SEWATO: KOSA LA DAMU (9)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
kile kiumbe kilimfukuza inspecta,angel halikuwa hakikohoa sana sababu alikabwa koo kisawa sawa,yule askari aliyekuwa akiitwa benedict,alimnyanyua angel na kuondoka naye japokuwa kulikuwa na giza tororo,

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
waliwaacha wale askari wengine wawili pamoja na dereva wakiwa bado hawajazinduka.

*******************************

Kulipambazuka jua lilikuwa lishaanza kuchomoza madam mary pamoja na Prof Moses wakiwa na askari wa mfalme mmoja tu aliyebaki kati ya 15,walikuwa wamejipumzisha juu ya mti mkubwa usiku mzima,Mary alikuwa kaukota hule mkufu,walishuka chini ya mti huo nakuanza safari ya kwenda kumuangamiza yule kiumbe kwa kutumia mkufu huo,matumbo yaliwauma kwa njaa na kiu kali iliyatesa ma koo yao waliishiwa nguvu kabisa,walitembea wakiwa makini huku wakishikana mikono,kwa bahati nzuri yule askari alikuwa ni mzoefu na msitu huo,aliwaongoza njia ya kuelekea kwenye mto iliwaweze kukata kiu,walifika nakunywa maji kwa pupa madam mary akampa yule askari wa mfalme ule mkufu aliuuweka kwenye kibegi alichokiokota msituni mkufu huo ulijinasa kwenye zipu ya kibegi hicho bila ya yeye kujua,

walikunywa maji kwa pupa baada ya kutosheka walielekea sehemu yenye matunda wakachuma na kuyafakamia,wakiwa wanaburudika na matunda ghafla wanakutana uso kwa uso na inspecta mkuta akiwa hoi katapakaa damu mwili mzima,kumbe yule kiumbe alimjeruhi,alidondoka chini huku akihema kwa tabu,walimchukua nakuondoka naye lakini kabla hawajafika mbali wanasikia sauti ya helicopter,wanapata matumaini mapya,wakiwa bado wanatahamaki yule kiumbe anatokeza mbele yao akiwa kashika mguu wa binadamu,inspecta aliugundua ni wa benedict kutokana na kiatu alichokuwa kakivaa marehemu,ghafla anawafata pale walipo,mary anamwambia yule askari wa mfalme autoe ule mkufu wamalize mchezo,

kabla ajautoa yule kiumbe alimvaa yule askari akiwa bado hanaangaika kuuchomoa ule mkufu kwenye mfuko wake ukiwa umekwama kwenye zipu,kile kiumbe kilimkwaruza na makucha yake usoni,inspecta akajitoa mwanga na kuokota kipande cha mti akiwa anachechemea nakumfata yule kiumbe,prof Moses naye alihisi kuchanganyikiwa ajui afanye nini,ghafla helicopter ya askari pori inafika nakushuudia lile tukio,wanaamulishwa na inspecta martin kumshambulia yule kiumbe,risasi nyingi zinalengwa kwa yule kiumbe nakumfanya azidi kukasirika,anaachana na yule askari wa mfalme na kuanza kukwepa risasi,Prof moses na wenzake wanakimbia kutoka sehemu hiyo,

yule kiumbe anaharibiwa aribiwa sura na zile risasi kutoka kwenye helicopter,kinaruka juu ya miti hadi kinaifikia ile helicopter na kuipa pigo moja liloisababisha ikose mwelekeo nakuanza kuyumba yumba ikitoa moshi,maaskari hao wanajishikilia kwa nguvu huku helicopter hikizunguka zunguka angani,rubani anajitahidi kuishusha lakini inamshinda,kwa bahati nzuri,rubani aliuona mti mkubwa wenye matawi mengi aliilengesha hapo,ilishuka kwa Kasi walijirusha nje na kuiacha helicopter ikienda chini bila mtu,mlipuko mkubwa ulitokea ndani ya msitu huo,wale askari waliumia na kupata majeraha madogo madogo.

************************

Prof Moses na wenzake walijikokota nakufika kwenye kambi yao,kabla hawajaingia ndani ya hema,wanamuona angel akiwa pekee yake bila ya yule askari pori,walimuuita ili aje,angel alipowaona alijawa na furaha,akapata nguvu kidogo,japokuwa aliishiwa chakula na maji alijihisi mwenye nguvu mpya,aliwakimbilia huku akiwa haamini kama hatakuja kukutana na walimu wake,lakini kabla hajafika ile sauti inasikika kichwani mwake ikimwambia"Angel usiende utauliwa kabla hujafika rudi".angel alisimama ghafla nakuangaza huku na kule,"jamani muondokeni hapo mtakuf....kabla hajamaliza kuongea yule kiumbe anatokea nyuma ya prof Moses tena kinapumua nakutoa moshi mweusi puani........

angel alipowaona alijawa na furaha,akapata nguvu kidogo,japokuwa aliishiwa chakula na maji alijihisi mwenye nguvu mpya,aliwakimbilia huku akiwa haamini kama hatakuja kukutana na walimu wake,lakini kabla hajafika ile sauti inasikika kichwani mwake ikimwambia"Angel usiende utauliwa kabla hujafika rudi".angel alisimama ghafla nakuangaza huku na kule,"jamani muondokeni hapo mtakuf....kabla hajamaliza kuongea yule kiumbe anatokea nyuma ya prof Moses tena kinapumua nakutoa moshi mweusi puani..Songa nayo sasa......

Angel alikiona kile kiumbe ila wao hawakukiona sababu walikipa mgongo,"prooofesa angaaliiaa nyuumaaa yakoo utakufa,ondoka haraaka"

Prof aligeuka nyuma nakumuona yule kiumbe uso kwa uso,kilimkaba shingo nakumrusha mbali,kisha kikamfata yule askari wa mfalme aliyekuwa na ule mkufu wakumfungia kiumbe huyo,askari huyo alijerehuriwa na huyo kiumbe kipindi akijaribu kuitoa cheni kwenye begi lake hivyo alikimbia kwa shida,kiliruka na kwenda kumrukia askari huyo,kikaangka naye chini kisha,kikamkaba koo,askari huyo alifumbua mdomo nakukoroma huku akitapa tapa kujaribu kijiokoa,kilitoa moshi mweusi puani mwake huku kikihema kwa hsira,kilitapika wadudu wengi jamii ya funza kutoka kinywani mwake,wadudu hao walitambaa na kuanza kumuingilia mdomoni yule askari.

Madam mary pamoja na angel wakiwa na inspecta mkuta walimkimbilia prof moses pahali alipodondokea,walimunyanyua kwa tabu nakukimbia huku nyuma walimuacha yule askari wa mfalme akisurubishwa na yule kiumbe.

Yule askari wa mfalme alijaribu kuufumba mdomo wake lakini kile kiumbe kilimkaba koo nakumfanya aufumbue ili wale wadudu wamuingilie,ghafla akakumbuka hana ule mkufu ndani ya begi,alipitisha mkono hadi ndani ya begi nakuushika lakini kwa bahati mbaya ulikuwa umenasa kwenye zipu ya begi,ikabidi haunyanyue hivyo hivyo na begi nakujaribu kumvaalisha yule kiumbe,lakini aliishiwa nguvu,kwa bahati nzuri ule mkufu ulimgusa yule kiumbe ukawaka nakutoa ile miyonzi kile kiumbe kiliona hatari ipo mbele yake kikapotea nakumuacha pale yule askari,iyo ndio ikawa pona pona yake,akaanza kuwatapika wale wadudu.huku akiwa haamini kama kaponea chupu chupu,alihisi kichwani kitu kikimuendesha alianza kutoka damu puani huku macho yake yanabadilika nakuwa kama ya yule kiumbe alihisi kutetemeka na mwili kuhisi baridi kali ajabu,akajikokota huku akiyumba yumba kama mlevi wa pombe aliutoa ule mkufu kwenye begi nakuushikilia mkononi

**********************************

Upande wapili baada ya kufanikiwa kuruka kutoka kwenye helicopter,kikosi cha askari pori waliotumwa kuja kufatilia wanachuo wana hali gani,Nao wanajikuta katika hali ngumu kila kitu Chao kililipuka ndani ya helicopter ikiwemo risasi na simu za satellite kwa ajili ya mawasiliano na makao makuu yao,walijikokota wakiwa hawajui waeleke wapi japokuwa walikuwa ni askari pori,walipiga hatua wakiwa makini,kwani tayali walishajua ndani ya msitu huo mkubwa wa sego,kuna kiumbe hanafanya mauaji,walikuwa jumla kumi na tano,silaha walikuwa nazo ila risasi zilikuwa chache,walipokuwa wanatembea walisikia sauti za ajabu zikiwafata,

zilikuwa zinawachanganya na kuwazidishia uhoga,sauti hizo hazikuwa na pahali sahihi zinakotokea,wao walishitukia tu wanasikia kama mtu anacheka nyuma yao walipogeuka nyuma zinazikika tena kwingine,ghafla askari mmoja alipotea kwa mazingira yakutatanisha wakiwa bado wanashangaa mwingine tena anapotea,kiongozi wao inspecta martin akatoa amri kila mtu ajiweke tayali kwa mashambulizi,kila mtu akachukua eneo lake nakujibanza,askari mmoja alijibanza kwenye mti mara akadondokewa na kitu kama maji maji kichwani alipotizama juu yule kiumbe kumbe alikuwa juu ya mti,alimnyofoa kichwa kikabaki kiwiliwili kikifyatua risasi ovyo,risasi hizo ziliwakosa kosa wenzake,walipoona hali imekuwa ngumu wakaamua kukimbia lakini kabla hawajakimbia maiti za wenzao wawili zinarushwa nakudondokea mbele yao zikiwa zimekauka kama zilianikwa juani miaka mitatu huku macho yamekuwa meupe pee,

Ghafla tena kile kicheko kinajirudia na hapo hapo askari mwingine anashikwa miguu nakuvurutwa nyuma kwa kasi na yule kiumbe,askari pori hao wanamfukuzia huku wakimumiminia risasi mithili ya mvua ,kile kiumbe kiliwacha hatua chache nyuma wale askari pori,ghafla kikakutana uso kwa uso na yule askari wa mfalme tena kaushika hule mkufu mkononi,kile kiumbe kilimwachia mguu yule askari pori kisha kikamfata yule askari wa mfalme kwa kasi huku kikianda kucha zake kwenda kumfyekelea mbali.........

Askari wa mfalme gumbo alijianda kupoteza maisha yake ila alihapa kufa na kiumbe huyo,yule kiumbe alizidi kumsogelea kwa Kasi ya hatari,ghafla kilisita nakusimama huku kikimwangalia yule askari kwa kumshangaa,yule askari wa mfalme alikuwa hoi kachoka baraa na yeye ghafla akasita kumsogelea yule kiumbe,kumbe wale wadudu waliomuingilia walianza kumbadilisha akili Yule askari wa mfalme,kile kiumbe kikaanza kucheka huku kikiangalia juu na kunyanyua mikono yake juu kuashiria ushindi,yule askari wa mfalme akaanza kubadilika usoni kwa kubadilika macho na kuwa kama ya yule kiumbe,

huku akitapika damu nyingi,kichwa kilimuuma nakuanza kuangaika lakini aliona huo ndio muda mzuri wa kumuangamiza yule kiumbe alimsogelea nakuunyanyua ule mkufu ili amvalishe yule kiumbe,wakati huo huo wale askari pori nao ndio wanafika nakushuudia mambo ya ajabu,yule askari wa mfalme alipotaka kumvisha yule kiumbe,alijikuta akili yake inabadilika hapo hapo nakuhairisha,ghafla anahisi kiu ya damu mbichi pamoja na njaa akiwa bado ajielewi hule mkufu unawaka nakumchoma kwakuwa na yeye sasa alikuwa ameishabadilika akili,alihisi maumivu makali aliurusha hule mkufu juu,ukaenda moja kwa moja na kumuingia yule kiumbe kwenye moja ya pembe zake nakukwama.

ghafla ukatoa miyonzi mikali nakumuingia yule kiumbe.mwili wake ukawaka moto kama wa petrol kiliangaika sana,kiliwaka moto huku kikimomonyoka kiuongo kimoja kimoja nakuwa majivu,kwa bahati mbaya wakati kinahaangaika hule mkufu ulichomoka kutoka kwenye pembe ghafla ule moto ukaanza kuzimika,bila kuchelewa wale askari pori walimwagia mvua ya risasi nyingi.kilipasuka pasuka nakuwa mchanga.Yule askari wa mfalme alitimua mbio nakutokomea ndani zaidi ya msitu huku akitetemeka kama aliyemwagiwa barafu.

Wale askari pori waliusogelea ule mchanga nakuushanga askari mmoja akauona ule mkufu,akafanya tena kosa jingine akaunyanyua kutoka kwenye ule mchanga,akawa amemuamsha tena yule kiumbe, ghafla ule mchanga ukamrukia usoni, akaanza kuungua kama vile amemwagiwa asidi.aliungua nyama zote nakubaki mifupa.hule mchanga ukaanza kutambaa nakuwafata wale askari pori wengine kwa kasi.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)