana baada ya kukumbushiana yaliyopita. John akaniomba msamaha nami sikusita kumsamehe. Kilichofuata hapo ni kurejesha hisia za zamani na kuanza kushambuliana, kila mmoja akijitahidi kuamsha hisia za mwenzake, baadaye kidogo.

Vita!!!Vita ya miili. Kila mmoja akitamani kuibuka mshindi, hapakuwa na mwamuzi. Wakati vita hiyo ikiendelea ikaanza kusikia kama sauti ikiniongelesha kwa kabila kama kihehe vile, lakini sikuweza kuielewa lakini niliwahi kuisikia mahali. Ni kweli niliwahi kuisikia mahali, lakini sasa sikuwa nakumbuka ni wapi. John alikuwa bize, huenda alikuwa akifurahia peke yake. Nilitamani kumwambia John azisikilize zile sauti lakini hakuweza kunisikia alikuwa ulimwengu mwingine.John alipokoma, na sauti zile nazo zikatoweka. Ni kama vile zilikuwa kando ya dirisha zikitusemesha ama zikinisemesha.

“John walikuwa wanasemaje?.”“Nani?. Hao wahudumu ama.?” Aliuliza kwa utafiti.“Hapana!!!anyway acha ilivyo.” Nilimaliza mjadala.John hakuuliza zaidi.Nilielekea bafuni kujisafisha, kisha nikarejea tena pale kitandani. John alikuwa amesinzia. Sikuwa na hamu naye tena bali nilizitafakari zile sauti zilikuwa zikisema nini.Lakini kama John , hajazisikia basi hakuna sauti yoyote!!! Nilijipa moyo.Asubuhi John alikuwa wa kwanza kuamka. Aliingia aliwatoni akajisafisha na kuniamsha. Nami nikafanya kama alivyofanya kisha tukaondoka. John akaelekea alipopajua nami nikaelekea chuoni.

Zile sauti nilizozisikia usiku ule sikuzikumbuka tena. Nilichokumbuka ni kwamba mimi na John tulikumbushia enzi.Sikuweza kujua ilikuwa ni saa ngapi, lakini niliamini ilikuwa ni usiku tena usiku sana. Kuna sauti zilikuwa zimezungumza nami, tena kwa lugha ninayoielewa, zilikuwa sauti zenye furaha sana.Nikiwa bado natafakari sauti hizo zilizungumza nini na mimi. Mara simu yangu iliita. Alikuwa ni rafiki yangu wa darasani. Nikajiuliza kulikoni. Nikaipokea simu.

“Isabella, Isabella….Jenipher jamani. Jenipher!!”“Amekuwaje tena. Eh!! Nambie.”“Jenipher yupo hoi hospitali hapa.” Alijitahidi kuongea bila taharuki lakini alisikika akitetemeka. Baada ya pale hata kabla sijamjibu, simu yake ilikatika.Nilipojaribu kumpigia hakupatikana. Nikajilazimisha kulala, huku nikiamini kuwa lile ni tatizo la kawaida tuAsubuhi palipopambazuka, taarifa ilikuwa nyingine, taarifa ya kushtua nafsi!! Jenipher msichana aliyekuwa akiishi na huyo rafiki aliyenipigia usiku uliopita.alikuwa amefariki baada ya jitihada za madaktari kugonga mwamba.

Ilikuwa habari ya kusikitisha sana kwani kilikuwa kifo cha ghafla mno.Sikuzikumbuka zile sauti za usiku ule zilikuwa zinasema nini na mimi.Sasa nikawa nawaza juu ya msiba huo!! Msiba wa ghafla!!Mwili wa marehemu uliagwa katika viwanja vya Raila Odinga. Kila aliyehudhuria alijawa na simanzi, hasahasa kutokana na kilio cha mama mzazi wa binti yule ambaye alikuwa haishi kumlilia mwanaye huyo wa pekee aliyefanikiwa walau kufika chuo kikuu.Tofauti na watu kuwa na majonzi niliweza kubaini sura ya mtu mmoja ilikuwa na hofu kuu. Huzuni ikiwa mbali naye.

Huyu alikuwa ni John. Sikujua kwa nini alikuwa katika hali ile. Niliyalaumu macho yangu kwa kumtazama vile huenda alikuwa sawa lakini hapana nafsi haikuridhika.Muda wa kuaga ulifika ilianza familia ya marehemu iliyoungana nasi pale chuoni, kisha wakafuata wanafunzi wa kike. Nilinyanyuka na kuungana na msafara mrefu uliokuwa na nia moja ya kumsindikiza marehemu.Jua kali lilikuwa likinisumbua sana na kunifanya nitokwe jasho sana, si mimi pekee niliyelalamika bali na baadhi ya wasichana waliokuwa nyuma yangu nao walilalamika. Lakini mwendokasi wa foleni haukuwa mbaya tuliamini kuwa muda si mrefu kila mmoja atakuwa amemuaga marehemu.

Kwa akili zangu timamu nilisikia mivumo kwa mbali sana. Sikuwa nimesinzia ili nijilaumu kwamba ni ndoto. Hapana nilikuwa najitambua kabisa. Mivumo ile ilikuwa mithili ya mkutano wa injili unaofanyika mbali kiasi na wanatumia spika kubwa kuhamasisha watu wengi waweze kusikia. Kisha sauti hizo kutwaliwa na upepo kisha kurudishwa. Sikuweza kusikia maneno yote na hata hayo niliyoyasikia yalikuwa nusunusu. Nilitaka kumuuliza aliyekuwa mbele yangu lakini bahati mbaya hatukuwa tukifahamiana. Lakini wa nyuma yangu nilikuwa namfahamu nikaamua kumuuliza kama kuna kitu anasikia.

“Eti dada unasikia nini?.” Nilimuuliza.“Sijui hata kuna nini huko mbele hata dah!! Jua kali kweli.” Alinijibu nje kabisa ya swali nililomuuliza. Nikameza mate kulainisha koo langu, alikuwa amenikera.Ghafla nikagundua kuwa foleni ile ilisimama, sasa nikagundua kwa nini yule binti alinijibu vile. Kumbe hakunielewa kabisa.Kimyakimya nikamsamehe!!!Foleni ile haikuweza kusogea mbele, nilikuwa bado katika kutafakari,kulikoni ghafla ilitawanyika. Haikuwa foleni tena bali purukushani. Kila mmoja akataka kutazama kilichopo mbele. Mwanzoni ilikuwa foleni ya wasichana lakini sasa ulikuwa mchanganyiko wa jinsia zote. Kila mmoja akijitahidi kwa kadri anavyoweza kutazama mbele kuna nini.

Nilikuwa mmoja kati ya walioparangana na kufanikiwa kuona mbele. Alikuwa ni Jesca , aidha kwa hiari ama lazima alikuwa amekumbatia ardhi isiyokumbatika. Alikuwa ametulia tuli kumaanisha labda amekipenda kitendo kile. Tulibaki kushangaa kwamba kuna nini kimetokea. Wasichana tukiwa katika mshtuko wanaume walijiongeza wakavua mashati yao na kuanza kumpepea Jesca. John akiwa mstari wa mbele kumtetea huyu mpenzi wake kutoka katika hali aliyokuwanayo.Niliweka kando hasira na chuki dhidi ya binti huyo ambaye kwa maksudi alininyang’anya tonge mdomoni kwa kumchukua mpenzi wangu John kutoka katika himaya yangu. Niliuvaa ubinadamu, huruma ikanishika.Jesca hakutingishika hata kidogo. Sasa alibebwa mzega mzega hadi akawekwa katika kivuli. Zoezi la kumpepea liliendelea.

Yule mwanadada mwingine aliyekuwa ametulia tuli katika jeneza na yeye alikuwa amesahauliwa kwa muda. Cha ajabu hata mama yake mzazi naye macho yake yalikuwa yakifuatilia kwa ukaribu tukio la Jesca kuanguka.Sio maajabu haya!!!!Harakati za kumpepea Jesca ziliendelea hadi gari ya huduma ya kwanza ilipofika eneo lile. Jesca alipakizwa na gari ikaondoka kwa kasi huku ikipia ving’ora vya kuashiria hatari ama dharula.Nilifanya ishara ya msalaba na kumkabidhi Jesca kwa Mungu kutokana na tatizo lililomsibu.

Zoezi la kuaga liliendelea tena upesi upesi. Wakati huu sikumuona tewa John. Bila shaka aliongozana na mpenzi wake alyekuwa amekumbwa na maswahibu.Ile kufikiria kuwa Jesca ni mpenzi wa John. Wivu ukanipiga kikumbo nikajisikia vibaya. Nikahisi kuwa naonewa. Kisha nikaukumbuka usiku wangu wa mwisho na John. Ulikuwa usiu wa kipekee….na…na……na usiku wa kwanza kusikia sauti zile zisizokuwa na maana. Sauti za maajabu.Sasa zinamaanisha nini? Hilo lilikuwa swali. Nje kabisa ya uwezo wangu kujibu. Lakini nani hasa wa kunijibia????Baada ya taatibu zote za kuuaga mwili kufanyika. Zilifuata taratibu za kifamilia. Kuondoka na mwili wao.

Mwili ambao ulikuwa umeagizwa kuja kusoma kwa lengo la kuisaidia familia hapo baadaye mwili huu sasa ulikuwa unarejeshwa nyumbani kwa ajili ya kuzikwa. Inauma sana.Baada ya watu kusambaa niliwasha simu yangu kwa ajili ya kumpigiaJohn na kumjulia hali Jesca. Lakini kabla sijapiga, iliingia simu ya Dokta Davis. Nilishtuka kwanza maana ile kazi niliyoagizwa hata siku moja nilikuwa sijaifanya. Nikaanza kutunga uongo kisha nikapokea simu.“Pole sana na kazi!!! Usijali utazoea. Naona unachoka sana hata kupiga simu inakuwa tabu. Bila shaka ulifika salama na kazi uliianza mara moja." Aliongea bila kuweka kituo Dokta Davis. Nilibaki kujichekeshachekesha, kisha nikakiri kuwa kazi inaenda vizuri sana.

“Safi sana …safi sana.” Alinisifia Dokta. Nikajisikia vibaya kwa kuwa nimemdanganya.Tulizungumza mengi huku akinisihi niangalie akaunti yangu maana kuna pesa ilikuwa imeangulizwa.Taarifa hiyo ilikuwa furaha sana kwangu. Kiukweli nilikuwa napenda sana pesa.Nilipotoka pale eneo la viwanja vya Raila Odinga nilijivuta taratibu hadi nikazifikia ATM, nikazama ndani nikadondosha kadi yangu. Nikatazamana na akaunti yangu ikiwa imekenua, kunifurahisha mimi. Milioni tatu, laki sita na elfu sitini na sita zilikuwa zimeongezeka katika akaunti yangu.

Nilitabasamu mwenyewe, huku nikichomoa kadi yangu. Sikuwa na haja na pesa kwani kwenye pochi laki moja na nusu ilikuwa inasubiri matumizi yangu.Nilipokuwa natoka katika kituo hicho cha kujichotea pesa. Nilianza kuwaza kuhusu umaarufu. Wanafunzi mia nne wa darasani kwetu pekee kunifahamu hilo niliona kama halitoshi. Nilihitaji walau nusu ya chuo waweze kunifahamu. Sikupata muda wa kufikiria kuwa sifa haziliwi wala hazinenepeshi.

Mawazo yangu hayo yasiyokuwa na maana sana yaliingiliana na mlio wa simu.“Isije ikawa taarifa mbaya…” niliwaza.Nikaipokea simu nimsikilize shemeji yangu alikuwa akisema nini. Huyu alikuwa ni rafiki yake na John.“Pole shemeji yangu…” Aliniambia kwa sauti iliyokata tamaa.“Mh!! Asante..bana ndo mipango ya Mungu.” Nilimjibu.“Haya bwana mi ndio naelekea huko kumpa kampani mshikaji.”

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni