THE STRANGER (9)

0

SEHEMU YA TISA
TULIPOISHIA...
Ilipofika saa kumi na moja, Haiba alirudi na kukutana na wageni.

“dada hawa ni marafiki zangu, tulivunjiwa wote pale kijiweni kwetu.” Aliongea na Haiba akawapa mikono.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
“huyu anaitwa Salumu na huyu mwengine anaitwa Fabi.” Aliendelea na utambulisha Bakari.

“basi waambie kesho waje waanze kazi, au ulikuwa unatakaje Beka?” aliongea Haiba baada ya kutambua ujio wa wale vijana pale.

Aliwapa elfu ishirini kila mmoja na kuwaruhusu waondoke.

Walifunga duka na kuondoka zao.

Haiba alirudi chumbani kwake na kwenda kuoga. Aliporudi alijilaza kitandani na usingizi ukachukua nafasi yake.

Baada ya kuzama sana usingizini. Alianza kuota yupo pamoja na Bakari. Mara wanaingia ndani na kuanza kupakatana. Mara akaanza kumuona Beka akivua shati na kumsogelea. Alipapaswa kila kona ya mwili wake. Joto lilipompanda, akajikuta anajibu mashambulizi kwa kuanza kumtomasa Beka. Vilio vya mahaba vilisikika kwa wote wawili. Baada ya hapo walianza kupata raha za dunia bila kujua nguo za chini zilichojokaje. Kwa ufundi wa Beka, ulimfanya Haiba aheme jujuu wakati wate.

“ooh gosh!!!”

Alishtuka Haiba na kujikuta amelowana. Alinyanyuka kitandani na kwenda kuoga. Alipokua anaoga, mawazo juu ya beka yalizidi kumuandama. Alimuwaza sana. Na kubwa zaidi kwa wakati ule ambao alikua na hamu kabisa ya kufanya mapenzi. Hakuwahi kujisikia hali hiyo alipokua kwao. Lakini toka alipokaribia kubakwa siku ya kwanza. Yule mtu japokua alimuua, lakini ndio aliyemjengea hisia nzito katika ubongo wake. Sasa alijisikia kabisa kushiriki hilo tendo. Ukijumlisha na ile ndoto ndio kabisa, aliouna utamu japokuwa haukua halisi.

Alitamani kwenda kwa Beka usiku ule ule. Lakini alianza kujihisi mkosaji baada ya kutupa macho yake kwenye dressing table na kuiona picha ya mke wa Beka.

“hii kazi nitaweza kuifanya kweli?” alijisemea na kuichukua ile picha.

“lakini huyu ni msaliti…anastahili adhabu,” aliongea na kuuendea mkoba wake na kutoa cheni.

Aligundua hela zimemuishia. Alifumba macho na kuongea maneno yasiyoeleweka na alipofumbua tu. Alikuta mabunda ya hela yamemzunguka.

“safi, bado kufanya kazi ya huyu dada.” Aliongea na kuunyanyua tena ule mkufu na kuuelekezea kwenye ile picha.

Ilikuja kitu kama Tv na kumuonyesha matukio ya nyuma kuanzia mapenzi yao mpaka mwanamke huyo alipoitoroka familia yake na kumfata huyo bosi mwenye hela.

Alipomuangalia kwa vizuri huyo bosi, aligundua kitu.

“kumbe mwanaume anayetembea naye ameshaathirika??....YES!!”

Alijikuta Haiba anashangilia baada ya kugundua ukweli kuwa hata mke wa Beka naye ameathirika na virusi vya ukimwi.

“ nipo huru na sina makosa nikimchukua Beka kwakua siwezi kumuacha afe kizembe.”

Aliongea na kuanza kuichana chana ile picha.

Usingizi haukua na nafasi kabisa kwa Haiba mpaka jua la asubuhi likapanda.. Alimpitia Beka kwa tax na kwenda naye kariakoo. Waliwakuta marafiki zake Beka wapo nje ya duka.

“safi sana, naona mmewahi?” aliongea Haiba baada ya salamu. Baada ya kufungua duka, aliwaachia duka wale vijana baada ya kuwapa maelekezo machache na wao wakaingia kwenye tax na kutoka tena.

Walienda hotelini na kumuachia Beka aagize anachohitaji kwa kua hakua amekunywa chai.

“samahani, naomba nikuulize kitu?” aliongea Beka wakati anapata kifungua kinywa.

“uliza tu.” Alijibu Haiba huku akimuangalia kwa umakini.

“huwa unakula nini?... maana sijawahi kukuona kula wala kunywa chochote.” Aliuliza Beka na kuendelea kunywa chai.

“huwa sipendi kula kula. Mi nikishakula mara moja tu kwa siku basi sili tena mpaka kesho yake.” Alijibu Haiba huku akiendelea kumuangalia Beka .

“duh?...ndio balance diet au?” aliuliza Beka kwa mshangao.

“basi tu, huwa sipendi kula.”

Alijibu Haiba na Beka akaridhika na majibu ya Haiba.

Kimya kikatawala kwa dakika kadhaa bila yeyote pale kunena kitu mpaka Beka alipomaliza kula.

“ hivi ukigundua kuwa mkeo nimeshindwa kumrudisha kwako utachukua hatua gani?” hatimaye Haiba alifungua mjadala uliomfanya Beka ataharuki kidogo. Hakulitegemea lile swali.

“ sitakulaumu, sana sana kwa sasa nakushukuru kwa kuyabadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa.” Alijibu Beka na kuonyesha kutojali.

“ nikikushauri uwe na mwanamke mwengine na umsahau kabisa mkeo. Utakubali?” aliongea Haiba na kumkazia macho kidogo Beka kuonyesha umakini wake na kutaka jibu kutoka moyoni.

“ yule ni mzazi mwenzangu tu, na kama yeye mwenyewe alinikimbia kwa kuwa nilikua na hali duni. Basi kavunja ahadi na viapo vya ndoa kwa kuishi maisha yote ya dhiki na faraja, shida na raha. Hata mimi simfikirii na nipo tayari kuoa msichana mwengine kama atakubali kuwalea watoto wangu.” Alijibu Beka na kumfanya Haiba avute pumzi ndefu kuashiria ameyakubali mawazo na mtazamo wa Beka.

“kuna kitu nimekigundua kutoka kwa mkeo, sio kitu kizuri na hafai kuwa wako tena” aliongea Haiba na kumuangalia Beka usoni ili asome riactions zake.

“vitu gani, na umemuona wapi?” aliuliza Beka kwa mshangao.

“mwanaume anayeishi na mkeo si anaitwa Philipo the don?” aliuliza Haiba ili kupata uhakika kutoka kwa Beka kama anamjua mume mwenzake.

“umejuaje?” aliendelea kushangaa Beka.

“ndio maana niliomba picha ili nimlinganishe huyo dada anayetembea na Mr. Philipo kama ni mke wako.” Aliongea Haiba kwa kujiamini.

‘ kipi kilichompata?” aliuliza Beka na kukaa vizuri kutaka kujua kitu kinachoendelea pale

“unajua kua Mr Philipo huwa ana tabia ya kubadili wasichana kama nguo, hivyo mkeo kaingia mkenge na hivi sasa anaishi na virusi vya ukimwi bila yeye mwenyewe kujua.” Aliongea Haiba na kumuacha Beka akiwa katika masikitiko makubwa.

“inaweza ikawa adhabu kutoka kwa mungu kwa kosa la kuisaliti ndoa yake.” aliongea Beka huku akonyesha wazi kuwa ile taarifa imemuhuzunisha kupita kiasi.

walirudi dukani na Haiba akarudi kwake. Ilimchukua dakika kadhaa beak kuamini maneno ya Haiba. Pia alitafakari ukaribu wake na yule dada ni nini, hata hilo swali halikuwa na majibu lililomridhisha. Akaamua kuacha ili ajue hatima yake.

“dada muda wako wa kukaa hotelini umeisha toka saa nne asubuhi.” ilikua kauli ya mtu aliyekua Reseption baada ya kumuita Haiba.

“ oh gosh!!siku tano tayari??” aliuliza Haiba kwa mshangao.

“tayari dada.” alijibu na kumtajia siku aliyoingia mpaka muda ule

Haiba alifungua pochi yake na kutoa noti nyingi na kumkabidhi. Aliingia chumbani kwake na kukaa. Hapo mawazo juu ya kazi ya mfalme yakamjia. Aliwaza juu ya muda alioupoteza kwa ajili ya Beka. Alijilaumu kidogo na kuchukua mkufu wake na kuanza kumtafuta Sam alipo. Aligundua alipo na hapakuwa mbali na pale. Alicheka na kuchukua kibegi chake na kutoka tena.

****************************

akiwa chumbani kwake Sam huku mawazo juu ya Jane yakichukua sehemu kubwa ya akili yake. Wakati akiwaza na kuwazua ni nini afanye ili amponyeshe mpenzi wake, alisikia mtu akibisha hodi katika mlango wake. Alishtuka kidogo kwa kua hakua na rafiki wala ndugu aliyekua anapajua pale alipopanga.

alinyanyuka kivivu na kwenda kufungua mlango kwa umakini mkubwa.

Hamadi! alikutana na msichana mwenye sura nzuri sana. Alikua kavaa nguo nyekundu ya moja kwa moja, masikioni akiwa ametoga na dhahabu zikiupamba mwili wake kila sehemu.

Sam mwenyewe alibaki amepigwa na bumbuwazi baada ya kukiona kile kifaa. Alimkaribisha ndani na kumsikiliza shida yake.

“naweza kukaa kitandani kwako?” aliuliza yule dada baada ya kuona kile chumba kikiwa na kitanda na godoro peke yake. chini kukiwa na tires na juu feni ndio lilikua linaleta upepo mule ndani. Harufu nzuri ya asili ya mwili wa Sam ndio kilikua kivutio kingine mule ndani.

“kaa tu usijali!” aliongea Sam huku akiendelea kuutathmini mwili wa mgeni wake huyo ambaye hajawahi hata kumuona. Tabasamu la mgeni lilizidi kujaza maswali kichani kwa Sam bila kujua yule mgeni alikua anamfahamu au la.

“bila shaka wewe ndio Sam?” aliuliza yule mgeni na kumfanya Sam kutumbua macho kwa mshangao. Alimuangalia yule mgeni na kuvuta picha labda ni wapi alishawahi kumouona yule msichana lakini jibu la haraka lilikosekana.

“vipi?......umeshanisahau kwani?” yule mgeni alizidi kuumiza akili ya Sam. alipomuangalia yule msichana bado kumbukumbu zake ziligoma kabisa kurudi nyuma. Ziliishia tu pale mpenzi wake alipokua kichaa.

Hakika Jane alimuathiri Sam kwa kiasi kikubwa. Mpka uwezo wake wa kufikiri pia uliathirika.

“naitwa Candy…. Mara ya mwisho tulikutana club tukacheza pamoja na baadae kukatokea vurumai na kiumbe cha ajabu kikatokea……..hukumbuki?” aliuliza yule dada na kumfanya Sam atabasamu baada picha ya yule dada kujichora tena ubongoni.

“mambo mengi……….umepajuaje hapa?” aliuliza Sam

“mi nakaa nyumba ya pili kutoka hapa. Leo nimekuona ukiingia ndio maana nimekuja coz nimekumiss sana” aliongea yule dada na kuanza kujichekesha chekesha.

“ karibu” aliongea Sam na kumuangalia yule dada

“nishakaribia, nilijua nitamkuta wifi?” aliuliza yule dada baada ya kugundua kuwa hakukua na dalili zozote za kuishi mwananmke pale. Kutokana na vitu muhimu kama juko na ndoo za maji. Hakukua na hata kijiko wala nguo yoyote ya kike mle ndani.

“naishi peke yangu humu.” alijibu Sam na kumuangalia yule dada aliyekuwa bize kukikagua kile chumba.

“jamani kwanini huishi na mwanamke??” aliendelea kudadisi yule dada.

“ni maamuzi ya mtu tu kwani kuna ulazima wa mtu kuishi na mwanamke?” aliuliza Sam na kuonyesha wazi kuchoka na maswali ya yule dada.

“sio lazima ila nilitaka kujua kama una mwenyewe au upo single” aliongea yule dada huku aking`ata vidole vyake kimahaba.

Ile harufu ya manukato ya ajabu ndio iliendelea kummaliza yule dada. Alijihisi anakunywa kilevi Fulani aina ya Amarula kinachomfanya ajisikie hamu ya tendo. Wakati mwengine mpaka sauti ya yule dada ilianza kubadilika.

“sijakwambia kuwa nipo single, ila sikai na mwanamke kwa sababu hayupo karibu na mimi kwa wakati huu” alijibu na kumkata maini yule dada aliyeonekana anataka kujiletaleta kwa Sam.

Sam alimuangalia na kunyanyuka na kuuendea mlango

“nahitaji kupumzika dada tutaonana baadae.” aliongea Sam na yule dada akatii amri na kuondoka zake.

Usiku wa siku ile yule dada alitoroka kwao na kwenda kwa Sam na kumgongea mlango.

Sam alifungua na yule dada akaingia ndani na kufunga mlango.

“sipati usingizi kwa ajili yakoSam, naomba uniokoe kwenye hili gharika la mahaba lililonikumba mwenzio kwa kulala na mimi japo usiku mmoja wa leo tu” aliomba yule dada na kumvaa Sam aliyekuwa kifua wazi huku akiwa na boxer peke yake.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)