
Mtunzi: Ally Mbetu 'Dr Ambe'
SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Mjuni nashukuru sana kwa yote uliyonifanyia, sina sababu ya kukulaumu kwa ajili ya kitendo chako cha kunidhalilisha kwa Lily. Najua umaskini wangu ndiyo unaniponza, lakini siamini msichana uliyekuwa ukimwita malaya ndiye anayevunja urafiki wetu leo, asante,”
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Shuku alisema huku akiondoka.
“Shu...shu...” MJ alijitahidi kumfuata rafiki yake, lakini Lily alimvutia kwake ili asimfuate Shuku.
Shuku hakutaka kugeuka nyuma, moyo ulimuuma alitembea huku akilia hadi kwenye kituo cha bodaboda na kukodi pikipiki.
“Niwahishe Tabata,” Shuku alisema huku akipenga makamasi mepesi.
“Elfu tatu mkubwa.”
“Poa twende.”
“Vipi kaka umefiwa?” hali ya Shuku ilimshtua dereva wa bodaboda.
“Heri ningefiwa.”
“He! Nini tena?”
“Wee acha tu.”
Dereva wa bodaboda hakutaka kuuliza zaidi, alipofika Xteno alimuuliza:
“Tabata ipi?”
“Wee umetaja bei bila kujua Tabata ipi?”
“Samahani mkubwa.”
“Mawenzi.”
Dereva alivuka barabara na kuelekea Tabata Mawenzi. Shuku alipofika alilipa anachodaiwa na kwenda ndani. Alipofika alichukua kila kilicho chake na kutimua zake kwake kurudi maskani kwake.
Aliamini maisha ya kutafuta mwenyewe yana uhuru kuliko kupewa na mtu na matokeo yake kudhalilishwa kama vile.
kwa vile alikuwa amejiimalisha kwake alirudi moja kwa moja kwenye chumba chake alichokuwa amenunua vitu vyote vya ndani kupitia fedha alizopewa na MJ.
Siku zote hakuamini maisha ya kupewa na alihofia akikosana na MJ anaweza kukosa pa kuanzia kimaisha na kuwafanya wenye mapengo wamcheke.
Kitendo cha Shuku kufumania siku ile kilimuuliza sana MJ na kupanga akirudi nyumbani amuombe msamaha kwa gharama yoyote. Aliamini akimtangazia fedha na dhiki aliyonayo atakubali tu na kumwachia Lily.
Lakini alishangaa kutomkuta nyumbani, aliondoka na mpenzi wake akiamini huenda kesho atamkuta. Siku ya pili aliporudi hakumkuta tena. Kwa vile alikuwa bize na Lily hakujua kinachoendelea nyumbani. Alimuachia Shuku fedha nyingi kitandani kwake akiamini bado yupo pale.
Wiki ilipokatika ndipo alipogundua Shuku hayupo, hata alipokwenda alipokuwa akiishi zamani aliambiwa amehama. MJ hakutaka kumtafuta aliendeleza mapenzi kwa Lily. Kwa vile MJ hakutaka kubanwa na mpenzi wake alimnunulia nyumba ili aweze kuendelea na tabia zake za kubadili wanawake kama nguo.
Mwanzo Lily alilifurahi penzi la MJ kwani muda mwingi alikuwa naye pia kila alichokitaka alikipata. Siku zote mjusi hawezi kuwa nyoka, siku moja wakiwa chumbani wanajiandaa kwa chakula cha usiku simu ya MJ iliita, alipoangalia alikuta ni mpenzi wake mtoto wa waziri aliyekuwa nje ya nchi kuonesha alikuwa amefika siku ile usiku.
“Sorry mpenzi,” MJ alisema huku akipunguza kuni kwenye jiko.
“Ya nini tena bebii?” Lily alilalamika kwa sauti ya mtu aliyekuwa akitafuna pilipili.
“Kuna simu muhimu nataka kusikiliza mara moja.”
“Jamani bebi, utasikiliza baadaye mwenzio zipo juu zinataka kumwagika zishushe mpenziiii.”
“Samahani mpenzi ni simu ya muhimu sana.”
“Jamani, basi wahi kurudi,” Lily alisema huku akijikunja kutokana na kunyemvuliwa na wadudu wadogo wadogo.
MJ alinyanyuka na kwenda kuzungumzia sebuleni kwa sauti ya chini.
“Halooo Sweet.”
“Bebi upo wapi, mbona nyumbani haupo?”
“Nipo club.”
“Upo club gani nikufuate, nimefika usiku huu na ndege siwezi kwenda nyumbani mpaka nikuone na unipe raha zangu nilizozimisi kitambo.”
“Kwa hiyo tukutane wapi?”
“Popote, utakapotaka kama kwako nikusubiri au hotelini?”
“Nikukute Prinsess Motel.”
“Utanikuta nimechukua chumba kabisa yaani nina hamu na weeewe.”
Baada ya kukubaliana MJ alijikuta amesimama kama mnara asijue akamwambie nini Lily kwani alikuwa kwenye hali mbaya alihitaji msaada wake kumrudisha kwenye hali nzuri.
Kwa mahanjamu aliyokuwa nayo Lily, MJ alijua kama atampa huduma ya kwanza lazima angekesha na anapokwenda lazima atachelewa pia angeonekana katumika.
Alirudi hadi ndani na kwenda kwenye nguo zake na kuanza kuvaa. Lily alishtuka na kumuuliza.
“Vipi sweet mbona hivyo?”
“Aisee kuna kazi inatakiwa kufanyika usiku huu ni mimi tu niliyekuwa nimechelewa kufika.”
“Jamani mpenzi waambie wenzako muifanye kesho. “
“Bebi kazi hiyo ndiyo inatupa jeuri ya mimi na wewe kufanya yote haya.”
“Basi nipe hata chozi la mnyonge, hali ni mbaya,” Lily alilalamika alikuwa kama kachambia pilipili.
“Bebi nachelewa wananisubiri,” MJ alisema huku akivaa haraka na kwenda kumbusu Lily aliyekuwa kwenye hali mbaya.
“Jamani mpenzi waambie wenzako muifanye kesho. “
“Bebi kazi hiyo ndiyo inatupa jeuri ya mimi na wewe kufanya yote haya.”
“Basi nipe hata chozi la mnyonge, hali ni mbaya,” Lily alilalamika alikuwa kama kachambia pilipili.
“Bebi nachelewa wananisubiri,” MJ alisema huku akivaa haraka na kwenda kumbusu Lily aliyekuwa kwenye hali mbaya.
***
MJ alionekana baada ya wiki na kusingizia alikuwa amesafiri nje ya nchi kutokana na simu yake kutopatikana hewani. Lily aliamini kabisa MJ alikuwa nje ya nchi.
Tabia za MJ kila kukicha zilikuwa zikimtesa Lily, hata haki ya kitandani hakuipata kama zamani, ilionesha huanza kutumika kwa wanawake wengine ndipo huenda kwake.
Mara nyingi amekuwa akiachwa njiani na MJ ambaye huonekana amechoka hata akijitahidi kumuamsha mnara ilishindwa kusoma network ulikuwa chini.
Siku zote Lily alimvumilia MJ kwa vile alikuwa akimpa kila alichotaka. Lakini karaha za mapenzi zilikuwa kubwa sana zisizo vumilika. Siku mmoja wakiwa katika maandalizi kuupanda mnazi wa raha, simu ya MJ iliita. Kama kawaida aliomba radhi na kunyanyuka kitandani akimwacha Lily na hamu zake.
MJ alikuwa ameitwa na demu wake mwingine ambaye naye alikuwa nazo.
“Jamani mpenzi mateso gani haya?”
“Bebi nakuja leo narudi.”
“Lakini kumbuka unanitesa, zimepanda wewe unaondoka, huna hata huruma jamani,” Lily alilalamika mpaka machozi yalimtoka.
“Narudi mpenzi sichukui hata dakika tano.”
“Mmh! Mimi nitafanyaje,” Lily alikubali shingo upande.
MJ alivaa pensi tishat na sandoz na kutoka kuelekea alipoitwa. Alipotoka Lily hakukubali alipitia gauni la kulalia bila kuongeza kitu ndani. Kuvaa viatu au ndala aliona anachelewa, alimfuatilia kwa nyuma. Kuchukua gari lake aliona mpango wake atavurugika alitoka hadi nje na kukodi teksi na kumfuatilia MJ ili ajue anakwenda wapi.
Baada ya mwendo mrefu kidogo alimuona MJ akipaki gari pembeni ya gari lingine. Baada ya muda alimuona msichana aliyekuwa amevaa nusu uchi akitelemka kwenye gari iliyokuwa imesimama na kuingia kwenye gari la MJ.
Alitulia kuangalia baada ya kuingia yule msichana MJ ataelekea wapi. Alipanga kama anakwenda hotelini basi fujo atakazomfanyia lazima uhusiano wake na Mj ufe siku ile, kwani alikuwa amechoka kugeuzwa futio la miguu.
Alitulia zaidi ya robo saa kusubiri gari la MJ liondoke, lakini alishangaa kuona muda unakatika bila gari kuondoka wala mtu kutoka. Alijiuliza anafanya nini muda wote wasiwasi wake ilikuwa labda anafanya biashara zake.
Kilichomshtua zaidi ni mavazi ya yule msichana alivyovaa ya nusu uchi. Wazo la kufanya mapenzi kwenye gari hakuwa nalo. Alimweleza dereva waendelee kusubiri mpaka waone mwisho wake. Baada ya nusu saa alimuona yule msichana akishuka nguo yake ikiwa imepanda upande mmoja na kalio moja kuwa nje. Kingine kilichomshtua alikuwa ameshikilia kufuli mkononi kuonesha kwenye gari kuna kitu kilikuwa kikiendelea.
Kabla hajafika kwenye gari lake MJ alimwita aligeuka wakati huo MJ alikuwa ametelemka na kumfuata yule msichana.
Alimsogelea na kumla denda na kuanza kupapasana huku MJ akizinyanyua nguo za yule msichana na kumfanya abakie makalio nje na kuonyesha hakuwa na kitu kingine zaidi ya kufuli alilolishika mkononi.
Lily roho ilimuuma sana, alishangaa kuwaona wakiingia kwenye gari la yule mwanamke na kupoteza tena zaidi ya dakika ishirini, Lily akiwa anashuhudia.
Wazo la kwenda kufumania alikuwa nalo lakini wasiwasi wake uwezo wa yule mwanamke. Pia ilionesha ni mwanamke wake wa muda mrefu hivyo asingefanya lolote. Alijikuta akimkumbuka Shuku na kujuta kujiingiza kwa MJ mwanaume mwenye tamaa ya wanawake.
Baada ya muda MJ alitelemka kwenye gari akiwa amesahau kufunga zipu. Aliishika suruali kwa mkono na kuingia ndani ya gari lake. Baada ya muda magari yote yaliondoka kwa kila moja kufuata njia yake.
Lily roho ilimuuma na kulia peke yake kilio cha kwikwi. Dereva wa teksi alishtuka kumuona akilia huku akiwa hajui nini kilichokuwa kikiendelea. Muda wote alikuwa akishangaa matukio aliyoyaona hata vazi la Lily lilimshangaza kuvaa gauni la kulalia bila kitu ndani tena bila hata viatu.
“Dada vipi?”
“Inatosha leo atanitambua,” Lily alisema kwa hasira.
“Yule ni shemeji?”
“Siyo muhimu kujua naomba unirudishe nyumbani.”
Dereva hakumjibu kitu aligeuza gari na kumrudisha alipomtoa. Walipofika Lily aligundua hakuwa na fedha alitoka yeye kama yeye bila kuchukua hata senti tano.
Alimuomba dereva akachukue fedha ndani huku akimweka dereva katika wakati mgumu kutokana na nguo aliyokuwa amevaa dodo zilizo jaa na kusimama vyema kifuani na makalio yaliyokuwa wakipishana wakati wa kutembea kama abiria wa Mbagala wakigombea kuingia ndani ya daladala zilimuweka kwenye wakati mgumu dereva wa teksi.
Baada ya kumpa chake alirudi ndani kuendelea msiba wake. Baada muda akiwa amejilaza kitandani akilia, MJ alirudi na kwenda moja kwa moja kwa Lily akiwa ameisha vua nguo na kujilaza pembeni yake.
“Bebi nini tena? Usilie nimerudi.”
Lily alitamani kumfukuza lakini alishindwa kwani hali yake kwa siku ile ilikuwa mbaya shetani mpenda shari alikuwa amepanda alitakiwa kushushwa. Alipanga baada kuzishusha ampe ukweli na kisha kila mtu ashike hamsini zake.
“Mpenzi mbona unanitesa hivi?” Lily alilalamika.
“Jamani si nimerudi.”
“Basi nipe raha zangu,” Lily alilalamika kama mtoto wa paka mwenye njaa aliyemuona mama yake. Kwa kinyaa alichokiona kama si kuzidiwa na mahanjamu asingekubali kuutoa mwili wake kwa MJ, kwa vile alijua anakula makombo japo harua haina makombo.
Kutokana na kuzidiwa na kiu ya dafu, Lily aliuvamia mnazi wa MJ ulikuwa umeinama na kuuupa mshikemshike, haukuchukuwa kunyanyuka. Aliurukia mnazi kama nyani mzoefu, hakusubiri usimame vizuri aliuparamia hivyohivyo.
MJ naye hakuwa mbali alianza kumsindikiza taratibu Lily aliyekuwa akitatalika kama bisi kwenye kikaango cha moto. Kutokana na kushikika hakutaka kutoa pasi baada ya kuuchukua mpira toka upande wa goli lake na kukimbia nao huku akiwapita mabeki waliokuwa wanamsindikiza.
Lily aliingia ndani ya kumi na nane na kutazamana na golikipa.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media