
Mtunzi: Ally Mbetu 'Dr Ambe'
SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Kutokana na kushikika hakutaka kutoa pasi baada ya kuuchukua mpira toka upande wa goli lake na kukimbia nao huku akiwapita mabeki waliokuwa wanamsindikiza.
Lily aliingia ndani ya kumi na nane na kutazamana na golikipa.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Wakati anakiandaa kupiga bao ghafla chombo cha MJ kilizimika ghafla na kumfanya Lily apige kelele za kukatishwa raha zake zilizokaribia kuwa utamu.
“Jamaniii, MJ ndo nini?”Lily alilalamika kama mtoto aliyenyang’anywa pipi.
Kwa haraka aliruka toka juu ya mnazi na kujitahidi kuunyanyua chuma kikiwa bado moto. Lakini ilikuwa kazi ngumu kila alivyojitahidi ilikuwa kazi bure. Alijikuta akitumia zaidi ya nusu saa kutaka kuunyanyua mnazi kwa kila mtindo anaoujua huku jasho likimtoka, kwa kupapasa kunyonya kuugusisha hasi na chanya lakini wapiii! Mtalimbo uliendelea kulala dolo.
“MJ unanifanyia nini lakini? Kama hunitaki si ungeniambia kuliko kunipaka upupu ushindwe kunikuna ni mateso gani haya jamani,” mtoto wa kike alilia madafu.
“Siyo sikutaki bali hali ndiyo ilivyokuwa hata mimi sikutegemea,” MJ alijitetea.
“MJ umetumika?”
“Sijatumika mpenzi wangu ni uchovu tu.”
“Muongo umetumika!”
“Sijatumika mpenzi.”
“MJ mbona unanitoa thamani hivyo? Yaani utumike kwa wanawake zako kwanza ndipo uje unipake makombo?” Lily alizidi kulalamika kwa uchungu huku hamu zake zikiwa juu.
“Hakuna mpenzi ni uchovu kazi zetu nazo zinatuchosha sana,” MJ alijaribu kujitetea.
“MJ usiniudhi, biashara gani ya kufanya ngono na wanawake kwenye gari?”
“Sasa nani kafanya mapenzi kwenye gari?” MJ alijifanya hajui kitu.
“MJ mi si mtoto mdogo, ninachokisema kikuhadithiwa bali nimekishuhudia mwenyewe kwa macho yangu.”
“Lily umeshuhudia wapi?”
“Kwani leo ulienda wapi?”
“Kwenye biashara zangu.”
“Na yule mwana mke uliyefanya naye ngono kwenye gari lako kisha mkahamia kwenye gari lake?”
“Mwanamke! Mwanamke gani?” MJ alijifanya kushangaa.
“Unaniuliza mimi wakati wa kufanya uchafu wenu tulikuwa pamoja?”
“Wee nani kakwambia uongo huo?”
“Usingekuwa uongo kama ungekidhi haja zangu, jamani kumbe kila siku naachwa njia panda kumbe kuna watu wanaokutumia kisha unamalizia kunisha makombo.
“MJ kama ulijua bado una hamu na wanawake zako kwa nini umenitoa kwa Shuku?”
“Lily mbona umefika mbali.”
“Siyo mbali, MJ sikutegemea mwanaume mchafu kiasi hiki, yaani unatoka kwa wanawake zako ndiyo unakuja kwangu, mimi Lily? Hata siku moja haitatokea tena.
“Sikiliza MJ, sijafikia hatua ya kuteswa kiasi hiki, jamani kila siku nakuwa kama nichambia pilipili na kuniacha njia panda maji moto na vidole ndivyo vimekuwa wapenzi wangu kuna faida gani kuwa na mwanaume kama wewe?” Lily alisema kwa sauti ya kilio huku akimwaga chozi.
“Lakini Lily unakosa nini kwangu?”
“MJ kumbe unaninyanyapaa kwa ajili ya kuwa napata kila kitu? Basi unajidanganya sana. Kuanzia leo huu mwili utaona kama kituo cha polisi kwa muuza bangi.”
“Kama umeamua poa.”
“Nilijua lazima utasema vile kwa vile una shehena ya wanawake.”
“We si umeamua poa.”
“Na si kuugusa mwili huu naomba kila mmoja ashike ustaarabu wake.”
“Hata hiyo haina noma.”
“Poa, ukitoka hapa tusijuane siwezi kuna na mwanaume malaya kama wewe.”
“Umalaya umeuona kwangu, usingekuwa malaya usingemuacha Shuku.”
“Nakuapia nitamtafuta Shuku kwa gharama yoyote ili kurudisha penzi letu la kweli kuliko wewe tapeli mkubwa.”
“Kwa taarifa yako Shuku ameoa,” MJ alimkatisha tamaa Lily.
“Hata akioa haikuhusu.”
MJ hakulala kwa Lily aliondoka usiku ule na kwenda kulala kwake. Lily alibakia na mateso yake na kuamua kuchemsha maji ambayo kidogo yalimsindikiza mpaka kupata usingizi kwani hali ilikuwa mbaya. Alikuwa kama mtu aliyechambia upupu na mkunaji alikuwa amekatika kucha. Baada ya kupewa kampani na maji moto kama mzazi aliyejifungua aliapa kumtafuta Shuku kwa gharama yoyote.
*****
Shuku baada ya kutoka kwa MJ aliamua kuhama kabisa eneo alilokuwa akiishi na kuhamia sehemu ambayo hakumweleza mtu aliamua kuishi maisha yake. Baada ya kutulia kwa muda aliingia kwenye kazi ya kulangua mazao na kuyauza sokoni Kariakoo kwa vile alikuwa na mtaji wa kutosha toka kwa MJ.
Maisha yake kila kukicha yalimnyookea, aliweza kuyaendesha maisha yake bila kumtegemea mtu yoyote. Lily akiwa na dada yake sokoni Kariakoo alishtuka kumuona mtu kama Shuku akiwagawia watu fedha baada ya kushusha mazao kwenye gari.
“Shuku,” alimwita kwa sauti ya mshtuko.
Shuku bila kuitikia japo sauti haikuwa ngeni aligeuka na kumwangalia anayemwita na kukuta ni Lily.
“Vipi Lily?”
“Samahani Shuku nina mazungumzo na wewe.”
“Ngoja nimalize kazi yangu.”
“Hakuna tatizo nakusubiri.”
“Sawa.”
Lily alisogea pembeni kumsubiri Shuku huku akishangaa kumuona akiwa katika afya zuri zaidi kuliko ya awali. Kingine kilichomshtua na fedha nyingi aliyoshika mkononi aliyokuwa akiwagawia watu walionekana wakivuja jasho baada ya kazi nzito ya kupakua magunia kwenye gari.
Baada ya kugawia washusha mzigo alimwita dereva wa gari.
“Saidi unanidai shilingi ngapi?”
“Laki mbili.”
Shuku alihesabu laki mbili na kumpatia dereva kisha alirudisha fedha iliyobakia kwenye pochi na kumfuata Lily aliyekuwa haamini hali aliyomkutana nayo tofauti na alivyofikiria.
Kilichomshangaza zaidi ni kauli ya MJ kumshangaa rafiki yake kuondoka kwa ajili ya mwanamke na kuacha gari na fedha taslimu milioni kumi. Aliamini hasira zake ndipo zilingemfanya arudi katika maisha ya kubangaiza na kuchoka kama mpira wa makaratasi.
Baada ya kusogea kwa Lily alimsalimia.
“Za siku?”
“Nzuri sijui wifi hajambo?”
“Halafu nikujibuje?”
“Kama hajambo au tayari anakula udongo?”
“Kwa kweli sina jibu, vipi MJ hajambo?”
“Mmh! Yule mwanaume hafai.”
“Kwa nini?”
“Yule mwanaume malaya hatari.”
“Umejua leo?”
“Hata sijui, unajua alinieleza mengi kuhusiana na wewe. Kwa kweli aliyonieleza yaliuumiza sana moyo wangu. Lakini kumbe alitengeneza uongo.”
“Uongo upi?”
“Kuwa wewe unamtegemea na pia una tabia ya kuwatia wanawake mimba na kukimbia, eti mpaka unakwenda kwake ulikuwa umekimbia mimba nne.”
“Aisee,” Shuku alijikuta akiangua kicheko.
“Usicheke Shuku, MJ amekusema mengi mabaya lakini kumbe ilikuwa njia ya kunipata.”
“Lakini imekusaidia leo una gari na nyumba tatizo lipo wapi?”
“Nimeamua kuachana naye.”
“Halafu.”
“Nirudiane na wewe.”
“Mmh! Mbona ngumu.”
“Usifanye hivyo Shuku japo nasikia umeoa lakini bado nakupenda.”
“Lily sina gari sina nyumba tutaishije, nami kabwela?”
“Nisamehe kwa maneno yale ilikuwa hasira tu, Shuku nipo radhi kuishi maisha yoyote ili tu nisikupoteze mpenzi wangu. Nipo tayari kuuza magari yangu yote ili kukuongezea mtaji kwenye biashara zako nami kuwa mama wa nyumbani.”
“Lily kwa vile nipo kazini nitafute baadaye tutazungumza vizuri.”
“Shuku nipo tayari kukusubiri muda wowote.”
“Hapana nipe nafasi nifanye kazi, nimekwambia nitakutafuta kwa hiyo vuta subira.”
“Sawa nimekuelewa.”
Lily aliondoka na kumwacha Shuku akiendelea na kazi zake, wakati huo gari lingine kutoka shamba lilikuwa likiingia.
****
Shuku akiwa anamalizia kazi alijiuliza maswali mengi juu ya kutafutwa na Lily mwanamke aliyemshusha thamani. Hakutaka kuumiza kichwa aliendelea na kazi zake na baada ya kazi aliamua kurudi zake nyumbani kupumzika kwani alikuwa amechoka sana baada ya kufanya kazi kwa wiki mbili bila mapumziko.
Kutokana na uchovu alisahau hata kuwasiliana na Lily, kwa vile hakupenda usumbufu baada ya kuoga na kula alipanda kitandani na kuzima simu zote kabla ya kulala. Toka Shuku aondoke kwa MJ hakuwa na mwanamke mwingine, alitulia atengeneze kwanza maisha yake, hivyo alikuwa akikaa na kulala peke yake, akili yake aliiekeleza kwenye kutafuta ili asiipate aibu kama iliyomkuta kwa swahiba wake MJ.
Upande wa pili Lily alitegemea kupata simu kutoka kwa Shuku, lakini muda ulikatika bila kuona simu ikiingia. Aliamua kumpigia baada ya kuona muda umekwenda sana, lakini alipopiga simu haikuwa hewani.
Lily alijikuta akichanganyikiwa na kuona kama Shuku ameamua kumpotezea. Alijikuta siku ile inakuwa chungu kwake kitanda kilikuwa kichungu alitapatapa kitanda kizima kama mzazi mwenye uchungu. Hakukubali kila dakika alipiga simu ya Shuku ambayo haikuwa hewani.
Lily alijikuta akikesha kuitafuta simu ya Shuku iliyokuwa haipatikani. Hakujua kama Shuku baada ya kutoka kwa MJ alibadili hata namba ya simu ili tu asiwasiliane na MJ.
Lily baada ya kumkosa kwenye simu aliamka siku ya pili asubuhi kwenda kumtafuta Shuku. Baada ya kuoga bila kutia kitu kinywani alielekea sokoni Kariakoo kumtafuta Shuku. Alipofika sehemu aliyomkuta Shuku jana yake alimtazama huenda atamuona.
Magari yaliyotoka shamba aliyaona yakipakuliwa, lakini Shuku hakumuona. Alijikuta akikaa zaidi ya saa mbili bila kumuona. Ilibidi amfuate kijana mmoja aliyekuwa pembeni ya gari akijifuta jasho baada ya kumaliza kupakuwa mizigo.
“Samahani kaka yangu.”
“Bila samahani dada yangu,” jamaa alijibu kwa ustaarabu kwa kujua labda anatafutwa mtu wa kumbebea mizigo yake.
“Eti kaka yangu, Shuku yupo wapi?”
“Shuku Zungu la roho?”
“Yule aliyekuwa akisimamia upakuaji wa gari la mazao jana.”
“Ndiyo huyo Zungu la roho.”
“Kwa nini mnamwita hivyo?”
“Yule dada ukifanya naye kazi utafurahi, wote tunapenda kufanya naye kazi.”
“Kwa nini?”
“Yaani hata siku akiwa hana kazi ukikutana naye akimuomba hela anakupa, pia hata kazi zake hana longolongo kwenye malipo.”
“Kwani yeye huwa anafanya kazi gani hapa?”
“Yule jamaa, zamani nakumbuka tumepiga naye sana kazi hapa kijiweni. Baada ya muda alipotea na kurudi akiwa na fuba la maana na kuanza kufuata mazao shamba. Alianza na gari moja sasa anapiga mpaka gari sita peke yake.”
“Kwa hiyo, hiyo ni kazi yake au ameajiliwa?”
“Yake mwenyewe, tena nasikia kuna mkoko wa nguvu anavuta muda si mrefu.”
“Usiambie!” Lily alishtuka.
“Dada kweli anayetoa Mungu humpa, yule jamaa ni zungu la roho kweli tofauti na wengine.”
“Leo mbona simuoni?”
“Mmh! Sidhani kama leo atakuja.”
“Kwa nini?”
“Jana kamaliza mzigo naona leo anapumzika kisha anaingia shamba.”
“Shamba kufanya nini?”
“Kukusanya mazao, wiki mbili zote alikuwa akija mjini alfajiri na kurudi kwake jioni.”
“Sasa nitampataje?”
“Labda uende kwake, zaidi ya hapo sijui namna ya kumpata.”
“Huna namba yake ya simu?”
“Mmh! Sina.”
“Kwake unapajua?”
“ Napajua, kwani we nani yake?”
“ndugu yake, naomba unipeleke.”
“Sister si unajua ndo gari la kwanza.”
“Una maana gani?’
“Yaani nikiondoka huku nyuma kazi zitanipita.”
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media