Mtunzi: Hussein O. Molito
SEHEMU YA NANE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“pole binti. Tumejaribu kwa uwezo wetu wote, lakini hatukufanikiwa kuokoa maisha ya mama yako…tayari ameshafariki.” Aliongea daktari huku akijaribu kumpooza Jane.
“mamaa, mama yangu mie” alilia Jane kwa sauti kubwa. Daktari alijitahidi kumtuliza Jane lakini wapi. Lilikuwa swala gumu kuliamini na kulipokea kwa Jane.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Maana tayari alishamzika baba yake miaka miwili iliyopita na hakuwa na ndugu hapa Dar. Mama yake ndio alikua kila kitu katika maisha yake.
Alilia na kujitupa kila sehemu. Madaktari walikua na kazi kubwa ya kumtuliza Jane kwa muda mrefu na kufanikiwa baadae sana.
*************************
Asubuhi ya siku ya pili, Haiba alienda kumtembelea Bakari nyumbani kwake akiwa na gari ndogo ya mizigo ya kukodi. Ndani yake kulikua na sofa la watu wawili, kabati, flat screen tv nchi 32 na kabati liliogawanyika mara mbili. Upande wa nguo na vyombo. Pia kilikua na nafasi kubwa katikati ya kuweka Tv.
Music systerm na deki havikukosekana. Bakari alishauriwa kubadilisha vitu vya zamani na kuviweka vitu vipya.
“ukiwa hivi…naamini mwanamke wako hatakataa kurudiana na wewe.” Aliongea Haiba baada ya kukaa na kuangalia tv kwa pamoja.
“nashindwa kuamini mpaka sasa, yaani sijui nikushukuru vipi dada yangu…maana si dhani kama kuna mtu mwingine duniani anaweza kufanya yote haya bila kuwa na undugu wa karibu.” Aliongea Bakari huku akimuangalia Haiba kwa uso wenye bashasha huku akitabasamu.
“usijali,..ni mabo ya kawaida tu.” Alijibu Haiba na kucheka.
“watoto wangu hawataenda tena kuangalia tv kwa jirani.” Aliongeza bakari na wote wakacheka.
“bado wewe baba mtu nikupeleke shooping utoke kivingine.” Aliongea Haiba na kumuangalia Bakari aliyejawa na furaha wakati wote.
Baada ya maongezi machache, Haiba na Bakari walinyanyuka na kuondoka pamoja.
“shoga kweli mungu hamtupi mja wake nakwambia!” aliongea dada mmoja aliyewashuhudia Bakari na Haiba wakiongozana na kupanda tax pamoja.
“kwanini shoga?” aliongea yule dada aliyefikishiwa zile habari na kuachilia kufua na kuanza kumsikiliza kwa makini yule dada.
“umekiona kitu cha Beka alichonacho sasa hivi?” aliongea na kukalia ndoo iliyokuwa karibu.
“nipe huo ubuyu shoga..yukoje?” aliongea na kumuangalia kwa uchu wa kutaka kujua uzuri wa huyo msichana.
“sijapata kuona toka nazaliwa..si unanijua shoga yako kwa kunanga… kwa yule nimekosa kasoro wangu.” Aliongea na kuonyesha ishara na kunyanyuka.
“yaani si mnene si mwembamba, ana hipsi kama kaficha panya dada, makalio madogo tu lakini yalivyotokeza. Mtoto mweupee mzungu si mzungu yaani shoga. Unywele unagusa makalio, shoga. Kuna watu wameumbwa wakaumbika.” Aliongea na mwenzake akavuta taswira na kuwa na hamu ya kumuona.
“akija tena niite wangu” aliongea yule dada.
“usijali mama, nimekuja maramoja kukupa huo umbea. Naenda kupika shoga,” aliongea na kuondoka zake.
Safari yao iliishia katika duka kubwa la nguo maeneo ya sinza. Walichagua nguo kadhaa kisha wakaingia salon iliyokuwa karibu na pale. Bakari alinyolewa na kuwekwa duke kishwani na super black kwa mbaali. Alikarabatiwa uso kwa scub na mask.
Baada ya hapo alitoka bakari mwingine kabisa tofauti na bakari wa jana aliyekuwa analialia kule kariakoo.
Alipendeza na kuonekana Handsome wa kupendwa na kila dada anayependa wavulana wazuri. Hakika shida huondoa thamani ya mtu mbele za watu.
“umependeza sana.” Alisifia Haiba baada ya kumuangalia Bakari.
“nakushukuru sana kwa kunipendezesha.” Alijibu Beka na kutabasamu.
Safari haikuishia hapo, walielekea hotelini ambayo ilikua karibu na bahari. Wakaa na kuanza kupiga story.
“unajua kuogelea?” hatimaye aliuliza Hiaba baada ya maongezi ya kawaida.
“najua!” aliitikia Beka .
“twende tukaogelee basi, napenda sana kuogelea.” Aliongea Haiba huku akitabasamu na kumuangalia beka kwa macho malegevu kama amekula wida.
“hamna shida” alijibu Beka na wote wakanyanyuka na kwenda kwenye swimming pool ambalo lilikua na watu wachache na kuogelea.
Haiba akiwa kwenye sidiria na Beka kwenye boxer peke yake. Walikutana na kugusana miili sehemu kubwa ikiwa wazi.
“oooosh”
Ulimtoka mguno matata kutoka kwa Haiba baada ya Beka kumgusa maeneo ya kiuno kilichozungukwa na cheni ya dhahabu.
“naomba tuondoke, maana muda umeenda sana.” Aliomba Haiba baada ya kuogelea kwa muda wa dakika ishirini hivi.
Beka alirudishwa kwake na Haiba akarudi hotelini kwake
*********************************
Sam aliporudiwa na hali yake ya kawaida. Alianza kulia na kujilaumu mwenyewe kwa kushindwa kuzizuia hisia zake baada ya kuona damu ya mama mkwe wake.
Aliamua kwenda hospitali alipoenda Jane kumpeleka mama yake baada ya kufumba macho na kuendeleza kilichotokea baada ya yeye kutoweka.
“samahani , namuulizia mama yangu anaitwa Suzana Jackson.” Aliongea Sam baada ya
Kufika kwenye mapokezi ya ile hospitali.
“pole sana kaka, mama yako amefariki masaa mawili yaliyopita.” Aliongea dada mmoja aliyekuwa kwenye ile mapokezi baada ya kuangalia Jina kwenye computer maalumu.
“duh.. sasa ndugu zangu wengine waliokuja huku wapo kwenye chumba cha maiti?” aliuliza Sam lengo lake kujua Jane yupo wapi.
“ kuna mdogo wako peke yake alikua analia sana . yupo chumba cha mapumziko namba 29” alijibu yule dada na kumuelekeza Sam hicho chumba.
Alipofika, alimkuta Jane akiwa macho huku akiwa mwekundu na macho yamevimba kutokana na kilio cha muda mrefu.
Jane alipomuona tu Sam alianza kucheka kwa sauti kubwa mpaka Sam mwenyewe akashangaa. Aliendelea kucheka na kushuka kitandani. Alimsogelea Sam na kumtekenya kisha akakimbia na kujificha chini ya kitanda uvunguni. Alianza kulia na kuongea maneno yasiyoeleweka. Alitoka kitandani na kuanza kucheka tena. Daktari alikuja mbio na kumchoma Jane sindano ya usingizi.
“imekuwaje dokta??” aliuliza Sam baada ya daktari kumuomba amuache na amfuate yeye ofisini kwake.
“ amechanganyikiwa baada ya taarifa za kifo cha mama yake.” Alitoa majibu hayo daktari huku akimuangalia Sam kwa jicho la huzuni.
“ tufanye nini daktari ili arudi katika hali yake ya kawaida?” aliuliza Sam huku akionyesha wazi kuchanganyikiwa.
“kuna uwezekano mkubwa asipone kabisa kwa jinsi vipimo vinavyoonyesha.”
Alijibu daktari na kumfanya Sam kuishiwa nguvu na kukaa chini.
Majibu yale yalimfanya apagawe na kuondoka pale hospitalini. Alijua kuwa uwezekeno wa kuwa na Jane kimapenzi ni mdogo sana.
Alijua kuwa kutokuwa karibu na Jane ndio mwanzo wa kutafuta damu yeye mwenyewe. Hivyo kumfanya aishi maisha ya kutanga tanga. Mawazo yalimsonga Sam na hakujua afanye nini.
Siku ya pili yake akaenda tena hospitalini kumuangalia mpenzi wake. Alikuta amehamishiwa katika ward ya vichaa.
Alienda na kumuangalia. Jane alikua anamshangaa tu, muda mwingine anamuogopa na wakati mwingine anacheka na hapo hapo anaanza kulia kitoto.
Yalikuwa maumivu mazito kwa Sam kila akimuona mpenzi wake akiwa katika hali ile.
Aliondoka na kurudi kule kwenye hotel na kuchukua card ya benk.
Alidroo hela ambazo zilimuwezesha kupanga chumba na kununua vitu vya ndani.
Alinunua kitanda na godoro lake. Kwake vilikua vitu vya muhimu sana. Maana alikua hapiki kutokana na chakula chake anachokula.
Hapo alijaribu kuanza maisha peke yake bila kujua hatima ya maisha ya kujitafutia mwenyewe.
*************************************************
Haiba akiwa chumbani kwake alikaa na kumuwaza sana Bakari na alijikuta amekuwa mwepesi sana kumsaidia. Hata ule usiku tu ulikuwa mrefu sana kwake na alitamani kukuche ili aende kuonana na Beka na familia yake.
Asubuhi alifunga safari na kwenda tena kwa Bakari.
“leo nimekuja mara moja tu, nataka kukupeleka kwenye duka utakalolitumia kuendesha maisha yako.” Aliongea Haiba baada ya kukaa kawa muda wa nusu saa.
“ poa, ngoja nikajiandae”.
Aliongea Bakari na kungia ndani. Hakuchukua muda mrefu alitoka akiwa amependeza sana. Zilikua ni moja kati ya nguo nyingi alizonunuliwa jana yake na Haiba.
“ safi” aliongea Haiba na kumuonyeshea dole gumba.
Walitoka na kuingia ndani ya Tax aliyokuja nayo Haiba.
“ndiye yule pale shoga umemuonaje?” aliuliza yule dada wa jana baada ya kumfata shoga yake na kumuonyesha.
“dah!..kwanza unamuona Beka anavyo shine dada… mama Hassani kaacha mbachao kwa msala upitao.” Aliongea yule dada mwingine na kuendelea kuwaangalia mpaka walipopotea katika upeo wa macho yao.
Walifika maeneo ya kariakoo na Haiba akamuonyesha Frem iliyokuwa imefungwa na kumwambia kuwa lile ndio duka lake.
“kuna kila kitu ndani, unaweza kuanza kazi siku yoyote.” Aliongea Haiba na kumkabidhi funguo Bakari.
“waooooooooooooooooooh”
ulikuwa mshangao mkubwa baada ya kuona duka likiwa limejaa makabati ya thamani na ndani yake kukiwa na simu aina mbalimbali. Rangi na taa za ajabu ambazo hajawahi kuziona toka siku anayozaliwa, ziliku kivutio kikubwa. Alikuta bidhaa nyingine zikiwa kwenye kichumba kidogo alichotambulishwa kama Store.
Alishindwa kuizuia furaha yake na kumkumbatia Haiba huku analia kwa furaha.
“ooooooooosh”
ulikuwa mguno mkubwa uliosikika kutoka kwa Haba. Alikua mgonjwa kila akiguswa na Bakari. Mpaka yeye mwenyewe alijishangaa na hakujua kuna nini katika mikono ya Bakari. Alijisikia raha kila akiguswa na kujihisi yupo katika wakati wa tendo.
“usijali…. Lini utaanza?” aliuliza Haiba na kumtoa mikono Bakari haraka baada ya kumuona anampa ashki kila akimpapasa.
“ leo hii hii” alijibu Beka na wote wakacheka
“basi mi naenda, nitakupitia jioni” aliiongea Haiba na kumuacha Bakari dukani.
Aliendelea kulikagua lile duka jipya kabisa. Bakari alifikicha macho yake labda aliku anaota. Lakini haikuwa ndoto. Zaidi alikuta amerahisishiwa kazi. Kila bidhaa ilikua imebandikwa bei yake.
Alitafakari jinsi ya kutafuta wasaidizi. Aliwakumbuka marafiki zake waliokuwa wamevunjiwa vibanda vyao na kuwapigia simu.
“ kaka, umejiunga na free mason nini??” aliuliza mmoja kati ya marafiki zake kwa mshangao baada ya kuliona duka la Beka.
“ hamna kaka, ni story ndefu. Achanane na hayo, nimewaita tufanye kazi washikaji…au mmeshapata vitengo??” aliongea Beka.
“tumepata wapi, tulikua tunachakaa tu kitaa.” Alijibu yule mwengine aliyekua kimya muda mrefu.
“ basi msijali, tutapiga kazi pamoja. Ngojeni bosi mkuu aje niongee nae kuhusu mishahara yenu.” Aliongea Bakari na kuwaangalia marafiki zake kwa zamu. Walionekana kufurahi na kumpa tano rafiki yao.
Ilipofika saa kumi na moja, Haiba alirudi na kukutana na wageni.
“dada hawa ni marafiki zangu, tulivunjiwa wote pale kijiweni kwetu.” Aliongea na Haiba akawapa mikono.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)