MUUZA CHIPS (92) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 23 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (92)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA TISINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Salma akiwa mtaani kuelekea stendi ili akapande gari, lakini kwanza alikaa mahari na kuanza kukumbuka maisha aliyokuwa akiishi na mume wake ambaye ni chidi,.. Alianza kujutia maisha yale na kumuacha mumewe.. Tena akikumbuka mbinu aliotorokea kule kijijini ilikuwa ni mbinu moja ya kijinga sana,…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"nitafanya nini mimi… Nitawaambia nini wakwe zangu"

Aliongea salma huku akilia, na hapo alioo ana mwaka mzima toka aje Dar es Salaam, hivyo hata mwili wake sio ule wa kijijini tena, kwa sasa anaonekana ni mdada mkubwa sana lakini hata miaka 20 hajafikisha lakini kutokana na maisha mazuri aliokuwa akiishi jijini Dar es Salaam, yamemfanya kunenepa kwa kiasi kikubwa, uzuri wake umezi kuonekana, alikuwa hana Shindu (chura) lakini kwa sasa ni balaaa,.. Lakini yote ya yote anajikuta kumbe alikuwa akiishi kama sanamu ndani ya nyumba hio, na yeye alichokifata kwa akina Jackson ni pesa, na pesa zenyewe azipate kwa kufunga ndoa na Jackson, sasa Jackson ndio huyo hana mpango wa kuoa mwanamke aliozaa,.. Hivyo baada ya kuligundua hilo aliona bora aachie ngazi afanye mpango wa kurudi kijijini kwao, ili akaombe msamaha…

Salma alitoka hapo na kuelekea stendi ili kufanya mpango wa kupanda basi.. Na hapo alipo alikuwa na pesa kidogo,.. Lakini alipofika sehemu moja ya mama ntilie aliingia ili kupata chakula, lakini kutokana na matatizo aliokuwa nayo, Salma alijikuta anapatwa na mawazo hata kula akajikuta hali,… Mama muuza akamuuliza salma

"we mtoto una nini"

Aliuliza mama huyo huku kama akimuonea huruma hivi,…

"we acha tu mama yangu nina matatizo, hapa sijui nitalala wapi, mabasi yenyewe nimechelewa"

"kwani wewe unatoka wapi mwanangu"

"nilikua nafanya kazi za ndani ila nimefukuzwa"

"oooohhh pole sana mwanangu…. Sasa unakwenda wapi"

"narudi tanga tu"

"jamani pooole"

"Ahsante mama"

Salma alikuwa akitoa machozi lakini keshadanganya kuwa yeye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani hivyo kafukuzwa,

"ila mwanangu, mimi nina shida na msaidizi wa hapa hotelini aniseidie, lakini sasa sina pakumlaza.. Hivyo kama utaweza kupangisha chumba, mimi nitakupa kazi"

Salma kuskia hivyo tu kanyoosha mikono juu na kumshukuru mungu, mana hakutegemea kama angelikutana na kazi kama hio mana mawazo yake yalishanyooka kwenda nyumbani…

Salma aliona ile ile pesa aliokuwa nayo aitumie kupangisha chumba

"Ahsante sana mama angu, mimi nitafanya mpango wa chumba mama angu"

Alionge salma huku mikono juu kwa kumshukuru mungu kwa kupata kazi kwa mama ntilie,… Kwahio swala la kurudi kijijini tena halipo kabisaaaa.. Mana keshapata kazi

"usijali mwanangu.. Sasa kama huna pa kulala, hebu nikupe siku hizi mbili utafute chumba, mana hapa Dar es Salaam chumba ni ngumu kupata, ila usipangishe mbali na hapa"

"sawa mama angu, ahsante sana mama"

Salma alimwona mama huyo kama mungu wa pili vile, mana hakutarajia kama angelipata hio kazi hapo,.. Basi salma anapewa siku tatu ili atafute chumba,.. Maskini pesa haitoshi kununua hata kagodoro kadogo, mana akilipa tu kodi ya nyumba, basi pesa yote imekwisha, hivyo itabidi aanze maisha kwa kulalia box,..

Sasa tukija huku arusha kwa mwanadada sarah akiwa ndio kafika katika eneo hilo,.. Sasa yeye alikuwa anaangalia nyumba nyingine ili akaingie chumba namba 14, lakini kila akiangalia bado haoni nyumba nyingine ya selfkontena ambayo vyumba vyake vina kila kitu ndani,.. Sarah alibidi aende tu kule kule kwenye chumba cha mpenzi wake.. Japo hana uhakika kama ni hicho,.. Lakini sasa Sarah alipofika kwenye boma hio, alions sura ya mtoto wa kike ambae alishawahi kumwona pale stendi, siku ileeeee chidi anakuja nae kutoka tanga, na ndio siku ile ile sarah na jasmini waligombana pale stendi..

Sarah aliona ni bora aingie mpaka ndani ili ahakikishe zaidi,.. Sarah mpaka ndani anakutana na magauni, kanga, sketi, na vingine vingi tu, sasa akaingia bafuni na kukuta nguo za ndani za kike tena baadhi zilikuwa mbichi kabisa kana kwamba masaa kadhaa yaliyopita alioga mwanamke hapo,.. Sarah alianza kulia huku hasira kali zikijongea katika kichwa chake,

Sarah aliketi kitandani huku akilia,.. Alikumbuka siku ile kama wiki moja hivi nyuma alimwona chidi akiwa anamiliki kadi ya benki ya miriam, lakini chidi alimwambia kuwa hio alipewa ili akanunue nyama,.. Lakini leo anahakikisha mwenyewe kuwa chidi na miriam ni wapenzi, tena sio wapenzi wa mchezo mchezo.. Sarah kwa hasira kashika simu huku machozi yakiendelea kutoka

"antiii unalia nini"

Aliuliza halima huku akiwa anamwangalia kwa huruma

"kichwa kinauma tu antii, lakini nipo sawa"

Alimjibu sarah huku simu ya miriam inaita,.. Miriam kuona simu ya sarah alifurahi kweli mana anajua fika rafiki yake keshamwona halima, na sarah hakuwa na haja ya kumuuliza huyu mtoto kuwa anaitwa nani, mana alishawahi kumwona akiwa na kaka yake chidi, hivyo mpaka hapo jibu analo.. Huku miriam anapokea simu kwa mbwembwe nyingi mno bila kujua tayari kimeshanuka baina yao

"haloo shost sarah, vipi umeshamuona wifi yangu??"

Urafiki uliodumu toka miaka hio, yaani kabla hawajawa matajiri toka wakiwa wanasoma shule za kimaskini kule iringa, na baadaye kuhamishiwa shule za pesa baada ya wazazi wao kuzipata pesa.. Marafiki hao waliishi pamoja kama ilivyo kwa mama yao, yaani jinsi walivyo kwa sasa ndivyo jinsi walivyo mama zao kipindi hicho,.. Marafiki hao walipendana sana lakini leo mmoja wapo anagundua kuwa, kumbe walikuwa wakimtumikia mwanaume mmoja na sii kila mtu na mwanaume wake,…

Sarah baada ya kuligundua hilo aliamua kupiga simu kwa Miriam..

Wakati huo Huku kwa miriam anapokea simu kwa mbwembwe nyingi mno bila kujua tayari kimeshanuka baina yao

"haloo shost sarah, vipi umeshamuona wifi yangu??"

Aliongea Miriam huku furaha ikimjaa katika moyo,.. Sarah anaijua vizuri furaha ya rafiki yake, hivyo hakutaka kuiharibu kwa wakati huo

"ndio nimempata"

"oooohhh thenx Sarah, nakushukuru ndugu yangu.."

"usijali… "

Sarah alikuwa akiongea huku akijikaza tu lakini naye alikuwa akilia, na huku miriam pia alikuwa akilia lakini ni kwa furaha, ila sarah yeye alikuwa akilia kwa uchungu wa hali ya juu,..

"sarah, wewe ni ndugu yangu.. Naomba ukae nae siku mbili hizi nikitoka tu huku chumbani nitakuja kumchukuwa"

Sarah roho ilikuwa inamuuma sana mana huyu mtoto anajua yeye ndio alitakiwa awe wifi yake,..

"sawa usijali miri"

Aliongea Sarah lakini alikuwa analia kwa uchungu wa kumkosa chidi..

Sarah alipanda gari yake na kurudi nyumbani,.. Alipofika nyumbani kwao alimkabidhi halima kwa mfanyakazi wa ndani kisha sarah yeye akarudi kazini mana alitoka kazini pale miriam alipomtoa..

Wakati huo miriam alikuwa na furaha baada ya kujua halima yupo salama salimini, tena yupo kwa rafiki yake kipenzi ambae ni sarah,… Sasa miriam aliitafuta namba ya shangazi yake pamoja na mama mkubwa wake, yaani aliitafuta namba dada wa baba yake, afu akamtafuta na dada wa mama yake,.. Aliwaambia kila kitu kuwa mpaka hapo alipo kafungiwa ndani kisa ni kupendana na mtu ambae hana pesa.. Wawili hao walikuwa wakimpenda sana mtoto miriam,.. Kwanini wasikusanyane wote,..

Tukija huku hotelini Sarah alikuwa ni mtu wa mawazo sana hata kazi ilikuwa haiendi kama ilivyotakiwa, yaani hata mama yake alishangaa sana kuona mtoto wake kudhoofika kiasi kile, na haikuwahi kutokea hata siku moja yaani sarah hata akasirike vipi hawezi kuwa hivyo alivyo leo. "wewe una shida gani huko ulipotoka"

Alimuuliza mtoto wake huku akisubiri jibu zuri toka kwake…

"wala tu mama sina kitu sema uchovu tu"

Alijibu sarah huku akijifanya anachangamka kwa kiasi fulani,

"hebu nenda nyumbani kapumzike mwanangu"

Mama sarah alimwambia mwanae kuwa aende nyumbani ili aweze kupumzika, mama sarah alijua hali ya mtoto wake japo hajui sababu ya hali hio…

BAADA YA MASAA KADHAA KUPITA

Jioni mama Sarah anarudi nyumbani kwake, moja kwa moja mpaka chumbani kwake ili aweze kuoga, baada ya kumaliza kuoga mama sarah au grace alitoka na kwenda chumbani kwa mtoto wake, mana anajua mtoto wake hana hali nzuri kiafya toka mchana…

Lakini mama sarah kufika chumbani alimkuta mtoto mdogo badala ya sarah,… Wakati huo sarah yeye alikuwa bafuni anaoga, mana alipokuja mchana alikimbilia kulala tu ili kutuliza akili yake,…

"shikamoo"

"marahaba Ujambo"

"sjambo"

Mama Sarah anamjua huyu mtoto na sio mara yake ya kwanza kumuona, bali alishawahi kumuona siku ile Miriam ndio anaingia ndani kwa chidi wakakutana mlangoni mama Sarah na Miriam, na miriam alikuwa kambeba halima,..

Ghafla sarah anatoka kuoga huku akiwa na taulo tu, jamani huyu mtoto ni shida, yaani mmmhhh nyie acheni tu mngemuona sarah mngelipiga saluti na huo weupe wake ulivyo mzuri..

"we sarah, haya huyu mtoto ni wa nani"

Mama Sarah alijifanya hamjui huyo mtoto, ila mama sarah kwa wakati huo alishapata presha kwa kumuona huyo mtoto… Mama alijua tu mtoto wake ana mahusiano na chidi na ndio maana presha imekuja,.. Mana huyo mtoto anamjua kuwa ni mdogo wake na chidi…

"huyu ni mdogo wake omari, mpenzi wake na miri"

Sarah alijikaza kudanganya, kana kwamba hajui kama mama huyo anajua kila kitu…

"aahhh wifi yake miri"

Alisema mama Sarah huku sarah akiitikia kinyonge sana

"ndio mama"

"aaahh sawa"

Mama alikubali lakini angelijua kuwa sarah nae yupo katika kundi hilo hilo la chidi..

"sasa huyo mpenzi wake yupo wapi"

Mama aliuliza kama vile hajui, na wakati anajua kila kitu kuhusu chidi,..

"anasema kachukuliwa na polisi"

Sarah yeye mwenyewe roho inamuuma mana huyo huyo mpenzi wake miri ndio huyo mpenzi wake afu yupo sero.. Hivyo hata yeye anaumwa na roho kwa kitendo cha chidi kuwekwa ndani ya sero,.. Lakini sarah alikuwa analia kabisa mpaka mama yake anajiuliza kwanini analia, kama aliokwenda sero ni mpenzi wa miriam, sasa mbona yeye analia kwanini, mama alianza kushtukia hio ishu ila hakuwa na uhakika sana…

BAADA YA SIKU NNE KUPITA

Chidi akiwa bado yupo sero na hakukua na mtu wa kumwekea mzamana, tena hata sero ya peke yake keshatolewa na kachanganywa na mahabusu wengine waliokuwa wakikamatwa kila kukicha,.. Chidi matese ya sero ndio alianza kuayaona toka alipohamishiwa huko kwa watu wengi,… Sema wengi wao walikuwa ni wapya wapya mana sio kuwa sero utakaa sana bali utakapopata mzamana ndio utatoka ila usipopata mzamana ndani ya siku 14 unapelekwa jela moja kwa moja mana hakuna wakukuseidia… Chidi alikuwa kama kapurwa, mfukoni hana kitu chochote hata waleti yake yenyewe haipo,…

Sasa tukija huku katika nyumba ya akina miriam wakiwa wamekaa kikao baada ya ile simu kupigwa na miriam, siku ile akiwa kafungiwa ndani,.. Sasa miriam keshafunguliwa siku ile ile lakini leo ndio kikao cha familia akiwemo dada yake wa mama, na dada wa baba, pamoja na dada yake miriam aitwaye neema, ambae ni mtoto wa mamkubwa wake,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni