SEWATO: KOSA LA DAMU (8)

Zephiline F Ezekiel
0

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
huku angel hakiwa bado hajazinduka tangu achomwe sindano ya usingizi,kutokana na gari kuwa kasi iligonga gogo la mti na kupinduka mara nne,askari pori walirushwa nje sababu walijisahau kufunga mikanda wote walipoteza fahamu huku hikisikika sauti kwenye kile kifaa maalum cha inspecta mkuta(yani radio call)kutoka makao makuu

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
"inspecta johny hapa umenisoma over,inspecta johny hapa umenisoma over..."

**(******😈😈🙈😈😈😈*********

Upande wa pili kulikuwa na mtafutano mkubwa,askari wa mfalme gumbo walipoteana ndani ya msitu huo mnene,prof Moses hakiwa na madam Mary pamoja na askari wa mfalme wawili,wanajikuta wakiwa pekee yao huku kila mmoja wao hakiwa na wasi wasi kwani hakuna aliyetegemea kazi kuwa ngumu kiasi hicho,wasi wasi uliongezeka hasa ile taswira ya mauaji yaliyofanywa mbele ya macho yao na yule kiumbe wa ajabu inapozunguka ndani ya vichwa vyao kama mkanda wa filamu ya kutisha. Ilikuwa yapata saa kumi na moja jioni jua likiwa lishapungua makali yake kuashilia kuukaribisha usiku,walitamani kurudi ila ni mwiko kurudi bila ya huo mkufu ni bora wauliwe kuliko kurudi kijijini bila ya mkufu huo,

prof hakiwa na wenzake waliendelea na safari,ghafla walikutana na wenzao wengine wawili jumla wakawa sita, walikumbatiana kwa furaha huku machozi yakiwatoka,hakika ujasiri wote uliwaisha askari hao mbele ya kiumbe huyo wa ajabu,ikabidi wajipumzishe kidogo,wakakaa chini ya mti mkubwa,askari mmoja aliona mti uliokuwa na matunda yalioiva vizuri(mti huo ulikuwa na asili ya mapasheni/passion),hamu ikamwiingia akaamuka na kuufata mti huo akachuma la kwanza akala,lilikuwa na radha nzuri,kwa uroho akaamua kuvuta matawi ya mti huo yaliyokuwa yamelanda kwenye mti,

alivuta tawi moja bila ya kujua kama kuna nyoka mkubwa,alilitikisa kwa nguvu ili matunda yadondoke wenzake walikuwa wanamwaangalia tu wakiwa hoi wamechoka,ghafla yule askari alishitukia anadondokewa na yule nyoka,nyoka huyo alimkaba kwa kujizungusha shingoni mwake,alishindwa kupiga kelele akabaki anakoroma,yule nyoka alianza kumuingilia mdomoni mwa askari huyo, alidondoka chini na kuanza kufurukuta kama kuku aliyechinjwa,wenzake walishituka na kumfuata kwa kasi, walipomfikia walipigwa na bumbuwazi baada ya kumshuudia yule nyoka ndo anaishilia mdomoni mwa mwenzao,

walijitahidi kumsaidia kwa kujaribu kumtapisha lakini walikuwa wameishachelewa,macho yaligeuka na kuwa mekundu mapovu yalimtoka mdomonina kukata roho,walisikitika sana,askari mmoja akawa kama vile amini alichokiona alinyanyuka na kurudi nyuma bila kugeuka huku machozi yanamtoka,alipokuwa anarudi nyuma alijihisi kujigonga kifuani mwa mtu lakini mtu huyo alikuwa kama vile amelowana alafu ni wa baridi sana,aliingiwa na wasiwasi akageuza shingo yake kumuangalia ni nani huyo,alipogeuka alipatwa na mshangao baada ya kumuona yule kiumbe kasimama mbele yake,alipiga kelele zilizowashitua wenzake,

kile kiumbe kikamshika shingo na kumtia meno yake makali na kumnyonya damu,askari mmoja aliingiwa na hasira akamfuata yule kiumbe akiwa kashika sime alinyanyua sime yake ili amshushie yule kiumbe,lakini yule kiumbe alimuwahi kwa kumpiga kofi moja lilimnyofoa kichwa kikabaki kiwiliwili kikirusha damu kama bomba la maji,kile kiumbe kikawageukia prof henry,mary pamoja na askari mmoja wa mfalme aliyesalia walitimua mbio,walikimbia hadi wakakutana na siso,siso aliwashangaa na kuwauliza kimetokea nini walimueleza kilechotokea siso hakaingiwa na hasira akachukua mshale wenye dawa maalum na kuuweka kwenye upinde wake kisha akarudi kule kilipokuwepo kile kiumbe,walimzuia lakini hakutaka kumsikiliza mtu,

alikimbia bila kujua amebakiwa na mishale mitatu tu,walimfukuza ili kumzuia ghafla kile kiumbe kikawatokea mbele yao,siso aliuvuta mshale na kuuwachia lakini yule kiumbe hakaukwepa siso akachukua wa pili nao kikaukwepa akachukua watatu na kuvuta kwa hasira mshale huo,ulilkwenda na kumuingia kiumbe huyo mguuni,siso alipopapasa kwenye podo lake la mishale akajikuta ameishiwa mishale yote ikabidi amvae yule kiumbe hivyo hivyo,lakini alishitukia ananyofolewa utumbo huku ana ona,prof na wenzake walipoona hali imekuwa ngumu wakakimbia,wakiwa wanakimbia madam Mary anajikwaa na kudondoka chini ,alipodondoka pale chini alifanikiwa kuuona hule mkufu................

*********************************

Ilikuwa mida ya saa moja jua ndo linaihaga siku hiyo na kuukaribisha usiku,angel anasikia sauti ikimwambia akiwa usingizini,"angel binti yangu amka haraka kabla ujachelewa kuna hatari ipo karibu yako"angel alishituka kutoka usingizini na kujikuta yupo sehemu ambayo hakuitambua,alipoangalia pembeni aliona ile gari ikiwa imebondeka bondeka vibaya,alipoangalia pembeni akawaona watu watano ambao hakuwajua wakiwa kila mtu upande wake wamelala chini hawajitambui,mara ile sauti ikajirudia tena kichwani mwa angel tena safari hii na ile cheni yake ikiwaka mwanga mkali na kutoa ishara kwa kumuangazia njia ya kupita ghafla ikazimika,

angel kila kitu alioona kama ndoto,kumbukumbu zake zilikuwa zimepotea,ghafla akiwa anawaza alisikia sauti ya ajabu ikitokea ndani ya msitu huo kama kicheko cha kutisha,alipojaribu kusimama alihisi maumivu makali kwenye bega lake la kushoto kikifuatiwa na kichwa kilichomfanya hajihisi kizungu zungu kikali,ghafla alishituka baada ya kumuona mtu wa ajabu hakitokea ndani ya msitu na kuja pale walipo huku wale maaskari wakiwa bado fahamu hazijawarejea.......

Mtu huyo alizidi kuwasogelea pale walipo kuwa,mara angel akasikia ile sauti ikimwambia kichwani mwake "jifanye umepoteza fahamu sababu umeishachelewa kuondoka huyo ni mzimu wa Sewato ni hatari sana ila ntakusaidia lala chini na usipumue,bana pumzi yako wala usitikisike anaweza kukisia umekwisha poteza uhai"ile sauti ikatoweka angel akaitii na kujilaza chini huku akiwa amebana pumzi,kile kiumbe kiliwafikia na kuanza kukagua mmoja mmoja hadi kikamfikia angel,kilimwaangalia kwa makini kikaiona ile cheni kifuani pake,

kikapeleka mkono kuishika.Kutokana kulikuwa na giza sana ndani ya msitu huo angel alikuwa anakichungulia kile kiumbe kwa kuibia ibia kwa kuyafumbua kope za macho yake pole pole ,alifumbua macho yake kidogo sana ili akione kinafanya nini sababu ya giza alilazimika kufumbua macho kwa kuyakodoa ili aone vizuri bila ya kujua kile kiumbe kipo karibu yake sasa nakinamsogelea sasa kuigusa ile cheni,angel alipoangalia vizuri alikiona kiumbe hicho kipo mbele yake na kinaleta mkono maeneo ya shingoni kwake,uwoga ukamuingia nakujikuta mwili wote unamsisimka,alianza kutetemeka hakisali kwa mungu amuepushe na hilo janga,

kile kiumbe kili hisi kama angel yupo hai sababu halikuwa akitetemeka hadi meno yanagongana kama mtu aliyemwagia barafu,kabla akijaishika ile cheni yenye mzimu wa mama yake angel(malkia),askari pori mmoja alipata fahamu aliamuka kwa kukurupuka sababu ya giza tororo, liliyazonga zonga macho yake,akujua yupo wapi,akawa anaita kama kuna mtu anamsikia bila ya kujua,yupo hatarini ....

**********************************

Uongozi wa chuo kikuu cha jijini Dar es salaam(UDSM)kinaingiwa na wasi wasi mkubwa baada ya kutopata taarifa yoyote kutoka kwa maprof walioenda na wanachuo kwa ajili ya utafiti nchini congo,hakukuwa na mawasiliano yoyote kwa siku sita mfululizo hali hiyo pia inawatia wasi wasi mkubwa wazazi wa wanachuo hao,,ambao pia wanakuja chuoni mara kwa mara kuuluzia hali za vijana wao ambao wamekuwa hawapati mawasiliano nao kwa siku sita mfululizo,chuo kinafanya mawasiliano na serikali ya congo ili kujua nini kinaendelea huko congo,serkali ya congo inawa ondoa hofu kwa kuwahaidi kulishughulikia suala hilo,

kikosi maalum cha maaskari kumi na sita wa congo kinaandaliwa kwenda ndani ya msitu wa sego kwenda kubaini tatizo ni nin,helicopter ya kijeshi inaandaliwa na kikosi hicho chini ya uongozi wa inspecta martin,wanaingia ndani ya helicopter kisha rubani anairusha juu kuelekea ndani ya misitu ya sego,kutoka kambini kwao hadi msituni ni mwendo wa saa moja na nusu,helicopta inawasili msituni na kuanza kuzunguka zunguka huku na kule kuangalia kama watawaona lakini hawaoni mtu kwa mbali wanauona mwili wa mtu ukiwa umetundikwa juu ya mti na umechunwa ngozi,hofu inawaingia juu ya usalama wawanachuo na maprof waliomo ndani ya msitu huo,wakiwa wanaendelea na safari yao wanaona tukio la ajabu likifanyika ndani ya msitu huo mbele ya macho yao nakufanya wakae tayali kwa vita huku wakizikoki silaha zao nzito za kivita......

😈😈😈😈🙈🙈😈😈😈***

Kile kiumbe kinaachana na angel na kunyanyuka pale chini kisha kinasimama na kutoa kicheko kikali na cha kutisha,moyo wa askari pori huyo unapata mshituko na kumfanya aingiwe na wasi wasi,"We nani"??,alioji askari pori huyo huku kumbukumbu zake zikiwa zinamrejea polepole,"Nakuuliza we nani na unataka nini"??!!.akuna aliyemjibu kumbukumbu za mauaji ya kutisha ya yule kiumbe zikamrudia na kumfanya hazidi kuingiwa na uwoga wa hali ya juu,halitetemeka huku aja ndogo ikimtoka,ghafla akahisi kushikwa bega kwa nyuma alitamani ardhi ipasuke atumbukie ndani kuliko kufa huku anashuudia kwa macho yake alipogeuka nyuma kumuona ni nani aliyemshika bega,

akumuona vizuri usoni sababu ya giza,kumbe alikuwa ni inspecta mkuta ndo kamshika bega,inspecta akamuonyesha ishara fulani iliyomuashiria anyamaze kimya,alinyamaza baada ya kugundua ni mwenzake,yule kiumbe halikuwa hakiwatizama tu bila ya wao kumuona,yule kiumbe akaamua kuwaacha kwanza na kumfata angel.Angel alimuona anavyokuja hakataka kusimama lakini maumivu ya bega yalimtesa nakujikuta akitoa sauti ya maumivu makali,yule kiumbe hanamfikia na kumshika angel kwa nguvu,angel anapiga kelele za kuomba msaada yule kiumbe ananyanyua mkono wake wenye kucha kali juu ili kumnyofoa angel utumbo huku kimemnyanyua juu kwa mkono mwingine.....

Angel alijaribu kujisaidia kwa kukipiga mateke kile kiumbe,lakini haikusaidia kile kiumbe kilizamilia kummaliza angel kabisa,kilinyanyua mkono wake juu lakini kabla akijakusudia kumuua angel kinahisi kuapigwa na kitu kizito kichwani kina muachia angel,kilikasirika sana na kumgeukia aliyemsababishia asifanikishe dhamira yake,alikuwa ni inspecta mkuta ndio aliyempiga na kipande cha chuma cha gari kichwani,kile kiumbe kilimfata inspecta kwa Kasi ili kummaliza lakini inspecta alitimua mbio na kuwa onyesha ishara angel pamoja na yule askari waondoke,kile kiumbe kilimfukuza inspecta,angel halikuwa hakikohoa sana sababu alikabwa koo kisawa sawa,yule askari aliyekuwa akiitwa benedict,alimnyanyua angel na kuondoka naye japokuwa kulikuwa na giza tororo,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

  Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Zaidi Naomba Share App kwa Wapenzi wa Simulizi Wapakue(Install) App ya CnZ Media

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)