SITOISAHAU FACEBOOK (16)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Emmy John Pearson
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Kuhusu utoaji mimba na madhara yake!Nikafikia maamuzi ya kutoa mimba! Kisha nitajua nini cha kufanya!Wakati natoka pale chumbani na kupita mapokezi nilikumbana na swali, "mwenzako bado yupo? Maana tunataka kufanya usafi". Mwenzangu? Mwenzangu nani? Wanamaamisha Dokta Davis.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Sikuwajibu nikajongea na kupotea eneo lile.Nikaamua kurejea nyumbani kwangu. Tayari nilikuwa na taarifa kuwa mama anaendelea vizuri kiafya!Tumbo! Tumbo! Tumbo lilianza ghafla kuniuma, upande wa kushoto!! Nililalamika sana, dereva wa teksi akaegesha pembeni akaniuliza kulikoni.“Nipeleke hopitali!! Nipeleke nitakulipa” nilimsihi huku nikizidi kuugulia.Kama nilivyoomba akaendesha hadi hospitali iliyokuwa jirani. Alikuwa ni kati ya masalia ya watu wakarimu waliobaki hapa duniani. Aliwahi kuwaita manesi. Japo walichelewa lakini walikuwa kunibeba kutoka ndani ya gari lile.Moja kwa moja nikakimbizwa wodi ya wanawake!!Nikapatiwa huduma ya kwanza!!
Baada ya muda damu ikaanza kunitoka!! Nilikuwa nimeingia katika siku zangu ama? Nilijiuliza bila kupata majibu!! Mjamzito naingia katika siku zangu!!Kadri damu ilivyokuwa inavuja ndivyo maumivu yalizidi kupungua na hatimaye kuisha kabisa.Majibu ya daktari yalikuwa kwamba. Ni tatizo la kawaida tu kwa mwanamke kuumwa tumbo akiwa anaingia katika siku zake. Lakini mimi nilikuwa mjamzito sasa!! Au mimba imetoka. Sikutaka kuondoka na dukuduku. Nilimvuta daktari tukazungumza kinagaubaga.Akafikia hatua ya kunipima ujauzito!!
Hakuchukua muda mrefu akarejea. Alikuwa hajachangamka na ni kama alikuwa na jambo anahitaji kunieleza.“Ina miezi miwili sasa!!.” Aliniambia katika namna ya mshangao.“Ni maajabu wewe kuingia katika siku zako!!” aliendelea. Mimi nikiwa msikilizaji.“Kwa hiyo ni nini Dokta.”“Rudi baada ya siku saba. Kama ikiendelea hivyo. Ama la basi utakuwa mshtuko tu.” Alimaliza.Nikaondoka zangu huku nikiitazama dunia jinsi inavyonizomea.
Maria hakushangazwa na hali yangu ya kuvuja damu!! Aliamini ni kawaida tu kwa msichana. Hakujua kama nina mimba!!Siri nikabaki nayo. Mimi na daktari!!Siku ya kwanza, ya pili, ya tatu….damu zinaendelea kuvuja tena bila kukoma!!!! Kazi ikawa ipo kwangu kila mara kubadili nguo zangu.Siku ya nne, ya tano….bado tatizo likawa lile lile. Mateso sasa!!! Mimba gani hii!!!Sikuingoja siku ya saba ifike. Nikarejea hospitali.Daktari alinipokea vizuri. Nikampa kwa siri kiasi fulani cha pesa ili aweze kunihudumia kwa upendeleo.
“Hadi leo bado damu inakutoka?” alishangaa daktari. Nikamthibitishia kuwa bado zinatoka tena mfululizo.Akakuna kichwa chake chenye mvi nyingi kasha akahamia kidevuni. Na penyewe akajikuna kwa muda.“Hebu njoo…” akanipeleka katika chumba kingine. Akanipima tena mimba.Daktari akashtuka!!!“Kwa mara ya kwanza katika miaka yangu 20 ya kazi!!!” alihamaki.“Nini? Nini dokta.” Niliuliza.“Wiki iliyopita ilikuwa na miezi mingapi vile.”“Miwili ulisema.”“Sasa imefikaje miezi sita leo???” aliniuliza. Nikahisi kuzizima. Nikakaa chini!!!Daktari naye alikuwa ana hofu!!Ni kama daktari alikuwa haamini ambacho amekiona, katika mwili wangu na alichokuwa akifanya pale ni kunitoa tu katika hofu.
Mabadiliko ya mimba yangu yalimfanya achanganyikiwe.Tulirejea katika chumba chake cha ofisi. Mazungumzo yaliyokuwepo ni juu ya kuitoa mimba ile.Daktari alikataa kata kata akidai kuwa mimba ikifikisha miezi sita na msichana akijaribu kuitoa basi lazima atapatwa na matatizo na kuna uwezekano wa kufa.Maelekezo ya daktari yaliyoambatanishwa na neno KUFA yalinipa ahueni ya nafsi kwa sababu nilikuwa nataka kufa. Sikuwa na ujasiri wa kujiua na hakika nilikuwa naogopa kufa.Lakini kufa kwa namna anayoitaja daktari hata hakunipa hofu badala yake nikavutika na kumsihi anisaidie kuitoa ile mimba.
Mazungumzo yalikosa kabisa muafaka. Daktari yule alikuwa mbishi sana hakutaka kushiriki katika utoaji mimba huu. Nilipoona daktari huyu amekuwa na msimamo sana niliamua kutumia njia fulani ambayo hugeuza ukweli kuwa uongo na uongo kuwa ukweli. Nikaangusha mezani shilingi laki mbili. Akazikataa, nikaaga nikatoka. Niliporejea niliziongeza zikafika laki nne.Daktari akazikodolea macho, kisha akatazama kushoto na kulia.“Umekuja na nani?” akaniuliza.“Mwenyewe!” nikamjibu. Akatazama tena kushoto na kulia kisha akazikwapua zile pesa akazizamisha katika sehemu zake za siri. Nikakwepesha macho.Akanifanyia ishara ya mkono. Nikamfuata hadi katika chumba kilichokuwa na harufu kali ya madawa. Akakifunga na funguo tukabaki wawili tu! Kimya.
Daktari alikuwa na hofu. Nililitambua hilo. Sikutaka kuuliza chochote.“Toa nguo zote.” Aliniamuru. Kauli yake ikanikumbusha kauli ya yule Mnaijeria aliyetaka kunibaka kwa kujifanya ananifanyia tiba ya asili. Huyu sasa alikuwa daktari, nikaamua kucheza pata potea. Kwanza nilikuwa natokwa damu. Sidhani kama angeweza kujaribu kunibaka.Nikaziondoa zote, wakati huo yeye alikuwa amejikita katika kuchanganya madawa yake ambayo sikuelewa kazi yake ni ipi. Nikabaki kumsubiri.Njoo hapa!! Aliniamuru huku akinielekezea kitandani.Geuka hivi!! Nataka kukuchochoma sindano. Nikageuka huku nikiwa katika uoga. Kifo! Nilikuwa naogopa kufa.
Nikahisi kitu cha baridi kikinipapasa. Nikauma meno yangu kungoja uchungu wa sindano. Nilingoja huo uchungu lakini hamna nilichohisi.“Acha kujikaza wewe sindano itakatikia ndani.” Alinigombeza daktari. Nikashangaa hizo lawama zinatoka wapi wakati mimi hata sijajibana. Alipoona simjibu kitu akanichapa kibao. Nikashtuka.“Mkubwa hivyo unaogopa sindano alaa!!” alinigombeza. Sikumjibu!!Nikatega tena aweze kunichoma!! Hali ikawa vile vile.“Sasa mimi nakuchoma hivyo hivyo.” Alichukua maamuzi yake binafsi.Nikageuka. Nikayasubiri maumivu!!Badala ya maumivu nikakumbana na yowe kubwa kutoka kwa daktari. Nilipogeuka na mimi nikiwa na hofu nikamkuta amekaa chini. Mbali na mimi. Alikuwa ana hofu!! Jasho likimtoka.
“Daktari!!.” Nilimuita. Hakunijibu, alikuwa katika mshangao. Alikuwa akinitazama kwa wasiwasi.Nilikuwa siijui tena thamani ya kuwa na mavazi na aibu ya kuwa uchi. Nilitapatapa hivyohivyo pale ndani. Daktari akiwa bado ananishangaa.“Vaa nguo!” aliniamuru kwa sauti ya chinichini. Nikaziendea nguo zangu na kuzivaa.Kisha nikamfuata hadi ofisini!“Chukua pesa zako!!” alinikabidhi pesa zile. Nilisita kuzichukua akanisihi nizichukue. Nikatii!!Nini kimetokea daktari? Nilimuuliza. Hakunijibu bali alisikitika.Kisha akaanza kunielezea juu ya nini alichokiona. Ilikuwa ni alama ya maajabu katika mwili wangu sehemu za makalio. Mwili wangu ulikuwa umetoboka na matundu hayoyaliweza kuonyesha alama ya ‘666’.Mungu wangu!! Nikashangaa, daktari yeye akawa ni wa kusikitika tu!
“Usipokuwa mkweli utakufa wewe na familia yako nzima kama wenzako.”“Wenzangu? Wapi”“Mnaomtumikia”“Nani?” nilihoji kwa hofu.“Mmiliki wa hiyo alama. Kwani siku wanakuwekea hawakukuambia.” Alinihoji kwa utulivu mkubwa.Nikawa kama mwendawazimu na sikuwa na lolote ninalojua kuhusu hiyo alama katika makalio yangu.“Daktari sijui lolote mbona.”“Haya shauri zako, atakufa mama, baba, mdogo wako, dada, shangazi, mjomba, wifi, na marafiki ikibidi kisha watakumalizia wewe tena kwa uchungu mkubwa.” Daktari alinieleza haya kama simulizi ya kawaida huku akinitajia orodha ya watakaokufa. Kwa lugha nyepesi alikuwa kama babu anayemsimulia mjukuu simulizi ya kutisha. Nikatetemeka sana!! Vifo!!
“Sasa daktari jamani mimi ninakuficha nini. Mimi sijui kitu.” Nilishindwa kuendelea kuongea nikaanza kulia. Nililia sana maana nilikuwa nimekata tamaa. Mbaya zaidi nilikuwa nimepigwa chapa ya 666.Badala ya maumivu nikakumbana na yowe kubwa kutoka kwa daktari. Nilipogeuka na mimi nikiwa na hofu nikamkuta amekaa chini. Mbali na mimi. Alikuwa ana hofu!! Jasho likimtoka.“Daktari!!.” Nilimuita. Hakunijibu, alikuwa katika mshangao. Alikuwa akinitazama kwa wasiwasi.Nilikuwa siijui tena thamani ya kuwa na mavazi na aibu ya kuwa uchi. Nilitapatapa hivyohivyo pale ndani. Daktari akiwa bado ananishangaa.
“Vaa nguo!” aliniamuru kwa sauti ya chinichini. Nikaziendea nguo zangu na kuzivaa.Kisha nikamfuata hadi ofisini!“Chukua pesa zako!!” alinikabidhi pesa zile. Nilisita kuzichukua akanisihi nizichukue. Nikatii!!Nini kimetokea daktari? Nilimuuliza. Hakunijibu bali alisikitika.Kisha akaanza kunielezea juu ya nini alichokiona. Ilikuwa ni alama ya maajabu katika mwili wangu sehemu za makalio. Mwili wangu ulikuwa umetoboka na matundu hayoyaliweza kuonyesha alama ya ‘666’.Mungu wangu!! Nikashangaa, daktari yeye akawa ni wa kusikitika tu!“Usipokuwa mkweli utakufa wewe na familia yako nzima kama wenzako.”“Wenzangu? Wapi”“Mnaomtumikia”“Nani?” nilihoji kwa hofu.“Mmiliki wa hiyo alama. Kwani siku wanakuwekea hawakukuambia.” Alinihoji kwa utulivu mkubwa.
Nikawa kama mwendawazimu na sikuwa na lolote ninalojua kuhusu hiyo alama katika makalio yangu.“Daktari sijui lolote mbona.”“Haya shauri zako, atakufa mama, baba, mdogo wako, dada, shangazi, mjomba, wifi, na marafiki ikibidi kisha watakumalizia wewe tena kwa uchungu mkubwa.” Daktari alinieleza haya kama simulizi ya kawaida huku akinitajia orodha ya watakaokufa. Kwa lugha nyepesi alikuwa kama babu anayemsimulia mjukuu simulizi ya kutisha. Nikatetemeka sana!! Vifo!!“Sasa daktari jamani mimi ninakuficha nini. Mimi sijui kitu.” Nilishindwa kuendelea kuongea nikaanza kulia. Nililia sana maana nilikuwa nimekata tamaa. Mbaya zaidi nilikuwa nimepigwa chapa ya 666.
“Ndio maana nimejishangaa sana, iweje leo nikubali kuchukua rushwa, nikubali kutoa mimba msichana. Ama kweli kila mwenye alama hii hatakataliwa na dunia kwa lolote.” Daktari alinong’ona kama anasema mwenyewe vile. Nilisikia kila kitu.Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa!“Nitakusaidia.” Alinyanyua uso daktari akanieleza huku akinitazama vyema usoni.Nilifarijika sana kusikia maneno yale. Kisha akaendelea, “Lakini uwe mkweli kwa kila kitu. Ukijaribu tu kuficha lolote lile. Nasema ukijaribu kuficha lolote lile. Wewe, marafiki na ukoo wako wote utatokomea.
Mimi nakueleza haya kama mzee wako, katika kipindi changu cha miaka ishirini ya udaktari nakutana na matukio mengi. Lakini hili ni la tatu katika maisha yangu. Wenzako wawili, mmoja miaka saba imepita na mwingine mwaka juzi, nilitaka kuwasaidia lakini wakaleta ujanja ujanja. Tuliwazika!! Aah!! Hatukuwazika insearch labda niseme tuliyafukia mabaki yao.” Alimaliza kunielezea kisha akashusha pumzi kali sana.Macho yangu nilihisi kama yanajilazimisha kutazama mbele. Machozi yalikuwa yamezidi. Mapigo ya moyo yalikuwa juu, sasa nikaanza kuamini niliyokuwa nayatazama katika filamu za kinaijeria.
USIKOSE SEHEMU IYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni