NYOKA WA KUTUMWA (8)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
KIJNA: Mzee sube mtukufu mfalme ameniagiza nije nikuite na amesema tufanye haraka maana mke wake wa pili aitwae Mana ameng’atwa na yule nyoka.

KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA NAYO...
MZEE SUBE: Sawa tangulia mwambie ninakuja mda sio mrefu.

KIJANA: Sawa ila amesema usichelewe maana hali yake mbaya sana.

MZEE SUBE: Sawa kijana nimekuelewa ila wewe tangulia.

Kijana akaondoka na kumuacha Sube akijianda, huku akimueleza mke wake kuhusu yule kijana

MZEE SUBE: Mke wangu nahis vijana wa hapa kijijini kama wanachuguza mambo yetu.

BIBI SUBE: He! Kwanini unasema hivyo mume wangu.

MZEE SUBE: Nilipotoka nje nimemkuta kijina mmoja kwenye kile kichaka akichambua chambua kama anatafuta klitu Fulani, aliponiona akashtuka, mimi nikamfukuza, ila leo ni mara ya pili naona kijana akisogea maeneo yale ilaw wala usiwe na hofu mke wangu maana hakuna kitakacho alibika.

BIBI SUBE: Mh! Iwe kweli tu maana mda mwingine huwa naogopa sana nikikumbuka hiki tunacho kifanya.

MZEE SUBE: Usiogope mke wangu haiwezekani kutokea jambo baya lolote lile. Sasa sikiliza mfalme kamtuma kijana aje kuniita, mke wake kang'atwa na Yoka kwahiyo anataka nikamtibu tena amesema nifanye haraka maana hali yake ni mbaya sana. Kwaihiyo nakuomba ukae pale nje ili endapo atakuja kijana yoyote umkataze kusogea wala kupita karibu na kile kichaka.

BIBI SUBE: Sawa mume wangu nmekuelewa.

Sube akaondoka na kumuacha mke wake akijianda kwenda kulinda kile kichaka. Kwa upande wa wale vijanawalipoona Sube ametoka walifurahi sana na kuona kazi yao itakamilika mda mfupi maana aliekuwa akizuia wao kuchunguza kwenye kile kichaka ameondoka, lakini dakika kadhaa mbele walimuona bibi sube akitoka ndani ya nyumba huku akiwa amebeba kitanda cha ukambaa na kwenda kukiweka karibu na kile kicha, huku akifuma mkeka. Kitendo kile kiliwafanya wale vijana wazidi kuamini kuwa wawili wale wana siri kubwa na kwenye kile kichaka kuna kitu wanakificha ndipo wakaanza kuongelea swala lile.

KIJANA 1: Jamani sasa hivi mimi naamini wazee wale kuna kitu wanakifanya haiwezekani wazuie watu kwenda au kupita kwenye kile kichaka, lazima kutakuwa na kitu sio bure.

Maneno ya yule kijana yalikubaliwa na kila mtu pale ndani ndipo wakaanza kutafuta mbinu zaidi za kuwakamata wale watu.

KIJANA 2: Mimi ninaaona bora tukamwambie mtukufu mfalme juu ya jambo hili. Ili tutakapofanya jambo lolote tuwe huru.

Wakiwa wanaendelea kuongea mara mwenzao moja akamuona mzee Sube anarudi ndipo akawashtua wenzake na kuanza kumchungulia kupita kidirisha kidogo kilichopo kwenye nyumba hiyo, Sube alipofika akaa alipokuwa mke wake na kuanza kuongea mambo ambayo wale vijana hawakuweza kuyasikia kutoka na wawili wale kuongea kwa sauti ya chini. Giza lilizidi kuingia wale vijana wakaamua kupumzika huku wakisubiria kwa hamu ifike siku nyingine wakampe taarifa mfale wao. Asubuhi ilipofika wakaondoka kwenye ile nyumba na kwenda nyumbani kwa mfalme, walipofika huko walipokelewa na kueleza shida yao.

KIJANA: Mtukufu mfalme tumekuja hapa kuna kitu tunataka tukuambie ukiwa kama kiongozi mkuu hapa kijijini kwetu,kama unavyojua hapa kijijini kwetu tumekubwa na janga la huyu nyoka na mara kwa mara tumekuwa tukitafuta suruisho lakini ilikuwa inashindikana.

MFALME: ni kwel kwahiyo nyie mnahitaji nini.

KIJANA: Kwanza kilichotuleta hapa tumekuja kukuambia kuwa tumemjua mtu ambae anasababsha haya matatizo na ndio maana kila tukivyopanga mambo yetu tulikuwa atufanikiwi kwa sababu huyo mtu amekua akienda kinyume na sisi yani ni msaliti.

Yule kijana baada ya kusema vile moja kwa moja mfalme kichwani mwake akajua wale vijana wanamzungumzia mzee bugu kwa sababu hata yeye amekuwa akimuhisi hivyo. Japokuwa alihisi wanamuongelea mzee bugu ila akaona bora awaulize wale vijana kuwa nani wanamuhisi ili endapo watamtaja mzee bugu atakuwa kapata uwakika kuhusu mzee bugu kuwa kweli ni msaliti.

MFALME: Ehe vijana nani huyo munamuhisi kuwa ni msaliti wa hiki kijiji na ndie chanzo cha haya matatizo.

KIJANA: Ni mzee SUBE mtukufu mfalme.

MFALME: Eeeee !!! Munasemaje nyie vijana?.

alishangaa sana kusikia vile maana hakutegemea kama wangemtaja mtu anae mwamini kupitakiasi.

KIJANA: Ndio hivyo mtukufu mfalme, mzee Sube ndio chanza cha haya matatizo.

MFALME: Hahaha nyie vijana munanchekesha sana. Mzee sube mimi ninamjua vizuri tena sana, katika wazee ambao nina waamini hapa kijiji mzee sube ndie namba moja alafu leo ndio mje mniambie kuwa yeye ndio msaleti.

Mfalme alicheka sana na kuhisi wale vijana wametumwa na baadhi ya watu pale kijijni kutokana mzee sube kuwa karibu nae.

KIJANA: Tunajua sio rahisi kutuamini kwa sababu mzee sube kwa sasa upo karibu nae kwahiyo uwezi kuona ubaya wake ambae amekuwa akiufanya.

MFALME: Najua mnasema hivyo kwa sababu mzee sube yupo karibu na mimi na nimempa cheo kwahiyo mkaona bora mje kumuaribia ili nisielewane nae au itakuwa mumetumwa nyie ?. Sasa nasema huo mpango wenu mmeshindwa kufanikiwa.

Vijana wliumia sana na kuona mfalme hana nia ya kusaidia kijiji bali yupo kwa ajili ya kumlinda mtu mmoja, lakini hawakukata tama wakaendelea kuongea nae.

KIJANA: Mtukufu mfalme sisi atujatumwa na mtu yoyote kama wewe unavyofikilia bali hiki tunachokuambia ni kweli na ipo siku utakuja kuamini tunachokuambia.

MFALME: Mh ! Leo nimeamini kuwa sio kila mtu anapenda mafanikio ya mwenzake bali kuna watu wanapenda kumuona wenzao wakiwa wanaiishi kwenye maisha ya shida. Sasa nyinyi mumekuja kuniambia hivyo ili mimi nifanye nini.

KIJANA: Kwanza tumekuja kukupa taarifa ya kumgundua mbaya wa kijiji pili tumekuja kuomba ruhusa ya kumchunguza yule mzee.

Mfalme akajibu kwa jeuri..

MFALME: Mkitoka kumchunguza yeye mje kunichunguza na mimi, endapo itaonekana mnamsingizia hukumu ya kifo itakuwa juu yenu .

KIJANA: Sawa mtukufu mfalme ila leo usiku tunaomba uje kwenye ile nyumba ambayo ipo karibu na nyumba ya yule mzee ili uone mwenyewe tabia zake, ila utamapokuja angalia asikuone na mtu yeyote sana sana mzee sube pamoja na mke wake.

MFALME: Sawa nitakuja ila narudia tena ikionekana mnamsingzia hukumu ya kifo itakuwa juu yenu.

Walipomaliza maongezi wakaondoka na kumuacha mfalme akitafakari maneno yao huku akipanga na adhabu ambazo watapata pindi ikijulikana wanamsingizia mzee sube. Kuanzia hapo masaa yalienda na hatiamaemda wa kwenda kwenye kazi ukawadia, wale vijana wakajikusanya sehemu moja na kwenda kwenye ile nyumba waliyokuwa wamekaa siku ya kwanza

Baada ya mda kidogo kupita mfalme akawasili sehemu ile na kuwakuta vijana wakiwa wamejianda na kila aina ya dhana kwa ajili ya kupambana na yule nyoka pindi wakifanikiwa kumuona, kijana mmoja ambae ndie alikuwa kama kiongozi wa wale wenzake akamkaribisha mfalme.

KIJANA: Karibu sana Mtukufu mfalme, tumefurahi kukuona maana ukweli utadhihrika mbele yako..

MFALME: Sawa lakini endapo sitaona kitu chochote mahara hapa nawaahidi adhabu ya kifo itakuwa juu yenu sitakuwa na msamaha na mtu, na wala sitaangalia umuhimu wenu hapa kijijini.

Japokuwa mfalme alikuwa akiongea maneno makali, wao hawakuogopa maana waliamua kujitolea kwa ajili ya kijiji chao, waliendelea kuongea nae huku baadhi yao wakiwa makini kuangalia kwenye kile kichaka wakisubilia kuona nini kitatokea. Mda ulienda bila ya mafanikio ya kuona kitu chochote hofi zikaanza kutawala nafsini mwao vijana wale kila walipokuwa wakikumbuka maneno ya Mfalme, baadhi yao walijuta na kujirahumu kwanini walienda kumpa taarifa mfalme lakini walikuwa wameshachelewa.

Ilipofika majira ya saa sita usiku wale vijana walijishukuru na kuona wameshindwa kuifanya ile kazi na kuhisi walidhania kitu kisichokuwa kweli, ndipo wakaamua kulala wakisubilia adhabu yao ikifika kesho yake asubuhi. Kwa upande wa mfalme hakuitaji kulala alijitahidi kupambana na usingizi ilimradi aone kile walichokisema vijana, japokuwa wenyewe walikata tama na kukili wamekosea. Sasa kwa upande wa Sube na mke wake na wao walikuwa macho wakiongea kuhusu Yoka.

SUBE: Kuna wazo nimelipata kuhusu Yoka.

BIBI SUBE: Wazo gani .

SUBE: Ninaona huyu nyoka tumwamishe tumpeleke msituni awe anaishi huko maana naona kama watu wameanza kutuchunguza.

BIBI SUBE: Sawa sio vibaya kama umeona hivyo, kwahiyo huku kijijini hata onekana tena.

SUBE: Ataonekana ila sio sana, ila sasa hivi ninataka awe anaenda mpaka kwenye kijiji cha Mbui kwa mfalme Koe ilituzidi kujulikana.

BIBI SUBE: Sawa nimekuelewa.

SUBE: Sawa, alafu twende tukamuangalie mdudu mwenyewe maana tuna siku nyingi hatujamwangalia.

Wakanyanyuka kuelekea kwenye kile kichaka, wakikwa awajui hili wala lile linaloendelea zidi yao. Mfalme wakati anaendelea kuangalia angalia huku macho yake yakilazimiisha kufumba, Ghafla akamuona Sube akiwa ameongozana na mke weka, kisha wakatazama pande zote kama mwizi anapoenda kuiba. Mfalme akashtuka na kufikicha macho yake yaliojaa ukungu kutokana na usingizi mzito aliokuwa nao, kisha akatulia na kuangalia kwa makini nini wawili wale wanataka kufanya. Sube alipoona nje hakuna mtu yoyote akaanza kupiga mluzi mara kwenye kile kichaka akatoka nyoka mkubwa mwenye kung’aa na kusogea walipo wawli wale.

Mfalme alishtuka sana utadhani yule nyoka alikuwa amemfuata yeye alitamani kupiga makelele kutokana na uwoga lakini akajikaza kiume na kuendelea kuangalia nini kitafanyika. Sube akachuchumaa na kumpaka unga Yoka kisha akaongea maneno Fulani ambayo mfalme hakusikia kisha nyoka akaondoka, wawili wale na wao wakarudi ndani kulala maana walikuwa tayari wamemaliza kazi yao. Mfalme alisikitika sana kisha akawatazama wale vijana alitamani awaamushe ili awaambie kile alichoona lakini moyo wake ulisita, kutokana na ukaribu aliokuwa nao yeye na mzee sube,

Ndipo akaamua kulala huku mawazo mengi yakitawala kichwa chake maana alikuwa ajui aanze wapi kuwaambia wanakijiji pamoja na wale viongozi kuhusu swala lile. ilipofika asubuhi na mapema mfalme aliamke na kurudi nyumbani kwake bila kumuaga kijana yoyote pale ndani maana wao walikuwa bado hawajaamka. Alipofika kwao mda wote alikuwa mtu wa kijiinamia, jambo ambalo lilimshangaza sana mke wake kwa sababu haikuwa kawaida yake kuwa vile, ndipo akahitaji kufahamu nini kimemkuta huko atokako.

MKE: Mume wangu mlikoenda mlifanikiwa au wale vijana walikuwa wanamsingizia yule mzee wa watu.

Mfalme kwa kuwa hakutaka mzee sube ajulikane akaona bora amdanganye mke wake japokuwa hakupenda kufanya hivyo.

USIKOSE SEHEMU IJAYO

Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)