
Jina: KABURI LA KAZULA
Mtunzi: Alexis Wamilazo
SEHEMU YA KWANZA
Licha ya umasikini aliokuwa nao kijana Kazula,lakini ndoa yake bado ilionekana kukumbwa na misuko suko ya hapa na pale,kwani kila kikicha mama yake alidai mtoto,hata mke wake nae ambae aliitwa mele,alikuwa akimlaum saaana mumewe kwa kushindwa kumpa ujauzito..kitu ambacho kilimnyima furaha kazula,akajiona hana bahati..hata ham ya kufanya tendo la ndoa lilipotea kabisa..kwani aliona haina maana yeye kujamiana na mke wake pasipo mafanikio ya kumpatia mimba.
Siku zilizonga miezi nayo ikasogea,kazula akizidi kukosa amani..hatimae miaka ipatayo miwili ikapita,ambapo ilikuwa asubuhi moja siku ya juma tatu,,kimvua cha vuli kilipokuwa kinanyesha..kwenye ukungu mwepesi alionekana mama yake kazula ambae alionekana kula chumvi nyingi..alikuwa akizipiga hatua kuelekea kwenye nyumba ya mwanae huku moyoni mwake akionekana kuwa mtu mwenye neno la kutaka kumwambia mwanae.
Mama Kazula baada kuisogelea nyumba ya mwanae,ghafla alisimama baada kusikia Mele mke wa kazula akizozana na mume wake..huku maneno machafu yakiwa ndio yametawala,mele akimtukana Kazula huku akitishia kurudi nyumbani kwao.
Hakika yale ya Mele yalimsikitisha sana mama kazula,ambapo aliweza kusema na moyo wake.."Ee mungu msaidie mwanangu apate hata mtoto mmoja ili alinde heshima yake ya ndoa.." alijisemea hivyo mama kazula,wakati huo mlango wa nyumba ya kazula ulifunguliwa,ambapo alionekana mele mke wa kazula akiwa na Begi lake akirudi nyumbani kwao..,Kazula nae hakuta mke wake aondoke,kitendo ambacho aliweza kumpigia magoti ili mêle abadili maamuzi yake ya kumwacha solemba.
Lakin mele licha ya kupigiwa magoti na kazula,bado alionyesha msimamo wake wa kurudi nyumbani kwao,huku akidai hawezi kuishi na mwanaume asie weza kumpatia ujauzito.
Mele akaondoka zake.
Machozi ya masikitiko aliyadondosha kazula huku magoti yake yakiwa chini,,na hapo hapo mama yake alimsogelea kisha akamwinua..akamwambia. "Yote mtihani mwanangu,natumaini mungu atakufuta machozi yako..nyamanza acha kulia chukulia majaribu haya kama mtaji kwako.." Kazula akitokw na kwikwi,alijifuta machozi yake kisha akaketi sebleni na mama yake..ambapo waliweza kuzungumza Mambo mbalimbali ya kuhusu maisha yao,,yote hayo mama kazula alitaka mwanae asahau kile kilichotokea muda mfupi uliopita.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Wakati hayo yakiendelea..upande mwingine nako alionekana Mele akiwasili nyumbani kwao.Hivyo mama Mele alishtuka baada kumwona mwanae akiwa na begi,,kwa mshangao mkubwa,mama mele alihoji "Kuliokoni mwanangu mbona asubuhi yote hii na vifurushi??.." Mela akajibu "Njoo ndani mama Nikuulize kila kitu.." Alijibu Mele,ambapo mama Mele aiachia fagio lake kisha akaingia ndani na mwanae.
Na mala baada wote kukaa sawa..wa kwanza kuongea alikuwa mele ambapo alianza kwa kumsalimia mama yake.."Malakhaba mwanangu..haya niambie kitu kilichokufanya asubuhi yote hii kudamkia nyumbani kwenu badala kulala na mume wake.." Aliongea hivyo mama mele baada ya salam akiyopewa na mwanae.
Hivyo mele baada kusikia..nae akionekana kukunja uso wake alijibu.."Mama mume wangu hana uwezo wa kunipatia mtoto..kwa hiyo mimi nimeamua bora niachane nae tu.." Alisema Mele.
"Hapana mwanangu mimi kama mzazi wako sikubaliani na uamuzi wako kwa sababu bado hujajua tatizo lipo kwake mumewe au kwako wewe.."
"Kwangu?? ." Alishtuka mele
"Ndio kwani wewe huwezi kuwa na tatizo la uzazi??.."
"Hapana mama mimi ninauhakika kabisa sinaaa tatizo hilo.."
"kweli unauhakika mwangu??.."
"Ndio mama uhakika ninao"
"Sawa kama unauhakika huna tatizo,,basi tatizo lipo kwa mume wako..lakini tatizo hilo isiwe sababu ya wewe kumkimbia kwa sababu linaweza kutatuliwa na furaha ya ndoa yenu ikarejea.."
"Kweli mama!
"Amini mwangu cha muhimu kisho twende kwa Mzee baluguza anaweza kututatulia tatizo hilo.."
Mama na mtoto walikubaliana hivyo,,ili waende kwa Mzee baluguza,,Mzee ambae ni mganga wa kienyeji.
Kweli asubuhi ilipofika Mama Mele na Mele walielekea kwa mganga Baluguza,,ambapo walipewa dawa huku mganga Baluguza akiaminisha kabisa kuwa Kijana kazula ndio mwenye tatizo la uzazi.
"Chukua dawa hii..muwekee mumewe kwenye chakula,pia hii nyingine utauweke upande anao lala yeye kitandani..Na hakikisha asikuone pindi utakapokuwa ukifanya haya...Ivo mnaweza kuondoka.." Alisema mganga Baluguza huku akiwakabidhi dawa mbali mbali za kienyeji.
Hivyo baada mama Mele kufika nyumbani na mwanae,,hatimae alimwambia arudi kwa mumewe huku akimtaka asisahau kufanya yale aliyoambiwa na mganga Baluguza.
Kweli Mele nae akirudi akionekana mnyenyekevu,,aliweza kumwomba msamaha Kazula kuhusu yale aliyomfanyia..Kazula nae kwa moyo mkunjufu akimpokea mke wake kwa mikono miwili.
Na usiku ulipoingia,chakula kiliandaliwa..M
ele akafanya kama alivyo ambiwa na mganga Baluguza..huku yeye ili asile kile chakula aliamua kujifanya mgonjwa wa tumbo kuhara..Hivyo alimwambia mume wake ale yeye atakula mpaka pale tumbo litakapo tulia.
Kazula alikula kile chakula..Na baada kumaliza walienda kulala..lakini kesho yake asubuhi Mele alishtuka baada kumgusa mume wake na kukuta mwili ukiwa wa baridi huku ukiwa umekakamaa...Mele alipagawa haraka sana alimfunua shuka ili amtazame vizuri mume wake..Mungu wangu,mele hakuamini kile alichokiona..Kazula alikuwa amefariki..kumbe Mele hakupewa dawa bali alipewa sumu ya kumwondoa mume wake duniani.
"Nitasema nini mimi kwa mama kazula?..Hali ya kuwa kazula ndio mtoto pekee kwa mama kazula? .." Alisema Mele huku akiupapasa mwili wa kazula ili ahakikishe kama kweli kazula kapoteza maisha.
"Nitasema nini kwa mama kazula? Hali ya kuwa kazula ndio mtoto pekee kwa mama kazula?.." Hayo ndio yalikuwa maneno ya Mele baada kugundua kuwa dawa aliyopewa na mganga Baluguza imemuua mume wake.
Hivyo Mele akionekana kuchanganyikiwa
,akatoka ndani.akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwa mama yake,kwenda kumwambia juu ya kile kilichotokea kwa mumewe ambae ni kazula,,hali ya kuwa upande mwingine nako,mama kazula alionekana akitembea kuelekea nyumbani kwa mtoto wake ili kumjulia hali kama alivyo kuwa amejiwekea utaratibu huo.
Wakati huo huo Mele akafika nyumbani kwao huku akilia kwa uchungu,na mama Mele ambae aliitwa Bi kibwana baada kusikia sauti ya mwanae akilia,haraka sana alitoka ndani na kisha kwenda kumsikiliza.
Hakika Bi kibwana alitaharuki baada kumwona mwanae akilia huku akimtaja mganga alie mpa dawa,kitu ambacho kilizidi kumshtua Bi kibwana ambapo alimwambia mwanae wakae kitako ili amweleze kitu kinacho mliza.
Lakini kutokana na uchungu aliokuwa nao Mele,kwa Hakika alishindwa kusimulia kitu kilichomkuta mume wake,,hivyo alizidi kulia kwa uchungu.Bi kibwana akamshika bega kisha akamfuta machozi yaliyokuwa yakimtililika mashavuni.Ambapo baada kufanya kitendo kile,Bi kibwana alimtaka Mele anyamanze ili amsimulie mkasa ambao unamfanya atokwe na machozi.
Na hatimae Mele akanyamanza,akayafuta machozi kwenye mboni zake kwa kutumia kiganja chake. kisha kwa huzuni kubwa Mele akamwambia ukweli mama yake kuwa mganga Baluguza hakuwapa dawa ya kumtibu Kazula tatizo la uzazi,bali aliwapa sumu ya kumuuwa.
Lakini cha kushangaza,baada Mele kumwambia hivyo mama yake..Ajabu Bi kibwana alicheka sana huku akipiga vigelele,,na mwishowe akasikika akisema hivi. "Mele mwanangu..kifo cha yule kijana ambae ndio alikuwa mkwe wangu,,wala kisikupe shida..bali we furahia maisha sasa..." Alisema Bi kibwana mama yake Mele.Wakati huo Mele akiwa ameduwaa,akishindwa kumuelewa mama yake kuhusu kile alichokizungumza mama yake.
Hivyo Moyo wa Mele ulizidi kutandwa na giza nene,akijutia uamuzi alio ufanya..uamuzi wa kwenda kwa mganga wa kienyeji akiamini kuwa mganga ataweza kumpatia dawa ya kumtibu mume wake ambae ni kazula ili aweze kumpatia mimba.
Lakini yote kwa yote Mele akajikuta akimkosa mume wake pia hata ile ndoto ya yeye kuzaa na kazula nayo iliyeyuka.. Kwa Hakika Mele alilia sana huku akijiuliza kuwa ataificha wapi sura yake kijijini kwao endapo kama atagundulika juu ya kifo cha kazula?
Na kabla hajapata jibu,ghafla Mama yake aliingia ndani na kutoka,kisha akafungua fundo iliyokuwa imefungwa kwenye khanga yake..ambapo Bi kibwana alipo fungua ile fundo,alitoa kiasi cha fedha shilling elfu sita..fedha ambayo moja kwa moja alimkabidhi mwanae..baada ya hapo akasema "Mwanangu Mele..usilie sana hadi ukamkufuru mungu..kazula tayali kafa hata ukulia Sawa na bure tu,,hatorudi...kilichobaki ni kumsahau kwa maana wewe bado mschana mdogo tu hivyo umri wa kuolewa na mwanaume mwingine bado unao..tena mwanaume mwenye uwezo wa kukujaza mimba,na sio huyo aliekufa...Hivyo hela hiyo mwanangu shilling elfu sita,nakuomba nenda kijiweni kawachukue vijana wawili ongea nao vizuri waufukie mwili wa marehem mume wako,,la sivyo jela litakuhusu na kama sio jela basi utapigwa hadi ufe.."Bi kibwana alisema.Mele akashtuka kusikia suala hilo,,papo hapo akawaza na kuwazua na mwishowe akaona hakuna namna zaidi ya kumzika kazula kimya kimya bila mwanakijiji yeyote kujuwa akiwemo na mama kazula mwenye.
Na wakati Mele alipokuwa akifikilia suala hilo,upande mwingine nyumbani kwa kazula,mama kazula alipiga hodi huku akimwita mwanae ili amsabahi,,lakini kazula hakuitikia kwani alikuwa tayali amesha fariki,,hivyo mama kazula aliamua kurudi nyumbani kwake ingawa nafsi yake ikimsuta kuwa aende tena nyumbani kwa mwanae ili ajue kwanini hajaitikia baada kumwita ili amsabahi.
Vilevile,Mele nae baada kuwaza na kuwazua.hatimae akaona wazo alilompa mama yake,ni wazo nzuri ingawa roho ilikuwa ikimuuma ila ilimlazimu afanye vile..
Baada Mele kuliafiki wazo la mama yake,Mele alizipiga hatua kuelekea kijiweni kwenda kuwatafuta vijana ambao watamzika kazula kimya kimya saa za usiku,na kwa bahati nzuri aliwakuta vijana wawili wakicheza mchezo wa bao la kete..vijana hao mmoja anaitwa Solomon na mwingine anaitwa Marongo.
Hivyo Mele alipowakalibia Vijana wale,aliwaza atanzaje anzaje kuwaambia kuhusu habali ya kumzika mtu kimya kimya?
"Ee mungu nisaidie"Alijisemea Mele huku akionekana mtu mwenye hofu kubwa kama mtu aliefumwa ugoni.
Lakini yote kwa yote,Mele akapiga moyo konde kisha akamwita Marongo faragha..ambapo Marongo nae kabla ya kusimama kumfuata Mele,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media