LISEME JINA LANGU (14) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 7 Aprili 2020

LISEME JINA LANGU (14)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: Pablo

SEHEMU YA KUMI NA NNE
Akiwa anachechemea mguu mmoja huku majasho mengi yaliokuwa yanamtiririka kwa kasi na kuzidi kulowesha shati akajikokota na kuchukua lile dude la shisha na kulinyanyua na kunielekezea mimi kwa lengo la kunitwanga nalo na kunifanya nibaki nimemtumbila macho huku Nikiwa najaribu kuinuka lakini maumivu ya mshale wa bega ulitosha kabisa kuniua nguvu na kubaki nikimuangalia tu Robertson aliyekuwa yupo tayari kabisa kunirushia dude lile.............................

SASA ENDELEA...
Bila hata ya huruma robertson akanirushia lile dude la kuvutia shisa ambalo lilikuwa lina moto wa kutosha ambalo baada ya kunifikia nikalivuia kwa mkono lakini mikaa mikaa ya lile dude lilitosha kabisa kuniunguza na kujikuta nikipiga kelele kutokana na maumivu makali niliyoyapata kutokana na moto ule.Mikono yangu ndio ulikuwa imebabuka kwa moto ule ambapo baada ya robertson kunirushia akaanza kucheka kwa nguvu na kuanza kunitukana wakati huo mimi nikiwa bado nipo katika maumivu makali yaliofanya nidondoshe machozi.nikiwa katika hali hiyo teke lingine kali la shingo lililorushwa na robertson likatosha kabisa kuninyong'onyesha lakini Hali nyingine ya mshangao ikatokea baada ya Robertson Mugalula kuanza kugalagala na kuugulia mguu ule alionipiga teke kwa maumivu kutokana na mshale niliompiga na kujikuta akijisahau na kuutumia kunipigia jambo lililosababisha aanze kuugulia.hali mpya ya nguvu zikanipanga na kujikuta nikinyanyuka kwa nguvu na kasi ya ajabu iliyosababisha maumivu makali ya kubabuka kwa mikono yangu iliyounguzwa na dude la kuvutia shisha alilonipigia nalo robertson na kujikuta nikipaniki na kumfuata palepale robertson na kuanza kumshindilia ngumi nzito nzito zisizokuwa na idadi na kumfanya aanze kuvuja damu usoni kutokana na ukali wa ngumi zangu nilizokuwa nampiga kwa hasira iliyovuka kipimo.Nikiwa katika hali ile yakumsindilia ngumi hizo robert aliyekuwa amelala tu hana la kufanya kutokana na kumdhibiti vizuri Baba moureen akanichoma kisu cha mgongo kilichoingia kidogo na kunishtua kutokana shambulio hilo lilikuwa la haraka.Akiwa anajiandaa kunichoma tena nikafanikiwa kunyanyuka na kumbidua na kufanikiwa kumlaza chini na kuchukua kisu chake alichonichoma nacho cha mgongo na kuanza kumuelekezea yeye tena mwenyewe baba moureen aliyekuwa ametoa macho kutokana na kushangaa nilivyombidua na kubaki akihema juujuu na kubaki akiwa ananiangalia.kipindi hicho mama moureen na moureen mwenyewe walikuwa wanalia na kunisihi nisichukue maamuzi magumu ya kumuua jambo lililonifanya hasira zianze kupungua kidogo kidogo na kubaki nikiwa nimeshika kisu kwa lengo la kumchomoa

"Anayekufanyia ubaya sio lazima umlipizie naye ubaya Najua mpaka sasa ushanifanyia mabaya mengi yalioniharibia maisha yangu kisha tu kumpenda mwanao ambaye naye hakusita kunionyesha mapenzi ya kweli na kunipa nafasi katika moyo wake.Kwa nini humchagulie mtu atakayemuoa wakati anao uwezo wa kuchagua na yeye ampendaye na mtu sahihi wa kumuoa.Najua na wewe wala haujachagulia mtu wa kumuoa ilitokea wote mkajikuta tu mkipendana.Mzee mimi Nishakusamehe kwa yote uliyonitendea lakini kumbuku pesa yako haiwezi kuzuia penzi la dhati hata siku moja" kwa hasira iliyochanganyika na machozi yaliokuwa yananitiririka katika mashavu yangu nikamwambia baba moureen maneno yale nakukiachia kisu nilichokishika katika sakafu na kunyanyuka kisha nikamnyooshea mkono baba moureen nikiwa katika lengo la kumnyanyua ambapo naye bila ya kusita akanipa mkono wake akiwa tayari kabisa kunyanyuliwa na mimi.Ghafla kabla hata sijamnyanyua nikapigwa kikumbo kikali kikiambata na mtama ulionifanya nidondoke mzima mzima na nilipomuagalia ni nani aliyenipiga nilikuwa nishachelewa kutokana na robertson mugalula niliyedhania awezi tena kunyanyuka alikuwa kashanikalia juu yangu mkononi akiwa ameshika kisu nilichokidondosha chini akiwa kabisa lengo moja tu kukitumbukiza katika kifua changu.Hata nilipojaribu kutetereka mwili wangu ulisita kabisa ganzi kubwa ikaingia na kunifanya nikibaki nimefumba macho sikutaka kabisa kuona kwa macho kisu hicho kilichokuwa kinateremshwa taratibu na robertson mugalula.

"Kwa herii malaya wa kiume wewe............Paaaaaaaaaaaaaaaaa" katika hali nisiyoielewa mlio wa risasi ukasikika kabisa katika mboni ya masikio yangu iliyonifanya nifumbue macho na kumuona robertson mugalula akiwa ameganda karibia kabisa na kifua changu huku kisu alichoshika kwa lengo la kunichoma kikiishia njiani.Macho yake aliyekuwa kayatoa huku domo akiuacha wazi kwa muda.Alama ya toba ya risasi ndio iliyojichora katika kichwa chake na damu nyingi zikianza kuvuja kwa kasi kisha akadondokea pembeni kwa kulala huku damu zikiendelea kuvuja.Nikajizoa zoa kuinua kichwa changu niangalie ni nani aliyempiga robertson risasi alikuwa si mwingine bali ni rafiki yake kipenzi ambaye alikubali kabisa kumpa binti yake baba yake moureen.hakika macho yangu yalipingana kabisa kuniwezesha kuamini kuwa alikuwa ni baba yake moureen ndiye alimpiga robertson risasi na kumuua jambl ambalo pia lilimuacha mdomo wazi mama yake moureen naye ambaye alikuwa kama kapigwa shoti ya umeme na kutotaka kuamini na kujikuta mikono yake akiweka kichwani na kusikitika.moureen akanifuata taratibu na kunikombatia pale pale nikiwa chini huku akiongea maneno ambayo sikuweza kuyakumbuka kutokana na mimi wakati huo nilianza kuona ukungu mwingi mweusi ulitanda katika mboni ya macho yangu na kuzimia na kutojua kilichoendeleaa wakati huo.

Macho yangu yalipofumbuka tena ikiashiria fahamu zangu zilikuwa zimerudi ilikuwa nipo hospitali iliyokuwa na mandhari yenye kumvutia mgonjwa nikiwa nimetundikwa dripu na kufungwa vungwa bandeji katika mikono yangu.ilichukua muda kidogo kukumbuka kilichonitokea nyuma mpaka pale mlango ulipofunguliwa na kuingia daktari wa kike aliyeambatana na moureen akiwa na baba yake na mama yake ambao kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nilishuhudia wazazi wa moureen wakiwa wanatabasamu na kunikombatia pale pale kitandani nilipolazwa.
"Hakika yaliopitwa si ndwele tugange ya jayo kama ulivyoweza kuokoa maisha yangu kwa kusita kuniua na mimi nikamuaa kukusaidia kumua adui yako kwa lengo moja tu ili umuoe binti yangu ambaye kwa kukusubitishia utapopata ruhusa ya kutoka basi mtafunga pingu za maisha" maneno yale matamu ya baba moureen yalinifanya nitabasamu kwa kiasi kikubwa na kuanza kumshukuru mungu kimoyomoyo kutokana na miujiza ambayo kaionyesha haraka kuliko nilivyotarajia.

"mmh sasa itakuaje maana nimefanya vitu vingi mapolisi hawatanikamata??"
"haha pablo ni kama pesa yangu iliweza kufanya vile vya nyuma ambavyo sitaki tena kuvikumbuka ndio hiyo hiyo pesa ndio imefanikiwa kuzima kelele zote za hapa mapolisi hawa wanapenda pesa tu na wala usijali."
"Daaa hata siamini"
"Amini sasa mume wangu kila kitu kipo salama". Ukurasa mpya wa maisha yangu ukaanza hii ni baada ya kupona tu Nikafungua ndoa kubwa ya mimi na Mrembo Moureen iliyowaacha gumzo miongoni mwa watu waliobahatika kuhudhiria kutokana na pesa nyingi iliyotoka mfukoni mwa baba yake moureen ambaye akatuzawadia nyumba kubwa nzuri ya kuisha na Mama moureen kutoa zawadi ya Magari mawili ya bei mbaya.
"Muwe wangu nimepata ujauzito"Yalikuwa ni maneno ya moureen baada ya miezi sita kupita baada ya kufunga ndoa wakati huo tukiwa ndani ya jumba letu la kifahari tulilopewa zawadi.
"Wooow kweli moureeen"
"Yeaah mpenzi"
"oooooooo jamani siamini ngojea nisikilize anavyoacheza cheza."
"Duu jamani pablo bado"
"Daa mke wangu siamini hebu sema jina langu mpenzi"
"jamani si pablo mume wangu" Hakika kilichoendelea ni utamu wa maisha ndio ulifuatia lakini haukuweza kunifanya nisahau yalionitokea ambayo kwa mara nyingi Nilitamani kujisahaulisha lakini haikuwezakana na haitawezekana mpaka nitakapo ingia kaburini.

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO



MWISHO

Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni