Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Sasa maumivu yakamtia ujasiri wa ajabu akajikuta anainuka kwa hasira na kumrukia Tajadir ili amshambulie lakini ilikuwa ni sawa na ‘Kukitoa kinu juani’ hakitanenepa wala kukushukuru, na hata ungekiacha juani kisingeungua.. Kazi bure! Akapokea kichapa kingine cha nguvu mpaka akaishiwa nguvu akaanza kupiga kelele sasa! Kelele hizo zilikuwa ni za maumivu yaliyochanganyika na kukata tamaa!
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Cha ajabu hekaheka zote hizo hazikumuamsha mtu yoyote mle ndani ya Selo wala hazikusikika kwa maaskari wa zamu usiku ule..
Komandoo Takadir akaendelea kumtesa sana Suhail ili aoneshe Pete ilipo.. Lakini ghafla katika hali ambayo hata Takadir hakuitegemea Suhail akatoa ukulele wa nguvu ukawafikia mpaka wale maaskari kule Kaunta.. kwa kasi na haraka Maaskari wakaukimbilia mlango na kuufungua.. kabla hawajafika ndani tayari Takadir alishafanya tukio jingine baya, alimpiga Suhail na miale kutoka katika macho yake, miale yenye nguvu kama umeme! Suhail hakuelewa kilichotokea zaidi ya kuhisi akirushwa na kitu kama Shoti ya umeme kilichombwaga chini na kumwacha akiwa hana fahamu!
Askari walipoingia ndani walishangazwa na hali ile ya ajabu, walimkuta Suhail akiwa ametapakaa damu lakini akiwa hana jeraha hata moja.. wakajaribu kumuinua ndipo wakagundua kuwa amepoteza fahamu haraka wakamtoa nje ili kumpatia huduma ya kwanza.. mpaka kufikia hatua hiyo hapakuwa na mahabusu hata mmoja aliyeshituka kutoka usingizini
“Humu kuna jambo limefanyika!” Aliongea Askari mmoja aliyekuwa akimpepea Suhail
“Bila shaka!.. haiwezekani mtu aumizwe halafu wenzie wawe wamelala tu”
“Kwani huyu kijana ana kesi gani humu?” Aliuliza tena Yule Askari anaempepea Suhail
“Kwani we hujamjua huyo? Huyo nd’o ukisikia Suhail Yule tajiri anaehusishwa na mauaji ya Msigwa.. Tena ngoja nimpigie simu Insp Kenja ndiye anayeshughulikia kesi yao” Baada ya majadiliano ya hapa na pale akapigiwa simu Insp Leonard Kenjah, akaahidi kuwasili kituoni muda si mrefu sana!
Alipofika akamkuta Suhail ameshazinduka lakini hali yake si nzuri, anaonekana kupewa matesomakali sana lakini hakuwa na jeraha hata moja mwilini
“Suhail,” Aliita Kenjah huku akimshika kichwa Suhail
“Afande,” Aliitika kwa sauti hafifu iliyobeba maumivu makali
“Imekuwaje tena hivi,” Alisaili Insp Kenjah.. ikamchukuwa Suhail muda mrefu sana kabla hajaanza kuwaelezea juu ya mtu aliyemtokea ghafla na kumwadhibu vilivyo.. ilikuwa ni kama simulizi za watoto vile maana hakuna hata mmoja aliyeielewa.. kuamini kuwa kuna mtu aliingia na kumtesa vile bila sababu halafu ukizingatia mlango ulikuwa umefungwa ilikuwa ni Ndoto.. kibaya zaidi hata Mahabusu wenzie hawakusikia chochote. Inspekta akaagiza Daktari aitwe kuchunguza hali ya Suhail, na hata alipowasili daktari na kufanya uchunguzi wake majibu yalikuwa ni ya kushangaza sana! Suhail hakukutwa na tatizo lolote!
Mapambazuko, siku mpya ikaanza! Habari zilizotawala kituoni ni tukio la jana yake usiku dhidi ya Suhail!
Insp Kenjah alikuwa ofisini kwake akisubiri taarifa kutoka katika vikosi vyake ambavyo vilikuwa tayari katika majukumu yao, Muda huo familia nzima ya Suhail iliwasili kituoni kuendeleza jitihada zao za kumwekea dhamana kijana wao! Safari hii zoezi halikuwa gumu kwani Insp hakuona sababu ya kuendelea kukaa na mtu asiyeonesha dalili ya kuhusika na mauaji yale ukizingatia na hekaheka ya jana yake usiku akaona asije kuwafia mikononi mwao, Akampa dhamana!
Hali ya Suhail iliwashangaza sana wazazi wake, Mkewe na hata wafanyakazi wake kwa jinsi alivyodhoofika! Wote wakaamini kuwa aliteswa sana na askari licha ya yeye mwenyewe kukana hilo.. walidhani pengine amekatazwa kusema ukweli! Baada ya kupewa dhamana na kufanya makabidhiano ya vitu vyake ikiwemo Pete(Khatam Budha) Wakamchukuwa mpaka nyumbani ambapo aliwaeleza kisa kizima cha kutokewa na Yule mtu! japo alificha kumfahamu, ilikuwa ni kisa kilichozidisha Hofu na mashaka! Sharifa amepona kimiujiza na Sasa Suhail anaumwa kimazingaombwe, Kazi ipo!
Japo aliivaa Pete yake lakini haikumfanya Apone, hali yake ilikuwa mbaya tu japokuwa kidogo aliingiwa na nguvu mwilini.
*****
Simu ya Insp Kenjah iliita, akaitoa na Kuiangalia kabla hajaipokea.
“Hallow”
“Yes Boss.. Tuko Ilala Boma nje ya Hotel ya Shree Godha, tunamwona Joram Ndege anaingia ndani ya ile gari tuliyokuwa tukiishuku.. na sasa natafuta mwelekeo wa kutoka barabarani.. amevaa suti nyeusi na mkononi ana brifkesi” Ilikuwa ni sauti ya Sajent malumbo akitoa taarifa
“Good news, Endeleeni kumfuatilia kwa uangalifu mkubwa.. akigundua tu kuwa anafuatiliwa mjuwe kesho tutayapigia mizinga majeneza yenu kabla ya kwenda kuwazika, Ni mtu hatari huyo..”
“Ok Boss” Simu ikakatwa.. Damu ikamchemka sasa Insp Kenjah akainuka na kuketi tena asijielewe anataka kufanya nini.. Dakika chache akapokea tena simu
“Ongea Sajenti,” Alinguruma Insp
“Ameshika barabara ya Uhuru, anaelekea Buguruni.. ndani ya gari wako wawili tu yeye na dereva wake,”
“Nimekupata.. kama nilivyokueleza,” Alijibu Kenjah na kukata simu kisha akampigia Koplo Malando
“Nipe habari za hospitali”
“Kila kitu kinaendelea vizuri Afande, hakuna mpya!” Simu ikakatwa. Insp akarejea kuketi
Dakika kama arobaini baadeye Insp akapokea tena simu ya Sajini Malumbo “Tuko Banana, Gongo la Mboto. Kwenye hii barabara inayochepuka kwenda kitunda mkono wa kushoto kuna Jengo moja kubwa la ghorofa moja limepakwa rangi ya njano kwa mbele ndipo gari ya akina Joram Ndege imeegeshwa.. na sasa namwona anateremka na kuanza kuelekea ndani”
“Kuna gari yoyote nyingine imeegeshwa hapo?”
“Ndiyo, zipo kama tatu hivi kuna Landcruiser G8, Prado, na Rangerover”
“Nakili namba za gari hizo haraka kisha nitumie kwa meseji.. usifanye mchezo wowote wa kitoto! Subiri hapohapo mpaka atakapotoka halafu uhakikishe unawaona watakaoingia ndani ya hizo gari zingine na ukishawaona jitahidi unijuze ni akina nani hao kabla hawajakuuawa, Sawa?” Ilikuwa ni ishara tosha kwa Sajent Malumbo kuwa akicheza tu atauawa na si vinginevyo!
“Sawa Boss” Simu ikakatwa
*****
Nyumbani kwa Suhail aliwasili Dokta wake na kuanza kumpa matibabu japo naye hakuuona ugonjwa wala athari ya mtu aliyeteswa.. Mzee Fungameza kwakuwa ni Muumini mzuri wa dini ya kikristo ambaye pia ni Mzee wa kanisa huko kanisani kwao Tabora akaanza kuporomosha maombi huku akisaidiwa na mkewe, Mzee Kusekwa naye kwa imani ya Dini yake ya Kiislam akawa anafanya dua kwa mwanaye.. Badala ya kuimarika hali ikazidi kuwa mbaya
Sharifa yeye hakukaukiwa machozi mashavuni mwake!
*****
Joram Ndege aliposhuka aliingia ndani ya Jengo lile na kupotelea kwenye Korido moja ndefu iliyosheheni vyumba vingi kulia na kushoto, kila chumba kikiwa na watumishi wakiendelea na majukumu yao taofautitofauti.. Korido ile ilimchukuwa moja kwa moja mpaka katika chumba kimoja kilicho kwenye kona, alipofika hakugonga mlango wala kubonyeza kitufe chochote Mlango ukafunguka wenyewe, bila shaka alikuwa akionekana kwenye camera maalum
Alipoingia akapokelewa na sura za vigogo na waheshimiwa kadhaa wakiwa na sura zilizomakinika hasa na jambo Fulani, akaketi bila ya kusalimia
“Nadhani tumekamilika?” Alifanya tashtiti Bwana Ibrahim Basha Bin Mende ambaye alikuwa ameketi katikati ya jopo lile haram akiwa kama mwenyekiti wao, Jina lake halisi ni Ibrahim Basha hilo la bin Mende alibandikwa tu kutokana na tabia zinazosemwa kuwa alipata kuwa nazo.. ni tabia chafu japo mwenyewe amekuwa akijitetea kuwa ni wabaya wake kisiasa nd’o wanamchafua.. Yeye ni mtu mwenye ushawishi mkubwa sana ndani na nje ya serikali. Upande wke wa kulia waliketi watu watano;
Mhe Hamid Humud(Naibu waziri wa nishati na madini), Mhe Abdiroush Warriya(Naibu Waziri wa fedha), Bwana Moris Kungurume(Mfanyabiashara wa madini), na Bwana Charles Bikoraimana(Mfanyabiashara wa masuala ya usafiri wa majini). Upande wa kushoto Pia kulikuwa na vibopa watano; Kamanda Katinda Kuya(Mkuu wa polisi kanda maalum), Joram Ndege(Muuwaji wa kutumainiwa), Bi Kapemba Kitivo(Mkuu wa mkoa wa Musoma), John Patrick Massawe(Kiongozi wa chama cha upinzani), Msimbe Abrahams(Mbunge wa mkoa wa Manyara) na Adams Gosh(Muwakilishi wan chi ya Ugiriki ambayo ndiyo unaofadhili mpango ule). Baada ya kufunguliwa kikao kile aliendelea kuongea Mwenyekiti Ibrahim Basha Bin Mende
“Mnaweza kushangaa Mhe 5051-10s na Mhe 42&2c hawajawasili.. imebidi tuwazuie kufika huku mara kwa mara maana kufuatia hili vuguvugu linaloendelea bila shaka watakuwa katika uangalizi mkali wa wana usalama hivyo si vyema kuwaalika huku kwa sasa.. ila wao kama Raisi wetu mtarajiwa na waziri mkuu wake watakuwa wakipewa taarifa za kila kinachoendelea kupitia mitandao yetu ya siri..”
Akasita kidogo na kuwatulizia macho vigoo walio mbele yake kisha akaendelea ”Kifo cha Yule Mshenzi Msigwa kimesababisha baadhi ya mambo yetu kusita kwa muda maana kuna uchunguzi mkali wa chini kwa chini unaendeshwa na Inpekta Leonard Kenja pamoja na vijana wake.. nimekuwa nikiyapata mawasiliano yake kwa kina kupitia mtambo wetu wa Divier japo upelelezi wao unaonesha kutogundua lolote kuhusu sisi ila kuna dalili zote kuwa maji yanaweza kuzidi unga muda wowote”
“Kivipi?” Alisaili kwa wahka Mhe Mlenda
“Kuna tetesi kuwa IGP Succa amekuwa akimdodosa sana Mhe 5051 kuhusu haya matukio ya watu kuonekana wametma meseji sehemu waklati hawakufanya hivyo.. cha kujiuliza kwanini ang’ang’anie kumuuliza yeye wakti kuna wahusika wa masuala ya mawasiliano? Pia kuna habari za kutekwa kwa Yule Sekretari wa kule alipokuwa akifayia kazi Msigwa.. inasemekana Msigwa alikuwa ana mahusiano ya kimapenzi ama ndo alikuwa katika mchakato huo na Yule binti hivyo inawezekana amemwambia mengi kuhusiana na sisi kabla ya kuuawa kwake lakini cha ajabu binti Yule ametekwa na sisi hatukuhusika na tukio lilesasa bila shaka ni mbinu tu imetumika na maadui zetu kumtowesha ili awape chochote akijuacho kutoka kwa Msigwa..Sasa tulichoamua ni kuwamaliza wote wanaoonesh dalili ya kutaka kung’amua chochote katika mpango wetu huu..”
Akatulia tena kidogo kuruhusu maneno yake yaingie vichwani mwa wana mkakati kisha akaendelea “ Kwanza kabisa inatakiwa tuwajue waliomteka halafu pili Yule Mhariri Bwana Bucha naye anatakiwa akamaliziwe huko hospitali maana sote tunafahamu kuwa walikuwa wakimgombania huyo Lilian hivyo kama Msigwa alivujisha habari zetu kwa mwanamke Yule bila shaka mwanamke huyo naye alivujisha kwa huyo Bucha..”
“Kuhusu Bucha.. nitaiendea roho yake huko hosptali baada ya kikao hiki,” alidakia Joram Ndege
“Kuhusu huyo aliyeteka baada ya kikao hiki nitaenda kwa IGP bila shaka atanitapikia ukweli wote,” akadakia Kamanda Kuya
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi