Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
“Naomba tuongee yale mambo ili niwahi kurudi nyumbani”
“Sawa Glory”
Dr Kanji alikata funda mbili za mvinyo glasi ikawa nyeupe akamimina nyingine na kunywa kidogo kisha akawa anamtazama glory kwa macho ya upole yenye hisia kali.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Dr Kanji kwa sauti ya upole iliyojaa utulivu alianza kwa kumsimulia Glory historia ya maisha yake tangu anazaliwa hadi pale alipofikia.
Ilikuwa ni historia nzito inayovutia sana ambayo ilimfanya Glory amsikilize kwa hisia kali sana, akili ya Glory haikuwaza tena kuhusu kuondoka kwani hisia zake zilitekwa na kile alichokuwa anakisikia kutoka kwa Dr Kanji.
Katika umri wa miaka 34 aliyokuwa nayo Dr Kanji tayari alikuwa na PHD huku akimiliki kampuni yake ya uagizaji wa Bidhaa za magari kutoka Ng’ambo.
Kikubwa kilichomteka Glory ni historia nzima ya dr Kanji tangu utoto, alivyonusurika kwenye ndege iliyoua Watu wote na kubaki yeye peke yake huku zaidi ya watu mia tatu na sitini wakiteketea wote.
Alimsimulia kuwa ndani ya ndege alikuwepo mtoto mwenzie ambaye mama yake alimtaka amuoe lakini nae alikufa kwenye hiyo ndege.
Aliendelea kusimulia kuwa kutokana na hali hiyo alijikuta akikosa hamu ya kuwa na mwanamke mwingine na alijiapia kuwa hatakuwa na mwanamke yeyote maishani mwake isipokuwa tangu alipoanza kazi pale chuoni na kumuona Glory alijikuta akipingana na adhma yake ya siku zote.
“Kwanini sasa ukatae msimamo wako wa siku zote”
“Glory unafanana sana na Yule msichana, japo alikuwa bado ni mtoto lakini kila nikikuangalia natamani hata kulia, nimekuwa nikipingana na hizo hisia huu ni mwaka wa pili sasa lakini nimeshindwa.”
“Mhhh” glory alivuta pumzi!
Hapo hapo Dr Kanji alitoa waleti yake na kumuonyesha Glory picha ndogo ya msichana mrembo kisha akamwambia.
“Ndio huyo hapo enzi hizo tukiwa tunaelekea kupanda ndege”
Baada ya Glory kuangalia ile picha yeye mwenyewe alibaki mdomo wazi maana msichana anayeonekana kwenye ile picha anafanana nae kopi, alizikumbuka nayeye picha zake za utoto jinsi ambavyo akiwa mtoto alikuwa anafanana kabisa na Yule aliyeonyeshwa kwenye ile picha.
Taratibuu Glory aliinua macho yake na kumtazama Dr Kanji ambaye alikuwa analengwa na machozi kisha akaishia kuvuta pumzi ndefu na kurudisha tena macho yake kwenye ile picha.
“Glory kila ninapokuona nahisi roho ya Yule msichana imefufuka, nahisi mama yangu angekuwa hai angesema neno alilolisema wakati ule”
“Dr nadhani ni hisia tu”
“Ni kweli Glory, sikupingi kwani hata mimi nilidhani ni hisia tu ambazo hata hivyo niimejitahidi kuzipinga kwa mwaka wa pili sasa lakini nimeshindwa, Glory kila ninachokifanya na kukiwaza najawa na hisia nyingi sana kuhusu wewe!”
“Hisia gani Dr?”
“Nataka kujua kitu kimoja kutoka kwako Glory”
“Kitu gani Dr?”
“Hisia hizo ni kwamba wewe hujawahi kuwa na mwanaume yeyote maishani mwako yaani wewe ni Bikra, kama sio Bikra basi hisia zangu zimenidanganya na kila ninachokiota kuhusu wewe basi nimekosea na nitasema ninayemuota sio wewe, ila kama wewe ni Bikra, hujawahi kuwa na mwanaume basi hisia hizi ni zako, ndoto na maono ninayoyapata nasi ni ya kwako ”
“Heee Dr ndio nini tena?”
“Please Glory kama ni wewe sema leo na kama sio wewe pia sema nijue”
…………………………………..
Sherehe kubwa ilikuwa imeandaliwa Nyumbani kwa RPC Mndeme ambaye alikuwa anastaafu huku Sam nae akiwa ametoka kuapishwa kwa ajili ya kuwa RPC mpya wa mkoa wa Tabora.
Lakini Pia sherehe hii ilihusu shukrani ya kumpata mtoto NICE baada ya kupotea kwa siku nyingi. Watu walikula na kunywa sana, mziki shampein kukata keki na kulishana kulipamba kwa kiwango kikubwa sherehe hii.
Kubwa ambalo Sam lilimshtua na hakulitegemea ni uwepo wa Gwakisa pale kwenye ile shughuli wakati hakualikwa. Lakini pia Gwakisa alionekana kuwa mchangamfu mno kwa Sam kitu kilichomfanya Sam ahisi kuwa huenda kuna jambo limepangwa.
Kwakuwa Sam alisomea ushushushu jambo hilo alilielewa vizuri na wakati wote alikuwa mtu wa kuchukua tahadhari.
Glory nae kwa upande wake alikuwa amependeza mno ndani ya vazi maridadi huku pembeni yake akiwa na Rafiki yake Charles ambapo kila aliyewaona alihisi kuwa ni wapenzi na hata kaka yake Sam alimtania mara kwa mara na kumuuliza kwanini hamtambulishi shemeji yake.
Dakika zilisogea sana na hatimaye muda wa kwenda kulala ukawa umewadia ambapo Sam na wageni wake wengine walikuwa wamepanga kulala hotelini huku wakiwa wamechukua Vyumba vya kutosha.
Wakati gari ya Sam inaelekea iliko hoteli ilipita kwenye Daraja moja ambalo lilikuwa na Kiza kutokana na kutokuwepo na nyumba jirani.
Hapohapo gari aina ya coaster iliziba njia almanusra watumbukie ndani ya daraja baada ya kupiga breki kali zilizoifanya gari ipoteze muelekea.
Wanaume wawili wenye bastola wakiwa wameficha sura zao walitoka kwenye kichaka kidogo pembeni ya daraja na kuamuru watu washuke kwenye gari!
Tangu alipoapishwa na kutangazwa rasmi kuwa RPC wa mkoa wa Tabora, Sam alipewa gari mpya na walinzi binafsi. Kutokana na hali hiyo hakupanda tena gari yake kwa siku ile isipokuwa alimuachia mdogo wake Glory ambaye alikuwa ameambatana na Charles na watu wengine ambao waliomba lifti.
Kwakuwa sherehe hii ilikuwa inafanyika Dar es Salaam sehemu ambayo Glory alikuwa hajazoea kuendesha gari askari mmoja ndie alikabiidhiwa gari ile awaendeshe.
Watu waliokuwa na nia mbaya na Sam walikuwa wamemvizia njiani ili wamuue na ndio maana walipoona gari lake wakajua yuko humo wakalizuia kwa kuingiza Coaster barabarani lakini kwa bahati mbaya walioshuka kwenye ile gari Sam hakuwepo.
Baada ya kugundua kuwa kwenye ile gari hakuwepo Sam wale watu walikasirika sana na kuamua kuipasua ile gari tairi na kisha kuondoka zao.
Huku wakiwa hawaamini kuwa wamepona Glory alimpigia kaka yake simu ambaye alifika pale na maaskari kisha wakairekebisha ile gari na kuriporti tukio kwenye mamlaka zinazohusika kisha wakaondoka zao. Kwenye moyo wa Sam aliamini kile ambacho alikihisi kuhusu Gwakisa.
……………………………………….
Ndani ya hoteli Charles na Glory walikuwa wamelala kila mtu chumba chake huku wanachat kwenye simu lakini ishu kubwa ilikuwa ni tukio lililotokea mda mfupi uliopita. Walichat masaa yakawa yanazidi kwenda mpaka ikatiimia saa nane usiku ambapo kila mtu alilala hadi kesho yake ambapo waliamka wakiwa wachovu lakini baaada ya kuoga na kupata kifungua kinywa walichangamka.
Walitembea maeneo ya jiji la Dar es salaam wakijinunulia baadhi ya vitu walivyopendezewa navyo kisha ilipofika kwenye saa kumi alasiri wakawa wapo hotelini walikofikia na kisha kujipumzisha kila mtu chumbani kwake.
Siku hii walikuwa peke yao kwani kaka yake (Sam) namoja na mkewe tayari walikuwa wameshasafiri kuelekea Tabora ambapo ndipo kilikuwa kituo kipya cha kazi cha Sam akiwa kama RPC.
Siku hii sio Charles tu lakini hata Glory alitamani kuwa karibu na mwenzake, uhuru waliokuwa nao uliwapa hamasa kubwa ya kufanya mambo makubwa.
Hatimaye Charles alikuwa chumbani kwa Glory amekaa wanatazama movie kwenye laptop, ilifika hatua wakawa wamesogeleana sana na kila mmoja kuhisi joto la mwenzake. Charles alikuwa anakifahamu kile ambacho kinaendelea na alifanya makusudi wakati mwingine kujisogeza zaidi.
Hofu ilikuwa imejaa kwenye moyo wa Glory akiwa hajiamini na zile hisia ambazo anakuwa nazo mbele ya Charles kwa muda ule, ndani ya akili yake aliamini kuwa hakuna urafiki wa kawaida kati ya mwanamke na mwanaume ambao sio ndugu, ukaribu wake na Charles umefikia hatua sasa unataka kuleta mambo mengine.
Kwa hofu ya kutokea kitu ambacho kilikuwa kinaanza kujijenga aliamka akidai anaelekea msalani, aliposimama tu Charles nae akasimama na kumshikilia kwa nyuma kisha akaanza kumpapasa.
“Charlesssss noooo!”
Pamoja na glory kusema hivyo lakini hakuondoka kwenye mikono ya Charles zaidi alikuwa anapumua kwa shida tu, Charles nae alizidisha uchokozi huku Glory akiwa sasa ameshafumba macho na kuzidiwa na kile anachofanyiwa.
Nguo zilikuwa zinadondoka moja moja na hatimaye Charles alikuwa anafanya kwa kutimiza lengo kabisa baaada ya kuona mdomo wake umepokelewa vyema na glory na sasa wanabadilishana ndimi na mate yake.
Utundu aliokuwa anafanyiwa Glory ilifika hatua akaichanua miguu yake mmoja kule na mwingine kule ili apokee mkong’oto lakini kabla Charles hajachomeka kuni jikoni kuna kitu Glory alikuwa amekumbuka kisha hapohapo akanyanyuka na kujifunga taulo kisha akaingia bafuni kujimwagia maji.
Alivyotoka alimkuta hakumkuta Charles pale chumbani akajua ameondoka zake, alivaa vizuri na kumfwata kule chumbani kwake ambapo alimkuta amelala kitandani kwa kulalia Tumbo.
“Charles am sorry”
“Usijali Glory najua mimi sio saizi yako”
“Kwanini useme hivyo Charles, labda hujui tu lakini mimi sijawahi kufanya hayo mambo tangu nizaliwe, naogopa sana, tafadhali naomba unipe muda kisha nitakuwa tayari kwa hilo, nakuahidi wewe ndie utakuwa wakwanza”
Charles hakuamini kile alichosikia kwa msichana mzuri na wa umri kama ule alio nao Glory, lakini baada ya kuambiwa yeye ndie atakuwa wa kwanza alifurahi sana kwani tangu alipomwambia anampenda hakuwahi kujibiwa lakini kwa maneno aliyopewa leo aliamini kuwa rasmi sasa Glory ni mali yake. Kwa furaha aliyokuwa nayo aliamka na kumkumbatia Glory kisha akamtazama kwa hisia machoni na kummwagia mabusu mfululizo yaliyoambatana na kumnyonya mdomo kisha wakaachiana.
………………………………………
Ndani ya mkoa wa Tabora kamanda Sam anakutana na mauaji ya vikongwe waliotuhumiwa ushirikina pamoja na changamoto ya mauaji ya Albino. Mambo haya yote Sam alipambana nayo kwa nguvu kubwa kitendo kilichomfanya aonekane ni moja kati ya makamanda wenye uwezo mkubwa sana.
Hata ule ujambazi nao ulipungua sana huku amani ndani ya mkoa huu ikiimarika mara dufu, askari waliokuwa chiini yake wakiwemo na makamanda wa wilaya walimpenda sana Bosi wao ambaye bado alikuwa kijana lakini pia walimuogopa kwani aliikuwa ni mtu asiyependa uzembe.
Siku moja alipata ujumbe kwenye simu yake ulioonyesha kuwa kwenye akaunti yake kiasi kiikubwa cha fedha kimeingia hadi akashtuka kwani zilikuwa fedha nyingi mno.
Kwa hofu ya kuchunguzwa kwanini anamiliki fedha nyingi sana kiasi kile aliamua kuzihamishia kwenye akaunti ya Glory kidogo kidogo hadi Glory mwenyewe akamuhisi kaka yake kuwa huenda kuna biashara haramu anafanya.
Kwa fedha ambazo alikuwa anaingiza na kuziweka kwenye Akaunti ya Glory alimruhusu mdogo wake kufanya mradi wowote ambao angeona unafaa. Glory alikubaliana na kaka yake lakini alimsihi kuwa asuburi kidogo amalizie masomo yake huku akiendelea kutafakari ninini cha kufanya.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)