
Mtunzi: Alexis Wamilazo
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
ambapo mganga huyo alichukuwa kitu frani ambacho kinafanana na mkia wa ng'onbe,kisha akachovya kwenye kibuyu chake na moja kwa moja akamnyunyuzia kazula..kitendo ambacho hakikuchuwa muda..
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
kazula kupotea pele juu ya kaburi..Baluguza akacheka kisha nae punde si punde akapotea pale kaburini.
Kesho yake asubuhi,mtu wa kwanza kuamka alikuwa ni mele,ambae yeye kama mama wa nyumbani ilimlazim awahi kuamka ili akamue maziwa kabla mume wake hajazipeleka ng'ombe porini kuchunga.Lakini baada Mele kumaliza shughuli zake zote,ghafla akaingiwa na hofu kubwa baada kuona mume wake hatoki ndani japo kunawa uso.Ambapo Mele alingia ndani kwenda kumwamsha mume wake..punde si punde Mele akajikuta akilia baada kumwona mume wake kavimba mwili mzima..Marongo ile dawa aliyojipakaa usiku ili weza kumuathiri ngozi yake,,
Hivyo mele akianguwa kilio,alizipiga hatia za haraka haraka kuelekea nyumbani kwao kwenda kumpasha habari mama yake juu ya kile kilichomkuta Marongo,lakini kabla Mele hajafika kwao,alisimama akakumbuka ushauri wa mama yake jinsi ulivyo yanghalim maisha ya mume wake wa zamani ambae anaitwa Kazula. "Hapana siwezi kurudia kosa" Alisema Mele kisha akageuka kuelekea kwa Bibi wa rafiki yake ambae nae alijihusisha na mambo ya kutibu magonjwa mbali mbali kwa kutumia miti shamba.
Na wakati mele alipokuwa akihaha kutafuta dawa ya kumtibu mume wake,nyuma ya nyumba mahali ambapo lipo kaburi la kazula..ghafla udongo tifu tifu kwenye kaburi ulicheza,na punde si punde kiganja kilionekana ikafuata goti..na mwishowe kabisa mwili wote wa kazula ulionekana juu ya kaburi,hakika kazula alitisha sana kwani mwili wake wote ulikuwa ukitoa wadudu mbalimbali,lakini punde si punde kazula alionekana akiwa katika mavazi yake yaleyale aliyozikwa nayo.
Kazula akatazama huku na kule,hakuona mtu,ambapo alizipiga hatua kuingia ndani ya nyumba,na moja kwa mojs alimkuta Marongo akiwa hoi kitandani.
"Marongo! Marongo! Marongo!.." Aliita kazula kwa ssuti ya huzuni kabisa..Marongo alikiwa ameyafumba macho yake,lakini aliyafumbua baada kusikia sauti ikimuita.na baada kufumbua hakumeona mtu yoyote.Madongo alichoka kukweli akatamani kuikkmbia nyumba...lakini uwezo huo hakuwa nao.
Na wakati huo mele alirejea na dawa ya kumtibu. Mume wake,lakini alipoingia chumbani dawa akaiweka juu ya meza kwanza ...na punde si punde ile dawa ikapotea kimazingara..kitu ambacho kilimsthua mele akajikuta akistaajsbu huku kijasho kikimtoka mwili mzima.
Mele alionekana kushtuka baada kuona dawa aliyokuwa ameiweka juu ya meza,imepotea kimaajabu.Hivyo akiwa na hofu kubwa,Mele alisema.Marongo unajuwa ya kuwa tangu tumzike kazula,nyumba hii imekuwa chungu? "Ndio mke wangu nafaham hilo,ila usijali tatizo kama hili kwangu la kawaida sana" Akajibu Marongo huku akijionyesha kujiamini,ambapo baada kujibu hivyo alijinyanyua kutoka kitandani,kisha akazama uvunguni.akatoka na mkoba uliochakaa,mkoba huo marongo aliufungua akachomoa kitambaa kilichokuwa kimefungwa fundo.akafungua lile fundo.Baada kulifungua lile fundo,Marongo akasema.
Mimi ndio marongo,naomba mizimu ya ukoo wangu mlisimamie suala hili.Alisema Marongo huku akijipakaa unga flani alioukuta kwenye lile fundo lililokuwa limefungwa kwenye kitambaa.. ambapo kwisha kusema hayo,Marongo alirudisha mkoba wake uvunguni..na hapo ndipo Mele aliposema.Marongo unajuwa mimi sijaelewa ulichokifanya,naomba uniambie unamaana gani? Hujaelewa nini sasa Mke wangu? Naomba ukae kimya kwanza,ndio maana nimekwambia mambo haya yakawida kwangu! Alijibu Marongo kisha akachukuwa mkuki na panga,akaelekea kwenye zizi la wanyama wake,ambapo ndani ya zizi,alimchagua fahali mmoja akawa ameondoka nae moja kwa moja mpaka kwenye mti mkubwa kuliko yote kijijini kwao.Mti ambao ulikuwa maalumu kwa kufanyia matambiko.Marongo akiwa na fahali wake yaani ng'ombe dume.aliusogele
a ule mti kisha akamfunga kamba yule ng'ombe miguu yote minne kisha akamwangusha chini ya ule mti mkubwa.Upepo mkali ulivuma,giza na mwanga hafifu ukatanda kwenye ule mti,na punde si punde vicheko vya kila lika vilisikika kutoka kwenye ule mti.Marongo hakuteteleka,kwa ustadi wa hali ya juu aliukamata vyema upanga wake akiwa tayali kabisa kumchinja Ng'ombe wake ikiwa kama kutoa kutoa sadaka kwa mizimu yao.
Lakini kabla Marongo hajamjicha fahali wake,ghafla kwenye ule mti alitokea mtu mrefu.Mtu wa ajabu akiwa amevaa mavazi yake ya sanda..Mtu huyo alimsogelea Marongo kisha akasema.Tunatambua kibarua kizito kilichopo mbele yako,nasi tupo tayali kukusaidia kwa sababu umejali kitu tunacho hitaji,pia pongezi kwako kwa kuwahi kufika mahali hapa,kwa maana jopo la mizimu likiongozwa na kazula lipo katika haraki za kulipa kisasi juu ya kile ulicho kifanya wewe na mkewe..Marongo alistaajabu kusikia maneno yale ya ule mzimu uliomtokea chini ya mti..Ambapo punde si punde ule mzimu ulipotea,na hapo ndipo marongo alipomchinja ng'ombe wake huku akijisia huru kabisa ndani ya moyo wake akiamini kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa mauzauza ya kitokewa na Marehem Kazula.
Hivyo wakati Marongo alipokuwa akifanya tambiko,upande mwingine nako.alionekana kazula juu ya kaburi.Kazula alikuwa ameketi huku akitazama kila pande ya dunia..kitu ambacho kilipelekea wapita njia kushtuka kumwona akiwa kwenye kaburi..ambapo habari hiyo iliweza kusambaa kijini huku baadhi ya wanakijiji wakionekana kutokukubaliana na habari ile ya kuonekana kazula kwenye kaburi..wakati hajawahi kusikia msiba wa kazula zaidi wao walikuwa wakijuwa mama kazula ndio aliefariki..Wingi wa wanakijiji walijisogeza nyumbani kwa Marongo kwenda kumshuhudia Kazula ambae alizikwa kimyakimya baada kuuliwa na Mele...Hivyo Mele baada kuona wingi ule wa wanakijiji wakija nyumbani kwake,alishtuka
.Wakati huo tayali jopo la wanakijiji limeshafika nyumbani kwake,,ambapo moja kwa moja walizunguka nyuma ya nyumba mahali alipozikwa kazula..Kwa hakika walistaajabu kumwona kazula.wakati huo Kazula alisimama,akatabasam na punde si punde akapotea pale kaburini..
"Jamini Mele na mume wake wako wapi" ilisikika sauti ya mmoja ya wanakijiji akisema hivyo,baada kuona kitendo kile cha kushamgaza katika macho ya watu.Hivyo alitaka kujuwa ukweli kuhusu kazula na ukweli kuhusu kaburi la siri lilopo nyuma ya nyumba yao.
Lakini kabla mwanakijiji yule hajajibiwa,kwa mbali alionekana Marongo akiwa na upanga pamoja na mkuki huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu kila kona kona..Marongo alishtuka na wingi wa watu uliokusanyika nyumbani kwake..maswali kibao alijiuliza kichwani mwake,ila yote kwa yote alipiga moyo konde kisha akazipiga hatua za pole pole akizidi kujongea nyumbani kwake..Na punde si punde wanakijiji waliokusanyika pale kwake,waligeuza nyuso zao kumtazama Marongo..ambapo ilisikika tena sauti kutoka kwa mwanakijiji,sauti hiyo ikisema "lazima huyo leo atuambie ukweli kuhusu hili kaburi,pia yeye na mke wake watueleze mahali walipo muweka Kazula.." Alisema hivyo mwanakijiji mmoja ambae jina lake aliitwa Mzee mkavu. .ambapo mzee huyo aliongea kwa ukali,kauli ambayo iliungwa mkono na wanakijiji wenzake haswa wale ambao waliomjuwa kiundani zaidi Kazula ambae alisifika kwa upole aliokuwa nao
Wanakijiji walionekana kuwa na shauku ya kutaka kujuwa ukweli kuhusu kaburi lilopo nyuma ya nyumba ya bwana Marongo,,lakini cha kushangaza Marongo hakutaka kusema ukweli kama kaburi lile lililopo nyuma ya nyumba yake,,ni kaburi la Kazula..kijana waliomzika kimya kimya pasipo kutambua mtu yoyote. Hivyo baada wanakijiji kushindwa kupata ukweli,hakika walifadhaika saana mioyoni mwao..kwani ilifikia hatua wakataka kumpiga Marongo,,ila Marongo alisimama kidete huku akidiliki kumtishia mwana kijiji yoyote atakae thubutu kumpiga. Na kwakua marehem baba Marongo alisifika kwa uganga wa kienyeji enzi za uhai wake,,hivyo wanakijiji walimwogopa sana Marongo..wakaamua kumuacha huku wakiamini kuwa hakuna siri chini ya jua..kwa kuwa Mele alimuuwa kijana kazula,,basi ipo siku itajulikana tu na haibu kubwa itawakumba wanandoa hao Bwana marongo na Mele.
Naam! Siku zilikwenda mapenzi ya Marongo na Mele yakizidi kunoga..kwa hakika Mele alidiliki kusema kwa kinywa chake..Afadhali nilivyo muondoa kazula nyoka kibisa..kumbe wewe ndio ulikuwa sahihi katika maisha yangu! Alisema Mele wakati huo akiwa ameketi chini ya mti uliokuwa kando kidogo na nyumba yake huku akimwambia maneno hayo mume wake ambae ni Matongo..Marongo alifurahi kusikia maneno yale matamu yakitoka mdomoni kwa mke wake..kisha baada kuachia tabasam..Marongo akasema. Unamaana gani mke wangu? Alijibu Marongo huku akiachia kicheko chenye furaha ndani yake.
Mele alishusha pumzi kisha akasema. Kiukweli miaka mingi sana niliishi na kazula,lakini licha ya kuingiliana kimwili mala kwa mala kama mke wake..ila hata siku moja sikuwahi kujihisi mjamzoto..hivyo nadhani kwako wewe unaweza kunipatia mtoto..kwa maana dalili zote naziona. Aliongeza kwa kusema hivyo Mele..kiukweli Marongo alifurahi saana kusikia maneno yale,,sifa nyingi alijisifia akasubutu kumponda Kazula ambae tayali ni marehem..utani kadha wa kadhaa uliendelea kwa wapenzi hao..Na mwishowe habari hiyo njema,Mele aliona bora akamueleze mama yake..lakini wakati akijiandaa kuondoka,,hatimae mama yake alifika..hivyo safari ya Mele ikawa imeota mbawa. Ambapo waliamua kukaa sehem tulivu chini ya mti,,kisha mazungumzo yakafatia kati ya mama na mtoto. Na katika mazungumzo hayo,habari ya Mele kunasa mimba ilimfurahisha sana mama Mele,,akacheka sana huku akipiga vigelegele asiamini kama kweli mwanae kapata mimba.
"Mwanangu,,naweza kusema kufa kwa kazula ni neema kwako..hakika uwanaume kazi,,na sio kuvaa suruali tu khaa.." Alisema mama Mele huku furaha kubwa akiwa nayo ndani ya moyo wake.. "kweli mama mimi nakuunga mkono" Alisema Mele.
Mama Mele hiyo taarifa ya mwanae kunasa ujauzito ilimfurahisha sana..hadi akatangazia baadhi ya marafiki zake..hivyo nao wakawa wamefaham kuwa Mele mtoto wa mama Mele amimba..Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda,,cha kushangaza mimba ya Mele haikuweza kukuwa wala kupungua..hali iliyompelekea kupata wasiwasi..hata Marongo nae alishtuka..na hivyo siku mojs usiku..Marongo aliamua kumuliza Mke wake kuhusu miezi ya ujauzito..lakini kabla Mele hajajibu, ghafla kule kwenye kaburi la Kazula ilisikika sauti ya mtoto mchanga akilia,,Marongo alishtuka..huku akiisikilizia ile sauti kwa makini,,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media