KABURI LA KAZULA (2)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
Lakini yote kwa yote,Mele akapiga moyo konde kisha akamwita Marongo faragha..ambapo Marongo nae kabla ya kusimama kumfuata Mele,

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
alizitazama kete zake jinsi zilivyo.akasema."Ole wako Solomon uvuruge bao,kete zote nimesha zikariri.." Solomon akacheka...wakati huo Marongo nae alikuwa ameshamfikia Mele.

Kwa Hakika kwa masikitiko na hofu kubwa Mele alimuelezea Marongo kila kitu kuhusu msiba alio upata,na kwa kuwa kwa kipindi kirefu sana Marongo alikuwa akiwaza jinsi ya kumpata Mele,,hivyo kupitia kifo cha kazula,Marongo aliona hiyo ndio itakuwa nafasi ya yeye kuishi na Mele.

"Sawa wewe usijali,tena kazi hiyo nitaifanya mimi peke yangu..Na sitohitaji malipo kutoka kwako" Alisema Marongo kwa tabasam pana..Baada Marongo kujibu hivyo,Mele alimsihi aje usiku nyumbani kwake kazula,kisha Mele akaondoka zake.

"Eeh je,umefanikiwa kuwakuta vijana watakao mzika marehem mumeo?..Alihoji mama Mele Ambae ni Bi kibwana.

"Ndio!.." Akajibu Mele.

"Nani sasa kwa maana vijana wa kijiji hiki si wote waaminifu.."

"nimeongea na Marongo.."

"Saaafi sana mwanangu..Eeh yule ndio mwanaume bwanaa sio hao wengine vikaragosi tu....Sasa niambie,Marongo amesema ataifanya kazi hiyo kwa bei gani?.."Hakika akionekana kuwa na furaha,mama Mele alihoji hivyo..

"Kasema bure!..

"Buree???...Eeh ha! ha! ha! ha!..kweli yule Marongo na huyo anakufaa awe mume wako kwa maana kitendo hicho anachotarajia kukifanya ni Mzigo mkubwa mno,lakini kijana wa watu kaamua kujitolea kukusaidia..".Mele hakujibu kitu akakaw kimya.

Na usiku ulipo ingia,kijana Marongo aliandaa mapema vifaa vya kuchimbia kaburi,ambapo alichukua sululu,chepeo pamoja vifaa vingine mbali mbali..kisha akazipiga hatua kuelekea nyumbani kwa kazula..wakati huo Mele kitambo alikuwa ameshafika,,ila alikuwa amekaa kitako na mama yake mkwe akijaribu kumdanganya kuwa,kazula alikwenda kuwinda tangu alfajiri.Hivyo hata yeye anashangaa hadi muda huu usiku bado hajafika...Kwa Hakika ulikua ni uongo ambao pia Marongo aliu-support,nia n'a mazumuni kumdanya mama kazula ambae nae alijawa na tumbo joto,ingawa nafsi yake ikawa inamsuta asikubaliene na maelezo ya Mele kwa maana haikuwa kawaida kwa mtoto wake kuondoka mahala bila kumpa taarifa mama yake.

Lakini wakati mama kazula alipokuwa katika sinzofaham kuhusu mwanae,,hali ya kuwa Marongo nae akisubili muda ufike ili amzike kazula..ndani ya nyumba ya kazula alitokea mganga Baluguza...!

Mganga baluguza alionekana chumbani kwa kazula,lakini punde si punde akawa amepotea..wakati huo maongezi mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea Kati ya mama kazula,Marongo pamoja na Mele..yalikatis

hwa baada mama kazula kuhisi usingizi,kitu ambacho kilimfurahisha sana Mele..zaidi alisubili mama yake mkwe anyanyuke aingie ndani ili na wao wakafanye shunghuli nzima ya kumzika kazula kimya kimya pasipo kujuwa mtu yeyote.

Kweli ni jambo walilofanikiwa,kwani baada mama kazula kuzama ndani,Mele pamoja na Marongo walizipiga hatua kwenda kuchimba kaburi nyuma ya nyumba na kisha kumzika kazula.

Hivyo baada suala hilo kufanikiwa..usiku ule ule kijana Marongo aliweza kuzungumza na Mele kuhusu hisia zake..Na kwakua Mele aliona msaada alioufanya Marongo..hatimae alimkubalia,ila alimtaka akatafute mahali na ndipo waoane.

Kweli ndani ya siku kadhaa,Marongo alifanikiwa kupata mahali aliyoambiwa ambapo aliuza mbuzi watatu na kondoo mmoja..kwa maana Marongo alikuwa mfugaji.Hivyo taratibu za wao kuona zilifuata,ambapo Bi kibwana ambae ni mama Mele alifurahi sana siku hiyo,alialika ndugu na jamaa zake kutoka vijiji jirani na wengine kutoka mjini,wote kwa pamoja waliungana kwenda kusheherekea sherehe ile ya Mele kuolewa.

Lakini wakati sherehe ile ilipokuwa ikiendelea,upande wa pili kule nyumbani kwa kazula,nyuma ya nyumba ambako lipo kaburi la kazula.kaburi lilofukiwa na kisha kufunikwa na majani ili lisionekane,ghafla juu ya kaburi alionekana paka mweusi paka ambae alilia kwa sauti Kali kisha punde akawa amepotea..ambapo baada paka yule kupotea,kando kidogo ya kaburi ambako kulikuwa na kichaka,alionekana nyoka mkubwa kiasi,nyoka aina ya cobra alijiburuza hadi kwenye kaburi la kazula,,ambapo aliingia ndani.bila shaka katika kaburi lile lilikuwepo shimo.

Wamati nyoka yule alipokuwa akiingia ndani ya kaburi la kazula,kwingineko mama kazula alianguka chini kwa mshtuko baada kusikia kuwa Mele anaolewa na mtu mwingine,,hivyo hapo mama kazula akawa amehisi ya kuwa Mele atakuwa kampoteza mtoto wake ili aolewe na mwanaume mwingine...Hakika hali hiyo ya mshtuko iliweza kumpeleka umauti mama kazula kwa maana miaka dahari alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa...Na baada mama kazula kufariki alizikwa na wanakijiji,ila sehem aliyokuwa akiishi ilipigwa bei na mdogo wake ambae aliitwa Mzee makumbuko kwani baada mama kazula kufariki,mrithi wa mali hakuonekana zaidi ya huyo Mzee makumbuko ambae nae kwakua alikuwa mlevi,aliona heri auze mashamba na kiwanja ili pesa akanywee pombe.

Hivyo kwa kuwa Marongo lasmi alianza majukum,hatimae aliamua kununua yale mashamba na uwanja ambao tayali ulikua na nyumba mbili..nyumba ya marehem mama kazula na nyumba ya kazula..

BAADA YA MWAKA MMOJA.

Maisha ya Mele pamoja na mume wake Marongo yalikuwa mazuri ya furaha na amani,lakini furaha hiyo ilitoweka baada siku moja saa sita usiku wakati Marongo anaelekea chooni kujisaidia,ghafla alishtuka baada kumwona mtu alievaa nguo nyeupe mbele yake,na punde si punde yule mtu akawa amepotea.

Marongo kwa woga,alizipiga hatua za haraka haraka kuelekea chooni,akajisaidia haja yake kisha akarudi ndani hima.

Na wakati akiwa kitandani na mke wake Mele,ghafla upepo mkali ulivuma ukipitia dirishani,,kiasi kwamba upepo ule uliweza kudondosha baadhi ya vitu vyepesi vya mle ndani.."Mele mele mele..! Marongo alimwamsha mke wake ambapo Mele nae baada kusikia sauti ya mume wake ikimwita,alishtuka kutoka usingizi.."Amka mke wangu..!! tutoke humu ndani,kwa maana upepo huu unaweza kuangusha nyumba..!

Wakionekana kuwa na hofu juu ya ule upepo,Mele pamoja na mume wake Marongo walitoka nje usiku ule ule,,ambapo baada kufika nje,cha ajabu upepo ule ulitulia kisha sauti ya ngoma na nyimbo za asiri zilisikika kutoka nyuma ya nyumba kule lilipo kaburi la kazula....Na mtu wa kwanza kuisikia ile sauti alikuwa ni Marongo,ambapo aliduwaa kwa muda wa dakika kadhaa kisha akamuuliza mke wake "Mele unasikia nini! "Sisikii kitu chochote,Kwani wewe unasikia nini?

Alihoji Mele kwa mshangao lakini Marongo hakutaka kumwambia,zaidi alimtaka mke wake warudi ndani kulala.Ila licha ya Marongo kurudi ndani na mke wake Mele,bado suala la kupata usingizi lilikuwa gum kwa upande wao,Kwan ilifikia hatua Mele nae akawa anaisikia ile sauti ya ngoma na nyimbo za asiri zilizokuwa zikiimbwa kutoka nyuma ya nyumba mahali alipozikwa kazula.

Kwa Hakika usiku ulionekana mrefu kwa wapenzi hao,kwani baada sauti ile kudumu kwa muda wa nusu saa,hatimae ilipotea kisha wakasikia sauti ya kazula ikimwita Mele kwa hisia na Kali,sauti hiyo Mele aliisikia aliogopa sana kiukweli..Marongo akahoji kwa kunong'ona "Hiyo sauti ni yakuzula?.."

"Ndio yenyewe.."Akajibu hivyo Mele,ambapo baada Marongo kujibiwa hivyo na mke wake,haraka asana alinyanyuka kutoka kitandani..kisha akazipiga hatua kulisogelea dirisha,ambapo baada kulifikia,aliifunua pazia ya dirisha kisha akatazama kule ilipo kaburi la kazula,,,kwa Hakika Marongo alistaajabu baada kuona kaburi la kazula likiwa limejengewa,wakati walipo mzika walilifunika kwa kutumia majani ili pasijulikane kama mahala pale kuna kaburi..."Mungu wangu,tume kwisha! Alisema Marongo ndani ya nafsi yake huku akitetemeka mwili mzima,,wakati huo kule kwenye kaburi,ulionekana mwanga wa touch,mwanga huo ulionekana kuusogelea nyumba ya Marongo..Marongo kwa woga alifunika dirisha kwa pazia kisha akarejea kitandani lakini kabla hajaulaza mwili wake,ghafla kibatari kilizima na punde si punde akasikia mlango wa nyumba yake ukigongwa.

Bwana marongo akiwa na mke wake mele,walisikia mlango ukigongwa nje.Wakati huo zile sauti za nyimbo na ngoma za asiri iliyokuwa ikitokea kule kwenye kaburi la kazula,ilikata.Ambapo Marogo baada kusikia mlango wa nyumba yake ukigongwa,ghafla akajawa na hofu kubwa moyoni mwake.Marongo akasimama kutoka kitandani,kisha akawasha kibatari chake,moja kwa moja akausogelea mkoba wake ambao ulikuwa na dawa mbali mbali za asiri,dawa ambazo bwana Marongo alipewa na marehem baba yake kwa niaba ya kulinda mifugo yake.Hivyo marongo akaona ajaribu kujipaka ile dawa ambayo ni maalumu kwa kuwapaka ng'onbe,kondoo au mbuzi ili pindi ambapo mnyama mkali atakapo vamia zizi,asiweze kuona mfugo wowote.

"Lazima nijaribu kujipaka hii dawa,na ndipo niende kumwona huyo mtu anae nigongea mlango usiku huu wote"Alisema Marongo huku akimalizia kujipaka ile dawa kwenye paji la uso wake.Na mala baada kumaliza,bwana marongo alizipiga hatua kuelekea mlangoni kwenda kufungua mlango.Lakini kabla hajafungu mlango! Ghafla marongo alishtuka baada kusikia sauti ya kicheko cha kazula kikitokea nyuma ya nyumba yake ambako ndiko lilipo kaburi la kazula..Bwana marongo aliisikilizia kwa umakini saana ile sauti,na wakati marongo alipo kuwa akitega sikio lake kuisikiliza ile sauti ya kicheko iliyokuwa ikitokea nyuma ya nyumba yake? Pale mlangoni alipokuwa amesimama akitaka kutoka nje,napo mlango uligongwa.Hivyo marongo kwa kujiamini kwa kuwa kajipa ile dawa,hatimae alifungua mlango kwa nguvu.Lakini hakuona mtu yoyote.

Hakika marongo alistaajabu sana,akatazama mbele kulia na kushoto,ila hakufanikiwa kumwona mtu yoyote.Ambapo Marongo akaona haitoshi,bora akachungulie kwenye kaburi la kazula ili aone kinachoendelea kwenye hilo kaburi.

Hivyo Marongo akiamini dawa imemfanya asionekane,alizipiga hatua za kunyata akilisogelea kaburi..na mala baada kuliona,kwa hakika marongo alipigwa na butwaa kwani hakuamini kama angelimwona kazula..kwamaana alijuwa kuwa vile alivyomzika,ndio misho wake..Kiukweli Bwana marongo aliogopa sana,haraka sana alirudi ndani,wakati huo kwenye kaburi la kazula..alionekana kwa mala nyingine tena Mganga Baluguza,ambapo mganga huyo alichukuwa kitu frani ambacho kinafanana na mkia wa ng'onbe,kisha akachovya kwenye kibuyu chake na moja kwa moja akamnyunyuzia kazula..kitendo ambacho hakikuchuwa muda..

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)