UZOEFU (20) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 9 Aprili 2021

UZOEFU (20)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

JINA: UZOEFU
Mwandishi: Elisha Msafiri

SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
" Afu we unaonekana mpole kumbe mtundu hivyo!" Aliniambia binti yule huku akinitizama mara mbili mbili usoni.
SASA ENDELEA...
Mvua iliendelea kunyesha na pamoja nakuwa kioo kilifungwa maji yalianza kuchuruzika ndani.
" ooooohooo!...naomba nikae upande wa huko wee usiloane!" Nilimwambia binti huyo huku nikionyesha sura ya majonzi.
" No thank you!...nitayazibiti tu!" Binti huyo alipingana na mimi huku akitoa mtandio kwenye mkoba wake kwa nia ya kuyazibiti maji.
"Ooh una akili wewe!" Nilimsifia baada ya kufanikiwa kuyazibiti maji kwa asilimia kadhaa.
" ha ha ha kama wewe!" Alinitania mrembo huyo.
" mimi naitwa Tom!" Nilijitambulisha ili niweze kujua na yeye jina lake
" Tomas!?" Alibashiri kirefu cha jina langu.
" Nop!.. only Tom!" Nilijibu kwa kingereza cha mikogo.
" Oh nafurah kukujua Tom!.... mi naitwa Caroline!"
" Nafurah kukufaham pia!, Caroline wee unasoma au unafanya kazi!?!
" Heeh!, me mfanyakazi wewe shule nilishamaliza siku nyingi sana!"
" Haa mbona bado mdogo ivyo ulikuwa unarushwa madarasa nini!" Nilimtania Caro naye akacheka sana kabla ya kunijibu.
" Hamna bhana!, vipi wewe!?"
" mimi ndo mfanyakazi wa halali sasa!" Niliuficha uanafunzi wangu pembeni kukwepa kujishusha hadhi.
" Ha ha ha! Wewe ndo ulirushwa madarasa sasa!...wapi unafanya kazi Tom!?"
" Kampuni moja ya kiburudani zaidi sijui utakuwa unaifahamu? Inaitwa Numerator's Entertainment!"
" Yeah nimeshapajua nilipitaga siku moja!"
" Kwani nyie ofisi yenu ipo wapi!?"
" hata usijali tukishuka ntakuonyesha coz unapita kwanza kwetu ndo ufike kwenu!"

Tuliendelea na story za hapa na pale hadi gari likafika mwisho. Bado mvua ilikuwa ikinyesha japo sasa yalibaki manyunyu madogo madogo.

Nilishuka na mtoto mzuri Caroline na wote tukajisitiri chini ya kijimwamvuli chake kidogo kuikwepa mvua. Ilinibidi nimshike bega ili tutembee vizuri kwa kuwa mwamvuli ulikuwa ni mdogo.

" Caroline samahani kuna kitu nataka kukuomba japo hujanijua vizuri lakini naomba uniamini!" Nilimwambia Caro baada ya kufika nnje ya ofisi yao naye akavuta umakini kujua nataka kusema nini!

Baada ya kurizika na umakini wake nikaendelea.

" Naomba uniazime huu mwamvuli wako afu saa ya kutoka ntakuletea!" Niliongea kwa unyenyekevu ajabu.

" Ha ha ha! ....hicho tu umepata sema kingine" Aliniambia Caro akiwa ameachia tabasam pana, swali lake likawa zuri sana kwangu.

" Kitu kingine your phone number ( namba ya simu) ili nikiuleta nikupate!"

Ingawa kwenye mwamvuli Caro alikuwa mwepesi sana kutoa majibu lakini kwenye swala la namba za simu akawa mziti kidogo.

" ok nipe zako basi mie ntakucheki!" Baada ya kufikiri kwa muda alifikia maamuzi hayo.

" Nop me ndo nimekuomba please!" Niliongea kwa sauti ya ushawishi huku nikimpa simu yangu aziandike.

" Wee andika me ntakutajia tu!" Aliongea Caro huku akikwepa kushika simu yangu. Ukweli nikuwa nilimpa aniandikie yeye sababu nilihisi mikono yangu inatetemeka, ila kwa kuwa aligoma nikawa sina budi kuandika mwenyewe.

" zero...seven......!"" Nilirudia namba alizokuwa akinitajia huju nikiishika simu yangu kwa mikono miwili kupunguza mtetemo na hadi muda sikuelewa ni kwanini nilikuwa natetemeka.

" Poa basi any time ukitaka kusepa we nistue tu me ntakuletea!" Nilimwambia Caro hali nikijua sitaonana naye tena badae, kwani me si mtu wa kukaa ofisini na siku hiyo show ( Onyesho ) lilikuwa linafanyika bwalo la Magereza, Ukonga.

Japo niliachana na Caroline lakini picha yake ilisalia kichwani, Ubongo wangu uliendelea kumtathimini mrembo huyo, maziwa yake yaliyosimama kifuani mwake mithili ya miiba ya mchongoma yalinivutia sana, Rangi yake nyeupe iliyotandikiwa zulia la vinyweleo vya brown vilivyolala sawia ndio ulikuwa haswaa ugonjwa wangu. 

Pia macho yake yenye boriti za rangi ya brown yalinipa hamu kila aliponitazama, si hayo tu umbo lake la kizungu lenye tumbo dogo na wezere la kiasi vilinishawishi kutaka kuongozana naye kila nnapokwenda hata mtindo wa nywele aliokuwa amesuka ulinifanya niamini huyo binti ni Africast. 

Kiufupi Caroline alikuwa ni mrembo aliyekamilika na alionekana anajitambua. kidume nikawa nimefanikiwa kuondoka na namba zake za simu huku kichwani nikiwa na mipango kebe kebe juu yake. Sijui nimualike chakula cha usiku kesho, sijui niende naye 21 century tukaangalie cinema, Sijui nimpeleke gym canner tukacheze golf, sijui nimwalike nyumbani mwisho wa wiki tucheki series, hayo yote niliwaza mimi.

Majira ya saa saba za mchana nilimpigia Caro simu.
" Hello!"
" hello!"
" unajua uko unaongea na nani!?!

" mmmh Tom!?" Caro alijibu kama anauliza lakini tayari alikuwa ashanijua.

" ha ha ha! How did you know that!" ( ulijuaje?) Nilicheka kizungu na kumuuliza king'eng'e!
" sauti yako me naiju tu!"

" Ok nakukaribisha lunch my dear!" Ingawa bado sikuwa nimeenda kula lakini nilikuwa nasumbuliwa na kisebu sebu cha kumpigia simu huyo mtoto ili mradi tu nisikie sauti yake.

" wow!... thanx....unakula nini!?"

" bado cjajua naomba unisaidie kuchagua basi!" Nilijitia kumdekea.

" mmmnh kula wali na samaki!" Alinichagulia caro.

" wow i like it!....sasa nishushie na nini!" Niliendelea kumsumbua mtoto wa watu kama namlipa vile.
" kunywa na juice ya embe!"

" duh!.. kweli we nouma umejuaje vitu nnavyopenda!" Nilimvika kilemba cha ukoka Caro kwani mimi ni mpenzi wa fanta orange, ila nilimfagilia tu kumvuta karibu zaidi.

" me nikimuona mtu tu naweza kujua anapenda nini!" Alijitapa Caro bila ya kujua kuwa maneno yangu ni punje za mahindi zinazompeleka kuku kwenye mtego.

Ni Caroline pekee alikuwa akinipeleka puta siku hiyo kiasi cha kunifanya hata nimsahau Malha niliyekuwa na miadi naye badae.

Hata mara baada ya kwenda na kukutana na Malha siku hiyo bado akili yangu ilikuwa ikimuwaza Caro kwa kiasi kikubwa hadi nafsi yangu ikaanza kunisuta ' yaani upo na huyu lakini bado unamuwaza yule?' Nafsi ilinishushua kwa sauti ya upole lakini sikujali sana.

" Tom jamani mbona wanifanyia hivi mwana wa mwenzio au kwakuwa nimeshakupa mwili wangu uufanye unachotaka?? .....nambie basi kama hilo ndo tatizo nisirudie tena!"

"Hamna sio hivyo!!"

" Sasa tatizo nini Tom mbona mwanzo hukuwa hivyo!...wajua ni jinsi gani nakupenda....wajua nimeachana na my boy kwajili ako lakini sasa mbona wanifanya nijute Tom!?"' Sauti laini sana iliyokuwa na lafudhi ya pwani ilikuwa ikitoa lawama zilizopenya moyoni mwangu kama msumari wa moto kwa kidonda. 

Malalamiko yote aliyokuwa akitoa Malha ilikuwa ni ukweli mtupu kiasi cha kunifanya nishindwe hata la kujitetea na kubaki nikijibaraguza kwa haya. Siku tatu tu baada ya kulala na Malha na urafiki wangu na Caro kuanza kushika kasi kulionyesha wazi kuwa kuna kitu kimeingilia kati kwenye penzi letu changa mimi na Malha. 

Kilicholibainisha hilo ni zile simu zetu za usiku tulizokuwa tukipigiana na Malha. sasa tangu Caro alipoongezeka naye amekuwa akitaka tuongee usiku, tena ndani ya muda huo huo nnaoongea na Malha. Je ntajigawanya vipi? Huo ndio ukawa mwanzo wa hitilafu kati yangu na Malha. 

Mara ya kwanza tulikuwa tukiongea hadi analala simu ipo hewani lakini hivi sasa haziishi dakika mbili nimeaga, mara simu iko bize, nikiulizwa nilikuwa naongea na nani, majibu ni rafiki yangu wa kiume, rafiki yangu gani wakiume naweza ongea naye nusu saa nzima usiku? Hilo halikumuungia akilini Malha, mara siku nyingine mtandao unasumbua.

Japo lipo neno linalosema huwezi kutumikia mabwana wawili lakini hata mabibi wawili huwezi kuthubutu, Mtaka vyote kwa pupa hukosa vyote na mshika mbili moja humponyoka. Methali hizo mbili zilikuwa zikiuogofya moyo wangu. Itakuwaje kama niking'ang'ana kuwa nao wote kisha nikawakosa wote, ama je ni nani uyo 

Mmoja atakayeniponyoka, baada ya kufikiria hayo ndipo nilipoamua kuwapandisha Malha na Caroline kwenye mizani ili kujua nani atamzidi uzito mwenzake. Kwa mtazamo wa macho na akili Caro alikuwa kamzidi Malha vitu vingi japo Caro naye alifunikwa na Malha kwa kishuzi lakini hiyo kwangu haikuwa sababu kubwa sana. 

Moyo hauna unafki kama mdomo, kura zote zilimuangukia Caro lakini nilipokumbuka kale kamchezo alikonipa Malha nilisita kidogo kufanya maamuzi ya moja kwa moja juu ya kumchinjia baharini, Hakika Malha alifunzwa unyagoni!... uongo dhambi nilitamani nipate tena walau mechi hata moja tu ya marudiano. Lakini kwa mara nyingine tena nilisita. 

Kitanda usichokilalia huwezi kujua kunguni wake, nawezaje kumuhukumu Caro juu ya mchezo wa kitandani hali yakuwa sijawahi kupanda naye. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, ile kura ya ndio iliyopigwa na moyo juu ya Caro ikawa imempitisha na kumpatia hatamu ya kuniendesha kama ataweza.

Urafiki wa mimi na Caro ukazidi kunoga. Hakuna kati yetu aliyeweza kuamka bila ya kutaka kujua mwenzake kaamkaje, hakuna kati yetu aliyekula bila kumkaribisha mwenzake, hakuna kati yetu aliyeweza kulala bila kuongea na mwenzake na hakuna kati yetu ambaye hakuwa na shauku ya kutaka kuonana na mwenzake kila siku, yote hayo yalifanyika kwa mapenzi makubwa huku jina la kaka na dada likiwa limeitawala midomo 

Yetu kila mtu alipotaka kumuita mwenzake. Ndani ya muda mfupi kutokana na maongezi mengi ya simu za usiku niliweza kufahamu vitu vingi dada ( Caro ) anavyovipenda na vichache anavyovichukia halikadhalika niliweza kujua yeye ni mtu wa aina gani na siku nikitaka kumshika nilielewa fika nimkamatie wapi na sijui kwa upande wake ila na yeye kama alikuwa ni mdadisi basi atakuwa ameshanijua vilivyo. 

Mahusiano yetu yaliendelea namna hiyo huku nikizidi kuyaimarisha kwa kwenda kumtembelea Caro mara kwa mara nyumbani kwao majira ya jioni na mara chache nikitoka naye kwenda kubaridhi ufukweni. 

Baada ya kumwamini Caro kwa kiasi kikubwa niliamua kumuingiza katika jaribio la kwanza ili kumpima ni jinsi gani ananipenda au kunithamini na majibu ya jaribio hilo ndiyo yangenipa jibu la kwenda ngazi inayofuata nnayoifikiria ama nibaki hapa kwenye ukaka na udada nilipo hivi sasa!

Ilikuwa ni kama sheria pindi niamkapo asubuhi nikiwa salama na kumshukuru muumba wangu kwa sala fupi basi kinachofwata ni kumjulia hali Caro iwe kwa kumpigia simu ama kwa kumtumia ujumbe mfupi, ali mradi nijue tu kuwa na yeye ni buheri wa afya na tangia sheria hii ipitishwe na nyoyo zetu haikuwahi kuvunjwa hata siku moja na kwa atakayeivunja basi atawajibishwa kwa kufanya kosa la jinai.

Siku hii niliamka nikiwa nimedhamiria kwa makusudi mazima kuivunja sheria hiyo. Nilipanga kumlia bati ( kumnyamazia) Caro kutwa nzima na jinsi atakavyoreact ndivyo atavyofaulu ama kufeli jaribio hilo. Haikuwa jambo la kawaida 

Hata kidogo mimi kutojibu ujumbe mfupi wa Caro lakini siku hiyo si kutojibu ujumbe mfupi tu hata alipopiga sikupokea, Hadi kufikia majira ya saa nne za asubuhi, Caro alishatengeneza missed calls ( simu zisizopokelewa) kumi pia alinitumia meseji nne katika mida tofauti, ya kwanza ilikuwa ni ya good morning na ya 

Pili na ya tatu alikuwa akijaribu kuuliza ni kwanini sipokei simu na ya nne ilikuwa ni ya lawama nayo ilisomeka hivi ' Tom hivi dada yako akikukosea si unamwambia tu anajirekebisha kuliko kumnyamazia kama hivi!!...Tom naomba unisamehe kama nimekukosea ila tafadhali usinifanyie hivi!"

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni