SEWATO: KOSA LA DAMU (3)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
hakangana lakini ikafeli,gari hilirudi nyuma kwa kasi kali,mashaka halivuta hand breki(breki ya mkono)ikasababisha gari igeuke kitendo hicho kilisababisha mizigo haliyoipakia kuizidi gari uzito na kupinduka mara nne.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Tajiri mmoja aliyekuwa anafanya kazi TRA,alikuwa hakitoka congo kuja tz,baada ya kwenda kumsaidia ndugu yake aliyekuwa anasumbuliwa na mauzauza nyumbani kwake kwa kumpeleka kwa sangoma mmoja maarufu congo ili amsaidie,alimwachako ndugu yake huyo congo,sababu alikuwa bado anafatilia mzigo fulani wa mbao aliyokuwa kagiza.

Tajiri huyo aliyeitwa brown,alikuwa kwenye gari aina ya prado vx nyeusi,alipita barabara kuu akielekea mpakani,ghafla alifunga breki baada ya kuona magunia yametapakaa barabarani kidogo hagonge gunia moja,alihamua kushuka na kuangalia kulikoni,alipoangalia vizuri aliona gari aina ya pick up ikiwaimepata ajari.............

Brown alitembea huku akiwa anatazama huku na huku,akiangalia kama kuna gari nyingine inakuja aliisogelea ile gari karibu na kutazama kuna nini,aliona michirizi ya damu ikiwa imetapakaa karibu na iyo gari,

Alipoangalia ndani aliiyona maiti ya mwanaume (ambaye ni mashaka) na kwa pembeni kuna maiti ya mwanamke ambaye anaonekana kama kuna kitu kakikumbatia,brown alivyoona hivyo akajiambia,duh kesi hii hapa nikikutwa tu ntabebwa nikatoe ushaidi polisi,na nchi yenyewe hii ya watu,haliamua kuondoka zake lakini hali hisi kitu kama kina nyonya kitu alihamua kurudi kwenye gari hiyo iliyokuwa imepinduka matairi yakiwa yanaangalia juu,ili mbidi hainame chini na kutafuta hicho kitu kilichokuwa kinatoa sauti kama mtoto anaye nyonya kitu,halipomwangalia mashaka alikuwa kaisha kufa,

alipomwangalia chausiku aliguna,mh! hina maana huyu mwanamke alikuwa na mtoto alisimama haraka na kwenda upande wa pili wa gari hiyo na kufungua mlango wa gari hiyo na kumchukua yule mtoto,alikuwa kaisha lia hadi akahamua kunyonya shuka aliyokuwa kafunikwa na mama yake,brown alimchukua na kuondoka naye fasta,ilikuwa ishatimia sasa saa kumi na mbili kamili,halijiuliza maswali mengi njiani juu ya mtoto huyo,mh mungu nisaidie nifike salama aliendesha kwa kasi hatimaye hakaingia bukoba mida ya saa mbili kasoro usiku alichukua chumba hotelini kisha akamuulza muhudumu mmoja hotelini hapo,

maduka yalipo hakarudi kwenye gari na kuelekea dukani alimnunua maziwa,baby diper,nguo na nyonyo ya kumnyweshea,kisha alirudi hadi hotelini alikopanga chumba,alimnywesha yale maziwa yule mtoto alinyonya yale maziwa kwa fujo,alimaliza pakti mbili za maziwa kisha alilala,brown naye alikula kisha hakajipumzisha,alipitiwa na usingizi hakalala fofofo.

Asubuhi na mapema aliwahi kuamka akamwandaa mtoto kwa kumpa maziwa hakamvua ile shuka aliona mkufu kwenye pindo la shuka hilo alichomoa hapo akamwosha kisha akamvalisha nguo na diper alizomnunulia kisha hakaoga na kuondoka hotelini hapo nakuanza safari ya kuelekea jijini mwanza kwa ajili ya kupanda private plane(ndege binafsi)yake iliyokuwa hikimsubilia,haliwahi sana kuondoka bukoba,alifika mwanza na kuruka na ndege alifika jijini dar usiku alikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwake,alipokelewa na wafanyakazi wake mfanyakazi mmoja alimbeba yule mtoto mke wa brown alitoka ndani nakuja kumsabai mumewe,karibu mpenzi,asante laazizi wangu,pole na safari,nshapoa ila niliyokutana nayo basi tu,nini tena.

Mara yule mfanyakazi akamleta yule mtoto,mh mume wangu na huyu mtoto umemtoa wapi,ni stori ndefu ila kwa ufupi wazazi wake wamefaliki,WAMEFALIKI aliuliza kwa mshangao,ndio nilipokuwa nakuja niliona pick up imepinduka alafu kuna damu nyingi zimetapakaa nilipoangalia vizuri niligundua wazazi wake wamefaliki ila kwa miujiza ya mungu huyu mtoto aliponea chupuchupu baada ya kumkuta kakumbatiwa na mama yake,mh maskini sasa tumpeleke kwanza hospitali tujaribu kumuombea kadi ya kliniki,wazo zuri twende.

*****************************

Baada ya miaka kumi na nane yule mtoto alikuwa kaisha kuwa binti mkubwa,alikuwa na sura ya kuvutia hakika halikuwa na sifa zote za kuitwa mrembo alikuwa kaisha maaliza form four anasubiria matokeo.

Angel,naam mama,ebu njoo uniletee pochi yangu chumbani,mi nmechoka yani we unanisumbua sumbua tu wakati kuna house girl,we naye humezidi kudeka mno.mama huyo hakujaliwa kizazi kwahiyo alimlea angel kama mwanae wa kumzaa,ila angel alikuwa ajuhi.

Baada ya mda kupita matokeo yalitoka halikuwa hamefaulu vizuri,baba yake alimlipia shule Australia alikwenda kusoma,baadaye alifaulu kwenda chuo kikuu,alirudi kusomea tz.alikuwa anasomea utafiti wa wanyama hasa sokwe,wakapangiwa field kwenye misitu ya congo kwenda kuwachunguza sokwe wa msitu wa congo........

Angel alifurahi sana,yeye pamoja na marafiki zake kwenda kwenye misitu ya Congo kwa ajili ya utafiti,Baraka rafiki mkubwa wa angel alikuwa hanampenda sana angel ila alikuwa hanaogopa kumwambia hakihofia kuvunja urafiki wao,maandalizi yaliaanza wakapewa maelekezo pamoja kuambiwa mahitaji yao binafsi ,tunaenda kule kufanya research yetu hii(aliiongoa professor Henry ambaye ndie mkuu wa safari),itatuchukua miezi miwili,mambo mengine tutakumbushana huko huko sawa,ndio professor waliitikia kwa pamoja,wakiwa wanarudi makwao mida ya jioni,baraka akiwa kwenye bajaji alichungulia nje nakuona gari ya angel ikiwa imepaki pembeni,mh! Ile si gari ya angel anafanya nini hapa,dereva ebu naomba usimamishe pembeni kidogo, alimwambia dareva wa bajaji asimishe bajaji

**********************

Angel aliwapa taarifa wazazi wake juu ya research yao wanayokwenda kuifanya congo,sawa si hatuna kipangamizi juu yako mwanetu mpendwa au siyo mke wangu,ni sawa ila ujichunge,huwe makini usije ukararuliwa huko na wanyama wakali hukatupa shida,mama mi ni mtu mzma sasa najua kuji take care,we jibu kila hisi la hisi ujue ukipatwa na matatizo ntakufa kwa presha m mama yako,wakati mazungumzo hayo yanaendelea simu ya angel ikaita namba ngeni(unknown number)mh! Sijui nani huyu(haliwaza angel huku hakinyanyuka na kwenda kuipokelea chumbani)hallow,(kimya),

we nani si uongee,(kimya),mh ngoja nikate watu wengine bwana sijui wakoje,halipotaka kukata mara hakasikia kicheko cha ajabu kwenye simu,haliitupa simu kitandani na kutaka kukimbia lakini mlango hukajifunga kwa nguvu wenyewe paaaa,kitendo hicho kikifanya hule mkufu wa malkia ambaye ndie mama yake mzazi na angel kudondoka kutoka kabatini angel alishangaa,aliokota ule mkufu hakiwa anaogopa,kichwani aliwaza,au nmesikia vibaya,akaifata simu yake pale kitandani,kisha akakagua ile namba

Nakujaribu kuipiga tena,akaambia haipatikana mara meseji ikaingia kutoka kwa rafiki yake recho,"we mda ushafika njoo unipitie home "alimkumbusha kwamba ampitie waende wakafanye shopping kwa ajili ya safari kesho kutwa.

Duh nilikuwa nishasahau,angel alikulupuka na kujiandaa haraka haraka,alipuuzia kile kicheko akihisi amesikia vibaya,aliondoka na gari aina ya Ford,akiwa njiani alitafuta kifaa maalum cha kunasa mawasiliano ya simu kiwekwacho sikioni kama earphone,wakati hanakitafuta aliuwona hule mkufu aliuvaa na kujiangalia kwenye kioo cha gari,alishituka baada ya kuona hule mkufu hauonekani shingoni,alifunga breki,ili auangalie vizuri,alipojitazama aliuwona akageuza kioo ili ajionea mara hakamuona mtu mwenye uso wa kutisha anaonekana kwenye kioo cha gari yake,

alipiga yowe lakini alipoangalia nyuma hakuona kitu,kidogo baraka anafika,angel alipomwona alifungua mlango na kumkimbilia na kumkumbatia kwa nguvu,please ni drive home naogopa mwenzio,kitendo hicho cha kukumbatiwa kilimchanganya baraka nakujikuta hakizidi kuzama kwenye penzi la binti huyo mrembo.kwani kuna nini angel,naona mauza uza kwenye gari,mauzauza,yeah,we hunazidi kuchanganyikiwa,hapana yani sielewi please naomba unipelekee,ok ngoja nimlipe dereva Bajaj, nilikuja naye ok fanya hivyo.alimpeleka mpaka nyumbani kwao,thanks baraka alimwaga kisha akaingia ndani kupumzika.

***********************

Siku ya safari ilipofka walikuwa wote ndani ya ndege huku wakiwa wenye nyuso za furaha,walikuwa wanataniana na kucheka,waliwasili congo baada ya safari ya siku nzima,walikwenda kwenye hoteli ya kitalii waliyokuwa teyali washaifanyia booking,walikuwa jumla kundi la watu 26,wkiwemo maprofessa wanne,kulipopambazuka wakaingia msituni kwa ajili ya kufanya tafiti yao,kila mtu alibeba vifaa vilivyoitajika,walizunguka humo porini wakiongozwa na guider walikuja nae(kiongozi,muelekezaji) walifanikiwa kufika kwenye lile pango ambalo ndiko kile kiumbe kilikofungiwa,kwenye pango la sego,jamani ebu angalieni ili pango linatakuwa very useful kwa research yetu au nyie mnasemaje,ni sawa waliikubali wote baada ya madam mmoja kati ya wale maprofessa kutoa wazo,

basi wakawa wanaingia ndani ya pango hilo,ghafla angel hali hisi kuchomwa na kitu kifuani alipojishika hali hisi hule mkufu aliouvaa hunamchoma,kumbe ile ilikuwa ni ishara ambayo ilikuwa inamzuia hasiingie mule pangono.(kama unakumbuka katiaka sehemu ya sita kabla malkia hajafaa ambaye ndie mama yake mzazi na angel alikuwa kauvaa huo mkufu,na alivokufa hule mkufu huliingiliwa na mmoja wa myonzi iliyomsambalatisha yule joka aliyetaka kuwaangamiza kipindi bado ni mdogo),kila alipotaka kuingia ilimchoma hafi hakaamua kuivua,mh!!hii cheni nayo imezidi mauza uza isingekuwa ni zawadi niliyopewa na mama ningekuwa nishaitupa ngoja nikirudi nimrudishie cheni yake,aliwaza angel huku akiwa hanaiweka kwenye begi lake,aliingia mle pangoni.............

Walizunguka zunguka kwa uangalifu mkubwa mle pangoni,wakiendelea kuelezewa na story za lile pango na yule guider,"kama mnavyojionea pango hili liligunduliwa miaka mitano nyuma na wataalamu wa jografia,ila lilitekelezwa,inasemekana ili pango kulikuwa na mnyama mkali aliyekuwa akiishi humu,hali hiyo iliziilishwa na baadhi ya mifupa za binadamu iliyokutwa humu,mingine ndio hiyo mnayoiona.kuna mwenye swali?"aliuliza, ndio mimi na swali(lameck alinyoosha mkono),ndio wewe hapo,aah ningependa kujua kwamba huyo mnyama anaesemekana alikuwa anahishi humu alikwenda wapi,asante kwa swali lako,ni kwamba aliuwawa na wenyeji wa humu msituni,alidakia msichana mmoja"kuna watu wanaishi humu msituni,hapana kuna kijiji kipo kama kilomita tatu kutoka hapa.

(Maelezo aliyekuwa anayatoa yule guider,hayakuwa ya kweli kwani humo pangoni yule kiumbe alifungiwa humo pangoni kwa kutumia hule mkufu uliovalishwa kwenye fuvu la kichwa cha mtoto miaka ishirini nyuma).

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)