SHEREHE KUZIMU (3)

Zephiline F Ezekiel
0
Mtunzi: Frank Silaa

SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
Akili mwake alitambua kuwa itakuwa ni zoezi gumu lakini, alijidhatiti kuhakikisha kwamba anafanikiwa. Jioni ya saa 11.55 aliteremka kwenye basi katika kituo cha Mianzini ambapo alimkuta mjomba wake anamsubiri kumlaki.

KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA NAYO...
Mjomba wake alifurahi sana baada ya kumuona mtoto wa dada yake akiwa amerejea mzima wa afya tele, tena na ushindi mkubwa katika masomo yake. Nelson aliongozana na mjomba wake hadi nyumbani. Mara baada ya kuoga kuondoa uchovu wa safari, Nelsoni alikwenda mezani kupata chakula cha jioni pamoja na familia ya mjomba wake. Alifurahi sana kwasababu mke wa mjomba wake alikuwa ameandaa kitoweo cha jogoo, kama heshima kwa ujio wake. Walikula chakula huku wakizungumza na kucheka sana kutokana na stori za Nelson kipindi alipokuwa Marekani. Maongezi yao motomoto yalikwenda hadi usiku wa saa sita na baada ya hapo kila mtu alikwenda kulala. Ingawa Nelson alikuwa amechoka kwa safari lakini hakuweza kupata usingizi kwa sababu ya mawazo kibao yaliyokuwa kichwani mwake dhidi ya binti mrembo Vivian.

“Hivi itakuwaje endapo nitakuta Vivian kaolewa na mtu mwingine?” Nelson aliwaza sana pindi alipokuwa kitandani kwake usiku akijigeuza huku na kule bila kupata usingizi. Mkononi alikuwa ameshika picha ambayo aliwahi kupewa na Vivian kipindi cha nyuma. Alipata wazo kwamba picha ile itamsaidia kumtafuta Viviani maeneo ya Sakina ambapo binti aliwahi kumweleza ndipo anapoishi. Ule usiku ulikuwa ni mrefu sana kwake kwasababu alitamani pakuche haraka kusudi aweze kutokomea mitaani kumsaka njiwa wake. Alizidi kumuomba Mungu binti aliekuwa anamuwaza kila siku maishani mwake awe mzima wa afya na pia awe hajaolewa. Palipokucha asubuhi alipata kifungua kinywa na kuondoka kuelekea maeneo ya Sakina kumtafuta mwanamke wa ndoto zake.

*************

Kwa muda wote ambao Vivian alipotezana na Nelson aliishi bila amani kabisa ndani ya moyo wake. Alitamani laiti kama angekuwa na mabawa angetua mbele ya Nelson ili aweze kumuona nafsi yake isuuzike. Alichoshwa na upweke wa kukaa kivyakevyake pale mtaani kwao. Ilipotimu mwaka wa tano akiwa nyumbani bila kujishughulisha na kitu chochote aliamua kurudi darasani kusoma. Alikwenda katika chuo cha ‘Tropical Institute’ kilichopo jirani na hospitali ya AICC kusomea ‘Hotel management.’ Kama kawaida uzuri wake uliwachanganya wanaume wengi sana chuoni hadi walimu walionekana kuvutiwa sana na uzuri aliojaliwa.

Wanaume wengi walimfuata kumshawishi, lakini aliwakatilia kwa kuwajibu kuwa anampenzi ambae anampenda sana. Watoto wa vigogo nao hawakuwa nyuma kwani walionyesha mbwembwe za pesa za nyumbani kwao ili waweze kumnasa lakini pia hawakufanikiwa. Baada ya vijana wote pale chuoni kushindwa kumshawishi kimapenzi walianza kumsema vibaya kwamba eti anaringa lakini haikuwa kweli. Japokuwa hakuwa na uwakika kuwa Nelson atamrudia tena lakini alijipa moyo kwasababu alishahisi kuwa Nelson alikuwa anampenda sana. Kijana mmoja ambae ni mwanasheria wa kujitegemea siku moja alikutana na Vivian na kutokea kumpenda sana.

Alimshawishi Vivian ili aweze kuwa mpenzi wake lakini Vivian alikataa katakata. Kijana yule hakukata tamaa aliendelea kumsumbua kila mara ili aweze kukubaliwa ombi lake. Vivian alikereka sana kwa usumbufu wa yule kaka kwasababu alikuwa akimfuata kila siku lakini aliendelea kubaki na msimamo wake, tena wakati mwingine alidiriki kumtukana kwasababu alikuwa ni msumbufu sana. Pamoja na hayo yote lakini bado kija yule hakukata tamaa. Vivian alijiuliza yule kaka ni mtu wa namna gani kwasababu alikuwa anamnyima amani kabisa. Kutokana na kero hizo aliamua kumkubalia kishingo upande lakini kwa bahati mbaya mahusiano yao hayakudumu kwani kijana huyo alipoteza maisha siku iliyofuata akiwa ofisini kwake katika mazingira ya kutatanisha jambo ambalo lilimshitua sana Vivian.

Mpaka kufikia muda ule Vivian alikuwa bado ni bikira kwasababu hakuwahi kukutana kimwili na mwanaume yeyote. Stori za wanaume alizisikia alipokuwa kwenye maongezi na marafiki zake. Hata alipowaeleza kuwa bado hajatolewa usichana wake marafiki zake wengine walionyesha kumcheka kwa na kumuona mshamba, na wengine walimuona ni mwongo wakiamini kwamba inawezekana vipi na uzuri wote aliojaliwa na Mungu awe hajawahi kupita katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote. Mara nyingi alipokuwa akiwaeleza hivyo marafiki zake huzua mjadala mzito wakimpinga lakini ukweli ndio huo. Sio kwamba hakuwa na hisia za kimapenzi la hasha! alikuwa akijihisi kama wasichana wengine lakini alitamani usichana wake utolewe na mwanaume mmoja tu ambae ni Nelson.

*************

Kumbukumbu za Nelson zilikuwa vizuri kwani aliweza kufuata ile njia aliyopita siku moja alipokuwa akimsindikiza Vivian. Alifika mahali na kuona kwamba, akimuulizia maeneo yale itakuwa ni rahisi kufahamika kwasababu alikuwa akipita mara kwa mara kipindi alipokuwa shule. Nelson alianza kuulizia kwa watu mbalimbali huku akiwaonyesha picha ya mtu aliyekuwa akimtafuta lakini kwa watu wote aliowahoji walionyesha kutomfahamu binti yule. Hakukata tamaa aliendelea kuuliza huku na kule na hatimae alikutana na kijana mmoja ambae alionekana kumfahamu Vivian.

“Ahaa! Huyu binti nampata ila kwao sipafahamu, lakini cha kukusaidia itakapofika mida ya saa 10 jioni, njoo maeneo haya utamuona kwasababu huwa anapita kila siku hapa asubuhi na jioni.” Nelson alipata maelekezo hayo kutoka kwa kaka mmoja ambae alijitambulisha kwake kwa jina la Mejooli. Taharifa hizo zilimfurahisha sana Nelson, alifurahi kupita kiasi kana kwamba ndio alikuwa amekutana na Vivia kumbe sivyo. Saa yake ya mkononi ilimwonyesha ni saa 4.01 asubuhi. Muda uliobaki kufika saa kumi, Nelson aliona ni kama dakika tano, kwahiyo aliamua kukaa pale pale hadi muda alioambiwa ufike.

Alikwenda katika supermarket iliyokuwa jirani na pale na kuangalia zawadi ambayo alihisi zitamfaa mwanamke wa ndoto zake. Alinunua pafyumu aina ya ‘Dolly Girl Lil’ Starlet’ pamoja na zawadi nyingine kadha wa kadha. Baada ya manunuzi alikwenda kukaa katika duka moja iliyokuwa kandokando ya barabara ili kujikinga na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha siku hiyo. Macho yake yalikuwa makini kutazama barabani kila mara ili Vivian asipite bila kumtia machoni ingawa muda aliokuwa ameelezwa ulikuwa bado haujafika. Masaa yaliendelea kuyoyoma huku akiendelea kusubiri.

Kwa jinsi Nelson alivyokuwa na shauku ya kumuona Vivian angekuwa na uwezo wa kusogeza muda mbele basi angefanya hivyo ili aweze kukutana na binti ambae alimpa thamani ya kipekee moyoni mwake. Ilipotimu saa kumi kamili macho yake yaliongeza kasi ya kutazama barabari kwasababu ndio muda alielezwa kwamba Vivian atapita. Saa 11.00 jioni ilifika akiwa bado hajakata tamaa aliendelea kusubiri huku macho yake yakigongana na sura za watu wengi waliokuwa wakirejea majumbani mwao wakitokea makazini. Saa 12.30 ilifika Nelson akiwa bado barabarani anasubiri. Alikata tamaa kwasababu giza lilianza kufukuza nuru. Aliondoka na kurudi nyumbani akiwa amefadhaika sana kwasababu lengo lake halikuwa limetimia.

***********

Ilipofika saa 9.20 alasiri muda wa vipindi chuoni ulikwisha kwahiyo Vivia aliongozana na marafiki zake wawili ambao ni Joyce na Miriam hadi soko kuu. Kwasababu Vivian alipata kampani ya kuelekea huko waliamua kutembea kwa miguu kutokea chuoni hadi sokoni jambo ambalo liliwafanya wachelewe sana. Walianza kutembea wakiwa watatu wakifuata barabara ya ‘Nelson Mandela’ hadi wakafika mnara wa saa (clock tower). Walikamata barabara ya Sokoine na kunyoosha nayo moja kwa moja hadi kituo cha sokoni ambapo walikunja kulia na kuingia soko kuu la Arusha.

Kutokana na mwendo wao wa taratibu na stori nyingi walitumia zaidi ya lisaa limoja hadi kufika sokoni. Walifanya manunuzi kwa pamoja hadi kila mmoja akamaliza. Saa kumi na mbili jioni ndio walikwenda kupanda gari ingawa kila moja alikuwa anaelekea njia yake kwani Joyce alikuwa anaishi ‘Matejoo’ na Miriam alikuwa anaishi ‘Kwa mrombo.’ Hadi daladala inafika sakina tayari ilikuwa ni saa kumi na mbili na nusu. Vivian aliposhuka aliamua kuchukua usafiri wa bodaboda ili aweze kuwahi nyumbani kwasababu alikuwa amechelewa sana. Alipokuwa kwenye pikipiki njiani alimuona mtu kama Nelson lakini alihisi kama amemfananisha.

Alitamani amweleze dreva asimamishe pikipiki ili aweze kujua kama ni kweli alikuwa amemuona Nelson ama la, lakini muda ulikuwa umesonga sana kwahiyo aliamua kupuuza. Alizidi kujiuliza yule ni mtu gani ambae alikuwa amefanana na Nelson kiasi kile. Aliishia kujilaumu ni kwanini hakumwambia dreva asimamishe pikipiki japo kwa dakika moja ili aweze kuridhisha macho yake. Kitendo kile kilimsababishia mawazo zaidi na zaidi juu ya Nelson. Kichwani mwake alipanga siku itakayofuata atajitahidi kuzunguka zunguka yale maeneo kama atafanikiwa kumwona yule mtu ambae alimfananisha na mwanaume wa ndoto zake.

Vivian alitokea kumpenda sana Nelson kwani hata wakati mwingine alikuwa anatingwa sana na mawazo kiasi kwamba hadi watu wanamuona mgonjwa. Mama yake pia alishawahi kulishuhudia hilo kwa mwanae lakini alipojaribu kumuuliza, Vivian alipotezea juujuu. Hakujua mama yake anakereka jinsi gani kumuona akiwa katika mawazo mazito kiasi kile. Kesho yake alikwenda chuoni kama kawaida lakini aliendelea kuwa na mawazo sana. Marafi zake waliamua kumuuliza kilichokuwa kinamfanya akose raha ni kitu gani na ndipo alipoamua kuwasimulia habari za Nelson kwanzia mwanzo mpaka mwisho hadi tukio la jana kumuona mtu aliefanana na Nelson alipokuwa kwenye bodaboda. Walimwona chizi baada ya kuwaeleza kwamba kijana huyo alipata ufadhili wa kwenda kusoma marekani.

“Wewe mwanamke hazikutoshi kabisa yaani mwanaume hajakutamkia kuwa anakupenda, isitoshe yupo nje ya nchi halafu bado unaendelea kujishauwa kuwa unampenzi.” Joyce aliamua kumweleza jinsi alivyoweza kumuona mpuuzi kutokana na maelezo yake. Badala ya kupata faraja kutoka kwa hao marafiki zake alipoteza matumaini kabisa kwasababu hakuna hata mmoja ambae aliamini kuwa Nelson bado atakuwa anamawazo ya Vivian kichwani mwake. Kiukweli alijisikia vibaya sana hadi akajuta kwanini aliamua kuwatobolea siri yake. Ile siku aliiona mbaya kwake kwasababu marafiki walimuhudhi sana. Saa 5. 17 asubuhi aliamua kuomba ruhusa chuoni na kuondoka kuelekea nyumbani. Hiyo yote ni kutokana na kwamba marafiki zake walimuudhi kupita maelezo. Alitoka chuoni huku akiwa amekasirika sana. Alipanda daladala ambayo ilimpeleka hadi stendi ambapo alipanda gari lingine linaloelekea Sakina kwa Idd.

USIKOSE SEHEMU IJAYO

Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)