MUUZA CHIPS (96) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 24 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (96)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA TISINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Sasa pale pale wakachukuana mpaka kwenye sebule ambayo ilikuwa ni kubwa sana, yaani ilikuwa ni kama sherehe ya kifamilia tu,.. Basi wale ndugu waalikwa walipiga vijiukelele vya hapa na pale baada ya kumwona mchumba wa mtoto wao,.. Yaani mama sarah alikuwa akitetemeka kwa hasira, yaani kaliwa yeye na mtoto wake tena mwanaume ni huyo huyo, bora ata wangelikuwa ndugu wawili, kuliko mtoto mdogo kama huyu kuwachanganya mtoto na mama yake,..

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Sasa Sarah kuangalia vizuri wageni waalikwa, alishangaa kutokumuona miriam, Sarah alishika simu na kumpigia miri wake

"haloo miri, mbona hujaja shost yangu, au ndio ushaanza kuntenga ivo"

"miri, mimi siwezi kuja tena huko… Siweziiii"

"heeeee miri, mbona unalia kuna nini tena"

"we acha tu sarah, nina bahati mbaya mimi"

"nini tena miri"

"nitakwambia kesho wacha leo nitulie tu"

Basi sarah alikata simu kisha kasherehe ka kuvalishana pete kalianza,.. Na unajua ni kwanini haikuwa sherehe kubwa? Ni kwasababu sarah anataka iwe fasta fasta tena alitaka iwe mbele ya miriam, lakini kwa bahati mbaya miriam kapata tatizo,…

Sarah alivalishwa pete na mpenzi wake chidi,.. Picha nyingi zilipigwa waalikwa walikula vizuri vinywaji, yaani kasherehe kalikuwa ni kakubwa haswa lakini mama sarah hakuwa na raha hata kidogo yani

Tukija huku hotelini kwa akina miriam, saidi akiwa ndio anafika kazini, alikutana na boss mlangoni..

"shkamoo boss"

Saidi alimsalimia mama miriam ambae ni boss wao,..

"marahaba… We huyo omari ndugu yako yupo wapi"

Aliongea mama miriam huku akijifanya kama hajui kama yeye ndio kampeleka sero

"niliskia yupo sero karibia wiki inaisha hii"

Saidi hakutaka kusema kama chidi keshatoka

"Ati nini? Yupo sero?"

"ndio"

Mama miriam alijifanya hajui… Sasa baada ya kuambiwa chidi yupo sero, alichukuwa simu yake na kumpigia mtu fulani…

"halooo… Mama sarah, si nilikwambia umtume mtoto wako akamtoe yule kijana"

"mbona keshatoka tayari mama miri"

"mbona kazini hafiki sasa"

"mimi najuaje sasa na safari zake"

"ok sawa"

Mama miriam alikata simu na kumgeukia saidi

"we unanidanganya si ndio"

Aliongea mama miriam huku akimkazia saidi jicho..

"ni kweli boss, omari katoka, lakini alisema nisimwambie mtu"

"anatakiwa afike kazini hapa… Afu mwambie aachane na mtoto wangu nitampoteza ndugu yenu"

Sasa saidi akaona kuliko rafiki yake aendelee kufikiriwa vibaya bora aseme ukweli tu…

"tayari wamesha achana"

Sasa maneno hayo yalimshtua sana mama miriam, wakati ndio alitakiwa kujiskia raha kwa kuambiwa wameachana…

"kwasababu gani?… Mana ana bahati nilikuwa nampeleka maweni kule tanga"

"omari alipokua sero, boss miri hakwenda hata kumuona, afu mdogo wake kaishi kwa watu afu yeye hakujali… Hicho ndio chanzo cha kuachana kwao boss"

"safi sana…. Ngoja nimpigie simu"

Chidi alipigiwa simu na boss wake aliomweka ndani takribani siku 5 hivi bila hata mzamana

"haloo we kijana… Nakutaka uje kazini sasa hivi"

"sawa boss"

Chidi hakuwa na chuki juu ya boss wake hata kama kamweka ndani lakini bado alikuwa anaipenda kazi yake,… Lakini mama miriam papo hapo alimpigia na mtoto wake aje kazini saa hio hio, sasa sijui alikuwa na maana gani… Ila tumeshajua kuwa huyu mama miriam ndio aliotoa amri ya kutolewa kwa chidi kule sero, ila alimtuma mama sarah ili mama sarah amtume mtoto wake.. Na ndivyo ilivyokuwa..

Dakika chache mbele chidi alikuwa keshafika ndani ya hoteli,.. Alifika mpaka kwa boss wake hata kama kamweka ndani lakini hakujali hilo..

"shkamoo boss"

"marahaba ujambo"

"sijambo"

"naomba uendelee na kazi… Tusameheane kwa yaliotokea… Unaweza kwenda"

Chidi hakutaka kuongea mengi aligeuza na kuingia jikoni kama kawaida yake ya kukaanga chipsi kiprofesheno zaidi..

Haikupita hata dakika tano miriam nae huyo, mpaka kwa mama yake..

"hali yako vipo mwanangu.. Afu mnona umekasirika hivyo"

"wala tu nipo sawa"

"ooohhhh shit, ebu kampe omari hii pesa ya pole kwa matatizo aliyo yapata"

"mamaaa… Mimi nitamuona wapi omari saa hizi"

"yupo jikoni"

"Whaaaaat… Ina maana omari kaja kazini mama"

"ndio.. Yupo jikoni huko"

Miriam kuskia hivyo aliinyakuwa ile pesa na kukimbia jikoni, lakini mama nae kumbe ana akili kama mchwa,.. Mama kiguu na njia, hatua ya miriam yakwake nyuma, kana kwamba anataka kuhakikisha ni kweli wamegombana au kadanganywa..

"jamani omiiiiii, nisamehe mpenzi wangu"

Yaani miriam alikimbilia kuomba msamaha, na hapo mama anaona kila kitu kinachoendelea

"miriam, niache bwana niache.. Familia yako hainitaki… Afu kwa roho yako ilivyo mbaya mimi nipo jela hata kuja kuniona hukuja.. Roho gani hio, mdogo wangu anaishi kwa watu kule wewe upo unakula raha tu… Roho gani hio… Niachieeeeeeee"

Chidi aliongea tena kwa sauti ya juu, mana hakuwa akitaka utani kweli..

"kwahiyo hunipendi omi"

"nakupenda sana,… Ila kwa roho yako ilivyo mbaya na ya kijinga bora nisikupende kabisa.. Afu kadi yako si nilishakurudishia asubuhi wewe.. Sasa wataka nini tena kwangu"

"omiiii"

"niacheeeeee"

Miriam alikuwa analia na kulia kabisa, tena kwa kupiga magoti, lakini chidi ndio kwanzaa haelewi la muazini wala la kanisa…

Mama miriam aliondoka taratibu huku akifurahi moyoni mwake, yaani hapo kuna kitu keshagundua, hivyo hana wasiwasi tena na mtoto wake,..

"uchunguzi wangu umekwisha… Ajiandae tu"

Aliongea hivyo mama miriam akiwa ofisini kwake, ila hatujui alimaanisha nini kusema hivyo..

Miriam akiwa bado anaomba msamaha, lakini kila akimkumbatia chidi kuna pafyumu anaisikia, na hio pafyumu inapendwa sana na rafiki yake sarah, na chidi mwenyewe hatumii pafyumu aina hio,… Miriam aliomba msamaha mpaka ikashindikana, miriam aliondoka na pesa yake mkononi kana kwamba chidi kaikataa, hapo miriam akaamini kuwa penzi lao ndio limekufa, yaani haamini kama kweli inakuwa hivyo, lakini ghafla simu yake inaingia sms akiwa ndio anaingia ofisini kwa mama yake,…

"mama, kakataa pesa yako"

"kwanini sasa"

Miriam alikuwa analia tu huku akiifungua hio sms… Kucheki zilikuwa ni picha zilizotumwa,… Lakini ghafla miriam anatoa macho na kushangaa… Sasa mama kumwangalia mtoto wake, anamuona anakwenda chini taratibu, yaani alikuwa anazimia kwa kile alichokiona katika simu…

"miri… We miri una nini lakini"

Mama yake aliita kwa sauti kubwa huku nae akianza kulia kwa mtoto wake kudondoka chini ghafla, na haijawahi kutokea, mama akaichukuwa ile simu ili aone kilichosababisha mpaka mtoto wake kuzimia.. Lakini hakuona chochote kwasababu simu iliingia lock….

Lakini Sasa cha ajabu tunamuona mama miriam anacheka, huku akiwa anatikisa kichwa,

Mama miriam ni mwanamke anaetumia akili nyingi sana, yaani hapendi mtoto wake aingia katika shida na ndio maana baadhi ya vitu vyake vinakuwa ni vya kutisha tisha tu, mtoto kadondoka chini lakini mama mtu anacheka sasa huoni ni balaa hilo,…

Chidi akiwa jikoni anaendelea na shughuli zake za mapishi ya chipsi, ghafla anamwona mama miriam kaja jikoni huku akiwa kama mtu mwenye wasiwasi sana

"jamani naombeni msaada miriam kadondoka kule ofisini kwangu"

Aliongea mama miriam huku akiwa analia kabisa… Ukweli ni kwamba UPENDO HUJITENGA MBALI NA HASIRA, chidi kuskia miriam kadondoka tu, upendo ulijionyesha wazi na hasira ilikaa pembeni,.. Kiukweli chidi anampenda sana miriam, lakini sema tu hasira zake za karibu ndizo zinazomfanya kukaa mbali na miriam….

Chidi alikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio ambako miriam kadondoka, Chidi kufika tu hakutaka maelezo, kamsomba mtu begani anatoka nae nje, yasni liwalo na liwe wacha aseidie mtu kwanza lakini kabla hajatoka nje, ghafla ambulance imefika, mana huyu ni mtoto wa tajiri, anaitiwa ambulance chap chap… Basi chidi alimwingiza katika gari hio huku mama akiwasha vogue yake kuifuata ile ambulance,…

Nusu saa mbele wakiwa wapo hospitalini chidi na mama miriam wakiwa wamekaa karibu na miri,.. Ghafla miriam anazinduka, mtu wa kwanza kumuona ni chidi, na wakati mama yake yupo apo apo,…

"jamani Omiiiiiiiiiii"

Miriam alizinduka na kumkumbatia chidi mbele ya mama yake yaani hakujali kitu chochote kile,… Kwa mara ya kwanza tunamuona mama miriam anaondoka mbele yao, lakini alipofika mlangoni alikutana na dada yake, na dada wa mume wake.

"grace,… hawa watoto hebu waache sasa, utamkosesha miriam mwanye upendo ukataka tajiri kumbe ni katili.. Waache sasa.. Kwani wewe ni pesa gani unazitaka tena?"

Aliongea dada yake, huku dada wa mume wake akifuata

"ni kweli wifi yangu… Unaweza kung'ang'ania aolewe na mtoto wa tajiri kama wewe, lakini wakaishia kugombana kila siku mana kila mtu anajivimbisha kwa pesa zao… Waache sasa"

Mama miriam hakumjibu mtu kati yao, bali aliondoka na kwenda wodi ya pili kukaa, ila alikuwa anaona kinachoendelea kule kwa akina miriam na chidi,.. Hata shangazi wa miriam na mamkubwa wake kuona chidi na miriam wamekumbatiana, wakarudi nyuma ili kuwapa nafasi, mana ndio walikuwa wanakuja kumjulia hali..

Sasa huku miriam akaona kabla chidi hajarudisha hasira zake, bora aongee ukweli, mana chidi hakawii kukasirika

"omari… Nakumbuka siku ile tulikamatwa wote, mimi nilijua unakwenda jela, lakini wewe hukujua kuwa mimi nakwenda wapi… Mama yangu alinifungia ndani siku tatu, chakula chenyewe napewa kwa dirishani,.. Mimi ningewezaje kutoka kwenda kumchukuwa mdogo wako,.. Na nani angejua kama mdogo wako yupo pale??…. Pia ningewezaje kuja kukuona huko jela,.. Nimefungiwa chumbani kwangu siku tatu, nilipofunguliwa, sikutakiwa kutoka nje ya geti, tena hiii leo ndio mara ya kwanza kutoka nje, lakini toka siku ile siijui nje ilivyo babuu,… Unanionea babuu, nisamehe"

Miriam aliongea hayo huku akishuka miguuni mwa chidi taaratibu kabisa kwa kuomba msamaha, lakini chidi kumbe kitambo tu keshamsamehe mana kuna sababu iliomfanya chidi atulie na kusikiliza maneno ya chidi..

Wakati huo mama anaona kila kitu kinachoendelea, yaani sijui alikuwa na maana gani kuwaangalia,..

"babuu, msamehe mkeo"

Miriam alikuwa akiongea huku machozi yakimtoka,…

Chidi hakusema kwa mdomo kuwa kamsamehe, bali alirudisha kumbatio kama la mwanzo tena likiwa limeambatana na makiss murua…

"lakini babuu, kuna kitu nataka nikuonyeshe hapa"

Sasa miriam anatafuta simu haoini, mara chidi kaitoa simu ya miriam na kumpatia

"shika"

Hata mama miriam alishangaa sana kwa kuona simu ya miriam inatokea mfukoni kwa chidi na wakati yeye aliiweka pembeni muda ule..

"heeeeeeee we umeipataje pataje hii simu"

Aliuliza miriam kisha chidi akakumbuka muda ule alipokuwa kaingia ofisini kwa boss, na kumkuta miriam kalala, na ukumbuke chidi baada ya kuambiwa kuwa miriam kadondoka yeye ndio wa kwanza kuingia kwenye ile ofisi,.. Alipofika kitu cha kwanza aliona simu ikiwa chini, Aliichukuwa ile simu na kuiweka mfukoni,.. Sekunde chache tu mama mtu huyo yaani ilibaki tu kidogo chidi afumwe akiwa anachukuwa simu ya miriam… Pale pale chidi akamsomba miriam mpaka kwenye ambulance,… Ukumbuke kuwa mama miriam aliifuata ambulance kwa nyuma akiwa na vogue yake… Sasa huku ndani ya ambulance chidi anajua kufungua lock iliopo kwenye simu ya miriam,… Chidi alipofungua tu ile simu, alikutana na picha za kumvisha pete sarah,.. Hivyo hapo hapo ndio akajua kuwa miriam alizimia kwa ajili ya hizo picha…. Na ndio maana hata pale odini chidi alikubali kukumbatiwa na akakubali kumsamege mana kuzimia kwa picha tu sio kitu cha mchezo Mchezo ni ishara kubwa kuwa kuna upendo mzito ndani yake..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni