SEWATO: KOSA LA DAMU (10)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
ghafla ule mchanga ukamrukia usoni, akaanza kuungua kama vile amemwagiwa asidi.aliungua nyama zote nakubaki mifupa.hule mchanga ukaanza kutambaa nakuwafata wale askari pori wengine kwa kasi.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
walitimua mbio kila mtu njia yake,ule mkufu ukabaki pale chini.

**********************************

Upande wa pili inspecta mkuta pamoja na angel na madam mary walimkokota Prof Moses hadi kwenye hule mto ambao walipelekwa na yule askari wa mfalme. Wakupumzika hapo giza lilikuwa lishaingia walikula matunda pori nakulala.asubuhi na mapema walidamka salama bila ya matatizo, Angel alikwenda kunawa uso mtoni kwa mbali akamuona mtu anakuja upande wao akiwa hoi kabisa,angel alihisi kusisimuka. Ghafla yule mtu akapotea machoni pake,mara akahisi tofauti tofauti ile hali ya kusisimuka ilikuwa tu ya kawaida tofauti alivyokuwa amevaa ile cheni mara ya kwanza,akajishika shingoni akuiona ile cheni wasi wasi ukamshika akakimbia nakuchukua kioo kidogo alichokuwa nacho kwenye kibegi chake nakujiangalia hakuuona,"mh! hii si kawaida mbona ile sauti siisiki tena alafu huu mkufu nao mbona si huoni?,au umedondoka?!!"

angel alijiuliza maswali ambayo akuyapatia majibu, akaanza kuutafuta kama chizi,alifunua hadi mawe kama umedondoka kapo,lakini akufanikiwa kuupata.hadi wenzake wakaanza kumshangaa,madam mary akumuuliza anatafuta nini,angel akaanza kulia.ikabidi madam Mary amsogelee nakumbebeleza huku akimuuliza kipole amepoteza nini.angel akamwambia kwamba amepoteza cheni yake aliyopewa kama zawadi na wazazi wake kwamba haitunze kama moyo wake.madam mary akampa pole nakuanza kumsaidia kuutafuta.

Kwa mbali yule askari wa mfalme aliwaona angel na wenzake,aliamua kuwafata,lakini alihisi njaa kali akaona matunda kwenye mti akayapalamia kwa pupa nakuyachuma akachukua moja nakulila kwa pupa,ghafla alihisi lina radha mbaya kama ya mwarobaini,akallitema alihisi kukosa nguvu akajikokota nakufika hadi kwenye mto alihisi kiu kali,akachota maji kwa mkono nakuyanywa mara akayatema baada ya kuhisi ni machungu sana,akakosa kabisa hamu,akaamua kuwafata wenzake safari hii aliishiwa nguvu kabisa alipauka ngozi na mdomo wake kuchanika chanika nakutoa maji maji,aliwafikia akadondoka chini kama mzigo,

walishituka sana kumuona walimgundua sababu ya mavazi yake japo yalikuwa yameraruka raruka,wakamfata nakumweka kimvulini angel akamchotea maji na kumpa,aliyanywa lakini akayatema walimsihii anywe ili apate nafuu lakini yalimshinda.aliyanyuka baada ya kuuona mti fulani ambao aliamini ni dawa aliufikia nakuuchuma,lakini haukung'ooka kwa bahati mbaya tawi la mti huo lilimkata kidoleni,akaamua kuinyonya damu yake ili isiendelee kotoka,alipopitisha kukiweka mdomoni kidole,pua zake zikahisi harufu nzuri ajabu,alipokiweka mdomoni kidole alianza kunyonya ile damu yake,alihisi radha nzuri ambayo akuwahi kuhisi maisha yake yote,alijingata aili damu iendelee kutoka,aliinyonya kwa kasi sana mara damu yake ikamkifu/ikamkinai.

angel alibaki mdomo wazi hanamushangaa tu.ghafla yule askari akaliona jeraha la inspecta mkuta akahisi harufu ya damu akaanza kumfata kwa kasi wakati huo huo askari pori mmoja kati ya wale walioruka kutoka kwenye helicopter alikuwa anakuja upande wao kwa kasi huku akihema,nyuma yake hule mchanga ulikuwa unamfukuza kwa Kasi sana,alifika na kudondoka chini.inspecta mkuta alimjua nakumuuliza kuna nini bila ya kutojua anafatwa na yule askari wa mfalme,yule askari pori alijikuta anashindwa kuongea kutokana nakuhema sana alibaki anaonesha tu kwa kidole kule hule mchanga unapotokea.ghafla yule askari wa mfalme alimn'gata kwenye mguu wa inspecta mkuta nakumunyonya damu........

inspecta alihisi maumivu makali sana,alimpiga teke moja lililomuondoa yule askari wa mfalme kwenye mguu wake,kila mtu akabaki mdomo wazi akiwa amini alichokiona,yule askari wa mfalme alipodondoka alinyanyuka huku akijiramba damu,akahisi nafuu kidogo baada ya kunywa damu,mara akamwangalia madam mary kwa uchu wa damu na kiu aliyokuwa nayo,wakati huo huo hule mchanga ukatia timu kwa kasi, ukaanza na yule askari pori,ulimrukia nakumuangamiza,alimomonyoka kama aliyemwagiwa asidi.

Angel alimshika mkono prof Moses hakisaidiana na madam mary wakatimua mbio nakutokomea ndani ya msitu huo.akabaki inspecta mkuta na yule askari wa mfalme.mkuta alitambaa kujaribu kujiokoa,yule askari alikuwa bado ana njaa akamfata inspecta mkuta,lakini ghafla hule mchanga ukamrukia yule askari wa mfalme,yeye akuungua ila alianza kubadilika mwili wake,inspecta alishuhudia tukio zima,hule mchanga ambao ndio yule kiumbe wa ajabu ukauungana na askari wa mfalme,mkuta alikata tamaa ya kuishi akabaki tu anasubiria yule kiumbe amuangamize kwani akuweza tena kukimbia wala kutambaa sababu damu nyingi ili mvuja kwenye jeraha lake ambalo sasa limetoneshwa kwa kung'atwa na askari wa mfalme.

baada ya ule mchanga kuungana na askari wa mfalme,alibadilika nakuota manyoya mwili mzima kichwani pembe zikachomoza nakurefuka kucha zikaongezeka nakuwa ndefu ajabu,meno yalitokeza nje kwa urefu,inspecta alipo ona hivyo aligahiri kufa sababu alikuwa anatisha sana yule kiumbe inspecta alipiga kelele za kuomba msaada,kwa bahati nzuri wenzake walikuwa karibu na eneo hilo wakasikia kelele za inspecta mkuta,walizifuatilia zinakotokea.

Kile kiumbe kiliuvaa mwili wa yule askari,kilijinyoosha kisha kilitoa kicheko cha ajabu na cha kutisha ghafla hali ya hewa ikabadilika,wingu zito likatanda angani,radi zilipiga zikifuatiwa na ngurumo kali,kilimgeukia inspecta mkuta pale chini akipiga kelele kuomba msaada kikapiga hatua za kibabe kumfata inspecta,kidogo wenzake wanafika nakumuona inspecta mkuta akiwa yupo chini na yule kiumbe anamsogelea,inspecta martin anawaamurisha kushambulia,walimumiminia risasi mfululizo,kile kiumbe kikahairisha kumfata mkuta kikawageukia walio kuwa wanamsambulia,

akikudhuhurika na zile risasi kwani ziliingia nakutoka kisha jeraha linapona,ghafla mmoja mmoja risasi zikamuishia hadi wakajikuta wamemaliza risasi wote na adui bado mzima kabisa,wakiwa wanaangaliana yule kiumbe anaruka na kumkamata mmoja wao kinamnyanyua juu kisha kinamnyofoa kichwa huku wanashuhudia,ikabidi wamcheze mchezo yule kiumbe martin alimfata yule kiumbe akiwa kashikilia kipande cha mti mkononi,anaanza kupambana nae,huku inspecta mkuta akinyanyuliwa na askari wengine kisha wakatokomea naye nakuelekea waliko kubaliana kukutana,inspecta martini alipoona wenzake wameondoka na yeye akaacha kupambana na yule kiumbe,akamrushia kile kipande cha mti yule kiumbe kikaudaka,

inspecta martini akageuka nakuanza kutimua mbio kama swala,yule kiumbe alimrushia kile kipande cha mti kikaenda na kumpiga kichwani akaanguka chini inspecta mart,kisha kikamfata kwa hasira na kumnyanyua juu kwa mkono wake mmoja,kisha kikamsogeza karibu na uso wake,wakawa wanatizamana uso kwa uso,martini aliogopa sana kwani kile kiumbe kilitisha sana,kikamnusa kwa pua zake,kisha kikafunua mdomo wake nakutoa meno yake nje ili kimn'gate shingoni nakumnyonya damu lakini kabla akijamtimia meno kikahisi hali ya hatari kikamuachia inspecta martini hakadondoka chini,kile kiumbe kikawa kinaangalia juu huku kikigeuka geuka rangi yake ya mwili wake nakuwa nyekundu ghafla kikapotea nakumuacha inspecta martini akiwa amini kama yupo hai,alisimama huku kashika kichwani nakukimbia kuelekea kule waliko wenzake..

****************************

Angel akiwa na walimu wake wanakimbia nakujikuta wamerudi kule ambako yule kiumbe alibadilika nakuwa mchanga wakiwa wamechoka,wanajipumzisha kidogo chini ya mti mmoja,Kimya kikuu kinatawala kati yao zikisikika tu pua zao zinavyovuta hewa safi ya oksijeni,Angel anahisi kumulikwa na kitu chenye mn'gao fulani kilichoakisi mwanga wa jua nakutoa miale sababu yakumulikwa na jua,angel anaamua kukifuata,anapokifikia hanagundua ni mkufu akauokota nakuangalia,"mh! Huu utakuwa wa nani??,aliwaza,akaamua kuutupa sababu akuzoea kuokota vitu hasivyovijua nakuvichukua sababu ya familia hanayotoka kujiweza kiuchumi.alipoutupa hule mkufu ukadondokea pale ambapo yule kiumbe alibadilikia nakuwa mchanga,pakafuka moshi ulioongezeka kidogo kidogo,Angel alirudi nakupumzika na wenzake,Ghafla akauona hule moshi akashituka.

Eeeh huo moshi umewashwa na nani??,akasimama haraka nakwenda kuuzima,alipofika alipigwa na butwaa baada ya kuuona hule mkufu ndio unatoa moshi,aliinama nakuokota ghafla ule moshi ukazima,akiwa anauangalia aliushangaa sana kwa hayo maajabu,ghafla yule kiumbe akatokea mbele yake akuwa amekasirika sana,Angel alipoinua kichwa kuangalia alipiga kelele nakutaka kukimbia lakini...............

Lakini yule kiumbe alimuwahi nakumkwaruza mgongoni na kucha zake za kutisha alidondoka chini,Angel alikuwa ameuondoa hule mkufu pale ulipokuwa unatoa moshi akawa ameushika mkononi,kwa hali hiyo yule kiumbe alirudi kwenye hali yake kwa kubadilika ile rangi nyekundu,kwani kipindi hule mkufu unapachoma pale chini kile kiumbe kilikuwa kinaumia.

Kilipojisikia vyema kikajinyoosha kisha kikaanza kumfata Angel pale chini,wakati huo madam Mary pamoja na Prof Moses aliyekuwa hajiwezi sababu ya kukoswa koswa na kiumbe wa ajabu,walikuwa wakimpigia kelele Angel amke pale chini kwani yule kiumbe alikuwa anamfata ili kummaliza,Angel aliugulia maumivu makali pale chini ghafla bin vuu yule kiumbe akamfikia kilitoa kicheko cha kutisha kilichowafanya wazibe maskio yao kwa mikono yao,Angel alijigeuzwa nakulalia mgongo yule kiumbe alimsogelea na kutaka kumnyonya damu,

Angel alinyanyua mikono yako ili kujaribu kumzuia yule kiumbe hasimdhuru,Angel alilia sana huku akimsihi yule kiumbe asimdhuru/asimuue.hule mkufu aliushikilia mkononi akiwa hana wazo lolote kuhusu mkufu, huo ndio hulikuwa wakati mzuri wa kumvalisha mkufu kiumbe huyo,yule kiumbe alimkaba kwa nguvu kooni nakumvuta kwake,Angel alimgusa yule kiumbe akiwa ameushika hule mkufu,ghafla hule mkufu uliwaka na kutoa miyonzi iliyong'aa kama moto,ilimwingia yule kiumbe kifuani nakumsababisha amwachie Angel,kikaanza kung'oa miti ovyo huku kikipiga kelele za kutisha,msitu mzima hulitulia tuli kelele zake tu ndizo zilisikika msitu mzima,ghafla kikapotea kimiujiza.

Angel alidondoka chini nakukohoa mfululizo madam mary alimkimbilia nakumnyanyua wakaondoka.

********_________-----------_______*** mvua ilianza kunyesha kwa Kasi ilikuwa ni mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)