
Mtunzi: Michael Mejah
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Nilitetemeka mwili mzima nikajisemea "ooh jesus christ help me" nikaenda ila kabla sijafika mara nikaona damu kuelekea chumba cha wageni nikafungua ule mlango kwa ujasiri wa kupambana na nitakacho kutana nacho mara fuuuupu!! Paka mkubwa mweusi amekufa sakafuni..
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
"ooh my Godness what the meaning of these?"
Niliurudisha mlango taratibu na kuanza kutafuta wapi kilipo chumba chetu nikakutana na mlango nikafungua na kumkuta mke wangu anavaa huku mtoto amemlaza kitandani.
"angel mke wangu humu ndani kuna mauzauza yani nahisi kuchanganyikiwa"
"jamani mume wangu uchanganyikiwe na lipi au bado yule jini anakusumbua?"
"nahisi itakuwa hivyo maana nilipotoka nje nikaingia moja kwa moja chumbani nikamkuta mtoto kitandani nikajua umemuasha peke yake sasa nilipokuja sebureni muda ule nilishangaa kumkuta mtoto umemuweka mgongoni nilizidi kuchanganyikiwa nikaingia jikoni kunywa maji nilipotoka nikakuta michirizi kuelekea chumba cha wageni nilipofungua nikamkuta paka mkubwa mweusi ndo nimetoka huku na kuja huku ndani bado nashangaa hiki nini"
"mume wangu unanitisha hizo ni demon spirits/roho za mashetani zinakufata mume wangu ebu twende tukamtoe huyo paka jamani mbona naogopa mume wangu"
"we twende ukaone"
Tulitoka nje ya chumba chetu mpaka kwenye kolido cha kushangaza hapakuwa na dalili ya kuwepo kwa damu wala huyo paka aliyekufa.
"yuko wapi sasa jamani"
"yani alikuwepo hapa muda si mrefu sijui ameenda wapi"
"mume wangu fumba macho tuombe ukiamini hayatakusumbua tena hayo mambo, unaamini?"
"ndio wife naamini niombee"
"tuombe, baba katika jina la yesu tunakwenda kinyume na hila zote za shetani na nguvu za giza zishindwe na kurudi kuzimu ktk jina la yesu na tunaziseka kuzimu kwa damu ya yesu, namuweka mume wangu mikononi mwako na shughuli zake pia na familia yangu mungu naomba uilinde naomba nikiamini. AMEN!!"
"AMEN!!!"
Nilipata amani kidogo baada ya yale maombi nikaoga nikala nikasali tena na kulala nikiamini ulinzi wa mungu upo pamoja nasi. Nakumbuka muda tuliolala ilikuwa saa na robo na hakichukua muda nikapitiwa na usingizi baada ya mke wangu kunipa stori mbili tatu za kule reba kipindi alipokuwa anajifungua nadhani alipoona kimya akajua nimeshalala nae akalala pia. Kwa mbali nilisikia simu yangu inaita nikafunua mto na kutoa simu alikuwa ni yule sekretari wetu ambae nilishatembea nae jana yake kazini na muda huo anapiga ilikuwa saa sita usiku sikupokea nikasikiliza pumzi za wife kwanza nikajua amelala nikapokea simu.
"hello"
"hello jamani dickson nimemisi penzi lako jamani"
"ndio najua jamani lakini si unajua nimeoa na muda huu nipo wife"
"najua lakini nashndwa kuvumilia dick unajua mapenzi me sikuachi ungekuwa muislamu ningekwambia unioe niwe nyumba ndogo"
"sawa nimekuelewa tutaonana asubuh kazini?"
"jamani basi tuchat mpenzi wangu"
"poa wangu"
Nilikata simu tukaanza kuchat kama vile tunafanya mapenzi_sex chat mpaka nikapitiwa na usingizi nikalala fofofo.
Katika ya usiku wa manane niliota nipo kwenye shamba kubwa la maua ya kila aina kwa mbali nilimuona msichana mrembo anakuja nilipo na aliponikaribia akanipita na kuendelea mbele kisha akageuka nyuma na kuanza kuniita lakini nikawa nasita kwenda mara ghafla ile ndoto ikakatika baada ya kusikia naamshwa.
"dickson amka dickson amka twende"
Nilikurupuka na kuangalia ile sauti ya kike imetokea wapi na mke wangu amelala fofofo.
Nilijisemea "inawezekana mke wangu anaweweseka, lakini mbna sijawah kumuona hata siku moja jamani?" niliwaza wee mwishowe nikapuuzia na kuendelea kulala.
Nikiwa nimelala tena nikajikuta nimeamka bila hata kujitambua nikaenda jikoni nikawa nasumbuka kufungua mlango nikawa naugonga kwa nguvu kumbe huku nyuma mke wangu alisikia zile kelele akaamka na kunifatia kwa nyuma wakati huo nilishafanikiwa kufungua ule mlango kisha nikaenda na kuchukua kisu kikubwa ili nije kumchoma mke wangu kama bahati alijibana nyuma ya mlango akapushi kile kisu kikadondoka chini akaingia kwenye friji akatoa maji na kunimwagia usoni fahamu zikarudi.
"mume wangu inabidi nikupeleka kwa mchungaji ona ulitaka kuja kuniua si unaona hiki kisu"
"dah yani mke wangu hata sielewi ni kwanini mambo haya yanatokea nahitaji msahada mkubwa sana"
"usijali mume wangu twende tukalale asubuh tutampigia mchungaji atwambie ratiba yake ili twende tukamuone"
Nililala pale kitandani na mke wangu alinikumbatia lakini bado nilikuwa naogopa sana kwakweli nilijuta sana tabia yangu ya umalaya na kupenda kutumia vitu nisivyovijua kama ile #body_spray ndo imeniletea mpaka yule jini ananitesa sana nashndwa kufanya mambo yangu vizuri.
Mauza uza yaliendelea kunisumbua ndotoni mara niliota sina maumbile yangu haikuishia hapo nilikuwa natoka sehemu na gari nikawa nakunja sehemu akapita mdada nikamgonga na palepale akadondoka na kufa palepale nilishtuka na kukaa.
"eeh mungu nisaidie nakosa raha jamani hali hii mpaka lini"
Nilinyanyuka na kwenda sebureni nikawasha tv na kuangalia hata kipindi sikukielewa ili mradi tu niangalie niepuke zile ndoto mbaya kwani nilichoka sana.
***
"mume wangu amka uende kazini muda umeshafika"
"aah nimechoka mke wangu yani nimekuja kupata usingizi saa kumi na moja yani nimechoka jamani"
"we nenda kazini ukirudi nitakwambia mchungaji alichoniambia"
Nilijiandaa vizuri kisha nikapata kifungua kinywa nikaondoka kazini, nilipofika nikamkuta yule sekretari na wafanyakazi wengine wamefika kabla sijaingia ofisini nikapewa barua ikabidi niulize imetoka wapi? Akaniambia nisome nitaona.
Sikuamini nilikuwa na safari ya kikazi ya kwenda sumbawanga nilifurahi sana kwani trip za mkoani zinakuaga na hela sana na ile safari nilitakiwa niende na judith msichana anadeal pia na mambo ya masoko.
***
Tulichukua ndege mpaka sumbawanga tukapanga hotel moja na judith sema vyumba vilikuwa tofauti nilijiona kama nipo sayari nyingne maana hotel ilikuwa ni nzuri sana nilimuita judith nikafungua laptop tukawa tunafanya mahesabu ya kiasi tutakachotumia tukiwa pale na pesa waliyotoa kampuni pia tukagundua tunatoka pale na faida kubwa tulicheka na kugonganisha mikono. Wakati huo tuliangalia kazi yetu ya kesho. Wakati huo nilishamuonyeshea judith dalili zote za kumtaka na yeye akawa anaelekea kabisa.
Kesho yake niliamka asubuhi nikaanza kazi iliyotuleta pale kwa siku 8 nilifanya kazi na kupita ofisi kama nne nikawa nafanya tafiti za hapa na pale, ilipofika kama michale ya saa kumi jioni niliingia hotel moja jirani nikapata chakula wakati nipo pale nikaona watu wa mazingaomba wanafanya mambo yao. Nilisogea na kuanza kuangalia.
"haha kaka njoo hapa ndio wewe uliyevaa suti njoo"
Nilisogea na kumsikiliza alichokuwa anakisema na watu walikuwa wanashangilia.
"huyu jinsia gani?"
"mwanaumeeeeeee" wote wakajibu
"sasa nataka nimbadilishe ili muone mimi noma"
Watu walitulia kuniangalia waone nitabadilika kweli, yule mwanamazingaombo alianza kunipuliza na kuniomba niteme mate kwenye kopo nami nikafanya hvyo.
"haya weka mkono ushke maeneo yako"
"mama yangu mganga nirudishie jinsia zangu sitaki hayo mambo"
Kabla hajataka kunirudishia jinsia yangu mara radi ikapiga ghafla watu wote walikimbia wakati yule mganga akitapatapa na kutoa povu mdomoni na puani.
Nilidhani inaweza kuwa ni hadithi ambayo bdo msimulizi alikuwa anaendelea kuahadithia lakini sikuweza kutoa mkono wangu ndani ya suruali yangu hali iliyozidi kunitia uchungu nikajikuta natokwa na machozi kwa nilipoteza sifa zote kama mwanaume.
"ebu tazama nimebaki haya mavazi ya kiume lakini si mwanaume nitamwambia nini mke wangu? Je jamii itanichukuliaje? Huu ndio mwanzo wa kukimbiwa na mke"
Nilitafakari moyoni nikajenga hoja na mawazo kedekede pamoja na maswali yasiyo na majibu nikatazama hata kuona kama kuna mtu aliyeniona jinsi nilivyokuwa nateseka lakini hapakuwa na mtu zaidi ya waliokuja kutoa ule mwili wa yule mwanamazingaombo na kuondoka zao wakiwa bize na mambo yao. Ebu tazama jambo ili lilivyogusa moyo wangu au ni jini sadia ameamua kunikomesha? Sasa mbona ananitafuta hivi jamani huku ni ktafutana ubaya kabisa.
Nilizungumza mwenyewe kama chizi huku nikienda pale mezani nikabeba beg lenye laptop yangu nikapanda kwenye gari nikawa narudi kule hotelini nikiwa naendesha kwa mwendo wa taratibu sana lakini cha kuogopesha ni lile wingu kama la mvua lililotanda angani hasa eneo la tukio. Ilikuwa ni safari ya takribani dakika30 mpaka kufika hotelini nilipofikia mimi.
Niliongeza mwendo nikiwa nataka kufika mapema angalau nipate muda wa kupumzika yale mawazo yanitoka. Kwenye ile barabara magari yalikuwa machache sana na kunipa uhuru wa mimi kuweza kuendesha kwa spidi niliyoitaka mimi wakati naendelea kuendesha mara usingizi ukaanza kuninyemelea wakti naendesha. "Ooh my God ni nini hiki" nilijitamkia baada ya kujikuta naasha njia na kuingia vichakani nilirudisha gari nyuma na kurudi tena barabarani safari ikaendelea, wakati naendesha nilimuona msichana mdogo wa miaka kama tisa au nane akiwa amesimama pale barabarani nilipiga breki nikasimamisha haraka.
"aah wewe unafanya nini hapa? Wewe nakuuliza uoni kuwa ni hatari?"
Nilijaribu kumsemesha yule mtoto lakini hakuonyesha kujari nilirejea kwenye gari nikafungua mlango ile nawasha gari sikumuona tena yule mtoto, nilizidi kuchanganyikiwa nikapiga moyo konde nikaendelea na safari mara nikaguswa bega langu nilikanyaga breki na kugeuka nyuma alikuwa yule jini anayenisumbua miaka yote.
"hahahaha dickson nilikwambia mimi sikimbiliki haya yote yaliyokukuta ni kwaajiri ya ubishi wako sasa kamwe sitakurudishia viungo vyako mpaka ufate masharti yangu"
"masharti! Masharti gani?"
"nataka kila mwanamke uliyewahi kutembea nae kamuue"
"nimuue ili iweje?"
"nimekwambia kama unataka usalama wako nisikutoe dunian kama yule mganga ebu fata masharti yangu"
"sadia nini lengo lako hasa? Mbona umenifanyia mambo mengi lakini uridhke unataka niue tena nimekukosea nini?"
"ebu fata masharti mwanamke wa pili kumuua nitakurudishia maumbile yako una siku 15 kufanya hvyo"
"hapana siwezi kufanya hvyo kama unaniua niue"
Nilishangaa nasukumwa hadi nje kupitia kioo cha mbele nikaanguka kwenye rami nikachubuka na vile vioo viliniumiza pia, akanivuta tena hadi ndani lakini akiwa amekaa ndani kwa kutumia nguvu za giza.
"basi nitafanya nisamehe nisamehe"
**
Safari ilianza kurejea dar lakini nilimtazama felista aliyekuwa pembeni yangu nikawa nasukumwa kufanya mauaji kwani nae pia alikuwa miongoni mwa wanawake niliotembea nao.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media