SHEREHE KUZIMU (6)

Zephiline F Ezekiel
0
Mtunzi: Frank Silaa

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
“Nani ndio mwanamke wa ndoto zako?” swali lingine lilimuangukia Nelson kutoka kwa Vivian.

“Vivian! the one I talk to her right now” (Vivian! ambae nazungumza nae muda huu.) Nelson alizungumza huku akimtazama Vivian machoni kwa tabasamu mwanana.

KAMA SIMULIZI HII UNASOMEA NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI KUPATA VIPANDE VYOTE KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA NAYO...
Vivian alishindwa kuzungumza chochote machozi yalianza kumtoka kwa furaha.

“Vivian! frankly speaking, I want to marry you, because you’re the type of girl I used to dream.” (Vivian! kiufupi nataka kukuoa, kwasababu wewe ni aina ya mwanamke ambae nimekuwa nikimuota kila mara.) Nelson aliamua kuonyesha hisia zake za dhati kwa mwanamke anaempenda.

“Thank you so much Nelson, I promise to love you forever and ever!” (Asante sana Nelson, nakuahidi kukupenda daima milele yote.) Vivian alizungumza kwa furaha sana baada ya kusikia Nelson anataka kumuoa.

Maongezi yao yalinoga sana, hadi walipokuja kushtuka ni saa moja kasoro jioni. Nelson alimchukua Vivian kwa gari lake na kumpeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwao. Ingawa hakusalimiana na mama yake kwasababu usiku ulikuwa umeshaingia. Nelson alishuhudia jinsi ambavyo mtaa aliokuwa anaishi Vivian ulivyokuwa umejificha. Alikiri kwamba hata kama angeelekezwa asingeweza kufika kwasababu kulikuwa ni mbali halafu kuna kona kona nyingi.

Baada ya kuhakikisha mpenzi wake amefika nyumbani kwao aliwasha gari lake na kuondoka. Moyoni alijawa na furaha sana kutokana na kitendo cha kukutana na mwanamke wa ndoto zake. Kutokana na furaha aliyokuwa nayo alifungua mziki wa kwenye gari kwa sauti kubwa. Alikumbuka jinsi ambavyo kijasho kilimtoka kipindi cha nyuma alipokuwa akimsaka Vivian kwa udi na uvumba bila mafanikio. Alifika nyumbani kwa mjomba wake lakini hakuweza kuficha hisia za furaha zilizokuwa zikitamalaki moyoni mwake. Alionekana wa tofauti sana na siku zingine kwasababu alikuwa kachangamka kupita kiasi. Mjomba wake alimshangaa kwasababu hakuwahi kumuona katika hali ya uchangamfu kiasi kile kwahiyo ilimbidi amuulize kulikoni meno yote thelasini na mbili nje.

“Mjomba leo upo tofauti kabisa na nilivyokuzoea, unaonekana kuwa na furaha sana vipi wamekupandisha cheo kazini?” Mjombwa wake Nelson aliuliza.

“Hapana mjomba furaha yangu haihusiani na mambo ya kazini ila usijali nitakueleza kwa utaratibu muda utakapofika. Ninaimani ni habari ambayo hata wewe itakufurahisha pia.” Nelson alizungumza kumjibu mjomba wake huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu bashasha.

“Sawasawa!” Mjomba alijibu huku akitingisha kichwa kuonyesha amekubali.

Siku iliyofuata Nelson alichelewa kuamka kwasababu alilala sana. Hakuna siku ambayo alipata usingizi mzuri kama ile siku. Hayo yote ni kwasababu alihisi mzigo mzito uliokuwa ndani ya moyo wake ameushusha. Alipoamka alijiandaa haraka haraka na kuelekea katika eneo lake la kazi. Mshangao alioupata mjomba yake pindi alipomwona Nelson akiwa tofauti na siku zingine ndivyo ambavyo hata wafanyakazi wenzake walionekana kushangazwa na furaha aliyokuwa nayo kwa siku ile alipofika kazini. Alicheka na kuzungumza na kila mtu vizuri kuliko siku zingine. Kiukweli alizua mjadala mkubwa wa chini kwa chini kwa wafanyakazi wenzie kwasababu hawakuwahi kumuona katika hali ile hata siku moja tangu alipoanza kazi.

Walijiuliza Nelson aliamshwa na nani siku zile. Ilipofika saa tisa alasiri aliwasha gari lake na kwenda hadi chuoni kwa kina Vivian kumchukua. Alimpeleka hadi kwenye duka la mfanyabiashara maarufu mjini arusha kwa jina la Benson na kumnunulia simu nzuri kwaajili ya kuweza kuwasiliana kwa urahisi. Alimchagulia simu aina ya ‘Nokia lumia 1320’ kwa gharama ya shilingi laki 8 za kitanzania. Vivian alifurahi sana kununuliwa simu na mpenzi wake. Baada ya hapo walikwenda kwa sonara ambapo Nelson alimnunulia mchumba wake mkufu, hereni na saa ya mkononi zote za dhahabu. Nelson alijitahidi kumuonyesha mpenzi wake ni njinsi gani alikuwa anampenda na kumthamini kuliko kitu chochote.

Baada ya hapo alimchukua na kumrudisha hadi nyumbani kwao na kumwacha na kuondoka. Moyo wa Vivian ulijawa na furaha isiyopimika. Alitamani Nelson amuoe haraka kwasababu alihisi kumpenda sana. Furaha aliyokuwa anapatiwa na mchumba wake ilimfanya asijutie msimamo wake wa kuwakatalia wanaume ambao waliwahi kumwitaji kimapenzi. Hali ya hewa ya jiji la Arusha ilitokea kumvutia sana Nelson na kuamua makazi yake ya kudumu yawe huko. Kwahiyo alichukua mkopo benki na kununua viwanja viwili na kuanza kujenga nyumba mbili kwa pamoja, yaani nyumba yake pamoja na ya mama yake.

Alipania kumuamishia mama yake mkoa wa Arusha ili aweze kumsaidia kwa ukaribu zaidi. Ujenzi ulikuwa unafanywa kwa kasi sana kwasababu Nelson alitaka siku ya harusi ndio na uzinduzi wa nyumba yake ufanyike. Mwezi wa pili baada ya Nelson kukutana na Vivian alikwenda kujitambulisha ukweni. Alisindikizwa na rafiki yake mmoja ambae anaitwa Lucas. Walifika na kupokelewa vizuri na mama Vivian. Walikula na kunywa vilivyokuwa vimeandaliwa. Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwasababu Nelson alifanikiwa kumfahamu mama mzaa chema. Nelson alifurahishwa na ukarimu aliouonyesha mama mzazi wa mke wake mtarajiwa.

Baada ya utambulisho wiki mbili zilizofuata Nelson alimvisha pete mchumba wake Vivian katika tafrija fupi iliyofanyika katika ukumbi wa ‘Tindigani garden’ iliyopo maeneo ya kimandolu jijini arusha. Kila mtu aliyemuona mchumba wa Nelson alipaza sauti kuusifia uzuri aliokuwa amejaliwa na Mungu. Wafanyakazi wenzake walimsifu kwa uchaguzi mzuri aliokuwa ameufanya. Pamoja ya sifa nyingi za ulimbwende ambazo Nelson alizisikia kutoka kwa watu mbalimbali waliokuwa wakimwagia mchumba wake, Nelson aliamini kwamba ni kweli Vivian ni mzuri sana baada ya kumsikia mama yake mzazi akimsifia Vivian kwamba ni msichana aliyeumbika kama malaika.

Mwezi uliofuata nyumba ya Nelson pamoja na ya mama yake ilikamilika japokuwa zilikuwa katika maeneo tofauti tofauti kwani mama yake alimjengea maeneo ya ‘Kambi ya chupa madukani’, na yeye alijenga maeneo ya Sekei. Baada ya nyumba kukamilika mama yake aliamia rasmi jijini Arusha. Mama huyo alimshukuru Mungu kwa uwezo ambao alimjalia mwanae kuweza kukamilisha ujenzi ule ndani ya muda mfupi. Zilibaki masiku kadhaa harusi ya Nelson na Vivian iweze kufungwa.

Maandalizi ya nguvu yalifanyika kwaajili ya sherehe kubwa ambayo Nelson alikuwa amepanga kufanya. Bosi wake aliekuwa amelazwa hospitali aliruhusiwa baada ya hali yake ya kiafya kuhimarika. Vivian nae alijisikia furaha sana kwasababu alikuwa ameshamaliza masomo yake. Nelson hakuomba mchango wa harusi kutoka kwa mtu yeyote lakini kutokana na kwamba alikuwa ni kipenzi cha watu, alipokea michango ya kimawazo na kipesa kutoka kwa marafiki zake. Nelson aliamua kuandaa kadi za mwaliko wa harusi yake kama njia nzuri ya kuwaalika ndugu jamaa na marafiki, kwahiyo ‘Baraka Stationary’ waliopo ‘Sanawari’ walipokea tenda ya kutengeneza kadi ya mwaliko wa harusi. Walitengeneza kadi nzuri sana ambayo ilikuwa inasomeka kama ifuatavyo.

“Familia ya Bw. na Bi. Richard P. Urassa.

Wanayofuraha tele kukukaribisha.

Bw, Bi, Mwl, Mchu, Dakt, Ndug, Bw/Bi

---------

Kwenye harusi ya kijana wao.


Na


Katika kanisa la ‘Alive God’ mianzini,

Jumamosi ya tarehe 22/12/2001,

Saa 8.30 mchana. Na baadae,

Kwenye tafrija fupi katika,

Ukumbi wa ‘Moon Hall’ saa 2 usiku.

Karibuni sana.”

Kusema kweli maandalizi yalikuwa ni motomoto kwasababu mambo yalikuwa yanafanyika kisasa zaidi. Marafiki wa nje ya nchi walialikwa kwa njia ya barua pepe. Marafiki 11 walijibu barua pepe na kusema kwamba watahudhuria katika sherehe ya harusi ingawa baadhi ya marafiki waliomba radhi ya kutohudhuria kutokana na ubize wa kazi. Iliundwa kamati ya harusi ambayo ni imara kwaajili ya kuhakikisha harusi inafanyika barabara. Mjomba wake Nelson ndie aliyeteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya harusi. Kamati hiyo ndiyo ilipanga wageni wote wa nje ya nchi wafikie katika hoteli ya ‘Snow crest’ iliyopo kwa mrefu jijini Arusha.

************

Sherehe ya mwago (send off) ilifanyika siku ya alhamisi nyumbani kwa kina Vivian kuanzia saa moja kamili jioni. Ni siku hiyohiyo ajali mbaya ya gari ilitokea mtaani kwao, baada ya gari dogo aina ya Toyota IST lenye namba za usajili ‘T 701 XWX’ kuwagonga watoto watano wa shule na kupoteza maisha papo hapo. Tukio lile lilisababisha Vivian akose raha kabisa kwasababu alishuhudia miili ya watoto ambao walikuwa wamepoteza maisha. Pamoja na hayo yote lakini hapakuwa na sababu ya kuhairisha sherehe kwahiyo mambo yaliendelea kama kawaida. Sherehe iliandaliwa na mama Vivian bila kumshirikisha mwanae. Ingawa Nelson alitamani kuwapa mchango wa pesa kidogo ya kuweza kuwasaidia katika maandalizi ya sherehe lakini mama Vivian alikataa na kusema kwamba anauwezo wa kumudu sherehe atakayoifanya.

Ilionekana ni sherehe ambayo ilikuwa ni ya kitamaduni japo kuwa ilikuwa na watu wachache sana. Mama Vivian alikuwa amevaa sare na watu ambao Vivian hakuwafahamu. Sare waliyokuwa wamevaa ilikuwa ni kaniki na kiunoni walijifunga mitandio mekundu. Mwonekano wao ulimtisha sana Vivian, ingawa alijikaza hofu yake isijidhihirishe mbele ya wageni. Uchache wa watu haukumshangaza Nelson akajua ndio sherehe za kisasa zilivyo siku hizi hakuna mlundikano mkubwa wa watu kama zamani. Mshehereshaji alikuwa ni mwanamke ambae pia alikuwa mgeni machoni pa Vivian kwani hakuwai kumuona wala kumsikia.

Sherehe ile ya mwago ilimpa mawazo mengi sana Vivian kwasababu watu waliohudhuria katika sherehe yake hakuwahi kuwaona tangu kuzaliwa kwake. Halafu isitoshe alishangazwa pia na vyakula vilivyokuwa vimeandaliwa kwani hapakuwa na wali wala pilau bali chakula ilikuwa ni nyama tu ambayo Vivian hakujua imepatikana vipi. Halikadhalika kwa upande wa vinywaji hapakuwa na soda wala bia bali kinywaji pekee kilichokuwepo ni supu iliyopatikana kutokana na nyama zilizochemshwa. Licha ya kushangaa lakini pia Vivian alijawa na uoga ndani yake, jambo ambalo lilisababisha atengeneze tabasamu la kinafiki usoni mwake ili asiweze kushtukiwa na wageni wake. Ratiba ya sherehe ile iliendelea ambapo muda wa chakula ulifika.

Roho ya Vivian ilikuwa inagoma kabisa kula zile nyama zilizokuwa zimeandaliwa lakini hakuwa na namna ya kukataa kwasababu ingeleta picha mbaya kwa wageni waliokuwa wamehudhuria sherehe akiwemo mume wake mtarajiwa na mama mkwe. Walianza kula zile nyama na kila mmoja alionekana kuzifurahia. Hapakuwepo na mziki kama kwenye sherehe zingine bali Mama Vivian pamoja na watu wake waliburudisha watu kwa kuimba nyimbo mbalimbali kwa lugha ambayo haikuweza kufahamika kiurahisi.

USIKOSE SEHEMU IJAYO

Ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi Share App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)