
Mtunzi: Yozz Piano Maya
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
mende..ng'e..tandu..mijusi..na wadudu wengi watambaao.....akafunua naironi lililokuwemo ndani ya jeneza hilo...alilotoa naironi hilo...zikaonekana zana za kutisha zikiambatana na nyundo misumari mikubwa na yenye unene waa milimita kumi na sita..
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
mkasi mkubwa shoka ndogo..msumeno kisu mundu..upanga,, nk.
akachukua shoka ndogo pamoja na kisu....kisha akatoka ndani ya chumba hicho na kuzipiga hatua kumtafuta chery....yeye hakujua kuwa ndani ya jumba hilo ,,,,,Latifa alikuwemo pia....
mwanamke yule wa kizungu aliamini kuwa chery bado yumo ndani ya jumba hilo kwa sababu chery alikuwa hajui milango na chemba za kutokezea upande wa nje.
************
wakati huohuo walionekana Latifa na Chery wakiwa wanazipiga hatua za kunyatia huku wakibahatisha njia kwa sababu giza lilitawala....ghafla Chery aliparamia kipande cha chuma kilichokuwa juu ya meza..kikadondoka na kutoa mlio....
yule mwanamke wa kizungu...akasitakutembea akabadilisha njia ya kupita ,,,,akaelekea kule aliposikia sauti ya kipande cha chuma kudondoka..
huku mkono wake mmoja umeshikilia shoka dogo
na mkono mwingine umeshikilia kisu kikali sana..
alipofika eneo hilo hakuona mtu...akaendelea kuzipiga hatua kimtafuta chery..
wakati huohuo latifa na chery walikuwa wanatimua mbio ili kuokoa maisha yao....walikimbia bila kujua ni wapi wanaelekea.....kwa sababu jumba hilo lilikuwa na vyumba vingi,wakaamua kuingia kwenye chumba kimoja kilichokuwa na giza kiasi.....wakajifungia humo....chery akaangaza angaza macho yake..akaona kuna sehemu inauwazi akamwamvia latifa kuwa watoke kupitia hapo huenda upande wa pili kuna njia yakutoka ndani ua jumba hilo chery akaanza kutangulia kupanda akaingia kwenye tundu hilo.....kabla latifa hajapanda.....akasekia kunamtu anasukuma mlango wa chumba hicho.....larifa akaingiwa na hofu akapanda harakaharaka...alipokaribia kuingia kwenye tundu..ghafla akatereza na kudondoka....
ikasikika sauti ya kitu kikipiga piga mlango...
kumbe alikuwa ni yule mwanamke wa kizungu akipiga mlango huo kwa shoka ili auvunje....akafanikiwa kuvunja mlango huo..lakini alikuwa ameshachelewa.. latifa alikuwa tayari ameshaingia ndani ya tundu hilo..kisha akafunga ufuniko wa tundu hilo na kuchomeka komeo ambalo lilikuwa upande wa ndani ya tundu...
yule mwanamke wa kizungu...akajaribu kujibadilisha ili awe kiumbe wa kutisha....akashindwa......alikasirika sana akaamua kutoka haraka ili awahi upande wa pili awanase kiurahisi kabla hawajatoka nje ya tundu hilo.......
alipofika alikuta bado hawajatokeza..akaamua kusimama hapo kuwasubiria....kumbe chery na Latifa waliona chemba iliyokuwa katikati,wakaamua kuifuata chemba hiyo....walipofika mwisho..wakatoka na kushuka uoande wa chini...wakahikuta wameingia kwenye chumba humo humo ndani ya jumba hilo......angalau kidogo chumba hicho kilikuwa na mwanga wa kutosha....chery akamuuliza latifa kumetokea nini?? na amejuaje kuwa yeye yupo ndani ya jumba hilo!!!ikabidi latifa amwambie matukio yote ya mauwaji ya kutisha na yakikatiri yaliyofanywa na kiumbe wa ajabu...kisha akasema""matukio yote yalifuata ufululizo wa hadithi ya kitabu chako ulicho tunga mpaka michoro...chery akastahajabu sana!!!! hakuamini kile alichokisikia kutoka kwenye kinywa cha latifa..
chery akajisemea moyoni""kama alikuwa anafanya mauwaji kufuata mtiririko wa hadithi yangu....inamaana kiumbe latifa atakufa!!! haiwezekani....wakati anaangaza angaza macho kutafuta namna watoke ndani ya chumba hicho..akaona kalamu ikiwa chini ya sakafu akazipiga hatua za haraka haraka akaiokota kalamu ile na kuichana karatasi iliyokuwa imeandikwa sehemu ya mwisho...kisha akabadilisha mwisho wa hadithi...ukawa hivi""
alionekana yule binti aliyekata minyororo na kufanikiwa kutoka ndani ya chumba kile chenye mwanga hafifu....kabla hajapata njia ya kutoka ndani ya jumba hilo la kutisha alionekana msicha mmoja akiingia ndani ya jumba hilo...ili kutoa msaada...ghafla kunamwanamke wa kizungu akajitokeza huku ameshikilia shoka na kisu...alipotaka kumkata na shoka yule binti aliyekuwa ametoroka ndani ya chumba alichokuwa amefungiwa kwa miaka kumi na mbili iliyopita. ghafla yule binti aliyekuja kutoa msaada akachukua kipande cha chuma na kumpiga kichwani yule mwanamke wa kizungu..alipodondoka chini wakamnyang'anya kisu na shoka....
*****************
yule binti aliye kuja kutoa msaada akachukua kisu
na yule binti alikuwa kafungwa minyororo akachukua shoka..na kumkata yule mwanamke wa kizungu katikati ya paji la uso..kisha akaanza kumkata vipande vipande.....
chery alipomaliza kuandika mwisho wa hadithi hiyo akakichana kitabu......na kukitelekeza humo.
kisha wakatoka ndani ya chumba hicho na kuzipiga hatua huku wakikimbia kutafuta njia ya kutoka ndani ya jumba hilo la kutisha....achecheeee.......
**************
kule upande wanje alionekana yule mwanamke wa kizungu akizipiga hatua kurudi ndani ya jumba hilo baada ya kuona hakuna mtu aliyetokeza kutoka ndani ya chemba hiyo...hivyo aliamini kuwa Chery bado yumo ndani...hakujua kuwa latifa pia alikuwepo......
aliooingia upande wa ndani akazipiga hatua kwenda kwenye chumba kimoja kilichokuwa kimefungwa....akaufungua mlango na kuinfia ndani....chumba hicho kilionekana kutisha sana...akabofya kitufe kilichokuwa ukutani...zikasikika sauti za milango ikijifunga kwa nguvu....kisha taa zikawaka,, jumba zima likawa na mwanga....
chery na latifa wakastuka kuona taa zimewashwa...wakajibanza kwenye kabati kubwa lililokuwa kwenye moja ya kordo za jumba hilo la kutisha....chery akachungulia akaona kivuli cha mtu akitembea kuja kwenye kordo hiyo....wakakurupuka na kuanza kutimua mbio wakakatisha kona na kuelekea kwenye kordo nyingine.....wakaingia ndani ya chumba kilichokuwa na giza wakajificha keenye magunia yaliyokuwrmo ndani ya chumba hicho...
chumba hicho kilikuwa kinanuka harufu mbaya enye uwozo...ghafla yule mwanamke wa kizungu akaingia ndani ya chumba hicho...akawasha taa..akaangaza macho lakini hakuona mtu akaamua kutoka na kuelekea vyumba vingine...
harufu ilikuwa kali sana walivumilia lakini wakashindwa....walipo ona mwanamke yule ameondoja dakika kadhaa zilizopita ikabidi watoke nyuma ya magunia hayo....ghafla gunia moja likadondoka chini likafunguka....zikaonekana maiti mbili zilizokuwa zimeoza na kutoa wadudu (funza)
huku zikiwa hazina baadhi ya viungo miguu na mikono pamoja na vichwa.....latifa akataka kupiga kelele chery akamuwahi akamziba mdomo....akamfanyia ishara kwamba asipige kelele ili yule mwanamke asijue wapo upande gani..
kumbe lile gunia lilivyodondoka yule mwanamke wa kizungu alisikia lakini kila akijaribu kuvuta kumbukumbu ya mwisho wa hadithi ya kitabu cha chery hadithi ilionesha kwamba yeye ndiye mtu ambaye anafuata kuuwawa.....alafu hadithi inasimulia kuwa kunabinti mwingine yumo ndani ya jumba hilo.....akastuka...hakujua ni kipi kimefanyika ndani ya kitabu cha chery..hakuweza kutambua kuwa chery amebadilisha mwisho wa hadithi yake akazipiga hatua za haraka haraka ili awahi kuwauwa kabla hawajamuuwa...
wakati huohuo latifa na chery walikuwa wanatoka ndani ya chumba hicho wakakutana uso kwa uso na mwanamke huyo wa kizungu...achecheee
yule mwamamke wa kizungu akamtazama latifa kwa macho ya mshangao....akauona ule mkufu aliomkabidhi miaka kumi na tani iliyopita...
wakati bado anamshangaa latifa chery akatimua mbio akajikwa na kudondoka chini...yule mwanamke akanyanyua shoka ili amuuwe chery...
latifa akachukua kipande cha chuma kilichokuwa chini...akampiga kichwani yule mwanamke wa kizungu akadondoka chini....chery akanyanguka haraka akamnyang'anya shoka..na latifa akamnyang'anya kisu...chery akanyanyua shoka ili amkate kwenye paji la uso....latifa akapaza sauti,,,""NOOOO usimuuwe..chery alistahajabu sana akamtazama latifa na kusema""huyu mwanamke katiri sana amenifungia kwenye chumba kwa miaka kumi na mbili alafu unamuonea huruma je angetuuwa sisi???....
chery akanyanyua shoka na kutaka kumkata mwanamke huyo...ukasikika mlio wa risasi..ikipigwa na risasi ikagonga ukuta wa pembeni yao....walipotazama latifa alimuona mama yake akiwa na maaskari.....wakamchukua mwanamke yule wa kizungu na kumfunga pingu.
kisha latifa na chery pamoja na maaskari wakatoka nje ya jumba hilo na kumpeleka mwanamke yule kwenye vyimbo vya sheria..akafunguliwa mashtaka....alielezea yote yaliyomsababisha yeye afanye mauwaji hayo ya kikatiri...lakini hakimu aliamua kumuhukumu anyingwe mpaka afe........
chery alirudi nyumbani kwao lakini alikuta wazazi wake walifariki na kuzikwa miaka tisa iliyopita...chery alilia sana..akapelekwa kuoneshwa makaburi ya wazazi wake...
*****BAADA YA MIEZI SITA KUPITA*****
Chery alianza kusahau matukio yaliyomtokea.. akaanza kuishi kwa amani..akapata kazi ya uandishi wa vitabu katika kampuni iliyopo hapa nchini...akaandika vitabu vingi vya hadithi zilizomfanya awe mtu maarufu kama alivyo YOZZ PIANO MAYA..
Urafiki wa Latifa na Chery ukazidi kuwa imara wakaishi kama ndugu mpaka leo.
Urafiki wa Latifa na Chery ukazidi kuwa imara wakaishi kama ndugu mpaka leo.
MWISHO
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media