
Mtunzi: Michael Mejah
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Happy alikuja kwa madoido mpaka pale mlangoninikiwa bado nimeshikilia kitasa alisogea na kuanza kunipa romance huku akilegeza macho nasauti ya kudeka huku mkono mmoja ameuweka kifuani, niliganda kama mnara ila nilikuja kushtuka alipoweka mkono wake usawa wa zipu na kutafuta dick yangu lakini hakuöna kitu,
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
alinyong'onyea ghafla na kuvuta pumzi uuuuuuuuh! Na kujitupa kwenye sofa puuu!"dick kwanini ukuniambia kama una tatizo?"nitaanzia wapi mpenzi wangu?"kwani ulitembea na mke wa mtu?""hapana happy ni story ndefu kidogo""haya njoo keti unieleze kinagaubaga""happy miezi mitatu sasa nipo katika hali hii, nakumbuka tatizo lilinipata nikiwa kikazi sumbawanga nilikutana na mganga aliyekuwa anafanya maajabu na mimi nikajikuta nakubali kubadilishwa jinsia kama mchezo lakini ghafla yule mganga alianguka palepale na kufa ndo mwanzo wa tatizo aliyeniroga ameshakufa""usiseme hivyo mpenzi mimi nitakusaidia kukupeleka kwa mtaalamu""mtaalamu! Mtaalamu yupi huyo wa wapi?"yupo bagamoyo uwezi amini tokea nipo form 4 hadi leo nimekuwa nikienda kwake hajawahi kushndwa mpaka leo unaniona chuo namtegemea yeye""sasa tunafanyaje?""kesho asubuhi sana tuamkie bagamoyo inabidi ulale hapa leo, weka alarm mapema tuanze safari"
***
Tulilala usiku ule mimi na happy lakini kama kaka na dada. Ule usiku niliota nimelala na mwanamke lakini ghafla nikaamka na kwenda kuchukua kisu jikoni nikarudi taratibu na kumchoma cha shngoni, palepale ile ndoto haikuendelea nami sikushtuka.Saa kumi na moja alarm ikaanza kuita kama mara mbili nikawa naona uvivu kuamka ila ile mara ya tatu niliamka mara nilitazama pembeni yangu."khaa! Hiki nini tena ooh my God!!
.Sikuamini macho yangu baada ya kukuta mwili wa happy ukiwa umeuliwa kikatili na bisu la shingo hata kuangalia mara mbili sikuweza. "ni nani ameingia humu ndani na kufanya ukatili huu? Binadamu sisi mbona hatuna utu jamani mtu unamuua binadamu mwenzio? Lakini huyu mtu kapitia wapi? Ina maana bila kushtuka now ningelala na maiti mpaka asubuhi?" nilinyanyuka na kukaa pale kitandani nikiwa na ujasiri mkubwa sana kwani kwa kawaida mtu yeyote angeanza kuchanganyikiwaÃla nikakumbuka mara ya mwisho niliota ndoto lakini matokeo ya ile ndoto niliua OMG! itakuwa ni mimi nimeua na ni jini sadia huyu mwanamke sijui ananitafutia nini?"sasa hapa nifanye kitu kimoja nichomoe hili bisu shngoni ili nisije kukamatwa kwa uwepo wa ushahdi" nilifumba macho na kuhesabu moja mbili taaaatu! Fyooooo, eeh jamani.
Tayari nilishaipata barabara kuu na nilikuwa naitafuta sinza sikujua kwanini naenda sinza lakini nilikuwa kama mtu aliyeshanganyikiwa haswaa. Nilipaki gari langu sinza makaburini ilikuwa ni alfajiri sana kisha nikazima gari na kuwasha taa ya ndani hapo nimechoka hatari."hivi ni nini malengo ya kufanya haya mauaji? Mimi nimeshakubaliana na matokeo sina maumbile yangu sawa nitaishi nitakavyojua lakini nakubalije kuendesha na lile zombi shenzi sana lile shetani"Nilitukana sana na kumchukia yule jini kwani ameniharibia maisha yangu sana.
Wakati nipo pale nikaanza kupata concept nzima ya lile tukio. Inavyoonekana yule jini alinichezea akili yangu kuwa lile tukio nilione kama ndoto kumbe naua kweli alafu baada ya kuua nilale na maiti mpaka asubuhi nitakapokamatwakirahisi kwasababu tulilala mapema jana yake lakini asubuhi nilikuwa na uchovu sana kumbe inawezekana ile mara ya tatu alarm inaita ningeendelea kulala uenda yangenikuta makubwa zaidi. Nimegundua kitu hapa huyu jini mimi anipendi kama anavyosema na ndio maana anataka niingie matatizoni.
Lakini sawa nitapambana mpaka mwisho."kaka mbona leo asubuhi sana kuna nini tena?""kaka we acha tu ebu tuingie ndani nikueleze vizuri" niliongea na rafiki yangu richard baada ya kufika kwake kama saa kumi na moja na nusu."sawa kaka nimekuelewa lakini kwa hapo naona kabisa una wakati mgumu cha kufanya ni kukata tiketi alaka kwenda dubai kwa sista mery kama unaenda kuchukua mzigo wa biashara yetu""dah kaka nashukuru sana kwa kunipa wazo zuri lakini nitamwambia nini wife""we achana na hayo mambo fanya nilivyokwambia kaka usipoteze muda, kama happy amekufa jeshi la polisi litataka kujua chanzo cha kifo chake na wataanza kufanya uchunguzi hapo ndipo utakapo tiwa nguvuni sasakabla hayo hayajakukuta ebu ondoka mapema"
***
Nilimaliza mipango ya visa na kila kitu nikawa nimekata tiketi ya kwenda dubai lakini nitapitia egypt kisha doha na kuingia dubai ni safari ya karibia siku nzima. Mke wangu na rafiki yangu richard walinisindikizahadi airport kisha nikaagana nao nikaingia hadi sehemu ya ukaguzi nikapita na kuingia chumba maarumu ya abiria wanao subiri ndege ya kwenda dubai. Tulikuwa abiria wengi mno na pale zilibaki dakika 15 kabla ya kuingia ndani ya ndege. Nilienda chuoni mara moja wakati namaliza kujisaidia haja ndogo maraaskari akaja sijui alijitambulishausalama wa taifana kuniambia nipo chini ya ulinzi nikasurender huku nikimlia timing na kweli akanipa upenyo nilimpiga ngumi kama nane za usoni kisha nikamkalisha kwenye sink la choo kama anajisaidia haja kubwa nikafunga mlango huyo nikaondoka wakati huo abiria walikuwa wanaingia ndani ya ndge na mimi nikajifunika na koti langu nikazama ndani ya ndge kabla ndege haijaondoka mara wale jamaa wa usalama walikuwa wanaranda randa nje mara wakaingia ndani ya ile ndge hapohapo mapigo ya moyo yalinienda mbio
Walianza kuangalia mule ndani kwa muda mfupi kisha mmoja akatoka na mwingne akawa bado anatazama tazama vizuri lakini nae akatoka wakati wapi nje alitokea mkuu wao sijui yule akawaamuru warudi tena ndani ya ndege wakague pass zetu za kusafiria maana tayari lile tukio alishaliona kwenye camera maalum zilizofungwa kila sehemu. Walirudi ndani tena wakati huo tumbo joto kama nimebeba madawa ya kulevya yani nilikuwa na hofu kubwa sana.
"kaka unaweza kutupatia pass yako ya kusafiria samahani kwa usumbufu""aah pass sawa hii hapa"Yule jamaa aliitazama sana tofauti na viti vyote alivyopita mwanzo au hata jirani yangu kisha akanirudishia akaenda nyuma zaidi alipomaliza akarudi tena kwangu."jamani vipi tena mnataka niwape tena pass yangu au?""kaka kama tunakutilia mashaka unaweza kuambatana nasi kwa dakika2 mpaka kwenye chumba chetu cha uchunguzi nadhani haitakusumbua sana unaweza kuasha mizigo yako""mbona sielewi kuna kipi hasa mpaka nikafanyiweuchunguzi ina maana nimeingiaje ingiaje hapa?"Mama wee wakaingia wale askari wa jeshi la polisi wa kawaida wakanitia nguvuni na kunipiga pingu mikoñoni."jamani mnanikamata nina kosa gani?""twende wewe unajaribu kuikimbia serikali? Ina mikono mirefu muuaji mkubwa wewe"
***
"Jamani mtaniua bure mimi sijui chochote""na hiki kitambulisho ni cha nani? Tumejaribu kuchunguza tukakuta kuna kitambulisho hapa katika nyumba aliyokuwa anaishi marehemu ebu tuambie ukweli kabla hatujakulazimisha useme""kwakweli afande happy alikuwa ni mpenzi wangulakini mimi nimeoa tayari na muda sasa tumekuwa hatuna mahusiano najua hapo kuna mtu amefanya mauaji na kuasha kitambulisho changu""je siku ya tukio ulikuwa maeneo gani?""nakumbuka nilikuwa bar mpaka saa kumi usiku nikalala guest na kesho yake nilirejea nyumbani""haukulala na happy wewe kisha ukatimiza matakwa yako kisha ukamuua?""hapana afande sikufanya hivyo""una ugomvi na nani?""hapana sina ugomvi na mtu nashangaa kwanini wamenifanyia hivi?""aah unadhani inaingia akilini hata ungekuwa ni wewe dickson unaambiwa hivyo ungemuelewa huyo mtu?"
***
Hakuna maisha magumu kama mahabusu yani kulikuwa na harufu mbaya na pia kulikuwa na giza muda wote ila nakumbuka siku ya nane toka nipo mule ndani alinitokea yule jini na kuniambia atanitoa mule ndani kwa kuigeuza ile kesi kwani yeye ndiye aliyeitengenezana ndio atakayo imaliza.Asubuhi yake nilikuja kuitwa na kuambiwa nimeashiwa kwa dhamana aliyenikatia dhamana simjui lakini sikutaka kuuliza ila niliambiwa siku yakusomwa kesi natakiwa niwepo mahakamani nikamshukuru sana mungu nikapewa vitu vyanguna kuondoka.Nilikuwa nikuhudhuria ile kesi mpaka nikaona kama haina nguvu tena hata watu pia waliisha kuja kusikiliza ile kesi mpaka nilipoambiwa na mahakama nipo huru.Sikuwa na la kumficha mke wangu nikamweleza yote yale ndo akanileta kanisani.
"jamani wapendwa napenda kuwaambia mungu yupo hayo ndo maisha yangu niliyoyapitia namshukuru mungu kwa kunipa mke muelewa kwa yale yote bado alikuwa mvumilivu kwangu, nakumbuka siku ambayo narudishiwa jinsia yangu niliambiwa na yule jini sadia kuwa nikutanenae daraja la salenda saa 9 usiku kwa lengo la kunirudishia jinsia yangu kisha nikaishi nae baharini kweli alifanya hayo yote ila baada ya hapo nikaliitia jina la bwana nilishangaa kuona kitu cha ajabu kama mwanga mweupe kisha yule jini akatoweka na kuniasha nikishangaa na tokea hapo ndo nipo huru sasa na familia yangu"Ile ilikuwa ni simulizi ndefu niliyoitoa kanisani na kuandaa kanda za kaseti na cd baada ya watu wengi kuipenda sana simulizi yangu.HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU..
MWISHO
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media