.jpg)
Mtunzi: Steve Ndegezy
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
itabidi tuwatafute wenzetu haraka na kurudi hotelini hii ishakuwa too much,wakati prof anaongea mara wanasikia kelele zikitokea kule walipokuwa mwanzo,ikabidi warudi safari hii walikimbia sana huku Henry akikoki bastola yake.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
kile kiumbe kiliwavamia neema na anety pale walipokuwa wanamlilia mwenzao kilimpiga kwa makucha yake neema kofi liliomrusha mbali kidogo kisha likamfata anety,anety alikiomba kiumbe kile kimwache lakini kilikuwa na roho ya ukatili ajabu,kikamtoboa tumbo na kumtoa maini huku neema anashuhudia hakiwa yupo chini analia kwa maumivu,kilimtoa maini anety na kumuwacha akigombania roho,kisha kikayatafuna yale maini na kumfuata neema pale chini
***************
Upande wa pili katika lile kundi la tatu wao hawakujua nini kinaendelea,walitembea huku wakiendelea kuwaita july na jofu,walipoona hawaonekani wakaamua kurudi hotelini kama walivyokuwa wamekubaliana,ilikuwaishatimia mishale ya saa kumi na mbili jioni,wakiwa porini humo kurejea hotelini baada ya kuwakosa wenzao,wanatumia muda huo kutalii kidogo msituni humo,kundi hili liliongozwa na raisi wa wanachuo ambaye pia alikuwa miongoni mwa listi ya waliokuja kufanya research/utafiti msituni humo,aliitwa hassan,mmoja wao alibaki nyuma kidogo aking'ang'ana kutafuta mtandao ili aperuzi mtandaoni lakini hakuunasa,alijikuta amebaki mwenyewe..........
Hawa nao wanajifanya wanawahi sijui hata wamepita njia gani,alijiongelesha mwenyewe huku akiwa hajui apite wapi sababu ya msitu huo kushonana sana na vichaka pamoja na miti mikubwa,ikabidi aanze kuwaita wenzake,aliwaita sana lakini hakuna aliyeitika.
Wenzake walikuwa tayali wanakaribia kufika kambini,kenedy ambaye ni kaka yake na latifa(aliyeachwa nyuma)aliangaza angaza kwa kumuangalia kila mtu lakini hakumuona latifa,hichi kitoto kitakuwa wapi,(alijiuuliza) ikabidi hawaulize wenzake,jamani hivi latifa yupo wapi ,we si halikuwa nyuma yangu hanachezea simu labda tumemuwa.........,kabla hajamaliza kuongea mara hakatokea mwenzao ambaye alikuwa kwenye kundi la pili(la wakina fide)alikuwa anakuja anakimbia yupo hoi,jamani hapa si salama,kuna nini wewe,hapana tuondoke hanakuja,nani anayekuja yu yu yule,NANI BWANA,muuaji,muuuwaji walishituka wote kwa pamoja.hacha masihara yako na prof moses yupo wapi si mlikuwa naye kundi moja alihoji Hassan,sijui hata cha msingi tuondokeni humu msituni si salama
********************
Upande wa pili yule kiumbe wa ajabu alimfata neema pale chini na kumkaba koo,na kumyanyua juu kwa mkono mmoja,neema alikuwa kaishika ile cheni,alipokuwa aking'ang'ana kujisaidia ile cheni(mkufu) ilimgusa yule kiumbe na kutoa ile mionzi mikali, kilimwachia neema na kuanza kupiga kelele za kutisha na kufanya ndege wakimbie mitini,wakati huo huo prof henry na kundi lake nao wanafika walimshuudia yule kiumbe live kabisa,henry alichukua bastora yake na kuhikoki,kisha akafyatua risasi kama mvua,zile risasi hazikufanya kitu kwani kila zinapoingia mwilini mwake zinatoka nje na jeraha linapona kwa sekunde,bastora yake ikaishiwa risasi,kwa bahati mbaya ule mkufu ulimtoka neema mkononi na kudondoka chini baada ya kuwa ameachiwa na yule kiumbe,ile miyonzi ikazimika kikapata nafuu,
kilimshika neema na kupotea naye huku wanashudia,kwa kitendo kile kila mtu alikimbia kivyake,angel alikimbia huku kashikwa mkono na baraka,prof halishindwa kuwazuia wasikimbie kwani teyali walikuwa wameishaiingia na hofu kubwa,kila mtu alitimua mbio huku wakipiga kelele,alibaki prof mwenyewe,hakaamua na yeye sasa kukimbia kuokoa nafsi yake,lakini kabla hajaondoka aliuona hule mkufu,nafsi ikawa inamwambia auchukue,lakini wazo jingine linamwambia auwache isije ikawa ni mkufu wa kimajini kama inavyosemwaga mitaani,lakini hakuipa imani wazo ile kwakuwa yeye ni msomi akauchukua na kuweka kwenye mfuko wake wa shati aliyovaa nakuondoka huku akioongeza risasi kwenye bastora yake.
************************
Wakati bado hawajahamini kwamba ndani ya msitu huo kuna muuaji ghafla wakasikia ile milio ya risasi kwa mbali kidogo hikisikika na zile kelele,ndipo wakaingiwa na wasiwasi,kenedy alipatwa na hofu juu ya usalama wa ndugu yake.ikabidi amurudie dada yake,
we kenedy unaenda wapi pekee yako ni hatari huko,lakini hakutaka kusikia jambo lolote ikabidi wale warudi kambini haraka,
Kenedy alimwita latifa kwa sauti,lakini hakujibiwa akazidi kuingia ndani zaidi ya msitu,mara hakakutana tena na wenzake wawili wanakimbia,no kenedy huko si salama usiende,hapana lazima ni mpate mdogo wangu siwezi kurudi mwenyewe bila yeye,akaongozana nao kumtafuta kwa bahati nzuri latifa aliwasikia wanamuita,akaitika kwa kuwaita,wakafanikiwa kumuona lakini wakati wanakimbiliana yule kiumbe alitokea katikati yao huku ametapakaa damu mwili mzima,kilimkamata rameck na kumyofoa moyo na kuutafuna,kikawageukia na wale wengine walitimua mbio huku wakimvuta latifa ambaye alikuwa kagoma kuondoka hakimlilia kaka yake huyo ambaye hawakuzaliwa naye tumbo moja,yeye alilelewa na baba yake na latifa tangu mdogo alipookotwa.
******************
walifanikiwa kufika kambini lakini hawakumkuta mtu,walishangaa wakabaki wanajiuliza wapi prof henry na wenzao wengine walipo hawakupata majibu.
Mita chache kutoka hapo kambini angel pamoja na baraka walikuwa wanakimbia kuelekea kule kambini,mara kile kiumbe kikatokea mbele yao na kumkabaa kooni angel,baraka alipoona angel amekabwa aliangaza angaza pembeni na kuona kipande cha mti halikiokota na kumchoma nacho yule kiumbe kifuani kwa nguvu,kilimuingia na kumtoboa yule kiumbe, kikatokeza upande wa pili,kilimpiga kofi baraka na kumrusha mbali halidondokea kichwa na kuvunja shingo akapoteza maisha hapo hapo kile kiumbe kikamwachia angel,na kuanza kuangahika kukichomoa kile kipande cha mti huku angel hakiwa hanakohoa pale chini,kwa bahati nzuri prof henry alifika alikiongezea risasi lakini hazikumzuru,
kilifanikiwa kukichomoa kile kipande cha mti lakini kilipata maumivu makali na jeraha lilikuwa kubwa halikupona haraka kama mwanzo,kilimrukia prof na kumkaba shingo mara hule mkufu uliwaka mle mfukoni mwa Prof Henry baada ya kuguswa na kiumbe huyo wa ajabu hukatoa ile mionzi na kumuingia yule kiumbe pale kwenye jeraha,kilimwachia Henry na kuanza kupiga kelele zilizozua upepo mkali mithili ya kimbunga,prof alimfata angel ambaye alikuwa anamlilia baraka ambaye tayali alikuwa kaishapoteza uhai na kumnyanyua pale chini kwa kutumia nguvu maana alikuwa ataki kumuacha baraka,lakini prof alimbebeleza wakaondoka huku yule kiumbe hakiwa hanageuka na kuwa moshi mzito mweusi........
Prof henry alifanya makosa kuondoka eneo lile kwani alivyoondoka tu ile miyonzi ikazima kwa kitendo hicho yule kiumbe aligeuka na kuwa moshi mzito mweusi ulisambaa angani kisha moshi huo ukasogelea maiti ya baraka pale chini,ukamwingilia ndani kwa kupitia pua zake,uliingia wote mara baraka akazinduka kwa kufumbua macho yake, akaanza kubadilika macho yake na kuwa mekundu na yenye mboni kama ya paka,ngozi yake ikawa kama vile imechunwa kwani nyama pekee ndio zilikuwa zinaonekana na baadhi ya mifupa yake kuonekana hasa ya mdomoni alikuwa hakipumua kwa kasi huku moshi mweusi hukiwa hunatoka kwenye pua zake,hakika halibadilika na kuwa kiumbe wa kutisha,alitoa kicheko kikali kisha hakapotea.
****************************
Prof Henry pamoja na angel walifika kambini na kukutana na wenzao,ilikuwa ishakuwa giza ikabidi wapumzike walipo weka kambi ili kuwasubiri wenzao ambao bado hawajafika ili warudi hotelini,angel muda wote alikuwa analia akimwaza baraka, alihisi kuhumia moyoni kwani akuwahi kumwambia kama anampenda ilizidi kumuumiza,akachukua kibegi chake na kuchukua leso ili ajifute machozi,wakati anachukua kitambaa hule mkufu wenye mauzauza aliopewa kama zawadi na wazazi wake hukadondoka aliuokota na kuwakumbuka wazazi wake bila ya kujua kwamba wale si wazazi wake,akaamua kuuvaa ule mkufu ghafla hakahisi kusisimuka mwili mzima,alijishangaa nakuhisi labda hule mkufu ndo unamsababishia hali hiyo ya kusisimuka,ikabidi auvue lakini cha kushangaza haukuwepo shingoni akaziidi kushangaa alipojipapasa hakuweza kuushika shingoni pake,akaamua kupuuzia,labda umepotea,aliwaza
Wakati huo prof henry naye alikuwa ndani ya ndimbwi zito la mawazo hakujua hatafanya nini,hakujua maprofesa wenzake wawili walipo,prof moses na madam mary,mara hakakumbuka ile mionzi iliyowaka kutoka mfukoni mwake,ikabidi aungalie ule mkufu, wazo likamuijia kwamba hii ndio kinga pekee waliyo nayo kwani alishuudia ile miyonzi ikimwadhibu yule kiumbe.
kulipambazuka wakiwa salama kipindi wanalala wote pale kambini waliofika walikuwa jumla kumi na tatu,prof akawahesabu asubui hiyo kuona kama wapo sawa cha kushangaza walikuwa kumi na moja tu,wakaingiwa na wasi wasi juu ya usalama wa wenzao wawili,mara angel hakawa anahisi kusisimuka mwili wake huku hakisikia sauti inamwambia akilini mwake kwamba geuka uangalie nyuma yako,alipogeuka tu alishangaa kuona michirizi ya damu chini,prof ona ona jamani ona hii si damu hii,aliongea kwa wasi wasi huku akiwaonyesha wenzake,
waliifuatilia michirizi hiyo hadi nyuma ya hema moja waliifuatilia hadi wakaa wanaiacha kambi mita chache nyuma walishituka baada ya kukuta mauaji ya kutisha,wanachuo wawili walikuwa wamenyofolewa baadhi ya viungo vyao,ghafla ile sauti ikasikika tena kichwani mwa angel ikimwambia waondoke hapo haraka,hakiwa haelewi elewi kama ni sauti ya kweli au ni mawazo yake na ni kwa nini anahisikia yeye mwenyewe,ghafla mmoja wao hanashitukia kafungwa mguu na kamba kama mizizi ya miti na kuvutwa nyuma,walitawanyika tena ovyo na kupoteana msituni baada ya mwenzao kuvutwa
********************
Prof moses alikutana na madam mary hakiwa hoi na kukumbatiana,wako wapi wengine,alihoji mary,sifahamu cha msingi hapa ni kutafuta njia ya kutoka hapa,kwa mbali wanasikia watu wanaongea,kumbe walikuwa karibu na kijiji cha sego,ikabidi waende kuomba msaada,walifanikiwa kufika walipokelewa na wanakijiji hao,wakapelekwa moja kwa moja kwa mfalme ambaye sasa alikuwa kaisha zeeka sana,waliongea lugha tofauti na kiswahili, kwa bahati nzuri madam mary alikuwa ni mtaalamu wa lugha kidogo alielewa baadhi ya maneno, kwa lugha mbovu mbovu aliwaeleza kilichowatokea kule msituni,mfalme alishituka sana kwani alijua lile tatizo halitokuja tokea tena,ikabidi aitishe kikao cha ghafla,wakajadili juu ya suala hilo.
Mfalme aliwahoji moses na mary huko wapi hule mkufu uliochukuliwa pangoni
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media