BARUA KUTOKA JELA (19)

Zephiline F Ezekiel
0
Mtunzi: Ibrahim Gama

SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...
Mara Inspekta Jamila akamshuhudia yule Ombaomba akigeuza uso wake kumtazama, huku mkono wake wa kushoto ukiwa na bastola iliyofungwa kiwambo cha kuzuia sauti isisikike {Silence} akimnyooshea pale upande wake usawa wa dereva.

Mara akaona kidole kikigusa kile kifyatulio cha risasi {Trigger}

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Inspekta Jamila kitendo bila kuchelewa aliipeleka gari upande mwingine wa barabara ile kule kwa watembea kwa miguu ‘Service Road’ kwa haraka huku akibonyea mle ndani ya gari na kukanyaga Breki.

Na wakati huohuo ikasikika mlio wa kuvunjika kioo cha gari iliyokuwa inasuasua iliyokuwa nyuma yake! na vipande vidogovidogo vikimwagika chini kwa kuwa chenga tupu!

yule Ombaomba alirusha risasi,aliyokuwa amemkusudia Inspekta Jamila, ila kwa kitendo cha yeye kukata kona ya ghafla na kutoka barabarani, risasi ile ikaipiga ile gari mkweche kwa bahati mbaya.

Gari aliyokuwa anaendesha Inspekta Jamila ilikipanda kikuta cha barabara ya watembea kwa miguu, huku ikiwa inasota kwa sababu ya Breki za ghafla alizokanyaga, na gari iliposimama akafungua mlango haraka na kutoa bastola mgongoni mwake usawa wa kiuno.

Huku mlango ule ukiwa umefunguliwa akaipitisha mikono yake katika uwazi wa mlango pale baina ya Flem ya mlango ule na mlango wenyewe, huku akiwa ameushusha mguu mmoja nje, na kuuacha mguu wake wa kushoto ndani ya gari ile, mikono yake miwili iliyoshika bastola ya kipolisi aina ya Rivolver akalenga shabaha kwa tabu kumlenga yule Ombaomba aliekuwa anakaribia kabisa kuingia katika barabara ile ya Mandela na kufyatua risasi moja.

Mlio wa risasi ya silaha ya Inspekta Jamila ulisikika sehemu kubwa kwani bastola yake ilikuwa haina kiwambo cha kuzuia sauti.

Yule Ombaomba ilimkosa risasi ile sentimita chache na ikaenda kupiga katika chuma cha ngao ya gari ya mizigo iliyokuwa inaelekea Ubungo na kutoa cheche za moto!

Kwa ustadi mkubwa yule Ombaomba akaanza kuiendesha pikipiki ile katika mtindo wa Zigzaga na kuingia katika barabara ya Mandela, akakata kushoto kuelekea Tazara, na kumuacha Inspekta Jamila katika mataa ya Barabara ya Mandela na Uhuru!

Inspekta Jamila sasa akiwa ameshuka chini nje ya gari, alilipiga teke tairi la gari kwa hasira! Huku akilaani msongamano wa watu na magari uliyokuwa katika eneo lile, kwani ndiyo uliomfanya asiendelee kurusha risasi nyingine akihofia kuuwa au kujeruhi raia wasiokuwa na hatia, lau kungelikuwa hakuna msongamano wa watu angeliendelea kumrushia risasi yule Zabania mpaka angemdondosha chini!

Inspekta Jamila akakumbuka kwa kina Afande Kubuta, na akafikiri kuwa kwa vyovyote vile, kutakuwa kumetokea Zahma kubwa, kwani yule ombaomba alikuwa ni mtu hatari kuliko anavyoonekana!

Inspekta Jamila akaingiza mkono wake mfukoni mwa suruali yake aina ya Kadeti na kutoa simu ili ampigie Afande Kubuta kumwambia kilichoendelea, akaiona simu yake imezimika!

“Shit jana sikuichaji simu, kwani umeme ulikatika na kurudi asubuhi.”

Inspector Jamila alijisemea kimoyomoyo baada ya kugundua kuwa simu yake imezimika kwa kukosa chaji ya kutosha.

Alijaribu kuiwasha na simu ikawa kama haikubonyezwa kitufe chochote, unaweza kuifananisha na ‘Toy!’ akakata shauri kurudi kule alipowaacha askari wenzake wakiwa na mualifu wao Dokta Masawe ili akajue kilichotokea.

Inspekta Jamila akaingia ndani ya ile gari, na kabla hajaufunga mlango wa gari ile, alisikia sauti ya chuma aliyokuwa ameizoea masikioni mwake.

Ilikuwa ni sauti ya chuma cha Bunduki aina ya SMG ‘Sub Mashene Gun’ ikikokiwa katika harakati za kupeleka risasi chemba tayari kwa kufyatuliwa wakati wowote!

Na namna kilivyolia chuma kile, wakati silaha ile ilipokuwa inavuta risasi, akatambua kuwa silaha iliyokokiwa, imekokiwa katika mfumo wa kutoa risasi mfululizo {Basta / Rapid}na sio ule mfumo wa kutoa risasi mojamoja ‘Single Systim’ na mara akasikia sauti ya mtu ikimwambia

“Upo chini ya ulinzi,shuka chini na usalimishe silaha yako!”

Inspekta Jamila akashuka kutoka katika ile gari huku akitii amri ile kwa kuiweka chini silaha yake.

Aliposhuka chini akawaona askari polisi wawili, waliokuwa wapo katika sare zao za jeshi la polisi.

Askari mmoja akiwa ameshika Bunduki aina ya SMG, na askari wa pili alikuwa amekamata simu ya upepo ‘Radio call’.

Eneo lile lililotokea kizaazaa, walikuwa wamejaa watu wengi sana.

Yaani lilikuwa jambo la hatari sana sehemu iliyolia Bunduki watu badala ya kukimbia, kinyume chake wao wanakimbilia! Wakiwa hawawazi kwamba risasi inaweza kumkosa mlengwa ikampata raia asiekuwa na hatia, kwa sababu ya kiherehere na kimbelembele kilichowajaa!

Ama kweli jambo usilo lijuwa ni kama usiku wa kiza!

“Afande mimi ni askari, nilikuwa napambana na Jambazi”

Inspekta Jamila alikuwa anajitambulisha kwa wale askari, huku akiwaangalia usoni moja kwa moja.

“Wewe ni askari kutoka katika kituo gani”

Yule askari alieshika “Radio Call” alimuuliza Inspekta Jamila.

Kabla Inspekta Jamila hajajibu swali lile, Afande kubuta alitokea na alikuwa anawatambua askari wale!

“Afande Majuto huyu ni askari mwenzetu, mwenye cheo cha Inspekta, anaitwa Inspekta Jamila, kutoka makao kakuu.”

Afande Kubuta aliyasema maneno yale huku akiiokota ile silaha ya Inspekta Jamila pale chini, iliyokuwa imesalimishwa na kumkabidhi Inspekta Jamila.

Wale askari wawili wakakakamaa na kutoa heshima ya utii kwa Inspekta Jamila.

Inspekta Jamila alipokea heshima ile kwa moyo mkunjufu, kutoka kwa wale askari waliokuwa katika ulinzi wa kawaida wa jeshi la polisi, katika kila kwenye makutano ya barabara kubwa na kwenye taa za kuongozea magari.

“Vipi Dokta Masawe ana hali gani huko aliko, kwani yule Ombaomba ni zaidi ya Jamba……”

“Yule ni Gaidi mkubwa!”

Afande kubuta alimkatisha kauli Inspekta Jamila, aliekuwa anataka kujuwa kilichotokea kule nyuma alipowaacha na kutaka kumuelezea yule Ombaomba.

“Yule ni Jeradi Mwaipopo au Gaidi, na Dokta Masawe hivi tunavyozungumza ni marehemu!”

Maneno ya Afande Kubuta yalimkata maini Inspekta Jamila na kumfanya kutingisha kichwa kwa masikitiko makubwa.

Inspekta Jamila sasa hakuwa na shaka kuwa Dokta Masawe ameuwawa na yule aliekuwa akimuona kama Ombaomba, kumbe ni Jeradi Mwaipopo mtu aliowafanya wawe maeneo yale kwa siku ile ili wamtie mikononi, badala yake amekuja na kuwaachia maafa, yasiyofikirika kabisa kutokea, hasa kukiwa na ulinzi kama ule!

Mara ikasikika sauti ya King’ora cha gari ya wagonjwa, ikija kwa kasi kuelekea kule kwenye Baa ya Y2K Buguruni kwenda kuchukua mwili wa Hayati Dokta Masawe.

Ilikuwa ni simu ya Afande Kubuta alipokata shauri, la kuwapigia simu pale katika Hospitali ya Amana Ilala, ili kwenda kuuchukua mwili wa Marehemu Dokta Masawe ili ukaifadhiwe katika chumba cha maiti pale Hospitalini Amana, na uchunguzi zaidi wa mwili ule, uweze kufanyika kwa kina.

Inspekta Jamila akawageukia wale askari wawili wa Doria, waliomuweka chini ya ulinzi muda mfupi uliopita, akawapa maelezo kwa harakaharaka, na alipomaliza akageukia upande wa pili wa gari ile na kupanda, huku Afande Kubuta akiingia upande wa Dereva wa gari ile na kuwasha gari na kuiingiza barabarani kuelekea katika barabara ya Mandela.

Afande Kubuta alipofika pale katika makutano ya barabara ya Uhuru na Mandela, akakata upande wa kushoto wa barabara ya Mandela, na kuelekea Tazara.

Wale askari wawili Afande Majuto na Mwenzie, walioachiwa maagizo na Inspekta Jamila, waliiendea ile gari iliyopata ajali ya kuvunjwa kioo cha mbele kwa risasi na Jambazi aliepanda cheo na kuwa Gaidi, Jerard Mwaipopo.

Gari aina ya Datsun Nissan Old Model, huku dereva wa gari ile akiwa haonekani eneo la tukio.

Wale askari walipoona kimya kila walipokuwa wanamuuliza dereva wa gari ile, yule askari aliekuwa na kifaa cha mawasiliano, Afande Majuto aliongea kupitia kifaa kile na muda wa kama dakika tano hivi gari mbili aina ya Land Rover 109, zilikuja kwa mwendo wa kasi katika eneo lile, na kuifunga mnyororo gari ile na kuivuta kuipeleka katika kituo cha polisi cha Buguruni. Pale mkabala na soko na kituo cha Basi cha Buguruni.

watu waliokuwa katika kushangaashangaa katika eneo lile, ilibidi wasambae na kuondoka kwani hakukuwa na jambo la kushangaa tena. Na kiasi ya dakika kama kumi baadae eneo lile lilirudi katika hali yake ya kawaida, kukawa kama halikutokea tukio lolote la hatari hapo kabla.

*******

Jeradi Mwaipopo aliendesha ile Pikipiki kwa kasi ya ajabu, kama aliekuwa katika mashindano ya kuendesha Pikipiki!

Alipofika katika eneo la Tazara akazikuta Taa za kuongozea magari, zimeruhusu gari za kutoka upande wa Buguruni kupita.

Hivyo akiwa bado katika mwendo kasi, alilala nayo ile Pikipiki upande wa kulia, akishika njia kuelekea upande wa uwanja wa ndege.

Kila alieiona Pikipiki ile namna ilivyolazwa pale kwenye kona ikienda sanjari na taa ya kijani iliyoruhusu vyombo vya moto kupita, alishika kichwa kwa masikitiko, kwani mwendo ule ukianguka tu, huwi majeruhi abadani ila kifo kitakutembelea!

Hususan dereva wa Pikipiki ile hakuwa na ile kofia maalum ya kuendeshea Pikipiki ‘Elementi’

lakini hata mavazi ya dereva yule, na Pikipiki ile, vilikuwa havifanani kabisa, ilikuwa tofauti kama maji na mafuta!

Lakini kila kwenye Welevu, na Wajinga hawakosi.

Wapo watu wachache waliokishangilia kitendo kile cha mwendo kasi, huku wakipayuka kuwa;

“Siku hizi wazee nao wamechoka, kwani wanaendesha Pikipiki kama hawana akili nzuri!”

Mwendo kasi aliopita nao Jeradi Mwaipopo kwenye taa zile za kuongozea magari pale Tazara, kuliwagutusha askari wa usalama Barabarani na askari wa doria wa Pikipiki waliokuwa wamebarizi pale kwenye kivuli cha mti kwenye kona ya Barabara ile.

Waliitilia mashaka pikipiki ile, wakawasiliana na askari wenzao waliokuwa doria pale katika eneo la Vingunguti, kwenye kona ya kwenda Vingunguti kiembe Mbuzi, kwa upande wa kulia na ile kona ya Bombom Kijiwe samli kwa upande wa kushoto, kwenye Njia ya Viwandani.

Huku askari wa doria wenye Pikipiki waliokuwa pale tazara, wakiifatilia Pikipiki ile kwa mwendo wa kasi vilevile.

Askari wale waliokuwa pale kwenye kona ya Vingunguti, na Viwandani walikuwa wamejiandaa na bunduki mikononi!

Lakini hadi wale askari waliokuwa wana Pikipiki waliotoka Tazara, walipofika pale kwenye ile kona ya Vingunguti na Bombom, bado waliwakuta askari wenzao, wakiwa na bunduki mikononi wakisubiri mtu aliepita na Pikipiki kwa mwendo wa kasi bila mafanikio!

Wote kwa pamoja walikuwa wamepigwa chenga ya Mwili.

Baadae wakapata taarifa zilizowafanya wakunje uso kwa ghadhabu, kwani taarifa ile kupitia Radio Call zao ilisema;

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

 Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Shawishi Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)