MUUZA CHIPS (91) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 23 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (91)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA TISINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
"sikilizeni, huyo msichana wangu hayupo mbali, na wanaonekana wanapenda mno, hivyo kama kuna mmoja wetu anaweza kutoa mateso kwa huyo kijana, atoe na miriam atatoka huko alipo"

Mama alitoa wazo moja zuri sana ambalo hata maafabde hao hawakuliwaza.. Chidi alishushwa juu ya gari na kisha akaanza kubanwa katika mbavu, maumivu aliokuwa akiyapata huku akiulizwa na afande kuwa

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"sema mtoto wa boss yupo wapi"

Sasa chidi kuina kuwa wao wametafuta mpaka basi na hawajampata, akaona wacha aendelee kukaa kimya japo alikuwa akiumia sana…

"Aaaaaaaaaaiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii"

Hizo ni kelele za kijana chidi zikiashiria kuumia sana kwa kutokusema ukweli…

Sasa huku ndani, kumbe pale alipokaa halima na kuonekana kama kiti kizuri kumbe ndio miriam alijiweka pale kama kiti fulani hivi afu akajifunika na kanga… Yaani kwa jinsi alivyokaa ni ngumu kujua kama huyo ni mtu, lazima ujue ni kiti, tena kwa juu kuna mtu kakaa, basi ni dhahiri kuwa huezi jua kama kuna mtu,.. Miriam kuskia sauti ya chidi aliamka pale alipokuwa kakaa na kutoka nje,.. Miriam alihisi anaumia yeye kwa jinsi anavyompenda kijana huyo,.. Lakini sasa ile anatoa tu mguu kuna sauti iliskika kwa nyuma

"basi mwacheni huyo kijana, kwani hamumuoni miriam huyo hapo keshakuja"

Iliskika sauti ya kike iliowafanya watu wote wageuke na kumwangalia huyo aliosema chidi aachwe, Lakini sauti hio haikuwa ya miriam wala mama yake,

Alikuwa ni mama sarah ndio alioongea kauli hio ya kuachwa kwa chidi,..

"mwache mpenzi wangu,.. Muachieeeeee"

Miriam alianza kugombana na maafande wakati wakiwa wamemshika vibaya.. Mama miriam kumwona mwanae alimfuata na kumnasa kibao kimoja saaafi kabisa, kisha akamsukumia ndani ya gari na milango ya gari ikafungwa…

"huyo kijana mpelekeni ndani akashike adabu"

Aliongea mama miriam huku akiingia kwenye gari yake aina ya vogue.. Na miriam alikuwa ndani ya hio gari ya mama yake akiwa anatafuta mahari pakutokea ili aweze kumseidia mpenzi wake…

Lakini milango yote ilikuwa imelokiwa vizuri,… Mama sarah baada ya kuona mama Miriam kaondoka, Aliwataka wale maafande wasije wakamtesa kijana huyo mpaka mama Miriam atakapo lizika kwa kutoa adhabu kwa kijana huyo.. Basi mama miriam alitoa fungu la kutosha kwa askari hao ili chidi asije kupitia matese akiwa yupo sero.. Unajua mama sarah anaheshimiana sana na mama miriam hivyo kwa wakati huo hawezi kumseidia chidi awepo uraiani kwasababu ataonekana yeye ndio chanzo cha miriam kutoroka, hivyo ikabidi atulie tu,… Mama sarah kaondoka zake na zile difenda nazo zinaondoka, ila sasa wakati wameshafika mbali chidi ndio anakumbuka kuwa kule ndani kuna mdogo wake, na mdogo wake huyo bado hajajua hata kujipikia mwenyewe,…

"afande naombeni dakika mbeli tu nirudi nyumbani"

"wewe, usitufanye tukiuke sheria ya yule mama kuwa tusikutese, we tulia hivyo hivyo"

Chidi alitulia tu lakini alikuwa akilia sana juu ya mdogo wake halima..

Na wakati huo huku nyumbani halima alikuwa akilia maana action zote kaziona, kamuona wifi yake akiingizwa katika gari tena kwa lazima, alimwona kaka yake akiteseka kwa kuminywa mbavuni, hivyo kwa sasa kabaki hana mtu wala hajui atakula nini na wakati huo njaa inamuuma sana, na pia walikuwa wakipiga chakula cha mchana yeye na wifi yake…

Sasa huku kwa akina miriam,.. Miriam alifungiwa chumbani kwake huko tena mama yake akafunga na ufunguo kabisaa,… Lakini miriam pia alikuwa analia kwa kumuacha halima peke yake kule ndani,.. Miriam bila kuchelewa aliiwasha simu yake, maana aliizima siku zote hizo alipokuwa anaishi kwa chidi,.. Namba ya kwanza kuitafuta ilikuwa ni ya sarah,… Alimpigia sarah

Lakini wakati huo huku kwa chidi nae ndio alikuwa anatupiwa sero,.. Lakini utamu wa sero ya chidi aliwekwa kwenye sero ya peke yake na yote hio ni kwamba polisi walihongwa pesa na pia waliahidiwa kuwa mama sarah atakuja kumwona kila mara, hivyo kutokana na pesa kuwepo chidi alitenganishwa na mahabusu wengine walipo eneo hilo,.. Mahabusu wengine walikuwa wakiulizana kuwa huenda chidi ni mtoto wa kiongozi fulani au kidogo fulani nchini, mana katenganishwa na wao….

Tukija huku Dar es Salaam katika hospitali kuu jijini hapo, Ibrahim alionekana kupata nafuu, kwani hata kula alikuwa anakula vizuri,… Ni siku tatu toka aende Dar es Salaam, na hali yake ilionekana kurejea, saidi akiwa ndio muuguzi wake, tena alikuwa yupo karibu mno,… Sasa hata kuingea alikuwa anaweza kuongea kabisa,…

Sasa turudi jijini arusha, Sarah akiwa anaiona simu ya rafiki yake miriam ikimpigia, alishtuka sana mana miriam alipoondika alimwambia nitazima simu yangu kwa muda usiojulikana,… Sarah aliipokea simu hio

"haloo miri… "

"Eeeee Sarah mambo best yangu"

"safi tu miri upo wapi"

"nipo nyumbani sarah nimefungiwa yaani hata kutoka sijui nitatokaje"

"heeeeee mama yako kajua ulipo"

"ndio ila mama yako ndio kamuinyesha mama yangu kule nilipo"

"Ati nini…. Kwani Huyo mama yangu anajuana vipi na mpenzi wako"

Sarah alishangaa sana kwa kusikia kuwa mama yake anajuana na mpenzi wa miriam

"mi sijui.. Ila kuna kitu naomba uniseidie"

"kitu gani tena…"

"mpenzi wangu ana mdogo wake wa kike… Sasa tumemuacha kule nyumbani kwake na hana mtu wa kuwa nae"

Aliingea Miriam huku akilia kwa uchungu mzito..

"kwani huyo mpenzi wako yupo wapi"

Aliuliza sara huku akisubiri jibu kwa hamu..

"kapelekwa jela"

Aliongea Miriam bila kumficha rafiki yake kipenzi..

"Mungu wangu jamani miriii, pole shost yangu.. Ila ndio hivyo vumilia tu"

"Sarah… Naomba please ukamchukue wifi yangu, ni mdogo hajui hata kupika please nakuomba Sarah wangu"

Sarah machozi yalishaanza kumtoka mana ilikuwa ni action ya aina yake juu ya swala hilo,..

"sawa, nitakwenda… Nipe namba ya nyumba nikamchukuwe"

Hapo sasa ndipo pabaya kabisaaa, mana Sarah anapajua nyumbani kwa chidi, maana alishakwenda mara kadhaa tena alishawahi kulala huko huko usiku mzima, hivyo namba ya nyumba sarah anaijua ila kwakuwa wote hawajuani, mi sijui nini kinatokea…

"Ni kule sakina, mtaa unaitwa mtaa wa sita alafu nyumba namba 42.. Chumba chake niiiii… Aaahhhh namba ya chumba niiiii,… Aaaahhh kama imenitoka kidogo"

Miriam alisahau namba ya chumba lakini sasa sarah yeye kwa jinsi mwanzo alivyotaja sarah alijua inaelekea kwa mpenzi wake… Sarah akaitaja namba ya chumba hicho makusudi ili ajue kama ni chumba hicho, mana namba ya nyumba ndio hio hio aliopo chidi lakini sasa namba ya chumba ndio noma…

"miriam taja namba basi niende"

"nimeisahau ila naikumbuka kwa mbali"

"ok… Ni chumba namba 14 au"

Sarah alitaja namba ya chumba hicho, lakini huku miriam alishaanza kukunja sura ghafla baada ya kusikia sarah kajuaje namba ya chumba cha mpenzi wake.. Miriam alimwita best yake… Kwa hasira ya chini

"Sarah????"

"Nini"

"Hicho chumba umekijuaje wewe"

Kila mmoja alikuwa na wivu juu ya mpenzi wake, hivyo kila akisikia ujirani mwingi baina ya mpenzi wake na mtu fulani hua hasira zinajaa kichwani mwake, kama miriam kuskia tu sarah kakijua chumba cha chidi basi hasira tayari zimeshapanda, tena wakileta utani huenda wakauvunja hata urafiki mana kila mmoja wao anampenda chidi, yaani kila mtu yupo tayari kufa kwa ajili ya kijana chidi, ila sasa chidi ndio kwanza juzi ndio anajua kuwa sarah na miriam ni marafiki wakubwa sana, hivyo hata yeye kichwa kinamuuma kwa siku ambayo ndio wanajuana, itakuwaje?…

Maongezi ya miriam kumwomba sarah aende nyumbani kwa chidi kumchukuwa halima, yalianza vizuri lakini ghafla yalibadirika na kuwa kama ilivyo..

"ok… Ni chumba namba 14 au"

Sarah alitaja namba ya chumba hicho, lakini huku miriam alishaanza kukunja sura ghafla baada ya kusikia sarah kajuaje namba ya chumba cha mpenzi wake.. Miriam alimwita best yake… Kwa hasira ya chini

"Sarah????"

"Nini"

"Hicho chumba umekijuaje wewe"

Aliuliza miriam huku akiwa makini kuskia sarah atasemaje kuhusu chumba hicho

"lakini miri, we utakuwa umekosea namba ya nyumba anayoishi huyo mpenzi wako.. Mana hata mimi mimi mpenzi wangu anaishi nyumba namba 42 chumba namba 14, sasa huenda mpenzi wako na wangu vyumba vyao vinafanana namba, lakini kwa namba za nyumba labda umekosea miri"

"aahhhhh lakini kwa namba ya nyumba naikumbuka ni hio ila sina uhakika sana, ila namba ni hizo hizo"

"basi wacha mimi niende… Huyo mtoto anaitwa nani"

Sarah aliuliza kuwa huyo mtoto anaitwa nani ili asije akabeba mtoto wa watu

"anaitwa halima"

"ok wacha mi niende… Kwahio wewe unasema umefungiwa ndani"

"ndio Sarah, yaani sina hata njia ya kufanya hapa"

"ok wacha nikamchukue wifi yako kwanza kisha, tutajua cha kufanya"

"sawa sarah asante shost"

"usjali"

Basi sarah alikata simu lakini kwa jinsi namba zilivyotajwa na miriam hata yeye zilimpa wasiwasi juu ya mpenzi wake,… Lakini yete na yote aliamua kuondoka na kwenda kumchukuwa halima ambaye hata yeye ni wifi yake..

Wakati huo huku kwa chidi akiwa bado yupo ndani ya sero au mahabusu, akiwa bado hajui nani atamtoa au nani atamtetea katika kesi hio, na mama miriam alikuwa yupo siriasi na familia yake hivyo hakuwa akitaka utani na mtoto wake,.

"oya afande njaa inauma jamaa angu"

Aliongea kijana chidi baada kuhisi njaa akiwa ndani ya sero,..

"kaa kimya mjinga wewe, tutakuchanganya na wale wenzio kule we tupigie kelele hapa"

Chidi akiangalia wale mahabusu wengine wanavyogombana kila mara, Aisee hatamani kabisa kuchanganywa na watu hao,.. Mpaka hapo alimshukuru sana mama sarah kwa kuhonga kuwa akiwa sero asiteseke,… Haikupita muda mara msosi huo umekuja na tena ulikuwa msosi wa maana,… Wale mahabusu wengine walikuwa wakimtamani chidi kwa vile alivyotenganishwa na vyakula vizuri

"kuna mama kaleta hicho chakula"

Aliongea askari aliokuwa akilinda sero hio

"anaitwa mama Sarah"

"sasa unamuuliza nani?"

"basi yaishe boss"

"kula fasta… Msenge wewe unakula chakula kizuri tu kisenge senge"

Chidi alitulia tu huku akila kwa haraka mana hapo alipo alikuwa na njaa ya hatari, afu pia haikuwa sehemu ya kula kistaarabu mana ni sehemu ya kijeshi jeshi…

Tukija huku Dar es Salaam kwa akina salma na Jackson, Salma akiwa anataka kutoroka nyumbani hapo na mabegi yake mana hakutaka kuonekana kama anatoka… Na kaamua hilo baada ya kujua kuwa hapo alikuwa sio kwa ajili ya kuolewa

"sasa nitatokaje na haya mabegi"

Aluongea Salma huku akichagua nguo za kutoka nazo, mana hatamani hata kukaa katika nyumba hio.. Siku zote alikuwa akizani kuwa kuna ndoa lakini sivyo kumbe alikuwa anachoreka tu kama sanamu,.. Salama alichukuwa tu baadhi ya chupi na nguo zingine chache sana na kuziweka katika mkoba wake wa kwapani (kipima joto).. Alivyotoka alitoka kama mtu anekwenda mjini na kurudi hivyo hakuna aliomtilia mashaka japo wengi wa familia hiyo hawapendi mtoto wao Jackson aoe mwanamke ambae tayari keshazalishwa na mijidume mingine,.. Salma akiwa mtaani kuelekea stendi ili akapande gari, lakini kwanza alikaa mahari na kuanza kukumbuka maisha aliyokuwa akiishi na mume wake ambaye ni chidi,.. Alianza kujutia maisha yale na kumuacha mumewe.. Tena akikumbuka mbinu aliotorokea kule kijijini ilikuwa ni mbinu moja ya kijinga sana,…

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni