.jpg)
Mtunzi: Steve Ndegezy
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
aliaanza kuishiwa damu macho yakawa meupe pee ngozi ikapauka ghafla kikamwachia akadondoka chini huku akitoka vumbi kama aliyeoshwa kwenye saruji,kisha kikapiga hatua za kikakamavu kumfuata inspecta mkuta akiwa ana angaza angaza huku na huko kumtafuta mbwa mwitu,bila ya kujua yule kiumbe anamfata kwa nyuma......
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Mauaji ya kikatili yanaendelea kutokea ndani ya msitu mnene nchini Congo,baada ya kiumbe wa ajabu kufunguliwa bila ya kotokujua na mwanachuo mmoja(jofu)na kusababisha maafa hayo,
Ndani ya msitu huo bado hali ni tete kwa wanachuo waliosalia research/utafiti wao unaingiwa dosari,angel akiwa ajitambui yupo chini kaanguka askari pori wanakuja kutoa msaada baada ya kusikia kelele/yowe zisizokuwa za kawaida wanapofika eneo la tukio wanakutana na jambo linalosababisha baadhi yao kupoteza uhai*********
kisha kikapiga hatua za kikakamavu kumfuata inspecta mkuta akiwa ana angaza angaza huku na huko kumtafuta mbwa mwitu,bila ya kujua yule kiumbe anamfata kwa nyuma..songa nayo sasa,,,,,
Kutokana na mafunzo haliyofundishwa jeshini,inspecta mkuta anahisi adui yupo nyuma yake,anageuka kikomando huku silaha yake ipo active kwa kutema risasi,anapogeuka anaona tu takataka za miti,kumbe yule kiumbe alipotea ghafla wakati alipogeuka,kiumbe huyo akatokezea kwa askari mwingine, kwa nyuma yake huku kikichilizika damu mdomoni kama maji,damu iyo ilimdondokea askari huyo na kumfanya ajiguse sehemu aliyodondokewa na kitu kama maji maji alipashika kwa mkono wake,
alipotazama mkononi pake alishituka baada ya kuona ni damu ndio iliyomdondokea,aligeuka kwa kasi ya ajabu ili apambane lakini alikuwa ameisha chelewa kile kiumbe kilimkaba kooni na kumyanyua juu kisha kikatoa moshi mweusi mdomoni na kumpulizia mdomoni mwa askari pori huyo,nayeye akawa kama yule askari wa kwanza,macho yakawa meupe kisha ngozi ikampauka kama kamwagiwa saruji/cement.
Purukushani hizo ziliwashitua askari pori wengine na kuwafanya kwenda mbio upande alio kuwepo,walishuudia mwenzao akiwa teyali kapoteza uhai na yule kiumbe ametoweka,ikabidi wamchukue angel na kuondoka naye kurudi walipo acha gari yao aina ya land cruiser,
*****😈😈😈😈🙈🙈😈😈😈😈😈😈😈😈****
Upande wapili askari wa mfalme gumbo walisikia milio ya risasi zilizofanya wagundue kuna watu mle msituni,lakini prof moses pamoja na madam mary waligundua iyo milio ya risasi si ya silaha ndogo walijipa matumaini ya kuwa salama kwani milio ya silahaa hizo zilikuwa ni za ma askari tu ndio wenye kuzimiliki silaha hizo,walikubaliana wasitengane walishikana mikono wote na kutembea kuelekea kule ulipo mkufu,walitembea hadi ikatimia saa 5:30 za jioni,walihisi kuchoka na kumuomba kiongozi wao aliyeitwa siso,wapumzike lakini haliwaambia hawana mda wa kupumzika,wakiwa wanatembea kivivu vivu huku macho yakiwa hayatulii sehemu moja kwa kuangalia juu chini,kulia na kushoto mmoja wao hanakanyaga sehemu iliyokuwa imechimbwa shimo na kufunikwa na matawi ya miti kama mtego,
mtego huo ulichimbwa na yule mwanakijiji aliyekutwa amepoteza maisha na maiti yake ikiwa haina kichwa,kwa kuwa walikuwa wameshikana mikono aliingia shimoni na kujikuta akimvuta mwenzake aliyekuwa ameshikwa naye mkono walidumbukia shimoni humo na kutobolewa na miti yenye ncha kali iliyowekwa kwa ajili ya kumnasa mnyama,wote walikufa hapo hapo huku mwingine naye akiserereka na kutumbukia shimoni humo sababu walikuwa wameshikana mikono,alichomwa na miti hiyo kwenye kanyagio za miguu yake,alipatwa na maumivu makali mno,
walimtoa shimoni humo na kubebwa na mmoja wa askari hao,huku madam mary naye hakiponea chupuchupu kuingia shimoni humo waliendelea na safari yao huku yule aliyechomwa hakitoka damu nyingi sana ikabidi wapumzike ili wamtibu mwenzao,haliwekewa madawa ya kuzuia damu isitoke,halikata tamaa ya kuishi huku hakimuomba mungu achukue tu roho yake kuliko kumpa yale mateso alioongea kwa lugha yao,wenzake walimwonea huruma na kumpa moyo kuwa hatakuwa vizuri mda si mrefu,ghafla bila yakutokutegemea kile kiumbe kinatokezea katikati Yao ,wanatimua mbio baadhi ya askari akiwemo prof Moses pamoja na mary,kile kiumbe kinamtia kucha za kifuani yule askari wa mfalme aliyechomwa miguuni na kumtoa moyo kisha kikautafuna huku kikicheka kwa sauti ya kutetemesha hadi nyasi,
siso anachukua hule mshale wa dawa na kuuweka ndani ya upinde analenga shaba ya mgongoni yule kiumbe,lakini yule kiumbe anahuhisi huo mshale na kupotea ghafla, hule mshale unapitiliza na kumchoma askari wa mfalme mwingine aliyekuwa na yeye akijaribu kumlenga yule kiumbe upande wa pili,kabla ajauachia hule mshale unamuingia kooni na kumtokezea kwa nyuma na yeye anauachia mshale wake sababu ya mshituko wa kasi ya hule mshale kumuingia kooni,mshale huo unaelekea moja kwa moja kwa siso.....
Kwa ustadi wa hali ya juu siso hanaukwepa ule mshale unakwenda moja kwa moja kuchoma kwenye mti,siso anakwenda kumwaangalia mwenzake,cha kushangaza siso hakumuona mwenzake alishangaa sana huku hakijiuliza ametowekaje haraka hivyo bila ya hata kumuona akiondoka,anahamua kuondoka zake kuwasaka wenzake waliokimbia,alipopiga hatua moja mbele alihisi kudondokewa na matone kama ya maji kichwani,alijifuta kwa mkono wake alishituka baada ya kugundua ni matone ya damu ndio yaliyomdondokea alipoatizama juu alishuudia yule kiumbe hakiwa anamnyofoa mwenzake viungo vyake na kuvitafuna,wazo likamuijia akarudi nyuma kwa kunyata ,kisha akachukua mshale wenye dawa maalum waliopewa na mganga ambao hutamtia jeraha lisilopona kwa haraka na kumpa maumivu makali,
Haliutia kwenye upinde kisha hakauvuta kwa nguvu na kuachia,mshale ulifyatuka kwa kasi na kutii amri ukazama moja kwa moja kwenye kifua cha yule kiumbe,kilipiga kelele kali huku kikiuachia mwili wa yule askari kisha kikajikunja kwa maumivu makali huku kikijaribu kuuchomoa,lakini siso alichukua tena mshale mwingine na kuuvuta, nao hukatii amri kwa kumuingia ubavuni mwa kiumbe huyo,kiumbe huyo wa ajabu alipoona hali imekuwa ngumu aliruka juu ya miti na kutokomea ndani zaidi ya msitu huo mnene,
Siso aliusogelea mwili wa mwenzake na kuanza kulia huku akimuomba msamahaa kwa kumsababishia kifo,ghafla hule mwili ukabadilika na kuwa majivu sababu ya sumu kali ya kiumbe huyo,siso halinyanyuka na kuanza tena safari ya kuutafuta hule mkufu,kwenye podo lake la mishale halikuwa na mishale mitatu tu,.
*******😈😈😈😈🙈🙈😈😈😈😈************
Upande wa pili yule kiumbe halionekana akiwa juu ya mti mkubwa akiwa anaichomoa ile mishale,kiliuchomoa mshale wa kwanza na kuutupa kilihisi maumivu makali kilishangaa jeraha aliponi, kiliingiwa na hasira kisha kikaushika mshale wa pili nakutaka kuuchomoa,ghafla kikawaona askari wa mfalme wakipita chini ya mti huo,kiliuchomoa ule mshale nakushuka kwa kasi chini na hule mshale,nakumchoma nao askari mmoja utosini askari wengine walitimua mbio bila hata ya kutoa msaada kwa mwenzao,kile kiumbe kilitia meno shingoni pa yule askari na kumnyonya damu yote,kisha yale majeraha yakapona ghafla,wakati yale majeraha yanapona yalimpa maumivu makali kilipiga kelele za ajabu zilifanya hali ya hewa kubadilika,mawingu mazito ya mvua yalitanda angani huku radi na ngurumo zikipiga kwa pamoja,kile kiumbe kiliangaza kushoto na kulia kisha kikatoweka ghafla.
******""**************~!!!!!""?*****((***
Wakiwa wamembeba angel walifanikiwa kuiifikia gari yao(land cruiser)walipanda askari pori hao,inspecta mkuta alichukua kifaa maalum kitumikacho kuwasiliana na makao makuu yao,mkuta alijaribu kuwasiliana na makao makuu yao lakini hali ya hewa hilikuwa mbaya na kufanya mtandao kupotea,ikabidi dereva awashe gari wakaondoka....
, Mara angel hakiwa yupo usingizini hanaoteshwa nakumuona yule kiumbe akijitokeza mbele ya gari lao kisha dereva anamkwepa na kutoka bararabarani gari inamshinda dereva na kuingia porini huku aking'ang'ana kufunga break lakini break zikilimsaliti dereva kwa kushindwa kupunguza mwendokasi wa gari,wakati hakiwa yupo ndotoni wale askari wanamuona angel hakiweweseka huku shingoni pake cheni yake inawaka na kuzima mwanga kama moto,askari mmoja anahamua kumwamusha lakini haamuki,ndipo alipoishika ile cheni huku akiishangaa ghafla ikazima ule mwanga ndipo angel anashituka toka ndotoni,unajisikiaje alioji mkuta,angel hakuwajibu kitu akabaki anawashangaa huku hakijiuliza hawa wakina nani nawananipeleka wapi,ndipo askari mmoja akamweeleza kwamba walimkuta kadondoka chini akiwa kapoteza fahamu baada ya kupatwa na matatizo,inspecta mkuta akamuuliza
eeh tuambie sasa ilikuwaje,angel alipoangalia nje alishituka baada ya kugundua yupo ndani ya gari tena likiwa linaendeshwa kwa kasi,ghafla ile sauti ikasikika masikioni mwake ikimwambia"shuka haraka mpo kwenye hatari shukaaaa..."angel alihisi kuchanganyikiwa ndipo kumbukumbu zikaanza kumuijia akakumbuka na ndoto aliyoiota angaunganisha matukio kichwani mwake,
wazo likamwijia akakurupuka na kumwambia dereva hasimamishe gari,"dereva dereva simamisha gari,"aliongea kwa wasi wasi,maaskari pori walidhahania kwamba labda kaingiwa na kichaa,ikabidi wamtulize kwa kumuhakikishia usalama wake."binti usijari upo na askari usi hofu tunakupeleka pahali salama"inspecta alimshawishi lakini angel halikataa na kuwaanza kufanya fujo kwa dereva ili gari isimame,ndipo ikabidi wamkamate kwa nguvu na kumzuia hasifanye fujo,
Jamani tutukufa huko mbele kuna...kabla hajamaliza kusema askari mmoja alimchoma sindano ya usingizi shingoni ili hatulie hasije kusababisha ajali,dereva alizidi kukanyaga mafuta na kuongeza gia,gari ikawa inaenda kwa kasi,inspecta mkuta alijaribu tena kupiga simu lakini yule kiumbe alikuwa kaisha fanya hali ya hewa kuwa mbaya na kufanya network kupotea,dereva aliendesha gari kwa kasi sana hadi wakafika eneo ambalo angel alioteshwa ndotoni......
Dereva alizidi kuonganyaga mafuta nakufanya gari iende kasi sana ghafla bila ya kutegemea dereva alishituka baada ya kuuona kitu cha ajabu kimesimama barabarani bila hata kuwapisha,alipiga honi mfulululizo lakini haikusaidia kitu kwani kile kiumbe hakikuwapisha,dereva alikanyaga breki kwa nguvu lakini hazikumtii,
ikabidi hakwepeshe gari,gari iliiacha njia na kuiparamia miti huku wakizidi kuingia ndani zaidi ya pori kila mtu alisali kumuomba Mungu kwa nanma yake,huku angel hakiwa bado hajazinduka tangu achomwe sindano ya usingizi,kutokana na gari kuwa kasi iligonga gogo la mti na kupinduka mara nne,askari pori walirushwa nje sababu walijisahau kufunga mikanda wote walipoteza fahamu huku hikisikika sauti kwenye kile kifaa maalum cha inspecta mkuta(yani radio call)kutoka makao makuu
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media