MUUZA CHIPS (104) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 27 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (104)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA MIA NA NNE
ILIPOISHIA...
Heeeeeeee watu wote walishangaa na kuamka kumwangalia huyo mwenye kipingamizi na ndoa hio, sii mwingine bali alikuwa ni sarah, tena alikuwa kashika mkanda wa video kumaanisha kiwa ana ushahidi wa kuipinga ndoa hio… Mama sarah haamini kitu anachofanya mtoto wake, mama miriam hata yeye haamini macho yake..

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"mama sarah?? mwanao anafanya nini sasa"

"mwache afanye anachotaka, kwani hata yeye ni mpenzi wake"

Mama sarah nae kamgeuka mama miriam, sasa Sarah na mama yake wamekuwa kitu kimoja…

Mama Mariamu haamini macho yake kuwa leo rafiki yake kipenzi kamgeuka na kuwa upande wa mtoto wake,… Na yule mwenye kipingamizi juu ya ndoa hio haruhusiwi kuzuiwa, kwani anatakiwa atoe pingamizi lake,.

Mariamu alipoinua macho yake haamini kwa kumuona sarah ndio mwenye kipingamizi na ndoa yake,..

Sarah alifika jukwaani na kushika maiki au kipaza sauti,…

"kwa jina naitwa Sarafina John… Ni mschana pekee katika familia yetu,.. Nina huzuni kubwa sana juu ya ndoa hii, kwasababu mwanaume anaekwenda kufunga ndoa ni mchumba wangu mimi na sio miriam au Mariamu kama alivyo silimishwa"

Aliongea sarah tena kwa kujiamini sana,…

"aahhh tafadhali sana dada yetu,.. Tunaomba utujuze ni kwanini una kipingamizi juu ya ndoa hiii"

Yaani mtu mwenye kipingamizi hua ana haki ya kuzungumza kile anachohisi kuzungumza,.. Yaani ndoa haitaki bughudha hata kidogo inatakiwa ifungwe mbele ya haki zote mana hata mwenyezi Mungu anaisimamia vilivyo, na hata malaika wapo karibu na ndoa hio kuwa kama mashahidi,…

"Mariamu ni rafiki yangu toka utotoni, lakini tumekuja kugombana kwasababu ya huyu huyu mwanaume"

Waalikwa wote wanashangaaa..

"haaaaaaaa jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiii dada wa watu kumbe ni mume wake"

Ni maneno ya waalikwa au wageni waliokuja hapo..

"Enheee endelea"

Wakati huo mama mariamu katulia kimyaa anasikiliza tu mana ni sheria kuongea kwa sarah hivyo haruhusiwi kuvamiwa na mtu yeyote yule…

"nina ushahidi wote wa video siku wakati tinavishana pete ya uchumba na huyu mwanaume"

Watu wanashika midomo kwa mshangao, yaani hawaamini macho yao… Mama mariamu alikuwa akipigiwa simu na kila anaemjua hapo na kuulizwa kuliko swala kama hilo….

"Enhee dada endelea"

Shekhe alimuamuru Sarah aendelee na maongezi yake yenye pointi kwa kila mgeni aliopo hapo…

"ushahidi wa CD hii hapa ninayo.. Lakini kwakuwa hapa karibu hakuna TV,.. Bado nina ushahidi wa sauti ya video hio,.. Naweza kuiweka hapa tusikie wote"

Chidi wakati huo aliingiza hofu juu ya swala hilo japo aliambiwa kuwa sarah alitumwa kufanya vile,.. Lakini mariamu bado alikuwa analia muda mrefu tu,… Chidi hakuelewa kwanini mariamu analia

Lakini kumbe chidi mkononi mwake kashika kirimoti kidogo tu,.. Alikibonyeza kile kirimoti walitokea wanaume wanne waliovalia suti nyeusi na miwani nyeusi,.. Wakati huo sarah alikuwa anaitafuta ile sauti ya ushahidi katika simu yake.. Hivyo nia ya chidi kubonyeza hio ripoti ni ili swala hilo la kuweka sauti mbele ya watu wote hawa lisikamilike,… Na hao watu ndio wale walipakia katika gari aliokuwa anaendesha Ibrahim wakiwa safarini kuja hapo.. Kuna watu wanne walipakiwa na Ibrahim kumbe chidi ishu kama hii aliijua tu na ndio maana akaandaa watu kama hao.. Lakini sasa wale watu walipotaka kumshika sarah ili wamtoe pale jukwaani,.. Iliskika sauti ya mtu mmoja ikisema

"Noooo, Muacheni Huyo mschana"

Watu walishangaa kuskia sauti hio, na hakuwa mwingine, bali alikuwa ni mama mariamu ndio kusema hivyo, huku akipanda jukwaani na kushika maiki au kipaza sauti…

"nashukuru sana wageni waalikwa kwa kufika katika hafla hii… Nashukuru sana,.. Na nitakayosema hapa ni ukweli mtupu, mbele ya Biblia na kitabu cha Kiislamu naongea ukweli"

Sasa hapo kila mtu akawa na amani kati ya chidi na mariamu….

"Enhh mama… Kwanini umekuja hapa kuna neno inalotaka kuongea??"

"ndio.. Nataka nifanye haki itendeke sitaki waje wagombane hapo baadae, wacha nichukue maamuzi magumu juu ya hili"

Mama mariamu aliongea hivyo huku akiseti maiki vizuri ili itoe sauti nzuuiuri sana

"Enheee toa neno mama mzaa chema"

Aliongea Shekhe anaefungisha ndoa, huku kila mgeni aliokuja kwa ajili ya mama mariamu kashika kichwa.. Hata mama sarah haamini kama mama mariamu kaenda kuvunja ukimya… Na wakati huo sarah yupo karibu na wale jamaa wanne, wanasubiri ruksa tu, wamtoe Sarah hapo jukwaani….

"mimi ni mtu mzima… Mimi ni mama wa huyu mtoto hapa mbele yenu,.. Mimi ndio mama mariamu,.. Anachokisema huyu binti sio uongo,.. Ni ukweli tena ukweli usiojificha"

Watu walishika kichwa na kuziba midomo yao, mana ni jambo la kushangaza… Sasa huku mariamu kaanza kulegea na kutaka kudondoka baada ya mama yake kusema ukweli.. Chidi kuona mariamu anataka kuzimia, akamzuia kimya kimya na hakuna mtu aliojua, mana mariamu kamuegemea chidi lakini keshazimia tayari, wakati mama mariamu anaongea kila kitu na kuiharibu ndoa ya mtoto wake.. Sijui mama mariamu kapewa nini kwa muda mfupi tu…

"sarah huyu ni sawa na mtoto wangu, hivyo sipendi kuongea uongo juu yake.. Anachokisema kuwa kavishwa pete ya uchumba na huyu kijana, sio uongo, ni kweli rashidi alimvisha pete huyu mschana……

Mama Mariamu alikuwa mkweli juu ya familia yake yaani hakutaka kuongopa hata neno moja,.. Mariamu wakati huo kamuegemea rashidi, na alikuwa kazimi kutokana na kauli ya mama yake iliodhibitishwa kuwa ni kweli chidi na sarah walifunga ndoa.. Chidi alimwita jamaa mmoja kati ya wale wanne,..

"nipatie maji baridi"

Aliongea chidi lakini ni kwa sauti ya chini mno, mana hapo walipo wapo jukwaani hivyo hata zile Action za kuambizana zinaenda kwa usiri sana, hawa jamaa ni maprofessional mpaka raha, kwani kila anachoagiziwa anacho papo hapo hivyo sio mpaka aondoke, japo maji hayo yapo kwenye kijichupa kidogo, na maji hayo ni spesho kwa ajili ya kuwaamshia watu waliozimia, mana hicho kijichupa kina sehemu ya kubonyeza na maji yanatoka kwa spidi kali, afu yabaridiiiiii…. Chidi alifanya hivyo kwa mariam ili amsikilize mama yake vizuri,..

Dakika mbili baadaye mariam alionekana kufumbua macho baada ya maji yale kumwagiwa usoni,..

Wakati huo mama yake ndio anaendelea kumwaga maneno makali juu ya mtoto wake…

"sarah huyu ni sawa na mtoto wangu, hivyo sipendi kuongea uongo juu yake.. Anachokisema kuwa kavishwa pete ya uchumba na huyu kijana, sio uongo, ni kweli rashidi alimvisha pete huyu mschana, Lakini pete hio mimi ndio nilioinunua kwa pesa yangu"

Watu wakazidi kushangaa kwanini mama mariamu kanunua pete ili kumuozesha sarah na sii mariamu,

"najua mtajiuliza sana kwanini nimenunua pete hio na kumpatia sarah,… Mimi ni mwanamke mjasiriamali, mfanyabiashara na kila kitu, na Namshukuru Mungu kwa kile alichonipa ili niweze kuihudumia familia yangu.. Nakumbuka walipokuwa wanaanza uhusiano hawa watu wawili, rashidi na mariamu, sikuwa na imani kama kweli walikuwa wakipendana, wazo langu nilijua tu huyu kijana atakuwa kampenda mwanangu kutokana na mali zao lakini huenda hampendi katika moyo, mwisho mtoto wangu akaanza kuteseka… Nilianza vituko vingi sana ndani ya mahusiano yao, lakini hawakujua nia yangu… Maana yangu ni kujua kuwa huyu kijana anampenda kweli mwanangu au anatania,.. Ilifikia mwanangu mpaka anatoroka nyumbani na kwenda kwa huyu kijana, na alikaa huko siku nne chumba kimoja, namshukuru sana huyu kijana mana kawa mvumilivu kwa mtoto wangu"

Watu sasa wakawa wamekaa mkao wa stori mana stori ilikuwa tamu na hawaijui, sasa wageni wakajikuta sasa wanamsikiliza mtu mzima na maneno yake, na sasa hata nyuso za wageni zilionekana kutulia…

"mtoto wangu alipotoroka nyumbani, sio kuwa nilikuwa sijui kama yupo kwa chidi, ila nilikuwa nataka kujua atarudi lini na je akirudi atakuwa kashindwa kuishi nae ndani ya hizo siku, na ndio maana nikawaacha siku nne nzima waishi ili wajuane tabia zao,.. Lakini nikashangaa siku zinazidi kwenda, mtoto hatokei,.. Nakumbuka kijana huyu ni mfanyakazi wangu katika hoteli yangu na mtu aliomleta alikuwa ni mama yake na huyu sarah, na mama yake sarah akasema kuwa huyu ni mtoto wa dada yangu, yaani huyu rashidi, nami kwakuwa nilimuamini basi nilikubali kumpa kazi huyu kijana na ndio wakaanza uhusiano na mtoto wangu….. Sasa wakati nawaza mtoto wangu harudi nyumbani basi huenda kafurahiwa na huyu kijana, hivyo nikampigia simu huyu mama sarah mana yeye ndio anaemjua mana si mtoto wa dada yake???.. Mama sarah aliweza kunipa ramani ya sehemu anayoishi huyu kijana,.. Lakini sikutaka kubabaisha namba ya nyumba na kuwasumbua askari,.. Hivyo nikawaamuru askari wale wamkamate kijana huyo hapo hapo kazini kwangu kisha tukaenda nae mpaka nyumbani kwake… Namshukuru mungu kwa kuwa nilimkuta mtoto wangu tena akiwa na afya nzuri sana hivyo sikuchukia kwa lile… Na hapo bado uchunguzi wangu wa kuwachunguza kama wanapendana kweli au wanapendana kwa pesa.. Kijana huyu nilimsweka ndani siku hio, na Mariamu nae nilimfungia chumbani kwake ili wasionane tena, lakini hapo ilikuwa ni uchunguzi bado… Nia ya kumfungia Mariamu ni ili asipate nafasi ya kwenda hata kumuona, ili rashidi atakapotoka lumande akasirike kwanini Mariamu hakwenda kumuona, na kama asipokasirika basi ningelijua kuwa hakuwa akimpenda mtoto wangu bali alikuwa akimpendea pesa, lakini rashidi alimpenda sana mtoto wangu kwani siku anatoka lumande alimjia juu sana Mariamu wangu mpaka nikaogopa na siku ile nilikuwa nawaona ila wao hawakuniona,.. Rashidi alifikia hatua mpaka anamtupia Mariamu kadi ya benki mana walipeana mpaka kadi za benki lakini siku hio chidi aliirudisha kuashiria kukasirika sana, na kingine kilichomkasirisha ni kitendo cha mdogo wake kuishi na sarah wakati yeye yupo, hapo ndipo nilijua wanapendana kweli"

Story ilikuwa tamu mapaka watu wanapiga mamofi, kuashiria kumbe wawili hawa walipitia misukosuko ya aina yake,.. Na wakati huo sarah katulia tu na hakuwa na la kusema na hakuruhusiwa kusema

"Lakini pia, sikutaka kumpima mwanaume tu peke yake,.. Mana nimeshajua kuwa chidi anampenda sana Mariamu,.. Sasa je na Mariamu anampenda Chidi kwa dhati??? Hapa sasa nampima mwanangu Mariamu kama kweli anampenda huyu mtoto wa kiume….

Akili nilioitumia ni hivi, Huyu huyu Sarah ndio niliomtuma akamtoe Rashidi kule lumande, yaani kule polisi,.. Lakini nikamwambia kuwa, ukishamtoa, nataka ununue pete kisha akuvishe pete hio na upige picha misha umtumie Mariamu wangu,.. Na hio pesa ya pete nilimtumia mimi pamoja na pesa ya kumpatia mana mi najua rashidi na sarah ni ndugu wawili mtoto wa mama mkubwa kwa mama mdogo hivyo kunichezea action kama hio nilijua wataiweza,….

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni