
Mtunzi: Frank Silaa
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Mwezi mmoja ulikatika akiwa bado hajafanikiwa kukutana na Vivian ingawa kila mwisho wa wiki alikuwa akitembelea maeneo ambayo alihisi ataweza kukutana nae lakini hakufanikiwa. Alipata wazo kwamba endapo atabahatika kukutana na Mejooli basi ampe namba za simu kusudi siku kijana huyo akikutana na Vivian aweze kumpa mawasiliano yake.
KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA NAYO...
Lakini tangu alipopata wazo hilo, hata Mejooli hakufanikiwa kumuona tena. Siku zilizidi kusonga huku akiendelea kusongwa na mawazo. Kutokana na jitihada zote za kumtafuta Vivian kukwama, ilisababisha muda mwingi awe mkimya na mwenye mawazo mengi sana. Wafanyakazi wenzake walikereka na tabia yake lakini mwishowe walihisi huwenda ndivyo alivyo. Baadhi ya wafanyakazi wa kike walitamani sana kuwa karibu nae lakini walishindwa kwasababu hakupenda mazoea na mtu yeyote. Fauku ya hayo, ufanisi wake wa kazi ulionekana kuwafurahisha wakubwa wake wa kazi.
***********
Vivian aliendelea kutumia dozi ya malaria na taifodi aliyokuwa amepatiwa hospitali. Baada ya wiki moja hali yake ya kiafya ilihimarika, na kurejea chuoni kuendelea na masomo. Wanafunzi wenzake pamoja na walimu walifurahi kumuona kwa mara nyingine kwasababu walikuwa wamemmisi. Yeye pia alifurahi kurejea chuoni kwasababu alikuwa amechoshwa na upweke wa nyumbani kwao. Mawazo juu ya Nelson hayakuwa yametoweka kichwani mwake kwani bado aliendelea kumuwaza kila mara. Siku zilizidi kukatika bila kuwepo kwa matumaini yeyote ya kumpata Nelson. Alianza kukata tamaa kwasababu hakuona dalili yeyote ya kukutana na mwanaume anaempenda. Hakujua kuwa Nelson amerejea Tanzania kwasababu na yeye pia angekuwa na jitihada za kumtafuta ili waweze kuonana. Akilini mwake alifahamu kuwa Nelson bado alikuwa nchini Marekani.
Alijiuliza ni kwanamna gani ataweza kuipata furaha aliyokuwa anahitaji kutoka kwa mtu anaempenda lakini aliishia kudondokwa na chozi kwasababu alizidi kupoteza matumaini. Umri nao ulikuwa unasonga kibaya zaidi alikuwa ameshawakataa wanaume wengi ambao walitaka kwenda kujitambulisha nyumbani kwao. Alianza kuona kwamba akiendelea na msimamo wake wa kumsubiri Nelson ataishia kuzeekea nyumbani kwao. Kwahiyo alianza kupata mawazo ya kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume ambae atajitokeza kumpenda kwa dhati. Alichoka kumsubiri mtu ambae hakujua atakutana nae kwa njia gani.
Alitamani na yeye kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kama ambavyo wasichana wengine wa umri wake wanavyofanya. Moyo ulimuuma sana pale ambapo alikuwa anaona marafiki zake wakifurahi na wapenzi wao. Ingawa alitamani sana kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote ambae atamuona anafaa lakini bado moyo wake ulizidi kuwa mzito akiamini kwamba furaha ya kweli haipatikani kwingine isipokuwa kwa Nelson. Kusema kweli Vivian alikuwa katika wakati mgumu sana wa kuweza kufanya maamuzi yenye tija maishani mwake. Baada ya mwaka mmoja, Vivian aliendelea kuwepo chuoni akiendelea na masomo yake kwa ngazi ya diploma. Bado hakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote kwasababu moyo wake ulikataa kabisa kumruhusu.
Siku moja wakati alipokuwa chuo, muda wa kuondoka kwenda nyumbani ulifika kwahiyo marafiki zake wakubwa ambao ni Miriam na Joyce walimtaka waondoke kwa pamoja kama ilivyo kawaida yao kuongozana. Miriam na joyce walitangulia taratibu na kumwacha Vivian akiwa anaazima kitabu cha stori kutoka kwa kijana mmoja ambae huwa anapenda sana kusoma vitabu vya hadithi. Walifika barabarani na kuvuka upande wa pili kusubiri daladala zinazoelekea mjini. Ghafla wakati walipokuwa wanamsubiri Vivian, Miriam aliona gari dogo likija na kuamua kujaribu kuomba lifti ya kuelekea mjini. Kwa bahati nzuri gari iliwasha endiketa ya kuingia katika kituo cha daladala walipokuwa wamesimama.
***********
Nelson alikwenda AICC kumjulia hali mkuu wake wa kazi Bibi ‘Chu-Hua’ mwenye asili ya China ambae alikuwa amelazwa katika hospitali hiyo tangu alfajiri ya siku hiyo baada ya kuugua ghafla. Tayari Nelson alikuwa amesha nunua gari ya kutembelea aina ya ‘Toyota Brevix.’ Alifika hospitali mida ya saa tisa lakini kwa bahati mbaya alikuta bosi wake amehamishiwa hospitali ya rufaa ya Mount Meru baada ya kuzidiwa ghafla. Aliamua kugeuza gari lake muda huohuo ili aweze kuelekea nyumbani.
Gari lilitoka katika geti la hospitali na kukunja kulia katika barabara ya Nelson Mandela kuelekea mjini. Nelson alianza kukanyaga mafuta kwa nguvu ili aweze kuwahi nyumbani kupumzika kwasababu ile siku alikuwa amechoshwa na kazi za ofisi. Kabla gari halijakole mwendo, macho ya Nelson iliwaona wanafunzi wawili wa kike walikuwa wanaomba lifti ya kuelekea mjini. Walikuwa ni wanafunzi wa chuo cha ‘Tropical Institute’ ambapo ndipo alipokuwa anasoma Vivian. Baada ya gari kusisimama wale wanafunzi walipanda harakaharaka, lakini mmoja alisikika akizungumza kwa masikitiko.
“Masikini tunamuwacha Vivi!” baada ya Nelson kusikia mmoja wa wale wanafunzi akilalama, aliuliza swali.
“Kuna mwenzenu mmemuacha?”
“Ndio! tumemuacha anachukua kitabu kwa mwanafunzi mwingine.” Mmoja wa wale wanafunzi alitoa ufafanuzi kwa Nelson.
“Mnauwakika anakuja sasa hivi?” Nelson alizungumza kwa msisitizo huku akibofya simu yake ya mkononi.
Kabla hawajajibu swali walilokuwa wameulizwa, Vivian alionekana akitembea taratibu kutoka njia ya chuo kuja barabarani.
“Vivi! Kimbia twende, tumepata lifti.” Mmoja wa wale wanafunzi alisikika akizungumza kwa sauti ya juu wakati alipokuwa ametoa kichwa chake nje ya dirisha la gari.
Kwa muda huo Nelson alikuwa bize akiendelea kubofya simu yake, kwahiyo hakuangaika hata kumtazama mwanafunzi aliekuwa anasubiriwa. Vivian nae hakufanikiwa kumuona Nelson ambae alikuwa ndani ya gari kwasababu viyoo vya gari vilikuwa ni vyeusi (tinted) Vivian aliongeza mwendo na kuvuka barabara kisha akafungua mlango wa gari na kuingia kwenye siti ya nyuma ambapo ndipo marafiki zake walipokuwepo. Baada ya kuingia ndani ya gari ndipo Nelson alipogeuza shingo yake kumwangalia mwanafunzi aliekuwa anasubiriwa. Ilibidi Nelson afikiche macho yake ili aweze kumwona vizuri msichana aliekuwa ameingia kwenye gari kwasababu alijihisi kama anaota.
“Am I dreaming?” (hivi ninaota?) Sauti ilisikika ikitoka kinywani mwa Nelson huku akionekana kutoamini kabisa kile kilichokuwa mbele ya macho yake. Vivian nae akionekana kushikwa na bumbuwazi kwasababu alijihisi kama vile yupo ndotoni.
“Are you Vivian?” (wewe ni Vivian?) Nelson aliuliza kwa sauti ya juu mithili ya mtu aliepagawa.
“Exactly, I’am.” (Naam, ndio mimi.) Vivian alijibu huku machozi ya furaha yakimtiririka mashavuni mwake.
“I cant believe!, I cant believe!” (siamini! Siamini!) Nelson alizungumza huku akifungua mkanda wa kwenye gari kisha akafungua mlango na kushuka. Alizunguka upande wa pili na kufungua mlango wa gari na kumshusha Vivian halafu akamkumbatia kwa furaha sana. Furaha ilizidi kifani kwa Vivian hatimae alikuwa akilia kama mtoto mdogo kwasababu hakuamini kabisa kilichokuwa kimetokea mbele ya macho yake. Marafiki zake walishikwa na butwaa kwasababu hawakujua kilichokuwa kikiendelea. Waliwahi kusikia jina la Nelson likitajwa na Vivian mara kwa mara lakini hawakujua kama ndie yeye yule walikuwa wamekutana nae kwa wakati ule.
“I have been looking for you for so long.” (Nimekuwa nikikutafuta kwa muda mrefu sana.) Nelson alizungumza huku akiwa bado amemkumbatia Vivian, wote wakilia kwa furaha.
“When did you come back Nelson.” (Umerudi lini Nelson.) Vivia alizungumza wakati alipokuwa akimtazama Nelson usoni huku machozi ya furaha yakizidi kumdondoka.
“Of course I have one year since I came back.” (Nina mwaka mmoja tangu nirudi Tanzania.)
Watu waliokuwa wakipita barabarani waliona kama mchezo wa kuigiza. Baadhi ya wapiti njia walidiriki kusimama na kuangalia kilichokuwa kikiendelea.
“Ok! let’s go.” (sawa! tuondoke.) Nelson alizungumza wakati akifungua mlango wa gari ili Vivian aweze kuingia. Mioyo yao ilijawa na furaha iliyopitiliza. Wote walijiona kama wapo ndotoni wanaota lakini ilikuwa mubashara kabisa. Kila mmoja alionyesha kufurahi kukutana na mwenzie. Nelson alikuwa akimtazama Vivian mara mbili mbili kwasababu alikuwa haamini kabisa kama amefanikiwa kukutana nae, tena pasipo kutegemea kabisa. Walipofika mjini Nelson aliwashusha wale marafiki zake Vivian na kuwashukuru sana. Alimpatia kila mmoja shilingi elfu kumi kwasababu kama sio wao pengine asingefanikiwa kumuona Vivian kwa siku zile.
Wale mabinti walifurahi sana, walimshukuru Nelson kwa zawadi nzuri aliyokuwa amewapatia. Saa ya kwenye gari ilionyesha ni saa 10.10 jioni. Walikubaliana kwenda kuzungumza katika hoteli maharufu sana mkoani arusha inayojulikana kwa jina la ‘Palace hotel.’ Kila mmoja alionyesha kuwa na furaha ya ajabu kukutana na mwenzie. Walifika salama hotelini huku kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kumweleza mwenzie juu ya hisia za kimapenzi zilizokuwa zikiwaka ndani ya nafsi zao mithili ya moto wa makaa ya mawe. Baada ya kufika waliagiza chakula pamoja na vinywaji. Nelson aliona kama uzuri wa Vivian umeongezeka mara dufu. Sura ya upole na tabasamu lisilokwisha katika sura ya Vivian ilisababisha Nelson azidi kupagawa zaidi. Kizuri zaidi ni pale ambapo Vivian alipokuwa akitabasamu vishimo vidogo mashavuni mwake vilijitokeza na kusababisha Nelson asitamani tabasamu la Vivian liishe. Walianza kula huku wakizungumza.
“Kwa furaha niliyoipata leo sijui kama itajirudia tena kwenye maisha yangu.” Vivian alizungumza kudhihirisha furaha aliyokuwa ameipata ni kubwa kuliko maelezo.
“Kusema kweli hata mimi nimefurahi sana kukutana na wewe. Nimejaribu mara nyingi sana kukutafuta lakini jitihada zangu zimekuwa zikigonga mwamba kila wakati.”
“Kweli Mungu anajibu maombi! Nimekuwa nikimuomba kila siku nikutane na wewe hatimae leo hii nimekuona kweli.” Vivian alizidi kuzunguma kwa furaha.
“Vivian!” Nelson aliita.
“Yes.” (Naam.)
“Are you married?” (umeolewa?)
“No! how about you, are you married?” (hapana! Vipi kuhusu wewe, umeoa?) Vivian aliuliza swali baada ya kujibu swali.
“No!” (hapana.) Nelson alijibu kwa kifupi.
“Why?” (kwanini?) Huku Vivian akitabasamu aliuliza swali ambalo lilikuwa linaeleweka lakini nigumu kulitolea maelezo.
“Kwasababu nilikuwa mbali na mwanamke wa ndoto zangu.”
“Nani ndio mwanamke wa ndoto zako?” swali lingine lilimuangukia Nelson kutoka kwa Vivian.
“Vivian! the one I talk to her right now” (Vivian! ambae nazungumza nae muda huu.) Nelson alizungumza huku akimtazama Vivian machoni kwa tabasamu mwanana.
USIKOSE SEHEMU IJAYO
Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi