MUUZA CHIPS (105) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 27 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (105)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA MIA NA TANO
ILIPOISHIA...
Lakini nikamwambia kuwa, ukishamtoa, nataka ununue pete kisha akuvishe pete hio na upige picha misha umtumie Mariamu wangu,.. Na hio pesa ya pete nilimtumia mimi pamoja na pesa ya kumpatia mana mi najua rashidi na sarah ni ndugu wawili mtoto wa mama mkubwa kwa mama mdogo hivyo kunichezea action kama hio nilijua wataiweza,….

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Sarah kweli aliniheshimu na kufanya hivyo kwasababu sarah na Mariamu nao ni marafiki sana tena sana.. Hivyo nikajua Mariamu atakapoona hizo picha,.. Kama kweli anampenda chidi basi lazima wagombane na sarah lakini kama hampendi chidi basi lazima angeachana na swala la kuendelea na chidi.. Nakumbuka kesho yake Baada ya Action ya kuvishana pete,.. Mariamu alipokea ujumbe wa meseji za picha ambazo alitumiwa na sarah wakati wa kuvalishana pete na huyu kijana,.. Mariamu wangu alizimia kabisa baada ya kuziona picha zile,.. Ila kwakuwa mimi ndio niliotengeneza ule mchezo sikuzishangaa picha zile mana mimi ndio chanzo cha picha hizo,…. Mpaka hapo nikajua hata mwanangu pia anampenda sana rashidi,.. Kwahio kutoka hapo nikawapa ruksa ya kuwa pamoja na sintowafatilia tena… Ndipo baada ya miezi mitatu nikawaita hawa wawili Rashidi na Mariamu, tena mbele ya baba yake na bibi yake… Tukawapa mipango ya harusi ambayo ndio hii leo tumekuja hap… Sasa ndio nashangaa kuskia Sarah anasema kuwa yeye ni mpenzi wake kabla ya Mariamu, na nakumbuka huyu ni mtoto wa mama mkubwa wake, sasa hebu niambieni kuna ndoa ya ndugu katika dunia hiii… Hebu niambie jamani,.. Au labda kaja kusherehesha kwa aina yake hapa… Na sauti ya kumwambia akanunue pete amvishe chidi ninayo hapa kwenye simu yangu.. Tena ngoja niiweke muisikie"

Wageni kuskia hivyo wakasema kwa sauti kuwa

"maneno yako yametosha kukuamini achana na hio sauti,… Shuka mama watu wafunge ndoa"

Mama Mariamu alifurahi sana na hata Mariamu pia alifurahi kwa hilo,

Sasa kwa Sarah baada ya kuona kabanwa sana na maneno ya mama Mariamu ikabidi ashike maiki au kipaza sauti na kusema kuwa…

"Eheheehehehe,.. Nashukuru sana kwa kuifanya harusi hii ijawe na wasiwasi juu yangu, kifupi ni kwamba hakukuwa na lolote juu yangu na rashidi,.. Bali nilitaka kuwatia watu wasiwasi juu ya ndoa hio.. Nashukuru sana mana nimefanikiwa kuwatia hofu"

Wageni walishangilia na kupiga kelele za furaha kuwa sarah alikuwa na maana hio…

Lakini ghafla sarah kazima maiki yaani kile kipaza sauti kakizima au kakiweka off, kisha akawasogelea mabwana harusi na kuwaambia kuwa

"ama zangu ama zenu.. Tutaonana peponi"

Sarah aliongea hivyo kisha akawasha maiki na kushuka jukwaani, lakini hakuna aliosikia baina ya chidi na Mariamu,.. Wakati huo wageni wanamshangilia sarah kwa jinsi aliwatia hofu watu,.. Laiti wangelijua kuwa tayari watu wameshatishiwa maisha, wasingemshangilia kiasi hicho,… Lakini kiukweli sarah alikuwa ana sumu ya kipekee yaani alikasirika kuliko siku zote na kama sio kule kuirudia maiki na kusema alifanya utani, basi angeaibika kwenye umati wa watu, hivyo kajiondolea aibu afu chuki ipo pale pale… Tena ndio kama wamemchokoza mtoto wa watu, yaani sumu imepanda upyaaaa…

"sasa ndoa ya vijana wetu inakwenda kukamilika,.. Na sina tena maswali juu yenu,.. Na mimi najua mnapendana,.. Tukianza kwa bwana Rashidi Kingazi Omary,.. Chukuwa pete hii na ufuate maneno haya nitakayo kwambia"

SHEKHE__"mimi Rashidi"

RASHIDI__"mimi Rashidi"

SHEKHE__"namvisha pete hii Bi Mariamu kuwa mke wangu"

RASHIDI__"namvisha pete hii Bi Mariamu kuwa mke wangu

SHEKHE__"nitamsikiliza katika maisha yangu yote na sintokuwa kaidi kwake"

RASHIDI__"nitamsikiliza katika maisha yangu yote na sintokuwa kaidi kwake"

SHEKHE__"Eeehh Mungu Ijaalie Ndoa Yetu mimi na mke wangu tuishi kwa amani na upendo katika maisha yetu yote"

RASHIDI__"Eeehh Mungu Ijaalie Ndoa Yetu mimi na mke wangu tuishi kwa amani na upendo katika maisha yetu yote"

"Haya mvalishe pete na uinue mkono wake juu kuuonyesha uma kuwa umeshalitekeleza agizo la Mwenyezi Mungu"

Wageni waliamka kwenye viti na kupiga vigelegele vya furaha

"Turururururururururururururururururururu"

Ilikuwa ni furaha kubwa katika familia hizo……

"tukimalizia kwa Bi Mariamu, chukuwa pete hii na ufuate maneno nitakoyo Kwambia"

Mariamu alichukuwa pete na kuanza kufuata maneno ya shekhe

SHEKHE__"mimi Mariamu"

MARIAMU__"mimi Mariamu"

SHEKHE__"namvisha pete hii bwana Rashidi Kingazi Omary Kuwa mume wangu"

MARIAMU__"namvisha pete hii bwana Rashidi Kingazi Omary Kuwa mume wangu"

SHEKHE__"nitamsikiliza katika maisha yangu yote na sintokuwa kaidi kwake"

MARIAMU__"nitamsikiliza katika maisha yangu yote na sintokuwa kaidi kwake"

SHEKHE__"Eeehh Mungu Ijaalie Ndoa Yetu mimi na mume wangu tuishi kwa amani na upendo katika maisha yetu yote"

MARIAMU__"Eeehh Mungu Ijaalie Ndoa Yetu mimi na mume wangu tuishi kwa amani na upendo katika maisha yetu yote"

"Haya mvalishe pete na uinue mkono wake juu kuuonyesha uma kuwa umeshalitekeleza agizo la Mwenyezi Mungu"

Wageni waliamka kwenye viti na kupiga vigelegele vya furaha

"Turururururururururururururururururururu"

Ilikuwa ni furaha iliopitiza kwa ndoa hio kukamilika….. Lakini watu wakiendelea kufurahi, ghafla mabibi wawili wanakuja, yaani bibi yake rashidi na bibi yake Mariamu,.. Walimuwa wameshika KITAMBAA CHEUPE kilichotapakaa damu, sasa chidi kuangalia akakumbuka kile kitambaa walikilalia asubuhi walipokuwa wanatafuta bikra kama kweli Mariamu alikuwa nayo… Sasa huo ni uthibitisho unaletwa mbele ya waalikwa wote waone kweli mtoto wa kike alikuwa bikra, na mtoto wa kiume ni rijali haswa…

Watu hawaamini kabisa mana ni Amaizing sana yani…. Mama Mariamu alikuwa analia kwa furaha, mana pongezi alizokuwa anapewa ni nzito mno,… Inashangaza sana kwa mschana wa umri huo kuwa na bikra, yaani mama Mariamu alikuwa na furaha mpaka ikageuka kilio,… Bibi wote na wamama zao walikuja kuwakumbatia watoto/wajukuu zao,..

Mama chidi anafurahi mpaka analia kwa kuamini kuwa mtoto wake ni rijali

BAADA YA MASAA KADHAA KUPITA

Ndoa ikiwa imeshakamilika na hata wageni walikuwa na furaha kwa kuja tanga mana kuna wengine hawaijui tanga walikuwa wakiisikia tu, hivyo walianza kutalii (kuzunguka zunguka kuangalia mandhari ya mji huo).. Walipakiwa kwenye gari kisha haooo wanakwenda kutalii talii….

Sasa huku nyumbani kukiwa kuna visherehe sherehe vilivyobakia bakia, chidi akiwa ndani na mama yake na mke wake Bi Mariamu,..

"mama, lakini toka nilipokuja sijamuona mtoto wangu"

Chidi alimuulizia mtoto wake ambaye ni Kingazi na mama yake ni huyu salma..

"na shamra shamra zile usingeweza kumuona, na hata kwenye harusi alikuwepo sema nilikuwa nimempakata… Tena sijui atakuwa kalala"

Aliongea mama yake chidi kisha Mariamu akaongea kuwa,…

"ndio huyo mtoto ulioniambia"

"ndio huyo"

"sasa yupo wapi jamani nina hamu ya kumuona"

Mara mtoto mwenyewe ndio huyo anakuja

"kaleeee ndio kanaanza kutembea"

Mama chidi aliwaonyesha akina chidi

Kingazi alikuwa kavalia suti kali tena wakati huo alikuwa na babu yake mzee kingazi,..

Mariamu alimkimbilia kingazi na kumpakata

"shkamoo baba"

Mariamu alimsalimia mzee kingazi ambaye ni baba yake chidi

"maraha mama poleni sana kwa misukosuko aliowapa mama enu huko mjini"

"Ahsante sana baba"

Basi Mariamu aliondoka na king na kuja nae huku walipo,… Wakati huo salma yeye alikuwa hayupo kaenda kwa mama yake yeye na mume wake mtarajiwa ambae ni Ibrahim, hivyo salma ataolewa ndani ya familia hio hio, lakini na mwanaume mwingine, ila ndoa yao bado haijafika..

"babuu, mi nataka nikaishi na huyu mtoto"

Aliongea Mariamu huku akionekana kumpenda sana yule mtoto,.. Mana king alikuwa ni chata ya chidi sana yaani chidi hua anafyetua machata yake tu,…

"mama unasemaje kuhusu hilo, mana kama vile tunakupokonya mjukuu sasa"

"jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiii…. Sasa jumba lote hili mnazidi kupungua tu, mimi nitaishi na nani, na baba yenu hakaagi hapa mchana hua anakwenda kazini sasa mkimchukuwa na huyo, mimi nitabaki na nani, na tayari nimeshamzoea kelele nyingiiiii mpaka raha nyumba inachangamka.. Haya mkiondoka nae je"

"mama… Wacha tukuondolee tabu"

Aliongea chidi, akachokoza moto

"we mshenzi nini, kwani nilikuambia nimemshindwa… Nipeni mjukuu wangu nendeni katafuteni wenu huyu ni wangu"

Basi ilikuwa ni furaha sana siku hio mana bibi hakutaka mjukuu aende mbali na yeye mana keshamzoea

"chidi mume wangu.. Tumuachie mama tu, ili asiwe mpweke ila nimempenda nikaishi nae mjini"

"sawa wacha tumuachie tu. Ila kata mimi nilipenda kwenda nae lakini kwakuwa hataki, basi tutamtafuta wakwetu"

Aliongea chidi wakiwa wapo chumbani kwao…

Walitoka na kumfuata mama tena

"nini mnataka tena kuniomba mjukuu wangu"

"aahh hapana mama…. Sisi tunataka kukuaga kesho sisi tunataka kuondoka… Ili tuwahi na shughuli zingine"

"sawa kwani si kesho tutaagana"

Basi akina chidi na mkewe waliingia ndani na kucheza ile kiutani utani…

BAADA YA SIKU HIO KUPITA

Na leo ni siku nyingine tena Magari yote yakiwa yanarudi mjini sasa, hata wale aliokuwa wana talii walisharudi na leo ni safari ya kurudi mjini,… Ibrahim aliapa kuja nyumbani kila baada ya miezi mitatu, yaani hatopotea tena kama ilivyokua awali, chidi aliwaachia wazazi wake kibunda cha pesa kama matumizi yao,… Jumba liling'aaaa ghafla likabakwa na watu wachache sana ambao ni familia ya akina chidi… Jumba kubwaaa lakini watu wachache…

BAADA YA WIKI MOJA KUPITA

Akina Mariamu wakiwa nyumbani kwao katika nyumba mpya huku mjini, mana lile geto kwa sasa anaishi Ibrahim na mke wake, mana chidi kamzuia kaka yake asiende Dar es Salaam tena hivyo wataishi wote hapo jijini Arusha,.. Hivyo Ibrahim anaishi kwenye ile selfkontena ya kupangisha aliokuwa anaishi kijana chidi… Na wakina chidi wamezawadiwa nyimba kubwa na mama yake Mariamu, hivyo kwa sasa wapo kwao katika jumba lao,…

"baby.. Kwanini tusitembee tembee huko mitaani"

"aahhhh kama nimechoka choka vile"

"buanaaaaa… Sasa si tuifanye mili ichangamke"

"mmhhhh sawa twende"

"lakini hatutumiii gari"

"haaaaaaa kwa mguuu"

"ndio kwani kuna nini, au utaumwa"

"hhhmm wala… Haya twende ila nakuhofia wewe"

"mimi sina shida wewe"

Basi chidi na mke wake walitoka nje kwenda kutembea tembea mjini, na wakati huo walikuwa wameshikana mikono kama mume na mke, yaani hapo hakuruhusiwi mtu kumtamani mtu mwingine,… Lakini sasa wakiwa mjini kati huko walikutana na sarah,..

"babuu yule sio sarah yule"

"yupo wapi"

"si yule pale anatoka supamaketi"

"Eehh ndio yeye… "

"twende tukamsalimie basi"

"achana nae"

Mariamu alikazania mpaka chidi akakubali kwenda kukutana na sarah

"sarah, we sarah we"

Sarah kugeuka anakutana na chidi uso kwa uso,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni