KABURI LA KAZULA (4)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
hata Marongo nae alishtuka..na hivyo siku mojs usiku..Marongo aliamua kumuliza Mke wake kuhusu miezi ya ujauzito..lakini kabla Mele hajajibu, ghafla kule kwenye kaburi la Kazula ilisikika sauti ya mtoto mchanga akilia,,Marongo alishtuka..huku akiisikilizia ile sauti kwa makini,,

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
sauti hiyo ambayo alikuwa akiisikia yeye peke yake..ila mwishowe ile sauti aliisikia na Mele..ambapo punde si punde ikakata. Kisha ikasikika sauti ya Kazula ikisema. "Mele bado nipo hai..na kwa hakika maisha yako yoote na mume wako yapo kiganjani mwangu" Ilisikika ikisema hivyo sauti ya marehem Kazula..sauti ambayo iliambatana na mwangwi mkali.

Mele aliogopa sana kusikia maneno yale ya Kazula,,na punde si punde punde mimba yake ambayo ilikuwa changa ilipotea kimiujiza..Mele akionekana kustaajabu aligusa tumbo lake baada kujihisi tofauti.."mungu wangu,nitaificha wapi sura yangu mimi mbele ya mama yangu? " Alijisemea Mele ndani ya nafsi yake,,wakati huo Marongo nae akiendelea kumwaga dawa zake za asiri ndani ya chumba chake,,na mala baada kumaliza alimtoa wasiwasi mke wake huku akiupeleka mkono wake kwenye tumbo,,lakini Mele aliushika ule mkono wa Marongo,,hali iliyomfanya Marongo kushangaa,,na punde si punde akasema. Kwa nini unanizuia nisimguse mwanangu ndani ya tumbo lako? Ah embu niache nimguse japo nisikie akihema" Alisema Marongo huku akiongeza na utani kiasi. Ila bado Mele alionekana kukataa,,kwani wakati ule tayali tumbo lake lilikuwa lipo kawaida tofauti na awali ambapo ilikuwa mimba ya ndogo ya kawaida.

"Nitaificha wapi sura yangu,mbele ya mama yangu? Au nitamueleza nini mume wangu ili anielewe maana nimeshamwambia kuwa tayali nimenasa mimba! Daah Eeh mungu wangu nisaidie" Mele aliwaza hivyo baada kujiona yupo katika wakati mgumu baada mimba yake kutoweka kimaajabu. Na wakati Mele akiwaza hivyo,Marongo nae alionekana akizidi kuwa king'ang'anizi kwa mke wake akitaka kumgusa tumboni ili asikie japo mtoto akihema. "Marongo mume wangu jaribu kuwa na staha basi, mimi mkeo na sio hawala yako. Hivyo nakuomba uniheshimu sawaee.. kwanza kwa vitisho vinavyo endelea humu ndani. Tafadhali nakuomba tuhame haraka sana" Alisema Mele kwa msisitizo mkali huku akiurudisha nyuma mkono wa mume wake ambao tayali ulikuwa ukiukalibia tumbo lake. Kiukweli Mele alikereka sana,na mwishowe Marongo alilitambua hilo. Hivyo akatulia.

Baada Marongo kutulia kiukweli aliwaza akajiuliza ni kitu gani kinachomfanya Mele akatae kuguswa tumbo lake? Swali ambalo lilimfanya achukie moyoni mwake ambapo aliamua kunyanyuka kutoka kitandani akazipiga hatua kuelekea sebleni kulala. Mele baada kuona hali ile akajuwa kabisa amemchukiza mume wake labda huwenda alikuwa anahitaji tendao. Mele alijilaum sana kiukweli akatamani kwenda kumuomba msamaha..wazo ambalo aliliona lifaa saana hivyo alinyanyuka haraka sana kutoka kitandani akitaka kumfuata mume wake ili amuombe msamaha. Lakini kabla hajatoka chumbani,ghafla akamuona Marongo kalejea tena chumbani. Kwa sauti ya upole Mele akasema "samahani mume wangu kama kweli nimekuudhi.

Hakika halikuwa tegemeo langu" alisema Mele Kwa sauti ya upole. Nae Marongo baada kuambiwa hivyo,alicheka kisha akamjibu "usijali mke wangu hayo mambo ya kawaida tu" Marongo alijibu hivyo huku akijalaza kitandani ambapo Mele nae ili kuyasawazisha makosa yake,aliamua kumpapasa mumewe na punde si punde tendo la ndoa lilifuata. Tendo hilo lilidumu kwa muda wa dakika tano. Na wakati wawili hao wakiendelea kufanya mapenzi, ghafla chumbani aliingia mtu mwingine aliefanana na Marongo. Mele alistaajabu kuona hali ile akamsukuma M arongo yule aliekua juu ya kifua chake. Akamtazama Marongo yule aliekuwa amesimama kando yake. "Mele nini sasa unafanya " Marongo aliekuwa kando ya kitanda alimuhoji Mele wakati huo huo Marongo yule aliekaa kitandani nae akimuuluza Mele "kwani huyo nani kwako? Daah Mele alichanganyikiwa kiukweli akashindwa amjibu yupi amuache yupi maana wakina Marongo hao wote walikuwa wamefanana kila kitu.

Lakini wakati Mele ikiwa amepigwa na butwaa akishindwa amjibu yupi amuache yupi,ghafla yule Marongo aliefanya nae mapenzi alipotea kimaajabu. Mele alishtuka hali iliyompelekea kupotezea faham hapo hapo mpaka asubuhi.

"Maisha gani haya ambayo tunaishi mume wangu? Tazama mimba yangu imetoweka kimaajabu! Ee kwanini lakini" Mele alimwambia mume wake mala tu alipozinduka. Ambapo katika sentensi zake akaamua kuingizia na suala la mimba kutoweka kimaajabu. Marongo alishtuka sana akalaani mizimu ya ukoo wao kuwa haimsaidii licha ya kuitolea sadaka Kwa kuichinjia fahali wake. Na mwishowe kabisa Marongo akamwambia mke wake. "Kwahiyo mke wangu ulipenda tuhamie wapi?

Mele kwa haraka haraka akajibu "Ili kukwepa haya mauzauza,nakushauli mume wangu tuhamie mjini tu kiukweli hapo tutakuwa tumemaliza kila kitu"

"Aaaah Mele kwa kupenda mji? Hahahaaaaa sawa bwana mke wangu usijal kwanza hapa kijijini wameshaanza kutuhisi vibaya juu ya kifo cha kazula,kwahiyo wazo lako ni nzuri sana..pia hilo suala la mimba kupotea kimaajabu. Huo woga wako tu amini mwanetu bado yupo sawa mke wangu"

"Sawa ahsante kwa Kwa maneno yako mazuri mume wangu,ndio maana nakupenda sana"

"Mmh kuliko kazula?

"Aaah Jamani mume wangu mbona hivyo sasa nitampendaje mtu ambae ameshakufa? Wewe ndio kila kitu kwangu sio huyo marehem Nyoka kibisa " Marongo na mke wake walicheka sana baada kuongea maongezi hayo..

Marongo alifanya mikakati ya kuhama katika imaya ile ya Kazula. Ambapo alifanikiwa kupata nyumba ya kupanga mjini kama mke wake alivyopendekeza. Hakika amani ilitawala baada wawili hao kuanziasha maisha mapya mjini. Hivyo Marongo akaona hana mpango wa kuishi kijijini ambapo aliamua kuuza mifugo yake akapata fedha nyingi ambazo aliweza kufungua biashara mjini alikohamia.

Maisha yake na mke yaliendelea kuwa raha mstarehe. Wakasahau kuwa kuna dhambi kumbwa waliyoitenda yote ikitokana na amani tele kutawala juu yao. Lakini siku moja asubuhi wakati Mele akiwa katika manunuzi yake sokoni. Kwa mbaali alimuona mtu aliefanana na Kazula, Mele alishtuka akawa haamini kama kweli yule mtu aliemuona ni Kazula au laa.. hivyo akionekana kuwa na Hofu kubwa moyoni alizipiga hatua kuelekea sehem ile aliyomuona yule mtu aliefanana na marehem Kazula, ,lakini kabla hajamkalibia ghafla yule mtu alitoweka kimaajabu. Kiukweli Mele alistaajabu. Haraka sana akarejea nyumbani kwake huku akimsubilia mume wake kwa hamu kubwa ili amwambie kile alichokishuhudia sokoni.

Na wakati Mele akiwaza hayo,upande wa pili nako Marongo akiwa katika biashara yake ya kuuza duka. Ghafla dukani kwake alitokea mtoto mdogo wa makamo ,mtoto huyo alimpa Marongo fedha shilling miambili kisha mtoto huyo akahitaji sigara. Marongo Kwa masihara akamuuliza yule mtoto. "Nani kakutuma sigara? Mtoto yule aliachia tabasam kisha akanyoosha kidole akimwonyesha Marongo mtu aliemtuma sigara. "Mungu wangu yule si kazula? Alisema Marongo huku akionekana kushtuka baada kumuona marehem Kazula akiwa amekaa kando kidogo na eneo lilipo duka lake. Na wakati Marongo akiwa amepigwa na butwaa..ghafla yule mtoto alitoweka kimaajabu pia muda huo huo Kazula nae alipotea. Hali iliyomfanya Marongo kupagawa zaidi,ambapo siku hiyo aliamuwa kufunga duka lake mapema akarudi nyumbani kwake.

Na wakati Marongo akiwa njiani akirejea nyumbani kwake,upande wa pili alitokea marehem kazula punde si punde akajibadilisha kwa kuchukuwa taswira ya Marongo kisha akazivuta hatua kuelekea nyumbani kwa Marongo. Mele baada kumuona alimpokea akijuwa kuwa kweli yule ni mume wake...hivyo kabla ya yote alimpelekea maji ya kuoga bafuni huku akimsubili kwa hamu ili amueleze kile alichokiaona sokoni . Ila wakati Marongo huyo alipokuwa bafuni kuoga,kwingineko alionekana Marongo mwingine ambae ndio mume wake Mele. Hakika Marongo alionekana kuchoka saana kwani alipakimbia kijijini kwa nia ya kuyakwepa mauza uza. Lakini cha kustaajabu akajikuta yule waliomkimbia kawafuata hadi mjini. Amakweli damu ya Mtu nzito. Mele akiwa ndani aligongewa hodi na mumewe,hivyo akajuwa dhahili mume wake atakuwa ametoka bafuni..Lakini baada kufungua mlango alishtuka kumuona mume wake ndio amerejea kutoka kazini...

Kiukweli Mele alijikuta akistaajabu baada kumuona mtu mwingine aliefanana na mume wake..asijue kuwa yule aliempelekea maji bafuni hakuwa mume wake bali ni marehem kazula aliechukuwa taswila ya Marongo ambae ndio mume wake Mele. Kwahiyo wakati Mele akistaajabu, Marongo nae alimshangaa sana Mele akishindwa kujua kipi kinacho msibu mkewe . Hivyo basi kwa sauti ya ukali kiasi..bwana Marongo akamuuliza mkewe hivi "Mele unanini leo? Mbona sikuelewi badala unilaki na kisha unihoji kilicho nifanya nirudi nyumbani mapema! Unanishangaa kama vile me mgeni kwako" alisema hivyo bwana Marongo lakini Mele hakujibu kitu,zaidi alizipiga hatua kuelekea bafuni ambako alimpelekea maji Marongo mwingine ambae ndio Kazula aliechukuwa taswila ya Marongo. Lakin baada Mele kufika bafuni,cha kustajabisha aliukuta mlango wa bafu ukowazi.

Mele akashtuka mapigo ya moyo wake yalimwenda mbio..ila alipiga moyo konde akaendelea kuzivuta hatua za kunyata na punde si punde aliukalibia mlango wa bafu ambao ulionekana kuwa wazi.. Baada kuukalibia zaidi,Mele alichungulia ndani ambapo hakuweza kumuona yule Marongo aliempelekea maji ya kuoga bafuni. Kiukweli Mele hofu ilizidi kumjaa moyoni wakati huo ile sauti ya mwisho aliyoitoa Marehem Kazula ilikuwa ilikuwa ikijirudia akili mwake..sauti ambayo ilikuwa ikisema "Nakufa na ndoto zangu Mele, ila ilaa. ." Neno "ila" ndilo neno ambalo lilionekana kumtesa mno Mele kwani lilikuwa kwenye fumbo. Mele alisononoke kiukweli. Na wakati Mele akiwa na sononeko moyoni mwake, ghafla kwenye kona ya chumba bafuni alitokea Kazula akiwa katika mavazi yake meupe yaani Sanda. Mele alishtuka akataka kutoka mbio bafuni lakini mlango wa bafuni ukajifunga kitu ambacho kilimpelekea Mele kupasa sauti "Mama nakufaaa" Sauti ambayo ilimshtua Marongo haraka sana akakimbia kuelekea bafuni ambako alisikia mayowe ya mke wake.

Marongo baada kufika bafuni, alikuta mlango bado umefungwa lakini punde si punde mlango ule ulijifungua...bwana Marongo akatazama bafuni akaona mwili wa mke wake ukiwa chini. Kiukweli Marongo alishtuka sana kwa woga aliusogelea mwili wa Mele kisha akaugusa Sehem ulipo moyo akakuta mapigo ya moyo yakiwa yamesimama..daah Marongo alitaharuki ghafla kijasho chembamba kilianza kumtoka wakati huo huo akimnyanyua na kisha kumtwaa begani..

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)