MUUZA CHIPS (83) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 19 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (83)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA THEMANINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Simu ilikata, lakini chidi haamini maneno ya Sabra…

"ana maana gani huyu mtu"

Aliongea chidi huku akitaka kupiga simu lakini roho haitaki…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"we mama, nipe dakika tano narudi sasa hivi"

Aliongea chidi na kuyafuata maneno ya sabra..

"chidi jamani, unaniacha kisa nimekataa ulichokitaka kwangu"

"ebu tuyaache ayo"

"chidi jamani, basi nimekubali njoo basi"

Eeehhh chidi kuskia mama sarah kakubali kurukwa ukuta, mana anampenda sana chidi na hatamani kumpoteza… Chidi alishaanza kuondoka lakini kuskia kakubaliwa tu, alijikuta anasita kutoka, mana anaitamani sana hio sehemu….

Chidi alirudi mpaka kitandani na kuanza kumshika shika mama sarah, wakati huo mama sarah tayari keshakubali na tena kakaa mkao ule ule unaorakiwa, mana kakubali kwa hali yake, na chidi alivyo mwehu wala hakutaka kumkopesha,…

Lakini kadri anavyozidi kumshika shika mama sarah, akili yake haikuwa sawa, yaani alikuwa anawaza maneno ya sabra kuwa akamchukue mdogo wake kule alipokuwa,….

Chidi hakuwa mjinga kiasi hicho

"kama ni huyu mwanamke yupo, nitamshuhulikia nikirudi"

Chidi alijisemea kimoyo moyo kisha akamuacha mama sarah bila hata kumgusa kitu,..

"we chidi una nini lakini"

"narudi muda sio mrefu"

"lakini mbona sikuelewi"

"narudi, tena nipe gari yako mara moja niwahi"

Chidi aliomba gari kwa mama sarah na kuondoka kwenda kule kwa akina sabra,..

Tukija huku kwa akina miriam tunamuona miriam anatoka na kupanda gari yake,… Alikuwa akimfuata sarah kule hotelini kwao, mana alimpigia simu ili aje lakini sarah alisema mama yake hayupo

Hivyo miriam akachukuwa jukumu la kumfuata sarah kule hotelini kwao…

Robo saa mbele miriam alishafika kwa akina sarah

"heeeee Miri umemuacha nani huko hotelini kwenu"

Aliuliza sarah baada ya kumuona miriam kafika hotelini kwao, mana kwa sasa hoteli ilishanunuliwa na akina sarah, hivyo sio ya akina miriam tena

"mama yupo na nimemuaga"

"Enhee sema shost, uliniambia kuna kitu unataka kusema"

"ndio shost,… Mama si alinifuma naongea na omary,.. Mwenzangu ila safari ya kwenda Uingereza imeanza tena"

"heeeeeeeeee mama yako nae, sasa anataka upate mwanaume wa aina gani, au anataka mzungu"

"mi ata sijui, yaani natamani hata kujiua sarah"

"apana miri, huko mbali sasa unapofika, usiseme hivyo"

"sasa nifanyeje sarah,.. Mana nikiumwa tena ataona ni kamchezo kangu"

"mmmhhh kiukweli leo sina hata cha kukushauri miri wangu"

Miri alikuwa anatamani kulia bila kujua atafanya nini mana anampenda sana omary wake,.. Na hatamani kumuacha

"Sarah, mi nachukuwa uamuzi mgumu, liwalo na liwe, ila naomba uniseidie kitu sarah please"

"kitu gani tena miri"

Walichokiongea walituficha mana waliongea kwa siri sana lakini tutajua huko mbele,..

Baada ya kufanya maongezi yao miriam aliondoka kurudi hotelini kwao… Alipofika tu alikutana na mama yake

"haya, umeshajiandaa… Mana kama ni tiketi nimeshakata mchana hivyo keaho nakutakia safari njema"

Miriam hakuwa na la kusema lakini moyoni mwake kuna jambo kalipanga baina yake na sarah, sasa sijui itakuwaje

Sasa tukija huku kwa chidi, akiwa ndani ya nyumba ya shemeji yake anamtafuta halima ambaye ni mdogo wake,.. Lakini hakumuona nyumba nzima,.. Aliingia mpaka chumbani kwa shemeji yake ambaye ni jasmini,

Aliangalia lakini hakumuona, sasa ile anaondoka, alishangaa kuona masanamu yakiwa ndani ya kabati la vioo, afu masanamu yenyewe, yameashiria alama za kishetani mambo ya freemason,.. Chidi aliduaa na kushindwa kuelewa, lakini mara simu yake inaingia sms, kucheki alikuwa ni sabra

"we chidi, sisi tupo karibu sa kama upo ndani toka haraka, mana dada kabadirika sana yaani sio yule unaemjua"

Chidi alipomaliza kusoma sms hio alitoka lakini hajamuona halima, alipofika kwa mlinzi akamuuliza

"oya eti kale katoto kametoka nje"

Chidi alimuuliza mlinzi wa geti hilo

"ndio ameenda twisheni"

"unapajua hapo twisheni"

"hapana sipajui"

Chidi alikasirika sana,.. Lakini hakutaka kupoteza muda alitoa gari mpaka nje ya nyumba na kuondoka mbali kidogo kule alipoelekezwa na mlinzi kuwa ni njia hio ndio ya kuendea tuisheni lakini hapajui twisheni penyewe..

Haikupita hata dakika tano jasmini na mdogo wake sabra ndio wanaingi, yaani angechelewa tu kidogo angelikutwa,… Lakini jasmini aliona kuna tairi za gari jingine…

"we kapwiku, ni gari gani imeingia huku"

Aliuliza jasmini

"ni yule kijana mdogo wake boss"

Mlinzi alijibu kuwa ni yule kijana mdogo wake boss,.. Jasmini alijua tu atakuwa ni chidi… Hakutaka kuuliza tena lakini moyoni mwake alikuwa akijiuliza kuwa

"huyu chidi kafata nini huku"

Alijiuliza mwenyewe kimoyomoyo huku akiingiza gari lake kwenye paking,… Lakini kabra hajaliweka sawa aliina ngoja aulize tena

"we kapwiku… Huyo kijana alifuata nini"

"alikuwa anamuuliza mtoto boss"

"mtoto gani"

"yule mschana"

Jasmini kuskia ni yule mschana aliwasha gari haraka ili awahi kumchukuwa halima mana yeye ndio anajua hio twisheni ilipo, ila wakati huo chidi kapaki pembeni kama atamuona mdogo wake, lakini huku kwa jasmini nae anakuja kuelekea twisheni,.. Mana keshajua kuwa chidi anataka kumchukuwa mdogo wake, hivyo amuawahi kabla hajakutana nae..

Sasa na wakati huo twisheni ndio wanatoka, sasa chidi akawa katulia tu hapo barabarani ili kuona kama atapiata hapa, lakini mara akaona katoto kamoja kamebeba daftari…

"mtotooo ujambo"

"sijambo shkamoo"

"marahabaaa… Unatoka wapi"

"natoka twisheni"

"twisheni yenu ipo wapi"

"pale mbele, unaingi hivi afu utaona kibao cha twisheni yetu"

Chidi kuambiwa hivyo aliondoa gari fasta bila kuchelewa, lakini kwa ile spidi anayokuja nayo jasmini sijui kama chidi atawahi,.. Mana mpaka aangaze macho afuate kibao mpaka lini,..

Sasa kama bahati tu, Halima katokea barabarani,

"dadaaa we dadaa"

Chidi alimuita mdogo wake kwa heshima

"abeee kaka"

"njoo haraka,… Ingia kwenye gari"

Alimfungulia mlango kisha akaingia… Yaani ile anaingia tu na jasmini ndio anafika hapo na kushuka kwa haraka kuelekea huko ndani ili akamchukue, lakini halima alishaingia kwenye gari saa mingi sana, na kwakuwa jasmini hajui gari ilioingia kule kwake, alishindwa kujua kama ndio gari hii alioipita hapa,… Chidi hakuchelewa, aliondoa gari ili kurudi nyumbani,…

Sasa jasmini kutoka alishangaa kuona gari alioipita hapa sasa hivi tu haipo,.. Ndio akajua basi keshachukuliwa… Lakini akilini mwake alikuwa akijiuliza, hii taarifa kapewa na nani.. Mana alikuwa hajui,..

Sasa chidi akiwa njiani mara simu iliita, kucheki alikuwa ni miriam.

"haloo boss"

"acha zako chidi, boss niwe mie"

"ok sema"

"naomba unipitie hapa mnarani"

"kuna nini"

"we njoo tu utajua baadae"

Simu ilikata lakini chidi hakuelewa kwanini aliambiwa ampitie hapo mnarani,

Sasa huku hotelini kwa akina miriam, mama alikuwa akimtafuta miriam ampe tiketi yake akae nayo hamuoni, lakini gari ya miriam ilikuwepo maeneo ya paking hivyo ilionyesha kuwa miriam yupo na hakwenda mbali,…

Chidi alifika mnarani na kumkuta kaketi chini ya mti, yaani alivyokaa utafikiri sio matajiri yaani alikuwa tofauti sana…

Miriam aliingia ndani ya gari lakini hio gari alioingia anaijua mwanzo mwisho..

"omary, hii gari umeipata wapi"

"ni ya mama mmoja hivi"

"mama sarah si ndio eee"

Sasa chidi yeye hajui kama anaitwa mama sarah, hivyo alikataa

"hapana anaitwa grace"

"sa ndio mama sarah huyo"

Sasa chidi kuona mbona kama kinasanuka kitu ikabidi akubali huku akisema

"ni yule mama alienileta kule hotelini kwenu"

"ndio huyo huyo, ana mtoto anaitwa sarah"

"ok sasa wewe vipi… Unaenda wapi"

"kwako"

Chidi alitoa macho kuskia miriam anakwenda kwake

"mamuu, unakwenda kwangu kufanya nini"

"ina maana ni vibaya kuja kwako"

"aaahhh mamuuu"

"nini babuu we twende… Afu huyu ni mtoto wako nini"

Aliuliza miriam huku akimuangalia kwa umakini ili kumfananisha na chidi na ni kweli walikuwa wanafanana kwa mbalii sema halima alikuwa ana uweusi kidogo na chidi yeye ni maji ya kunde yaliong'aaa,

"hapana ni mdogo wangu"

"muongooo"

"kweli"

"waooooo basi ni kawifi kangu… Njoo mwaya wifi yangu"

Miriam alimchukuwa halima na kumpakata,.. Halima alikuwa na umri wa miaka kama saba au nane, ni mkubwa kidogo alikuwa ana kaumbo kazuri hivyo kila mwanamke anaemuona basi anampenda tu,..

"mamuu mi sijakuelewa unajua"

"chidiiiii, mi nataka leo nikalale kwako"

"mi nadhani unataka kuniletea kesi mamuu"

"nimeaga nimesafiri hivyo nitakuwa kwako kama siku mbili hivi"

"mamuuuuuuu… Siku mbili?… Hapana aisee utaniletea shida… Sasa huko uliposema umesafiri wakiulizwa afu wakisema haupo"

"usijali"

"mamuuuu"

"please baby… Naomba uniamini"

Chidi alichoka hata kuongea hivyo aliwasha gari na kuelekea nyumbani kwa chidi mahari alipopangisha kijana huyo,..

Lakini chidi roho inamdunda kwasababu mama sarah yupo kule, afu mbaya zaidi alimuacha yupo uchi, afu ana miriam je itakuwaje, yaani ni bonge la msala,..

Chidi alimtumia mama sarah sms kuwa

"mamy vaa nguo zako nakuja na mdogo wangu"

"ujinga gani huo chidi jamani, mbona unanikata mudi"

"kweli kuna shida imetokea hivyo nakuomba mamy"

Chidi aliweka simu pembeni wakati huo miriam na halima walikuwa wanacheka mno, yaani miriam tayari keshazoeana na halima ndani ya dakika chache tu..

Punde sii punde gari inaingia nyumbani kwa chidi,.. Miriam anashuka kwenye gari huku akiwa kampakata halima,..

Na chidi nae kashuka na kuzima gari

Lakini miriam alishtuka kwa kuona viatu vya kike, tena haviukuwa vya kitoto,… Unajua miriam yeye anajua chidi kaachiwa gari na mama sarah lakini hajui kama mama sarah yupo ndani,.. Yaani anajua kaachiwa tu gari,..

"omary.. We omary"

"nini tena si uingie"

"hebu njoo babuu"

"nini…"

Chidi alitoka nje tena mana alikuwa keshaingia

"hivi viatu ni vya nani"

Sasa mama sarah nae kasikia sauti ya kischana schana, ikamshawishi atoke ili amuangalie huyo mschana anaeongea na chidi, mana chidi alimtumia mama sms na kumwambia kuwa anakuja na mdogo wake,.. Sasa mdogo gani mkubwa hivyo, sasa mama sarah ile anapanua pazia aone huyo mdogo wake chidi,..

Alishangaa kumuona ni mtoto wa rafiki yake, tena anaheshimiana nae kupita maelezo,.. Sasa miriam nae kupiga jicho kamuona mama sarah,… Na alikuwa hajui kama atakuwepo huku ndani japo kajua kuwa gari ni yake, lakini hajui kama atamkuta humu ndani..

"we miriam umekuja kufanya nini huku"

Aliuliza mama sarah huku akitoka nje ili aulize vizuri… Wakati huo miriam kimyaa

"si nakuuliza we mtoto, umefuata nini huku"

Mama sarah alikuwa anachimba mkwara lakini hata yeye alikuwa anaona aibu kukutwa ndani tena peke yake kwenye chumba cha kijana ambae hajaoa..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni