Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA KUMI NA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Wakufunzi walikuwa wanateta kuwa Sam atakuwa ni Sniper mzuri kuliko ilivyozoeleka, ma sniper kama hawa ni muhimu sana wakati wa mapambano kwani wanapunguza idadi ya Risasi za kutumia huku kila risasi kwao ikiwa imetimiza lengo.
Hawa ndio ambao wakiasi wanatumika kufanya uhalifu wa kuua kwa kulipwa kwani akijitega sehemu na kumlenga mhusika hamkosi.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Ni rahisi kama akiwa jambazi kuua askari wengi kwani akijificha sehemu na kuminya jicho lake atakapoachia risasi inadondoka na askari mmoja.
Walengaji kama Sam ndio walioweza kumuua aliyekuwa Rais wa Marekani John F Kenedy! Sam alivuta Hisia za wakufunzi wengi sana hadi kufikia wakati akawa burudani kwa maaskari wenzake.
………………………………….
Siku zilikuwa zinakimbia sana ambapo wakati huu Mafunzo yalikuwa yanaenda ukingoni, Sam alikuwa amepewa doria katikati ya mji wa Moshi akilinda mazingira ya Mji yasichafuliwe,
JUkumu lao kubwa ilikuwa ni kuwakamata watu wote ambao wanatupa takataka hovyo na kuwapeleka kwenye ofisi za Halmashauri na kutozwa faini ama kupelekwa mahakamani na kusomewa mashtaka.
Akiwa kwenye eneo la kazi yake alimuona Mama mmoja akiwa anakula mahindi ya kuchoma huku anatembea Barabarani.
Alimfwata Nyumanyuma kwa umbali mrefu akivizia adondoshe gunzi barabarani amkanate, ari ya kufanya kazi ilikuwa juu sana kwahiyo wakati mwingine alikuwa anatafuta makosa, aliendelea kumfwata Yule mama kwa umbali mrefu kutokea stendi akashuka nae mpaka wakafika CRDB wakaenda mpaka wanafika karibu na YMCA Yule mama akaangalia huku na kule akadondosha lile gunzi chini.
Kama mshale Sam alimuendea na kumshika mkono kwa nyuma….
“Uko chini ya urinzi wewe mama, unachafua mji makusudi arafu unajifanya mpore eeeh” Sam nae alikuwa ameiga lafudhi ya kikurya utadhani ndio lugha ya Jeshini.
Mama Yule alishtuka sana kwani hakujua kwamba alikuwa anaonekana, maaskari waliokuwa wamefuatana na Sam walimsaidia kumkamata Yule mama huku wakimlazimisha waende ofisini.
Sam alipigwa na ganzi asijue cha kusema baada ya Yule Mama kugeuka na kuonyesha sura yake ambayo ilimshtua sana Sam.
“Mamaaaaaaa!”
“Haaaaaa, Sam!”
“Mama unafanya nini huku?”
“Acha tu mwanangu, niko hapa huu ni mwezi wa tatu”
Sam alikuwa tayari machozi yanamwagika usoni kwake kwa kitendo cha kumuona mama yake tena katika mazingira yale huku hali ya MAMA yake ikiwa haimridhishi kabisa.
Ukakamavu wote wa Kiaskari ulikuwa umemuishia, alikuwa amepigwa ganzi na tayari miiko ya kiaskari ilikuwa imeshamshinda kwani katika zoezi la uhalifu huwa hakuna cha undugu.
Sam alishindwa kabisa na kujikuta akimkumbatia mama yake huku wote wakiwa wanalia.
“Mama twende huku”
Wenzake walikuwa wamemwangalia tu na mwishowe wakaamua kuondoka kuendelea na mambo mengine huku Sam na mama yake wakiondoka na kutafuta sehemu ya kukaa.
Walienda hadi kwenye baa moja wakakaa huku Sam akiagiza soda za baridi na kuanza kunywa,
“Mama mbona afya yako imezorota hivyo”
‘Naumwa Sam’
“Nini mama?”
“Nina TB”
“Nimelazwa hapa KCMC kwa mwezi mzima ndio saivi naanza kutembea mtaani”
“Dah pole mama, nilikuwa nawakumbuka sana lakini sikuwa na namna ya kuwapata hata kwenye simu”
“Usijali mwanangu…nimefurahi sana kukuona, Nilitamani sana nikuone kabla sijafa”
“Mama kwanini unasema hivyo…”
“Nina HIV Sam, siku zangu za kuishi sio nyingi, nimeamiwa CD4 zangu zimeshuka sana sifai hata kutumia ARV”
“Mama usiseme hivyo, nahangaika kwenye maisha kwa ajili nije nikutunze, sitaki ufe”
“Sitaki nife Sam, lakini nafurahi kukuona ukiwa hapo maana najua utaendesha maisha yako bila kuteseka, nitakifurahia kifo changu”
Machozi yalikuwa Mengi sana kwenye mashavu ya Sam, alikuwa anaemia moyoni mwake kama anachomwa na moto kwenye kidonda.
Maneno ya mama yake yalikuwa ni zaidi ya mkuki moyoni, hali ya afya ya mama yake ilikuwa ni majonzi matupu.
Alitaka amuone mama yake akiwa mzima na mwenye furaha ili amhudumie baada ya kuajiriwa kama askari.
“Sam mwanangu nisikilize kwa umakini………”
“Mpumbavu mkubwa….hiki ndicho ulikuja kufanya hapa, badala ya kufanya kazi unakaa na malaya huyu hapa baa, eenh Malaya mwenyewe kachoka hivi huoopi magonjwa….twendeeee ukajibu huko chuoni”
Sam alikuwa mikononi mwa maaskari wawili wenye mbavu nene wakiwa wamemkamata kwa kitendo cha kukiuka miiko ya kazi…hakuna kipindi kilikuwa kigumu kwa maaskari kama kipindi hiki cha mafunzoni, suala la nidhamu lilikuwa linazingatiwa sana. Ufwatiliaji wa siri ulikuwa mkubwa sana kiasi kuwa kila askari alikuwa anachunguzwa kwa kiwango cha juu mno!
Sam hakukubali kuachanishwa na mama yake tena kwa matusi ya kiwango kile, aliamua kupambana potelea mbali hata kama atafukuzwa chuo lakini mama yake ndio ilikuwa furaha yake!
“Niacheni nimesema niacheniiiiiiiiiiiiiii”
Purukushani ilikuwa kali mno kiasi kwamba ngumi zilianza kutembea, pamoja na kuwa wale maaskari walikuwa wawili tena walioshiba kikamilifu lakini hawakuweza kumkamata Sam.
Walikuwa wamepigwa ngumi na mateke mfululizo wakajikuta wote wakiwa chini na Sam yuko na mama yake amemshikilia waondoke.
“Sam nenda, nenda usije ukapoteza kazi uliyopigania kwa mda mrefu, nenda kamalizie mafunzo Mungu akipenda utanikuta”
“Mama kwani unaenda wapi saivi”
“Sam nimekwambia nendaaaa”
Mama Sam hakutaka kusema anakoenda kwani alijua atamliza Mwanae zaidi kwani hakuwa na pakwenda wala nauli ya kurudi nyumbani na siku zote baada ya kutoka hospitali alikuwa analala kwenye maeneo hatarishi.
Sam alitia mkono mfukoni akatoa kiasi cha fedha zote alizokuwa nazo kutokana na mishemishe za siku nzima hapo maeneo ya mjini na kumpa mama yake, ilikuwa ni zaidi ya Laki na nusu.
Alivyomaliza tu kotoa hela alijikuta akivalishwa pingu mkononi kisha kama kuku akakamatwa na kupakiwa kwenye gari ya Chuo cha Polisi.
……………………………..
“Sasa wewe utakuwa mfano”
“Nisamehe Afande”
“Nikusamehe mimi ni Basha wako?”
“Nisamehe nilishindwa kujizuia”
“Ukiendelea kuongea nakutia dole la mkund…”
Sam alikuwa anapewa mateso makali kiasi kwamba alikumbuka siku alipokuwa anateswa na akina Afande Miraji.
Alikuwa amechakaa kwa kipigo huku akifanyishwa mazoezi makali kama pushap, kuruka kichura, kubiringishwa uwanja wa kokoto na kuminywa kwenye maji.
Kwa siku tatu mfululizo Sam alikuwa amechoka kupita maelezo, wakati wote huu kesi yake ilikuwa inasikilizwa huku uwezekano wa kufukuzwa chuo ukiwa nje nje!
…………………………..
“Mama mbona kuna wageni wengi sana leo hapa nyumbani”
“Verity anatolewa Posa”
“Haaaa anaolewa?”
“Mwenzangu acha tu, ni vituko!”
“Vituko gani?”
“Hataki kuolewa na huyo mwanaume”
“Sasa kwanini?”
“Hataki kusema lakini nahisi ana Mimba!”
“Mimbaaaaaa?”
Verity alikuwa amekaa chumbani peke yake akitafakari maisha yakemjinsi yanavyoenda.
Alikuwa amemaliza chuo ambacho alikuwa anachukua Diploma ya Uhasibu, kila kitu kilikuwa kimeenda Vizuri isipokuwa tu moyoni mwake alikuwa na Donge moja.
Donge hili lilikuwa ni Donge la Mapenzi, tayari alikuwa Mapenzini na wanaume zaidi ya mmoja lakini moyo wake ulikuwa umedondokea sehemu moja, hii ni kama ile Riwaya ya “Three Suitors One Husband”.
Verity alikuwa amedondokea Kwa Kijana Sam ambaye hivi sasa yuko chuo cha usakari polisi cha CCP Moshi.
Wakati mapezni yakiwa yanautesa moyo wake jambo jipya linaibuka kwa kasi, jambo hilo ni la Mmoja wa wapenzi wake ambaye ni askari wa JW aking’ang’ana sana kuwa anataka atoe posa ili amuoe Verity moja kwa Moja.
Kijana huyu ambaye ana cheo cha Meja wa Jeshi huku tayari akiwa ana nyota tatu begani alikuwa kwenye Mapenzi mazito sana na Verity.
Siku ya kwanza alipomuona kwenye graduation ya chuo cha IFM branch ya Mbeya ambapo alienda kumsindikiza dada yake ambaye nae alikuwa anahitimu alichanganyikiwa kabisa.
Aina ya Mwanamke kama Verity ndio aina ya wanawake ambao walikuwa wanazikonga nyoyo za Meja Emmanuel Mwambashi.
Hakuweza kuvumilia bila kutafuta namna ambayo anaweza akamuweka Verity kwenye Himaya yake, kwa kumtumia dada yake aliweza kuyapata mawasiliano ya Verity na kufanikiwa kuzungumza nae maneno machache kwa siku hiyo huku wakipeana ahadi ya kuonana siku za mbeleni.
Mawasiliano kati ya Verity na Meja Emma yalikua siku hadi siku na hatimaye wakaonana kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Hoteli ya HighLands view iliyoko Tukuyu.
Emma aliingia na gari yake aina ya Subaru aliyozawadiwa na Baba yake baada ya kupata cheo cha Umeja, gari hii ilikuwa nzuri na Mpya ambayo kila ikipita mjini watu walikuwa wanaitolea macho.
Siku hii ilikuwa ni siku ya kiubaridi lakini verity alikuwa amevaa gauni fupi lililoishia mapajani huku akiwa amevaa Sendoz nyepesi miguuni.
Rangi yake ya kung’aa ukijumlisha na gauni hili Jeusi pamoja na Umbo lake matata ambalo sio nene wala Jembamba ila likiwa limejipanga vyema kabisa vilimfanya avutie kiasi cha kila mwanaume kumtolea macho ndani ya eneo hili.
Hata wazungu waliokuwepo maeneo haya waliweza kumfananisha Verity na Mrembo Paris Hilton waliyemzoea kule Marekani.
Meja EMMA baada ya kumuona mgeni wake alinyanyuka na kumfwata kwa bashasha kubwa kisha akamkumbatia ishara ya salamu nzito kisha akamshika mkono na kumuelekeza sehemu ya kukaa.
Watu wote ndani ya eneo lile walikuwa wanamkodolea macho Meja Emma kwa wivu baada ya kuona mrembo Verity kaishia kwenye mikono yake.
…………………………………………
Waliongea mengi sana siku hii lakini mengi yalikuwa yanahusu maisha yao na Mapenzi yao kwa ujumla.
Emma alisisitiza sana jinsi ambavyo alikuwa anampenda Verity na alitamani sana awe nae maishani, Verity alikubaliana nae lakini alitoa kigezo cha mda kuwa wapeane muda wa kutosha.
Sio kwamba Verity alikuwa hamtaki Emma, la hasha! Moyo wake ulikuwa umefunikwa na Sam, wakati wote alikuwa anamuwaza Sam na ndio maana hakuweza kuwa deep kwenye mapenzi na mwanaume yoyote kwa kuwa moyo wake tayari ulikuwa REHANI kwa Sam.
Tayari savannah nne zilikuwa zimepita kwenye koo la Verity huku Meja EMMA akiwa tayari amebwia Heinkein sita, hapa walikuwa wanakula kuku wa kuchoma na ndizi za kukaanga.
Kuku mzima alikuwa amejaa kwenye sinia huku wakijiachia kwa kunyofoa minofu na kufurahia burudani ya vinywaji vyao.
Masaa yalisogea na tayri ilikuwa ni saa mbili usiku, Verity alikuwa amechangamka hali kadhalika Meja Emma.
Walikuwa wameshaanza kusogeleana tofauti na mwanzo, kila ambapo Emma alikuwa anajaribu kuyashika mapaja mazuri meupe ya Verity mkono wake ulikuwa unasita kwani alikuwa anahofia kumkosa Verity kwa kuonekana mwanamme mpenda Ngono na asiye na Subira.
Wakati yeye akiwaza hayo Verity yeye alikuwa ameshamgusa mara kadhaa Emma Kifuani, mapajani na hata kumlalia.
Laity kama EMMA angelijua asingekuwa na hofu aliyo nayo, wakati wote Verity anapokuwa amekunywa Savanna hisia zake kimapenzi zinakuwa juu sana na kama angemgusa tu basi angepewa kila kitu.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)