SEWATO: KOSA LA DAMU (6)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
ikabidi aitishe kikao cha ghafla,wakajadili juu ya suala hilo.

Mfalme aliwahoji moses na mary huko wapi hule mkufu uliochukuliwa pangoni

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
mary alikuwa haujui na hata hajawai kuuona,alimwambia mfalme kwamba hawakuchukua mkufu,mfalme alikataa akamwambia kwamba kama hawajauchukua yule kiumbe asinge hamuka,ikabidi sasa mtaalamu wao haitwe aangalie wapi ule mkufu ulipo na ni kweli yule kiumbe amefufuka.

**********************

Wakati huo prof alikuwa na angel pamoja na hassan wakikimbia kuelekea hotelini,mara ile sauti ikamwijia angel kichwani tena na kumwambia kwamba huko wanakoenda si salama asiende,akuitilia uzito sauti hiyo na kuipuuza akaendelea kwenda ghafla prof alichomwa na mkuki kwenye paja lake na kudondoka chini,ule mkufu ukadondoka kutoka mfokoni mwake,

yule kiumbe alikuja huku hakiwa kashika kichwa cha mwanakijiji mmoja anakinyonya macho,prof aliuchomoa ule mkuki na kwa kusaidiwa na angel pamoja na hassan haliuvuruta mguu wake na kuendelea kukimbia bila ya kujua ule mkufu kauacha pale chini.kile kiumbe kiliwafata kwa kasi na kumshika hassan na kumtia kucha za tumbo na kuuvuta utumbo nje,angel alipiga kelele hakiwa hajui hafanye nini,prof henry alijipapasa mfukoni kuutafuta ule mkufu lakini hakuupata,

hakajua huo ndio mwisho wake,akamwambia angel aendelee kukimbia amuwache yeye kwani wakiingozana wote watapata matatizo, angel akakimbia na kumwacha prof mwenyew,prof henry alioona bora tu afe kuliko kuendelea kushuudia mauaji ya wanafunzi wake,ntapambana na wewe hadi nikuue,alijihami huku akichukua bastola yake na kuikoki alianza kumshambulia kwa kufyatua risasi mfululizo,lakini ziliingia nakutoka kisha jeraha linapona kwa sekunde.....

Kile kiumbe kilizidi kumsogelea prof Henry,risasi ziliisha kwenye bastora yake alijipapasa kwenye mifuko yake kama bado hana risasi,halifanikiwa kuzipata aliziweka kwenye kitako cha bunduki yake na kuikoki lakini alikuwa ameisha chelewa kwani kile kiumbe tayali kilikuwa kisha mfikia karibu yake,kilimrukia pale chini na kumnyonya damu,prof henry alipiga kelele huku hakifyatua risasi ovyo ovyo mfululizo,milio ya risasi hilisikika hadi kwa askari pori waliokuwa wamepigiwa simu na yule guider kabla hajauliwa na kiumbe huyo wa ajabu,

waliulizana askari hao tisa,kengele ya hatari ililia vichwani mwao,inspecta mkuta pamoja na kikosi chake waliingiwa na wasi wasi wa wageni walioingia msituni humo baada ya kusikia milio ya risasi ikitokea msituni humo,walifanikiwa kufika kwenye kambi yao waliofika wageni hao (wanachuo)lakini hawakukuta mtu,askari mmoja aliona michirizi ya damu nyuma ya hema moja,alilikwenda kuripoti kwa mkuu wao inspecta mkuta,afande kuna michirizi ya damu upande huu,walikwenda kushuudia, walifata michirizi hiyo ya damu na kuziona zile maiti mbili za wanachuo walio uwawa usiku,walikoki bunduki zao na kugawanyika pande mbili na kuingia ndani zaidi ya msitu kumtafuta muuaji na kujua wapi walipo wengine.

***************"**

Angel alishitushwa na milio hile ya risasi pamoja na makelele ya prof alitamani kurudi lakini ile sauti ilimuambia asiendee, tena safari hii hakihisii kuungua shingoni alikimbia sana hatimaye hakakutana na wenzake watano waliosalia kati ya 25,wakiwa wapohoi wanakimbia huku hawajui wapi pa kuelekea,walipumzika chini kidogo ya mti,kutokana na uchovu walipitiwa na usingizi,lakini angel hakupata usingizi kwani ile sauti ilimwamuru aondoke haraka kile kiumbe kinakuja,halipowambia wenzake waling'ang'ana wapumzike kidogo kwanza,lakini angel halisisitizwa huku ile cheni hikiwa ina mchoma shingoni,ikabidi hawalazimishe,wakiwa bado wanabishana yule kiumbe alitokea nyuma ya angel huku hakiunguruma kama simba aliyejerehuliwa..

******😈😈😈🙈🙈🙈😈😈*****

upande wa pili kule kijijini haliitwa yule mtaalamu(mganga),alifika na kuanza mambo yake halichukua kitamba cheupe na kukitandika chini kisha akachukua vipande vya mti fulani na kuviweka juu yake na kuwasha moto ulitoa rangi ya bluu alinyunyizia dawa zake huku akiongea maneno yasiyo eleweka mara ule moto ukalipuka na kuwa mwingi, ajabu ni kuwa lilionekana lile tukio ndani ya pango jinsi jofu alivyoitoa ile cheni pahali pake,wote walishituka hasa madam mary na prof Moses hawakuamini macho yao,kisha likaonekana na lile tukio la Prof Henry kuuchukua ule mkufu alafu ukadondoka toka mfukoni mwake,matukio yote hayo yalionekana ndani ya moto huo,ghafla ule moto ukazimika,mfalme alikasilishwa na kitendo kilichofanywa na wageni hao,

ikabidi kiandaliwe kikosi cha mfalme ili waende kuutafuta ule mkufu,na wafanye juu chini wahakikishe wanamvalisha kiumbe huyo shingoni na huo ndo utakuwa mwisho wa kiumbe huyo,yule mganga haliwapaka madawa iwe kama ndio sumaku ya kuwaonyesha wapi huo mkufu ulipo,"yeyote kati yenu hatakaye usogelea huo mkufu hutatoa miyonzi na kuhumilika mwili wake sababu ya hiyo dawa niliyo wapaka,mtauchukua na kumwiinda adui yetu mkimpata hakikisheni mnavalisha shingoni mwake na sio sehemu nyingine,na ntawapa dawa ambayo mtaipaka kwenye silaha zenu,dawa hii mkimchoma na kumuingia kiumbe huyo haitomuangamiza ila itamsababishia jeraha lisilopona sawa"sawa waliitikia askari hao kumi na moja shupavu baada ya kupewa maelekezo na mganga huyo,kisha safari ilianza kwenda msituni kumuwahi kiumbe huyo kabla hajaja ndani ya kijijii chao na kuzua maafa makubwa.

Kutokana na makosa walioyafanya wenzao mfalme alitoa amri Prof Moses pamoja Mary nao wapakwe ile dawa waende kusaaidia na askari hao wa mfalme kumi na moja kwenda kumuangamiza kiumbe huyo.

Wakaanza safari mida ya jua kali ilikuwa kama mishale ya saa sita mchana,waliingia porini humo huku wakiangaza angaza huku na kule kuangalia hali ya usalama,walikwenda kwa kufuata maelekezo, jinsi walivyoelekezwa na yule mganga sehemu ulipodondokea mkufu kutoka mfukoni mwa prof Henry,walifika katikati ya msitu huo na kuamua wapumzike kwanza kidogo huku wakiweka silaha zao sawa,mmoja wao aliamka na kwenda kujisaidia haja kubwa pembeni kwenye kichaka,akiwa huko linajitokeza joka kubwa ajabu na kumkamata yule askari wa mfalme kwa meno yake yenye ncha kali.......

joka hilo la humo msituni lilikuwa na hasira na watu kwani ndio waliofanya mwenzake afe,(lile joka lililokufa baada ya kuchomwa na miyonzi ya ule mkufu wakati likitaka kumdhuru malkia akiwa bado mdogo angel)lilimtafuna mzima mzma,kelele zake ziliwashitua askari wengine,wakaja kupambana nalo,liliwakamata askari wengine wawili na kuwatupa mbali kwa mdomo wake kisha likawa linawachapa na mkia wake wale askari wengine wa mfalme ,askari mmoja kwa ujasiri aliruka kwa kudunda juu ya gongo la mti na kwa jambia lake halilikata kichwa lile joka likadondoka chini na huo ukawa ndo mwisho wa joka hilo la humo msituni,

wale waliokuwa wametupwa mbali na joka hilo mmoja alikufa baada ya kupiga mgongo kwenye mti,waliendelea na safari yao kuingia ndani zaidi ya msitu huo,wakiwa wanatembea tembea walikutana na maiti ya mtu haina kichwa walipoichunguza vizuri waligundua ni ya wanakijiji mwenzao,maiti hiyo ilinyofolewa kichwa na yule kiumbe,waliifunika maiti hiyo kwa matawi ya miti,nakuendelea na safari yao,huku kila mmoja wao hakiingia na wasiwasi juu ya usalama wao kutokana na mauaji ya kikatili yanayofanyika ndani ya msitu huo,prof moses alijilaamu kwanini alikuwa prof,ghafla wanasikia milio ya risasi mfululizo nakuwafanya wazidi kuingiwa na wasi wasi.

********😈😈😈🙈😈😈😈😈😈********

Upande wa pili kile kiumbe kilikuwa kimetokea nyuma ya angel,wakati wakiwa wanabishana kuondoka,kilitoa mlio kama simba,akili ziliwaruka wote walitimua mbio na kumuwacha angel akiwa anatetemeka akiwa ajui afanye nini,alibaki ameganda kama sanamu huku jasho likimchirizika kama kamwagiwa maji,aligeuka nyuma taratibu huku anatetemeka,alipogeuka alimwona yule kiumbe uso kwa uso,uzalendo ukamshinda alijikuta anapiga yowe,nakumfanya yule kiumbe amfate kwa kasi,kilipomfikia kilijaribu kumkaba angel lakini kilishangaa hakiwezi kumgusa kila kikijaribu hakimgusi,angel mda huo alikuwa kadondoka chini na kupoteza fahamu,kilipoona hakimwezi kilikasirika na kuanza kung'oa miti ovyo na kuirusha mbali,

Wakati huo huo wale askari pori walizisikia zile yowe alizokuwa akizipiga angel,wakajua kwamba muuaji hayupo mbali na wao,wakakimbia kufatilia zile yowe wakiwa wanakimbia askari mmoja alijikwaa na kudondoka alipokuwa akisimama kipande cha mti mkubwa ulio rushwa na yule kiumbe kilimwingia mgongoni na kutokezea kifuani,alikufa papo hapo huku damu nyingi zikimrukia askari mwingine,walishangaa kwa kitendo cha miti kurushwa rushwa ovyo bila shaka huyu si binadamu wa kawaida.mwenye uwezo wa kung'oa miti namna hii,aliongea askari mmoja huku wakiendelea kusonga mbele,walifanikiwa kufika eneo la tukio na kumshuudia yule kiumbe akiwa anafanya yake huku chini yupo angel akiwa ajitambui,inspecta mkuta alitoa amri,"open your fire""shoot"open youre fire"...

walimimina risasi nyingi sana kwa kiumbe huyo,kutokana nakuwa na silaha nzito za kivita zilimtoboa toboa kiumbe huyo mwili wake na kumfanya hasiifurukute,risasi zilimzidi ujanja ikabidi kiumbe hicho kijibadilishe na kuwa mbwa mwitu mkubwa mweusi,wale askari walishituka kidogo lakini hawakuacha kumshambulia kiumbe huyo aliyebadilika sasa na kuwa mbwa mwitu,kwa ustadi mkubwa mbwamwitu huyo alikwepa risasi hizo huku hakiwafata kwa kasi,askari walishambulia huku wakirudi nyuma,kile kiumbe kilitimua mbio nakuwapotea,walihisi kakimbia nakuondoka zake ghafla bila ya kutegemea askari mmoja aliuwawa kikatili kwa kupitiwa utumbo na mbwa mwitu huyo aliyekuja kwa kasi na kumtia meno ya tumbo na kutoka na utumbo,ndipo sasa askari pori hao chini ya uongozi wa inspecta mkuta,

walimfyatulia risasi kwa kumfukuza,yule mbwa mwitu aliwaacha mbali,akabadilika tena na kurudi katika umbile lake la kutisha,safari hii alitisha zaidi kwani pembe zake kichwani ziliongezeka urefu,meno na kucha zilikuwa ndefu zaidi,huku akiwa katika umbile la kibinadamu asiye na ngozi(yani nyama hazikufunikwa na ngozi)kilipotea na kutokezea nyuma ya askari pori mwingine na kumziba mdomo kisha kikampulizia moshi mweusi puani,aliaanza kuishiwa damu macho yakawa meupe pee ngozi ikapauka ghafla kikamwachia akadondoka chini huku akitoka vumbi kama aliyeoshwa kwenye saruji,kisha kikapiga hatua za kikakamavu kumfuata inspecta mkuta akiwa ana angaza angaza huku na huko kumtafuta mbwa mwitu,bila ya kujua yule kiumbe anamfata kwa nyuma......

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)