SITOISAHAU FACEBOOK (2) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatatu, 29 Aprili 2024

SITOISAHAU FACEBOOK (2)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa


SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
Macho yalisoma tarakimu hizo, nilitumia mkono wangu kuzihesabu moja baada ya nyingine huku nikijiuliza kuwa hiyo ni elfu sitini ama laki sita? Jibu lilikuwa laki sita. Kijasho!!Niliondoka ATM na shilingi laki mbili. Kinyago gani angenibabaisha pale chuoni? Mimi ndio mimi

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Usiku mzima nilikuwa naitafakari pesa na kazi niliyoahidiwa na Dokta Davis. Nilianza kujiuliza ni nani ambaye anafaa kuwa nami katika msafara wa kwenda kumpokea mtu huyu muhimu, Dokta Davis. Niliwachambua marafiki zangu mmoja baada ya mwingine, hatimaye nikamchagua Mariana. Huyu alikuwa ni rafiki yangu hasa, lakini tatizo kiingereza kilikuwa kinampiga chenga..nikamsikitikia sana kwa kuikosa nafasi hii hadimu. Mwishowe nikamchagua Happy ambaye hatukuwa karibu kivile lakini alikuwa ana vigezo. Vigezo alivyotaka Davis

MCHEZO RASMI UKAANZA
Ndege ilitua muda ambao dokta Davis alikuwa amenieleza kabla, alitupigia simu baada ya kuwa ameshuka na tukafuata maelekezo ya jinsi ya kuonana naye.Happy alikuwa mkimya sana kwani hakuwa akijua mengi hivyo aliniachia mimi majukumu yote.Hatimaye tukaonana na Dokta Davis. Kwa jinsi alivyokuwa muonekano wake na sisi basi ilimpasa yeye aje kutupokea sisi na wala si sisi kwenda kumpokea yeye. Lakini ndio hivyo ni sisi tulienda kumpokea yeye.Lafudhi yake ilikuwa na mchanganyiko wa kiingereza cha Afrika magharibi na Marekani. Alikuwa na mwili mdogo tu usiokuwa na chochote cha kuvutia sana. Hakuonekana kuwa mtu mwenye pesa.

“Happy, huyu ni rafiki yangu wa siku nyingi.” Nilimtambulisha Happy kwa Davis bila kumwambia kama tulikutana facebook. Nikamtambulisha na Happy huku tukienda kwenye taksi iliyotuleta.“Nipeleke hoteli nzuri kabisa.” Alizungumza Dokta. Nami bila kusita nikamuelekeza dereva kwa kiswahili hoteli nzuri ya kifahari. Moyoni nilikuwa na wasiwasi bado kama Dokta Davis atazimudu gharama za hoteli hiyo. Muonekano wake bado ulikuwa kikwazo kwangu. Hakufanania kabisa kumiliki pesa nyingi!!Alipolipa kwa mfumo wa dola bili za hoteli alinikata wasiwasi wangu!!!Hapo kabla nilikuwa sijawahi kuingia hoteli yenye hadhi kama ile.

Nilikuwa nashangaa shangaa tu pale ndani, sikujua ni wapi mlango unafunguliwa, sikuona mahali pa kuwashia taa baada ya kuingia ndani, na ilinishtua kengele iliyopiga kelele baada ya kuwa mlango haujafungwa vizuri. Hata Happy naye nilimwona akishangaa shangaa, lakini Davis alionekana mzoefu sana wa sehemu kama hizi. Heshima ikaanza kujengeka.Tulizungumza mengi sana na Davis, alitawala maongezi kutokana na maswali aliyokuwa anatuuliza. Tulimweleza maisha magumu tunayopitia pale chuoni. Alisikitika sana na kuulaani umasikini.

****Siku hiyo alitupatia shilingi laki moja kwa ajili ya nauli za kurudi chuoni kila mmoja ya kwake. Happy alipagawa nayo kila mara alirudia kusema asante huku Davis akimwambia asijali ni hali ya kawaida.Nilipofika hostel niliyokuwa ninanishi nilitamani kila mtuanitambue Isabella nilikuwa nina shilingi ngapi mfukoni. Nilifika ndani na kujibweteka huku nikijisikia mwanamke mwenye bahati kupita wote. Nani wa kunisumbua!!Nilimkumbuka John Paul, huyu alikuwa ni mpenzi wangu ambaye licha ya kuachana bado nilikuwa nampenda.

John aliniacha kisa sikuwa na pesa, aliniacha kwa sababu umasikini ulikuwa damuni mwangu, huenda John alidhani naweza kumwambukiza umasikini, John akaniacha na kuunda uhusiano na msichana wa kitajiri, aliyekuwa anamiliki gari yake mwenyewe na kila mara alibadili nguo za bei ghari. Aliitwa Jesca.Niliumizwa sana na hali ile ya kuachwa na John, nilijipa moyo kuwa siku moja nami nitapata bahati ya kupendwa tena. Lakini bahati mbaya kila aliyekuja alionekana kuwa ni mdanganyifu.

Yale matendo ya kejeli aliyonifanyia John, niliamini sio kwa kupenda kwake bali msukumo kutoka kwa Jesca yule binti wa kitajiri.Hasira ikanipanda maradufu sasa nikauona ule wakati wa kulipiza kisasi ulikuwa umefika.Wakati wa kumwonyesha John kuwa sasa nina pesa!!! Nikawaza kumiliki gari, nikawaza kuwa mwanadada asiyepitwa na vazi lolote jipya. Na kubwa zaidi nikamuwaza Dokta….dokta Davis.Nikamjengea picha kaka huyu iwapo atakuwa mpenzi wangu, kwanza nitakuwa na amri juu ya pesa zake, na pili nitakuwa Mrs. Davis. Lolote analofanya lazima nishirikishwe.Mh!! Itawauma kweli Isabella nina mchumba kutoka Marekani. Nilijisemea huku nikitabasamu.

Zile picha za dokta Davis ambazo mwanzoni niliziona kuwa hazina mvuto sasa nikaziona kuwa hazina mfano dokta akawa dokta kweli. Uchafu gani mwingine wa kunisumbua humo facebook?? Nilijiuliza. Kisha nikagundua nilianza kujengeka kiburi kichwani!!!Usingizi ulinipitia nikaja kushtuka saa kumi na mbili asubuhi.Ni kama niliamka wakati sahihi. Dokta akapiga simu.“Mchukue gari ya kukodi, mwambie dereva tutamtumia sikunzima.” Alitoa maelekezo hayo Davis. Nikafuata maelekezo.Baada ya saa zima nilikuwa katika gari la kukodi.Kabla ya kwenda kwa dokta nikaamua kwanza kulipa kisasi, nikamuamuru dereva twende chuo. Bahati ilikuwa upande wangu, ile nashuka kwenye gari kwa mbwembwe zote. Karibia wanafunzi kumi niliosoma nao darasa moja waliniona.

Macho yao yalionyesha kutoamini nami sikuwajali.Nikajizungusha zungusha hapo kisha nikamwamrisha dereva, tukaenda kumchukua Happy. Huku nyuma najua niliacha gumzo!!!Tulipofika nyumbani kwa Happy, Happy hakuwepo!!! Nikajaribu kupiga simu yake, haikupokelewa. Niliwauliza majirani wakadai kuwa alitoka lakini hawajui kama alirudi ama la.Anachezea bahati huyu!! Nilijisemea.Nikapanda ndani ya gari. Safari ya kwenda kwa dokta ikafuata.Maajabu nilimkuta Happy akiwa amefika tayari!! Alikuwa na dokta wakinisubiri.Mchomo wa wivu ukanishambulia na kunijeruhi moyoni, nikaanza kuhisi zile ndoto zangu zimeanza kufifishwa. Happy alinisalimia akiwa na tabasamu mwanana. Dokta akiungana naye kutabasamu. Nami nikajilazimisha nikatabasamu!!!

“Kesho nitarejea nyumbani mara moja….kuna dharula imejitokeza. Lakini kitu kimoja nahitaji mfanikiwe kupitia mimi.” Alianza kutueleza dokta, tukiwa ndani ya gari la kukodi. Kisha akaendelea, “Nitarejea hivi punde tu!! Na nikiwa huko nitakuwa nawasaidia, msisite kunieleza lolote nami nitawasaidia, hata mimi kufika hapa nilikuwa nasaidiwa kwa hiyo ni zamu yangu kusaidia.” Aliongea kwa ukarimu mkubwa.Kwa mahesabu ya harakaharaka zile dola thamani yake ilikuwa milioni sita za kitanzania. Hizo ndizo Dokta alituachia tugawane.Kwangu mimi ilikuwa kama ndoto ya mchana!!!Siku iliyofuata dokta huyu wa ajabu akarejea huko anapojuayeye!! Hakutaka kusindikizwa uwanja wa ndege.

Ile hali ya kumshuhudia Happy akiwa na Dokta Davis ilinitia mashaka sana na kuhisi kwamba muda wowote ule nitanyang’anywa tonge mdomoni. Hivyo nikalazimika kuchukua tahadhari na kuanza kumpeleleza Happy kujua iwapo ana mawasiliano ya ukaribu na Davis ama ni wasiwasi wangu tu.Niliamini kabisa Davis alikuwa ni mali yangu na si ya mtu mwingine hivyo, Happy kama alitaka kunizunguka basi alikuwa hanitendei haki hata kidogo.

Ilikuwa siku tulivu ya jumamosi nikiwa chumbani kwangu. Chumba ambacho kwa sasa kilikuwa na mabadiliko kidogo tofauti na awali. Simu yangu iliita alikuwa ni dokta Davis. Nikapokea.Dokta alizungumza mengi huku kubwa zaidi akinigusia kuhusu biashara tuliyozungumza. Ni hapo ndipo nikaikumbuka biashara ya mtandao. Siku tulivyochat naye katika mtandao wa facebook huenda sikumuelewa vyema. Sasa alikuwa ananielewesha vyema ni jinsi gani mimi nitahusika katika biashara hiyo inayolipa mamilioni mengi kwa muda mfupi.

“Sasa hapo biashara hiyo inafanyikaje? Huo mtandao uko vipi?.” Nilimuuliza kwa utafiti. Kwani hakuwahi kunielekeza moja kwa moja juu ya biashara hiyo ya mtandao.“Umeuliza swali hili wakati muafaka sana. Nilitaka kukueleza kuwaumependekezwa kuwa mwakilishi wetu katika nchi yako. Hongera sana.” Aliniambia na kabla sijauliza chochote aliendelea, “Ni lini utapata walau siku nne za kuwa free uweze kunitembelea huku niweze kukupa maelekezo zaidi?”“Wewe upo wapi??” Nilimuuliza.“Lusaka Zambia, lakini tutakutana Ndola.”“Ndola ndio wapi?.” Nilijawa na maswali mfululizo.

“Mkoa mmoja hapahapa Zambia.”“Kwa sasa nipo free sana. Hatujaanza kuwa bize.” Nilimjibu huku nikiwa nafurahia mazungumzo hayo.“Waweza kukimbia mara moja kuja huku ofisini kwetu kwa ajili ya kusaini mikataba?.” Aliniambia, nikacheka kimya kimya yaani yeye Zambia alipaona karibu sana eti ananiambia nikimbie mara moja.“Naweza ila…”“Usijali mambo ya nauli na kila kitu kampuni itakulipia. Kesho zitaingizwa kwenye akaunti yako.”Ni hilo haswaa nilitaka kumuulizia na sasa alikuwa amenipa jibu tayari.

Baada ya kukata simu ile nilitamani sasa kila mtu aitambue furaha yangu, nipo chuo mwaka wa pili napata kazi nje ya nchi, mshahara zaidi ya milioni mbili. Nani kama Isabella.mara nikamsahau Happy aliyekuwa anakisumbua kiichwa changu.Nikafumba macho, nikatamani sana kumshrikisha mwalimu Nchimbi ambaye ni mama yangu mzazi lakini nikaona ni mapema sana, nikataka kumwambia Happy lakini nikahisi huyo alikuwea mpinzani wangu katika kumuwania Davis. Nikakaa kimya sikumwambia mtu yeyote.

Siku moja kabla ya kuondoka nilizungumza na kiongozi wa darasa letu Class Represenative ‘CR’ kuhusu kazi zitakazokuwa zinatolewa darasani awe ananiandika kuwa nipo japo sitakuwepo, mwanzoni alinikatalia lakini nilipotoa noti moja baada ya nyingine hadi zikafika noti kumi nyekundu alilainika na kugeuka kibaraka. Tena akawa mzungumzaji mkuu!! Pesa bwana!!(Safari ya Zambia)Kesho yake asubuhi nilikuwa katika basi la kampuni ya Abood kuelekea Mbeya kisha Tunduma halafu safari ya kwenda Ndola. Kusaini mkataba!! Mkataba nisioufahamu!!

Nilijihisi kama malikia na lilikuwa kosa kubwa sana kujaribu kunifananisha na mwanafunzi yeyote wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino ambacho nilikuwa nasoma. Hata wale wa huko Dar pia hawakutakiwa kufananishwa na mimi Hakuna ambaye angeweza kukaa ngazi moja na mimikwa sababu wengi wao waliishi kwa kutegemea mkopo sasa mimi nilikuwa nina pesa yangu na kubwa zaidi nilikuwa naingia kazini. Hao watoa mikopo ningepata fursa ya kukutana nao nadhani ningekuwa na jeuri ya kuwashushiamvua ya matusi.

Nikiwa safarini kuelekea Mbeya nikitokea mjini Dodoma baada ya safari ndefu kutoka Mwanza siku iliyopita, tulipofika Makambako nilianza kuifikiria familia yangu niliwaza kumjengea mama yangu nyumba ya kifahari kisha nimtoe baba yangu katika ulevi sugu kwa kumuwekea pombe za kisasa ndani. Hizo niliamini zitamnenepesha badala ya kumkondesha. Wadogo zangu waliokuwa wakisoma shule za kata nao nadhani walitakiwa kusoma shule zenye hadhi ya mshahara nitakaokuwa napokea dada yao.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni