
Mtunzi: Ally Mbetu 'Dr Ambe'
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Nina imani ukipata ukweli utazidi kuchanganyikiwa. Nakuahidi baada ya kupata ukweli nitakufuata ili kukutuliza akili.”
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
“Ila nakuomba kitu kimoja fanyia yote kazi niliyokueleza na kama utakuta nilichokisema ni uongo mwambie Shuku na nipo tayari kufanywa lolote na wewe kunikataa.”
“Nimekuelewa MJ nitafanyia kazi naomba uniache nimechanganyikiwa kweli.”
“Una bahati angekupa mimba usinge muona angekutimulia vumbi.”
“Sawa nimekuelewa, MJ niache kwanza basi jamani,” Lily alichanganyikiwa na kuona malengo yake ya kuwa mke wa Shuku yamekwenda ndivyo sivyo alijikuta akiwa
njia panda. MJ kabla ya kuondoka alimuachia milioni mbili keshi huku akisema:
“Najua baada ya kuujua ukweli utaumia sana, hizi zitakusaidia kutafuta sehemu tulivu kutulia, ukinihitaji nikupe kampani siyo mbaya tutakuwa pamoja.”
“Nimekuelewa ziweke hapo yaani nimechanganyikiwa sana MJ,” Lily alijikuta kwenye maumivu makali.
MJ baada ya kumwaga sumu alitoka, akiwa ndani ya gari lake alimpigia simu Shuku.
“Haloo best, lete stori,” Shuku alipokea upande wa pili.
“Ni hivi gari zote hazitakiwi kutoka mpaka wiki ikatike. Nitazitumia mwenyewe ila nitakupa fedha ya kutumia teksi hata kukodi ili kuhakikisha unafanya mambo yako
bila tatizo.”
“Hakuna tatizo best.”
“Tafuta gari zuri kulingana na hadhi yako si unajua sasa hivi upo matawi ya juu, sawa best?”
“Hakuna tatizo,” Shuku alikubali bila kujua kama kaingizwa kwenye mtego.
Wakati Shuku akiingizwa kwenye mtego Lily alikuwa amechanganyikiwa asiamini alichoambiwa. Dada yake aliyekuwa ametoka mara moja aliporudi alimkuta mdogo
wake hayupo kwenye hali ya kawaida.
“He! Mdogo wangu kuliko nimetoka upo katika hali nzuri lakini nakuona umechananyikiwa, na hizi fedha?”
Lily huku akilia alimueleza yote dada yake aliyoelezwa na MJ na kumfanya dada abakie mdomo wazi.
“Mmh! Unajua mdogo wangu japo inauma kuna ukweli ndani yake.”
“Dada ukweli gani zaidi ya kutaka kuniachanisha na mpenzi wangu, nilikubali kuwa naye lakini kila kukicha manyanyaso na mateso.”
“Mdogo wangu tatizo nini? We umepata bahati unapewa kila kitu una gari na bado anataka kukunulia gari jingine pamoja na nyumba. Wengine wanaitafuta bahati hiyo
kwa waganga wewe unaikimbia.”
“Pamoja na yote, bado nampenda sana Shuku.”
“Lily inawezekana Shuku ni mpambe mshika pembe tu, ukweli unakuja kutokana na ahadi zake zisizotimia. Lakini usikurupuke hebu lifanyie kazi hili la gari tutapata
jibu.”
“Sasa nifanye nini?”
“Mpigie Shuku mwambie hujisikii vizuri ili aje kila kitu kitajulikana.”
“Mmh! Sawa,” Lily alisema huku akichukua simu na kumpigia Shuku.
“Haloo bebii,” simu ilipokelewa upande wa pili.
“Sweet upo wapi?”
“Nipo home.”
“Naomba uje sijisikii vizuri.”
“Ooh! Bebi nini tena?”
“Sijisikii vizuri tu naomba uje.”
“Nakuja bebi.”
Kwa vile ilikuwa haraka alichukua laki tano na kuziweka mfukoni na kutoka nje na kukodi teksi yenye hadhi ya juu ya kwenda nayo kwa mpenzi wake bila kujua
amekwenda na ushahidi wa kummaliza.
Shuku aliwasili nyumbani kwao Lily kama kawaida, alipiga honi ili atoke. Lily baada ya kusikia honi alichunguliana na kuliona gari tofauti na aliyoyazoea. Alimwita
dada yake aliyekuwa chumbani.
“Dada njoo.”
“Lily mbona unanitisha, kuna nini?”
“Shuku amekuja.”
“Tatizo nini?”
“Jamani dada, wewe si ndiye uliyeniambia nimpigie simu aje tuthibitishe maneno ya MJ.”
“Ooh! Nilisahau vipi amekujaje?”
“Twende ukaone,” Lily alijibu huku akimsogeza dada yake dirishani na kuona gari alilokuja nalo Shuku.
“He! Gari si nzuri lile, tena gari la watu wenye fedha?”
“Dada yale siyo katika magari yao, lile lazima kaazima tu kama alivyosema MJ.”
“Kwa hiyo MJ amesema kweli?”
“Inawezekana.”
“Tusiandikie mate mfuate ukamuulize mwenyewe.”
“Yaani kama kweli, basi leo nitampaka, kumbe mbwembwe zote hana kitu mwanaume suruali, Lo!” Lily alisema akiwa amechanganyikiwa na matarajioa yake kwa
Shuku kuwa ndivyo sivyo.
“Lily hebu kwanza shusha munkali, kamuulize taratibu.”
“Yaani dada wee acha tu, usingekuwa wewe ningekwenda kumfukuza kama mbwa. Kumbe mwanaume muongo, tapeli kibaya zaidi hana kitu anaishi maisha ya
kufungwa kama mwanamke.
“Ndiyo maana kila siku ukimuomba kitu subiri, kumbe anasubiri kupiga mzinga,” Lily alisema huku akibana pua.
“Lily wewe jifanye hujui muulize kisa cha kuja na gari tofauti.”
“Sawa ngoja nimfuate,” Lily alisema akitupia mtandio begani.
Alipokaribia kwenye gari aina ya Toyota Harrier Lexus Rx 300, Shuku alitoka kama kawaida yake kapiga pamba za kufa mtu shingoni kachafuka kamba ya bei mbaya.
Lily alimtazama Shuku kuanzia chini mpaka juu kisha akaangua kicheko cha dharau kilichomshtua Shuku.
“Vipi mbona unacheka?”
“Nimefurahi tu.”
“Vipi hali yako?”
“Mbona umekuja na gari hili?” Lily hakujibu zaidi ya kuuliza swali.
“Magari mengine yameisha bima, tulijisahau kukata ila kesho kama kawaida.”
“Muongo!”
“Kweli bebi.”
“Wewe na MJ mpoje?”
“Mbona unaniuliza hivyo?”
“Shuku naomba jibu siyo swali,” Lily alimuuliza Shuku kwa sauti kavu.
“Ndugu yangu.”
“Na ile mali ya nani?”
“Yetu.”
“Wewe na nani?”
“Na MJ.”
“Kweli?”
“Kweli, kwani tatizo nini?”
“Shuku, MJ si ndugu yako ni rafiki yako na ile mali ni yake, wewe ni mpambe mshika pembe tu, huna lolote kila kitu unapewa na MJ.”
Kabla ya kujibu tuhuma Shuku alicheka sana kisha akamuuliza.
“MJ ndiye kakwambia hivi?”
“MJ aniambie nini naye mshamba kama wewe, unaniuzia mbuzi kwenye gunia kumbe ndiyo zako kuwaharibu watoto wa kike kisha unawapiga chini.”
“Mimi?” Shuku lilimshuka.
“Kwani nazungumza na nyani?” Lily alimpa makavu Shuku.
“Mpenzi si kweli, mali ile ni yetu sote.”
“Shuku, mi si mtoto najua kila kitu juu yako na MJ, japokuwa mlikuwa mkificha lakini ukweli wewe umeokotwa na MJ na pale unakaa kwa kumtegemea yeye kila kitu.
“Hebu jionee huruma ataweza kunimiliki mwanamke kama mimi? Gari kila siku linataka mafuta, nataka toleo jipya la gari nataka mapambo ya kike, bado nataka jumba
la gharama. Shuku utawezaaa?
“Hebu waache wenye kisu kikali wajilie nyama, kama msaada wa penzi nimekupa inatosha. Naomba kuanzia leo tukomane.”
“Lakini..”
“Lakini nini? Nasema uongo?”
“Lily mpenzi naomba unisikilize.”
“Haya sema.”
“Ni kweli MJ rafiki yangu lakini amenipa uhuru mkubwa, hivyo nilikuwa na uamuzi wowote na kufanya chochote bila kunikataza.”
“Shuku unachekesha, sasa hayo maisha utaishi mpaka lini?”
“Kuna fedha alisema atanipa ili nifanye biashara.”
“Kwa nini ulinidanganya?”
“Nisamehe mpenzi wangu.”
“Sasa Shuku naomba unisikie, ukiondoka hapa nisikuone tena.”
“Kivipi mpenzi?”
“Mimi na wewe basi.”
“U..u..sifanye hivyo.”
“Shuku nilikupenda sana, lakini umekuwa si mkweli. Wanaume waongo nawaogopa sana. Nasikia ndiyo tabia yako kwa hiyo hapa umenoa.”
“Lily mpenzi uamuzi huo utaniumiza sana.”
“Kuliko ulivyoniumiza mimi, kwa kuamini nipo na mtu mwenye fedha kumbe kapuku.”
“Lily nitajitahidi kutimiza mahitaji yako.”
“Utaweza wapi, baiskeli huna unaweza kununua mafuta ya gari langu?”
“Kuna kitu nitafanya muda si mrefu utafurahi tu mpenzi wangu.”
“Umewadanganya wanawake wangapi, leo wanakutafuta kama Osama. Shuku kwa ustaarabu naomba uondoke kimyakimya.”
“Vipi kuhusu hali yako, nilikuwa nimekuja kukupeleka hospitali tu,” Shuku alisema akitoa laki nne mfukoni ili ampe Lily.
“Shuku kwa kifupi siumwi ila nilikuita nimalizie ushahidi wangu ambao umekamilika, hivyo baba tukomane.”
“Basi chukua fedha ya dawa.”
“Shuku unataka kunipa fedha zote hizo wakati una kazi? Hizo fedha kapangie chumba uache kulishwa na wanaume wenzako. Angalia mwenzako anakupa kila
unachotaka nawe unakubali. Naona mwenzangu umesahau kula uliwe.”
“Sasa hayo matusi.”
“Siyo matusi Shuku, hebu ona aibu kununuliwa hata nguo ya ndani na rafiki yako, sasa una tofauti gani na mtoto wa kike?”
“Kwa hiyo umeamua kunitukana.”
“Shuku sikutukani nakuambia ukweli, ungenieleza mapema ningejua niishi na wewe katika muundo gani. Lakini uongo uliweka mbele, sawa ulifanikiwa kunipata kwa
gia unazo, nina imani sina deni na wewe.”
“Kwa hiyo?”
“Naomba uondoke.”
“Kwa hiyo umeamua kunitukana.”
“Shuku sikutukani nakuambia ukweli, ungenieleza mapema ningejua niishi na wewe katika muundo gani. Lakini uongo uliweka mbele, sawa ulifanikiwa kunipata kwa gia unazo, nina imani sina deni na wewe.”
“Kwa hiyo?”
“Naomba uondoke.”
“Sawa,” Shuku alisema huku akielekea upande wa dereva na kukaa kwenye uskani bila kufunga mlango.
Lily baada ya kusema yale, aligeuka na kurudi ndani. Alipoingia ndani alikimbilia chumbani na kuanza kulia kilio cha kwikwi na kumfanya dada yake kumfuata.
“Lily unalia nini mdogo wangu?”
“Dada najuta kupoteza muda wangu kwa mwanaume suruali.”
“Kivipi?”
“Hakuna kilichobadilika, nimembana kakubali yote, unafikiri kweli yule ni mwanaume sahihi kwangu?”
“Si sahihi, kwa vile sasa hivi gharama ya maisha imepanda kila kitu kinahitaji fedha, kwa hiyo umeamuaje?”
“Nimempiga chini.”
“Kwa hiyo MJ umemfungulia moyo wako?”
“Inabidi nifanye hivyo, tena kwa malengo.”
“Na kweli mdogo wangu, sasa ondoa hasira za kijinga ili kufanikisha malengo yako. Nina imani sasa hivi MJ atakupa vitu vingi.”
“Dada wivu wa kijinga nauweka pembeni ili kufanikisha malengo yangu, nikipata magari mengine mawili na nyumba hapo nitakuwa na jeuri kama hataki kubadilika naye nampiga chini.”
“Hayo ndiyo maneno ya mwanamke mtafutaji, sasa mtaishije nyumba moja na Shuku?”
“Kila kitu MJ anajua, labda amepanga kuniweka hotelini mpaka atakapo ninunulia nyumba yangu.”
“Mdogo wangu utumie mwili na uzuri wako kuyabadili maisha yetu.”
“hilo si lakusema,” waligongeana mikono na kukumbatiana.
****
Shuku baada ya kuingia kwenye gari na kujifungua kwa ndani, alitulia zaidi ya robo saa bila kufanya kitu chochote akiwa haamini kilichotokea muda mfupi.
“Hivi kweli Lily kaniacha?” Shuku alijiuliza huku akipiga mikono kwenye uskani.
“Nani kampa siri hii? Hapana..hapana any way, wacha niondoke mpenzi siyo lazima.” Shuku aliwasha gari na kuondoka kurudi nyumbani. Alilirudisha gari kwa mshikaji wake kisha alikodi bodaboda mpaka home.
Alipofika aliingia ndani na kujifungia chumbani kwake, akiwa na mawazo mengi, kwa kuiona aibu yake ya kukaa na MJ kama ndugu ipo nje.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media