Mtunzi: Hussein O. Molito
SEHEMU YA KUMI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“sipati usingizi kwa ajili yakoSam, naomba uniokoe kwenye hili gharika la mahaba lililonikumba mwenzio kwa kulala na mimi japo usiku mmoja wa leo tu” aliomba yule dada na kumvaa Sam aliyekuwa kifua wazi huku akiwa na boxer peke yake.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
“naomba uondoke, dada sijisikii vizuri” aliongea Sam baada ya kuona kizunguzungu kimempata mara tu baada ya kuguswa na damu changa ya yule mtoto mzuri.
“naomba nionee huruma Sam, nipe hata kamoja tu nitasuuzika moyo wangu” aliongea yule dada na kuupapasa mwili wa Sam alifanya hayo na Sam hakuongea kitu tena zaidi alianza kulegea miguu na kuangukia kitandani.
Yule dada alianza kusaula nguo zake baada ya kumuona Sam kalegea kwa kujua alikua ammempatia kwa kumshika Sam sehemu zake zenye mihemko mikali.
Alimfata na kumkalia juu huku akiendelea kuchezea vinyweleo vidogo vilivyokua kifuani kwa Sam.
ghafla aliona vile vinyeleo vinaongezeka na mwili wa Sam unabadilika rangi na kuwa wakijani. Mara Sam akabadilika na kuwa mnyama wa ajabu.
yule dada aliruka pale kitandani na kuanza kupiga kelele. Alikimbilia kufungua mlango lakini hakufanikiwa. Kwani tayari Sam alishamrukia na kuanza kumnyonya damu yake shingoni. Hakua na uwezo wa kupiga kelele tena sana sana alianza kupapatika kama kuku aliyechinjwa na kuachiwa. Dakika moja baadae akaaga dunia
“Sam, nakuomba usighairishe safari!” aliongea Haiba baada ya kumuona Sam akiwa haeleweki.
“ siwezi kwenda popote mpaka nimshuhudie mwanangu” aliongea Sam huku akimuangalia Jane aliyekua anacheka cheka bila kujua kinachoendelea.
Haiba alijitahidi sana kumbembeleza, lakini Sam alikataa katu katu. Mida ikazidi kuyoyoma mpaka usiku ulipoingia. Haiba jasho lilimtoka mpaka machozi lakini wapi. Hazikufua dafu kwa Sam. Mida ilipokaribia, Haiba alimuaga Sam na na kutangulia kwa safari maana chombo kilishafika. Alipofika na kupanda, kwa mbaali alimuona Sam akija huku anakimbia. Alifurahi na Sam akapanda kile chombo na safari ya kuelekea katika sayari ya Mars ikaanza.
Walitumia usiku wote angani na mchana wa siku yapili chombo kilitua kwenye uwanja maalumu uliofurika watu wote wa jamii ya Baikiri. Watu walianza kushangilia na milango ikafunguliwa na watu wawili muhimu walishuka. Watu hao ni Haiba na Sam.
Walikaribishwa kwenye viti malumu na mfalme ambaye alidhoofu kwa mawazo juu ya mwanaye, alisaidiwa kwa kushikwa mkono na Msemaji mkuu na kupelekwa kwenye kiti cha enzi na kukaa.
Haiba na Sam walimsogelea mfalme na kupiga goti na kuinamisha vichwa vyao kama ishara ya kumuheshimu.
Mfalme aliwakumbatia wote wawili na na kuanza kulia. Wote wakaungana naye na kuanza kulia. Aliwaangalia kwa zamu na kutoa shukurani kwa Haiba kwa kumletea mwanae wa kiume.
“Sam mwanangu” aliongea mfalme huku machozi yanamtoka.
“naam baba” Sam aliita baba kwa mara ya kwanza. Uwanja woote ukashangilia na furaha iliyotoweka kwenye jamii yote ya Bikiri ikarudi tena.
******************************
Haiba na mama yake walipewa nyumba moja kati ya nyumba za ikulu kama zawadi yake. Alipewa cheo kikubwa na mali nyimgi. Yalichongwa masanamu mawili makubwa yenye sura ya Sam na Haiba kama maashujaa wapya wa jamii ya Bikiri.
Baada ya miezi miwili mfalme Josh akaaga dunia na Sam akatawazwa kama mfalme mpya akiwa na umri mdogo. Ilikua ngumu kuongoza bila kuwa na mke. Akaambiwa achague mke na kuamua kumchagua Haiba kwakua alikua anampenda pia.
Harusi ya aina yake ilifungwa kwa mashujaa hao walioishi sayari ya tatu bila kupata madhara yoyote.
Haiba alishika mimba na kujifungua mtoto wa kike. Wakaenda kupima na kukuta Sam hawezi kuzaa tena maana watoto waliisha.
“sina budi mke wangu, natakiwa nirudi duniani nikamchukue mtoto wangu” aliongea Sam na kumwangalia Haiba.
“sina neno mie, ila tutaenda wote. Maana nakujua jinsi unavyompenda yule msichana unaweza kubaki huko huko.” Alitania Haiba na wote wakacheka.
*************************
Safari ya kuelekea duniani ilitimia na Sam na mkewe walitua salama duniani. Haiba alichukua mkufu wake wa ajabu na kuanza kuangalia maisha ya Jane kuanzia pale walipomuacha Hospitali.
Walimuona Jane akijifungua mtoto wa kiume na huyo mtoto kulelewa katika kitua cha watoto yatima. Cha ajabu huyo mtoto alikua anakula vyakula vya duiani bila shida. Alifanana kabisa na Sam. Haiba alikatisha na wakaamua kwenda kituo cha kulea watoto yatima.
“mtoto mnayemuulizia anaitwa nani?” aliuliza mlezi baada ya salamu na utambulisho.
“ jina hatulijui ila mama yake anaitwa Jane James” alijibu Sam na kumfanya yule mlezi kumuangalia usoni. Alistaajabu kumuona anafanana sana na mtoto wake.
“bila shaka wewe ndio baba yake, ulikua wapi siku zote?” aliuliza yule mlezi swali lililochelewa kujibiwa.
“ nilisafiri na nimerudi ndio nimepata taarifa kuwa mtoto wangu analelewa humu.” Aliongopa Sam.
“huyo mtoto anaitwa SAMJE. Hilo ndilo jina alilokua analiimba mama yake toka alipokua anajifungua”.
Sam alicheka baada ya kugundua kua japo Jane alikua hana akili kabisa, lakini aliunganisha jina lake na lakwake na kutoa jina la mtoto. Alijisemea moyoni kuwa Jane alikua ana mapenzi ya kweli moyoni mwake juu yake.
Walipewa maelekezo na kumchukua mtoto na kwenda naye hospitalini.
Jane alipomuona tu Sam alinyanyuka alipolala na kumuita.
“SAM!!” Aliita Jane kwa sauti kubwa.
“JANE!!” aliongea Sam na kumuangalia machoni Jane.
Jane aliamka na kumkumbatia Sam. Sam alishangaa kumuona mpenzi wake akiwa amerejewa na fahamu. Daktari alikuja mbio na kushangaa kumuona mgonjwa wake karudiwa na akili zake. Alimchukua na kwenda kumpima. Akagundua kua amepona.
Waliongea mengi sana ikiwemo kumwambia ukweli kuwa kaoa mwanamke mwengine nay eye kurudi kwao. Pia walimwambia Adhma yao ya kuja kumchuku mtoto.
Mwanzoni Jane alikataa, lakini walipompa mkufu wa ajabu utakaomuwezesha kupata mawasiliano ya moja kwa moja na wao wakati wowote. Akakubali kwa shingo upande. Pia walimuelekeza jinsi ya kuomba hela na chochote anachokitaka.
Waliagana kwa vilio wapendanao wa zamani na kabla hawajaondoka, walipitia anapoishi Beka kwa sasa. Alikua kanunua ghorofa tatu na magari kama uchafu. Pia alikua na kituo cha kulelea watoto yatima na watoto wenye vichwa vikubwa walifanyiwa operation bure kwenye hospitali yake kubwa.
Haiba alimpa mkono wa pongezi na kumsifia mke wa Beka wa sasa hivi kwa kuwajali watoto wa Beka. Waliaga na kurudi kwao ambapo waliishi kwa furaha. Walizidi kuwasiliana na Jane.
Waliamua kurudi tena Duniani kuhudhuria Harusi ya Jane na tajiri mkubwa afrika nzima. Jane alifurahi ugeni huo kutoka Sayari ya Mars wakiwa na mwanae na kuwashukuru. Maisha yaliendelea na walizidi kuja na kuondoka Duniani kama wageni wengine bila kudhuru watu.
Naamni mtakua mmepata elimu ndani ya burudani. Mi ni binaadamu. Sijakamilika.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
MWISHO
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)