Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA THELATHINI NA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“Kuhusu Bucha.. nitaiendea roho yake huko hosptali baada ya kikao hiki,” alidakia Joram Ndege
“Kuhusu huyo aliyeteka baada ya kikao hiki nitaenda kwa IGP bila shaka atanitapikia ukweli wote,” akadakia Kamanda Kuya
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
“Good..huko kote mimi sina shaka napo ila ninataka kukazia jambo moja tu kuwa tujiepushe na matumizi yasiyo ya lazima ya mtambo wa Divier maana nd’o umeleta yote haya.. tujaribu kuyaheshimu makubaliano yetu juu ya mtambo ule na ikiwezekana kwa kuwa si mkubwa sana hata humu uhamishwe tu maana hata siku likitokea la kutokea tusijegundulika hila zetu mapema..” aliongea kwa Utulivu Mhe Humud
“Yeah, hilo kweli ni la msingi sana.. na kuanzia tulipomaliza kadhia ile ya Msigwa kwa sasa mtambo ule haufanyi kazi nyingine yoyote zaidi ya udukuzi wa mawasiliano.. kwa mfano kila siku kasoro juzi na jana nimekuwa nikipata habari zote za huyo Kenjah na mbwa wake..” Baada ya hapo ukafuatiwa mjadala mwingine ambapo Msemaji mkuu alikuwa Mr Adams ambaye alikuwa akawasilisha majibu ya maombi ya fedha na silaha kutoka kwa Black Scopion kwenda nchini kwao
Baada ya nusu saa ya kikao wakapangiana majukumu kisha kikao kikaahirishwa na kila mmoja akatoka.
Simu ya Inspekta Kenjah aliita, alikuwa Sajenti Malumbo akipiga kutoa taarifa, Kenjah alikuwa akiisubiri kwa hamu simu hiyo maana zile namba za magari alizotumiwa kwa meseji kama alivyoagiza hazikuwa na majibu ya haraka maana hazikuwa za serikali wala watu binafsi
“Hallow.. lete habari Sajent”
“Naona wanatoka sasa ndani”
“Umemjuwa hata mmoja?”
“Ndio” Sajent Malumbo aliwajua wale mawaziri, mfanyabiashara mmoja pamoja na Kamanda wa Polisi, akamwambia Inpekta
“Hii sasa ni hatari, naomba muendelee kumfuatilia Joram Ndege. Hao wengine achaneni nao”
“Ok Boss”
*****
WAKATI Inspekta Kenjah akiinua simu yake kumwarifu IGP juu ya taarifa ile ya kushitusha tayari Joram Ndege alikwishaingia ndani ya gari aliyofika nayo pale na kuanza kuondoka. Sajenti Malumbo naye kama alivyoagizwa akawa nyuma yake akimfuatilia kimyakimya huku akitoa taarifa hatua kwa hatua.
Baada ya ghasia za foleni na shtighali za hapa na pale hatimaye msafara ulikomea nje ya hospitali ya taifa Muhimbili, Joram Ndege alitoa mguu mmoja baada ya mwingine ndani ya gari ikifuatiwa na kiwiliwili chake kilichojazia misuli minene, huku nako nako Sajenti Malumbo akitoa simu yake maalum na kumpigia Inspekta Kenjah
“Bila shaka sasa amedhamiria vita..” alijibu Inpekta kisha akakata simu, na kumpigia Koplo Malando aliyekuwa Doria hapo hospitalini kwa muda mrefu
“Meno ya dhahabu ameshaingia hapo, hakikisheni haingii kwenye wodi aliyolazwa Bucha.. nami nafika hapo sasa hivi siko mbali sana,” Aliongea Inspekta
“Nimemwona tangu anaingia.. amevaa suti nyeusi ila ameipita tu Wodi aliyomo Bucha, hapa namwona anakwenda kule Wodi za Mbele kabisa.. Namwona kuna wodi ameingia sasa hivi” Alijibu Koplo na kuendelea tena “..Kuna nesi pia namwona anaingia humohumo alimoingia Joram”
“Huyo ni mjanja zaidi ya sungura itakuwa napoteza malengo tu.. kuweni makini sana, mfuate haraka na kwa hadhari ya hali ya juu, Kama atataka kufa kabla hajakamatwa muue tu.” Simu ikakatwa
Haraka Koplo Malando akawahimiza vijana aliokuwa nao pale wakaweka silaha zao tayari tayari kisha yeye akajitosa.. akaenda mpaka usawa wa ile wodi alimoingia Ndege, alipofika hakupoteza muda akausukuma mlango…
Patupu!
Chumba kilikuwa kimya hapakuwa na mtu mwingine zaidi ya mgonjwa aliyelala kitandani akiwa amejifunika Shuka. Koplo akaanza kupepesa macho yake chumba kizima..
Kimya!
Akapeleka mkono wake kiunoni kuiangalia silaha yake, akaikuta ikimsubiri yeye tu, akaiacha na kuendelea kukikagua chumba. Akafungua makabati yaliyokuwamo mle ndani lakini hakukuta mtu, akachungulia chini ya uvungu wa kitanda nako Hola! Akapiga hatua kadhaa mbele na kumsogelea yule mgonjwa aliyefunikwa shuka.. hapo sasa ndipo Moyo wake ulipopiga almanusura ya kuchana kifua chake.. Hakuwa mgonjwa Kamwe!
Ulikuwa ni mwili tu uliotengana na roho, ni mwili wa Yule nesi aliyeingia mle Wodi akifuatana na Joram Ndege! Loo salale,
Sasa kwanini amemuua huyu dada asiye na hatia? Na amejificha wapi sasa? Alijiuliza Koplo bila majibu. Akataka kutoa simu yake ampigie Inspekta lakini akahofia kuusumbua utulivu wa chumba kile cha wagonjwa
*****
Askari kanzu watatu walikuwa mbele kidogo ya Wodi aliyolazwa Bucha, japo walijifanya kuwa bize na mambo yao lakini macho yakiwawaka kwa kuhakikisha usalama wa eneo lile.. walifanikiwa kuulinda usalama lakini si kuizuia shari ya Joram Ndege.
Ndani sasa ya Wodi Bwana Kareem Bucha alikuwa amelala kitandani huku akiwa hajarejewa na fahamu, hali yake ilikua tiamajitiamaji, Mbele ya kitanda chake palikuwa na mrembo mmoja amesimama na kujaribu kumfunika vizuri mgonjwa, bila shaka mrembo alikuwa ni Nesi kwa muonekano wa mavazi yake
Nesi huyo aliyekuwa akiendelea kumfunika na kumwangalia mgonjwa wake alikuwa akikabiliwa na hatari bila ya kujijua! Usawa wa kichwa chake kwa juu kidogo, dari ya chumba kile cha Wodi ilifunuliwa taratibu kwa kipande kidogo cha ‘Singibodi’ kuwekwa pembeni kasha mwanaume mwenye meno ya dhahabu akawa akichungulia kwa chini kama popo. Alikuwa ni Joram Ndege katika ubora wake!
Alichokifanya ilikuwa ni mchezo mdogo tu, kumvunja shingo Yule nesi aliyejipendekeza kwake kule wodi ya mbele kisha akanyakia dari na kuanza kutembea juu kwa juu mpaka huki katika wodi aliyopo Bucha akidhamiria kushuka kuumaliza mchezo!
Kwa mtu wa kawaida ilikuwa ni kazi ngumu kushuka tokea kule juu wakati ndani kuna mtu usiyetaka ashuhudie ukiichukua roho ya mgonjwa wake hivihivi ila si kwa Joram Ndege, angeweza hata kuzinyakua roho zao wote wawili ila tu akaamua kufanya subra mpaka nesi Yule atakapotoka, Haikuwa hivyo! Nesi hakutoka..
Kwa joram Subra ni kitu adhim hivyo alikienzi daima! ikapita dakika ya kwanza, ya pili, ya tatu.. wakati mishale ya sekunde na dakika ikiendelea kukimbia ndani ya saa yake, Moyo nao uliendelea kukimbia ndani ya kifua chake akitambua kua muda si mrefu hospitali nzima itakuwa katika uangalizi kufuatia kifo cha yue nesi, Hakuiona tena haja ya subra ile!
Akachungulia chini, akajiridhisha juu ya ukaaji wa Yule Nesi, akamalizia kuifunua vizuri sehemu ya dari iliyosalia kisha kama umeme akajitoma ndani! Lilikuwa ni tukio la ghafla ambalo kwa nesi wa kawaida angetoka mbio lakini si kwa dada Yule Mrembo mwenye umbo lililokatika mithili ya namba nane na weusi wa kung’aa watoto wa mjini huuita ‘Blaki byuti’
Lengo la Joram sasa likabadilika toka kwenye kuchukua roho moja ya Buchan a kuwa roho mbili pamoja nay a nesi huyu!, kilichotekea Joram Ndege alibaki kinywa wazi. Alipokea mapigo ya judo mfululizo kutoka kwa Yule Nesi, dakika mbili uso wake ukawa hautamaniki! Alijaribu kujiinua kutokea kule sakafuni alikuangukia baada ya kupata dozi ya nguvu lakini kabla hajakaa sawa tayari Nesi alikwishawasili eneo lake na na kumshindilia maketeke ya mbavuni mpaka akaguna! Ilikuwa ni kimyakimya.
Nesi naye akafanya uzembe kumwacha Joram ainuke japo alikuwa ameshalegea kwa kichapo cha nusu dakika tu, Ndipo Macho ya Joram yakakutana na Nesi Yule.. akamtambua, akaachia tabasamu ambalo lilibadilika ghafla baada ya kumwona mrembo Yule aliyevalia sare za manesi akimjia kwa kasi ya kumshambulia, akajiweka sawa na kulikwepa pigo jingine kutoka kwa dada Yule mwenye wepesi wa miguu kisha akaachia Pigo kali la ngumi lililokita katika mbavu za Nesi mpaka akatoa muungurumo mithili ya vyura wa majarubani.. Nesi akaanguka chini kama kifurushi na kabla hajatahamaki akafuatwa hapo chini na kunyanyuliwa mzobemzobe na kabla hajajua afanye nini akapokea ngumi nyingi za uso, Damu ikakutana na vipodozi alivyojiremba vikasambaa hovyohovyo usoni na kuwa mfano wa Upinde wa mvua!
Kiza kitanda usoni mwake huku nyotanyota zikiyadhihaki macho yake!
Bila kuchelewa Joram akamkata Ngwara Nesi yule na kumsindikiza na Teke la kichwa mpaka chini, lakini kwa wepesi wa ajabu Nesi akaruka tena juu mithili ya mtu aliyekalia kaa la moto, aliposimama tu hakutaka kufanya urafiki na muda, akaingiza mguu wake katikati ya miguu ya Joram aliyekuwa ameshitushwa na wepesi wa dada Yule na kumtandika teke kali katika Korodani zake! Yowe la uchungu likamtoka Joram. Yowe hilo ndilo lililowashitua wale maaskari waliokuwa wanaendelea na Lindo pale Hospitalini, Wakaivamia Wodi ile silaha zao zikiwa mikononi.. walipojaribu kuufungua mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, Wakauvunja!
Walipoingia tu wakakutana na hali ile ya Sintofahamu, Wekundu wa damu ukiwa umetapakaa katika nguo nyeupe za nesi yule aliyekuwa amekunja ngumi akimwangalia Joram ambaye alikuwa ameyabana mapaja yake huku uso akiwa ameukunja kwa maumivu kiasi cha kufanya meno yake ya rangi ya dhahabu kuonekana waziwazi..
Kilichowashangaza zaidi ni namna watu wale walivyoingia mle Wodini maana si Nesi wala huyo mwanaume wote hawakuingilia mlangoni hivyo hakuna mlinzi hata mmoja aliyeufahamu uwepo wao! Sasa kabla hawajajua cha kufanya Joram alikwishafanya jambo. Risasi mbili kutoka ndani ya Bastola yake aliyoitoa kibindoni zilipenya katika mbavu za askari kanzu mmoja kati ya wale walioingia mle wodini, alipomgeukia askari mwingine ili naye amtende kama mwenzie alikuwa amechelewa maana teke kali kutoka kwa yule Nesi aliyekuwa akipambana naye na kuisambaratisha Bastola yake na hapo sasa ikawa ni vurugu na patashika ya nguo kuchanika
Joram akapata upenyo na kutoka Wodini kwa kasi akifuatiwa na wale askari pamoja na Yule Nesi asiyejulikana, Kasi aliyotokana nayo Joram ilimchukulia kama nusu dakika tu kulifikia gari lake na kujitoma ndani, Muda huo Koplo Salum alikuwa akitoka kule wodini akifuatiwa na msururu wa madaktari aliowaita kuangalia maafa yale yaliyomkumba mtumishi wao ndipo sasa akaona ile vurumai ikitokea kule Wodini, Akajitahidi kukimbilia lile gari huku akitoa Bastola yake na kuanza kuirushia risasi lakini haikufaa kitu, gari ile ilikuwa hairuhusu risasi kupenya ndani yake, na hata hakupata fursa ya kuisogelea gari ile kwani dereva wa Joram Ndege aliyaelewa majukumu yake,
Gari liliacha vumbi tu!
Haraka baadhi ya madaktari wakakimbilia kule Wodini kumwangalia mgonjwa, Alikuwa akiendelea na utaaban wake wa mwanzo wala hakuumizwa zaidi ila chini kwenye sakafu alikuwa amelalia dimbwi la damu askari kanzu mmoja
Wakiwa bado wanashangaa kule nje, Yule Nesi naye akiwa ametapakaa damu waliishia kumwona tu akijitoma ndani ya gari nyingine iliyokuwa imeegesha pembeni na kutoweka kwa kasi ileile, Koplo Salum alimtupia macho yule nesi haraka
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi