Notifications
  • MY DIARY (21)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJATULIPOISHIA...Nilichomeka simu chaji na kuiweka hewani ili nione kama kutakuwa na sms yeyote iliyoingia.Hofu ilizidi kunitawala na wakati naendela kufikira simu yangu iliita niakzani labda ni Joyce na nilipoiangalia nilimkuta ni Msouth. Sikutaka kuipokea nikaiacha iite mpaka ikate yenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nikajiuliza kwani amepatwa na nini usiku huo mpaka…
  • MY DIARY (20)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINITULIPOISHIA...Nikamwambia kuhusu namba zangu za simu amuombe aliyemtuma anisaidie na kuhusu hilo la pili je hatuwezi kufanya kesho kwa sababu kuna mahali nilikuwa nikienda? Alifikiria kwa sekunde kadhaa na kuniambia kuwa hapana anaomba nimsaidie leo kama yeye alivyonisaidia mimi kwa sababu ningekuwa kwenye foleni nisingeweza kuondoka kirahisi hivyo kama ninavyofikiria.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (19)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TISATULIPOISHIA...Baada ya hapo niliendelea kumdadisi juu ya tukio lile lakini hakuwa tayari kufunguka zaidi ya kusema aliumia sana. Hapo nikaamua kuutafuta ukweli kwa kutumia mbinu za kike.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilimwekaa mikono begani na kumwambia pleaee dear naomba uniambie ukweli ili nijue nakusaidiaje? Basi Ramadhani akaanza kulalamika kuwa baba yake amekuwa akimwingilia…
  • MY DIARY (18)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...Halafu eti akawasha simu na kuonesha zile picha alizotupiga kweli huyu rafiki yangu alikuwa hamnazo sio picha tu alituchukua video kabisa na sauti. Akanambia ngoja ampigie paparazi mmoja hivi aje ili atengeneze habari tupate hela. Kauli hiyo ilinikosesha amani na kunikera sana akanmabia eti kuna namna ya kufanya ili sura yangu isitokee.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (17)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Nilijifikiria mara mbili nikajikuta namkubalia kwani alionekana ni mpole na mstaarabu sana.Basi tukaenda hadi kwake ambapo haikuwa mbali na hapo tulipokuwa na kweli alikuwa na chumba na sebule na sebuleni kwake niliona picha ya ukutani akiwe yeye na mke wake nahisi ilikuwa siku ya harusi yao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nikasema huyu kijana atakuwa amefunga ndoa…
  • MY DIARY (16)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Mwanamke akaamua kuingia jikoni na kukarangiza viazi na nyama rosti na kilipoiva kililetwa mezani tukaendelea kujenga afya. Sikuaamini kama Joyce alikuwa anakumbuka hata kupika kwa sababu alibadilka sana na alikuwa akiishi maisha ya starehe.. Lakini aliniprovu wrong kwa kutoa rost ya hatari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baada ya kula alinambia kuwa alikuwa amechoka…
  • MY DIARY (15)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Hapo mzungu wa watu hakuweza kuvumilia tena aliichomeka yote.Mmmmmh mmmmmh ishiiiiiiiiiiii yeaaaaaahhhhhhhh yeaaaaaaah ni miguno niliyoitoa mara baada ya kusikia joto tamu la kiungo hicho.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Ikabid nijivute kwa nyuma ili lengo likiwa ni kukaa vizuri ili kichwa cha nyoka kiwe juu juu ya pango langu ili niweze kukisugua sawa sawa na pia…
  • MY DIARY (14)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Nikamuuuuliza hivi wewe haugopi maradhi? Akanijibu kuwa angekuwa haogopi basi angeshakufa. Sikiliza Leah hapa nipo na vile vipimo vya ukimwi hivyo usiwe na wasiwasi tutapima wote wanne kama wapo fresh tutaingia kazini wewe si unatafuta hela ya kujiunga na chuo au?IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kabla sijajibu akanambia nitakupa na dawa ya kumeza ya kuzuia mimba na pia…
  • MY DIARY (13)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...Joyce akaanza kujimiminia mwenyewe, kweli dunia ina mambo wakati wenzake wakichanganya nay ale maji makubwa yeye alikuwa akinywa kavu kavu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi mimi sikuwa na jinsi zaidi ya kuaagiza ile bia yangu ambayo alinifundisha yaani savanna. Safari hii hakusubiri ili ifike mwisho ili anitambulishe bali tulivyoanza tu kunywa akawaambia wale…
  • MY DIARY (12)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...Niliamua kufanya ziara ili nijue pakoje na mwisho wa siku niliamini kuwa kutokana na umaarufu wa marehemu baba yangu isingekuwa kazi sana kulipata shamba lake..IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilitembea kijiji hadi kijiji huku nikijaribu kuuliza kwa wenye viti wa mtaa kama walikuwa wakimjua marehemu Bura. Kwa kweli kazi ilikuwa ngumu sikuweza kuvimaliza vijiji…

JULIANA (1)

Jina: JULIANA

SEHEMU YA KWANZA
Gideon alitulia kwenye kochi lililokuwa sebuleni kwake katika jumba lake la kifahari lililokuwa Masaki jijini Dar es Salaam. Alikuwa akimwangalia mke wake, Juliana Marcel jinsi alivyokuwa amekongoroka na kubaki mifupa mitupu. Alitia huruma pale alipokuwa amekaa, hakuwa mwanamke mrembo tena, uzuri wake ulipotea kabisa machoni mwa Gideon.

Mwanamke huyo aliyesifika kwa urembo kipindi cha nyuma, alichakaa, hakuwa kama Juliana yule aliyepita ambaye aliwatingisha wanaume kutokana na uzuri wake.

Gideon alikumbuka jinsi Juliana alivyokuwa kipindi cha nyuma, kipindi walichokuwa wakisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kipindi ambacho wanaume wote walikuwa wakivutiwa naye. Alikuwa na urembo wa ajabu, aliwavutia wanaume wengi lakini mwisho wa siku, aliwakataa wenye magari na pesa zao, akamkubalia yeye, mtoto wa mama ambaye hakuwahi hata kumiliki milioni moja mfukoni.

Leo hii, miaka kumi baada ya kumuoa na kuzaa naye mtoto mmoja aliyeitwa Jesca, Juliana hakuwa yule wa miaka ile, alichoka, uzuri wake wote ukapotea na kubaki mifupa mitupu. Kila mara Gideon alipokuwa akimwangalia, alitamani kulia, alitamani kumwambia kwamba hakumpenda tena, wakati mwingine alitamani kumpa talaka lakini kwa sababu alikuwa Mkristo, alishindwa kujua afanye nini.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

“Kwenye shida na furaha, uzima na ugonjwa nitakuwa na wewe,” aliyakumbuka vilivyo maneno aliyosema mbele ya mchungaji, mbele ya kanisa zima kwamba kamwe asingeweza kumwacha mwanamke huyo.

Leo hii hakutaka kukumbuka tena, asingeweza kuendelea kuishi na mwanamke huyo, wakati mwingine alitamani kumuua, alitamani kwenda jikoni, akachukue kisu na kumchomachoma. Hakuwa na mapenzi naye tena, kisa tu alikuwa amechoka, kisa tu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Saratani ya Damu.

“Mume wangu!” aliita Juliana huku akimwangalia Gideon.

“Unasemaje?” aliitikia Gideon kishari, kwa jinsi alivyomchoka mkewe, hakutaka hata kuisikia sauti yake.

Juliana akanyamaza, moyo wake ulichoma, kipindi hicho kilikuwa ni cha jaribu kubwa maishani mwake. Gideon aliyemzoea hakuwepo, tabasamu pana alilokuwa akimpa kipindi cha nyuma halikuwepo tena, kile kicheko alichokuwa akikiona usoni mwake kilipotea, kwa kifupi, Gideon huyu hakuwa yule wa zamani, hakuwa yule ambaye alizoea kumwangalia na kumwambia ni jinsi gani alikuwa akimpenda.

“Ninakufa mume wangu! Kansa inaendelea kusambaa mwilini mwangu,” alisema Juliana kwa sauti ndogo kabisa.

“Kwa hiyo?” aliuliza Gideon.

Wakati mwingine alihisi kwamba mtu aliyekuwa akizungumza naye hakuwa Gideon yule wa nyuma, alihisi kulikuwa na msichana aliyekuja na kumchukua Gideon wake na kumwachia Gideon mwingine, asiyeeleweka, Gideon aliyekuwa na hasira na asiyetamani kumuona mbele ya macho yake.

Juliana akasimama kutoka kwenye kiti, akamsogelea pale alipokuwa na kukaa karibu yake. Gideon akakunja sura zaidi, hakutaka kabisa kumuona mwanamke huyo akikaa karibu naye kama vile na ndiyo maana hata muda wa kulala alikuwa radhi kulala sebuleni, ang’atwe na mbu lakini si kuona akilala na mke wake, Juliana.

“Unanipenda?” aliuliza Juliana huku akimwangalia mume wake huyo.

“Maswali gani hayo?”

“Nimekuuliza!”

“Ili?”

“Nijue?”

“Hivi wewe mwanamke mbona hutaki kunielewa? Mbona hutaki kunisikiliza?” aliuliza Gideon huku akimwangalia Juliana kwa macho yaliyojaa chuki.

“Gideon! Unanipenda?” aliuliza Juliana.

“Naomba uniache! Niache nipumzike. Nimekuachia chumba ukalale kule ili nilale sebuleni, cha ajabu, usiku sana, muda kama huu unakuja sebuleni, kufanya nini? Au unataka kulala sebuleni ili nikalale chumbani?” aliuliza Gideon kwa hasira.

“Nimekukumbuka mume wangu! Nimekumbuka tabasamu lako, nimekumbuka joto lako, naomba unikumbatie, hata kwa dakika moja tu, nakuomba mume wangu,” alisema Juliana kwa sauti ndogo kabisa, tena yenye kubembeleza.

“Nikukumbatie wewe?” aliuliza Gideon.

“Ndiyo!”

“Unanichekesha sana. Naanzaje kwa mfano?”

Moyo wa Juliana ukachoma, akahisi kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake, hakutegemea kusikia maneno kama hayo yakitoka mdomoni mwa mume wake. Alimkumbuka, alihitaji faraja, alijua kwamba alikuwa akipitia katika kipindi kigumu, alitakiwa kubembelezwa, alitakiwa kufarijiwa na kutiwa moyo sana lakini kwa mume wake huyo, hilo lilionekana kuwa kama ndoto. Angeanzaje kumkumbatia?

“Unalala sebuleni au chumbani?” aliuliza Gideon.

“Popote utakapolala! Siwezi kulala peke yangu tena! Gideon mume wangu! Kumbuka tulivyokuwa, kumbuka ulivyoahidi mbele ya kanisa, shida na raha, ugonjwa na afya! Umesahau yote hayo mume wangu?’ aliuliza Juliana huku akimwangalia Gideon.

“Clock is ticking…” (muda unakwenda tu)

“Gideon! Pleasee..” (tafadhali, Gideon..)

Gideon akasimama, kwake, maneno yote aliyokuwa akiambiwa na mkewe hayakuonekana kuwa na maana kabisa, hayakumuingia hata kidogo moyoni mwake. Alimchukia Juliana, hakumpenda, alikuwa radhi kulala na mbwa lakini si kulala na mtu kama Juliana.

Alibadilika, hakuwa mzuri, hakuwa na mvuto, kila alipomwangalia, alionekana kuwa kama kituko. Bosi yeye, milionea, eti alale na mtu kama Juliana! Ili iweje? Thamani ya mwanamke huyo ilipotea moyoni mwake, mapenzi yakapotea, chuki ikaingia moyoni mwake.

Kila alipomwangalia, alitamani kumuua, alitamani kumchukua na kwenda kumtelekeza mahali fulani lakini si kuendelea kukaa ndani ya nyumba yake, yaani kila alipokuwa akiamka, amkute chumbani humo. Alimchukia kupita kawaida.

“Kuna siku nitamuua tu! Nitakuja kumuwekea sumu kwenye maji,” alisema Gideon huku akipiga hatua kuelekea chumbani, hakuyajali machozi ya Juliana, jinsi alivyokuwa akilia, kwake alimuona kama muigizaji wa Bongo Muvi ambaye alikuwa kwenye filamu kali ya majonzi.

Huo ndiyo ulikuwa msimamo wake, alimchukua mkewe, yuleyule mwanamke ambaye kipindi cha nyuma alimwambia kwamba alimpenda kwa moyo wote, alimpenda hata zaidi ya alivyokuwa akiwapenda wazazi wake.

Kansa ikabadilisha kila kitu, ikayaondoa mapenzi aliyokuwa nayo na kupandikiza chuki moyoni mwake. Hakukuwa na jingine alilokuwa akilifikiria zaidi ya kumuua mwanamke huyo ambaye bado alikuwa akiteseka kila siku.

2004, UDSM, Dar es Salaam

“Gideon! Unampenda kweli Juliana?” alisikika jamaa mmoja akiuliza.

“Nampenda sana! Nakiri kwamba nitampenda maisha yangu yote, niwe naye kwanza, nitamthamini na kumlinda,” alisema Gideon huku akimwangalia rafiki yake huyo aliyeonekana kushangaa, tangu awaone watu wakipenda, hakuwahi kumuona mtu akipenda kama alivyokuwa Gideon.

“Ila si unajua mtoto wa kishua, halafu watu wengi wamemfuata na magari, pesa, sasa wewe majalala utampata kweli?’ aliuliza rafiki yake huyo aliyeitwa Amos.

“Kwa nini nishindwe? Nitashindwaje sasa? Nitampata tu! Mapenzi si pesa, mapenzi hayatengenezwi benki kaka! Hutengenezwa moyoni,” alisema Gideon huku akionekana kuwa na uhakika juu ya kile alichokuwa akikizungumza.

“Kama una uhakika! Haina shida.”

Gideon alichanganyikiwa, hakukuwa na kitu kilichokuwa kikimuumiza moyo wake kama kumuona msichana Juliana akiwa anamkataa kila alipokuwa akimfuata.

Moyo wake ulikuwa na kiu kubwa, alikuwa kwenye presha kubwa, hakukuwa na msichana aliyeuteka moyo wake vilivyo kama ilivyokuwa Juliana. Alimpenda, kila alipokuwa akilala, mtu wa mwisho kumfikiria alikuwa msichana huyo na alipoamka asubuhi, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kumuweka kichwani mwake.

Alilewa, hakuelewa kitu, alihitaji mapenzi, alijua kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakipenda mno lakini kila alipokuwa akijiangalia, jinsi moyo wake ulivyokuwa kwa msichana huyo, alijiona akishika namba moja.

Aliwahi kumfuata Juliana na kumwambia ukweli kwamba alikuwa akimpenda na hakuwa akijiweza. Msichana huyo, kama kawaida yake akamkataa Gideon na kumwambia kwamba aokoke, aachane na maisha ya mapenzi na aukabidhi moyo wake kwa Yesu kristo.

Hakuumia sana moyoni kwa kuwa alikataliwa kwa staili ambayo hakuwahi kuifikiria kabla. Hakutaka kukata tamaa, maneno hayo hayakumrudisha nyuma, bali yalimtia nguvu ya kusonga mbele. Akajifanya msumbufu, kila alipokuwa akimuona Juliana, alimfuata na kuanza kumchombeza.

“Nimesema sitaki! Nimekwambia uokoke, ndivyo Biblia inavyosema,” alisema Juliana huku akimwangalia mwanaume huyo.

“Sawa. Lakini Biblia hiyohiyo inaagiza upendo. Halafu wewe hunipendi, sasa hiyo Biblia ya wapi Jully?” aliuliza Gideon huku akimwangalia msichana huyo katikati ya macho yake.

“Naomba unielewe!”

“Lakini hujanijibu swali langu Jully!”

“Hakuna kujibu swali. Biblia haimaanishi huo upendo unaozungumzia wewe. Naomba uniache,” alisema Juliana huku akionekana kuchukia.

“Daah! Unaniumiza Jully!”

“Hivi wewe mwanaume hutaki kunielewa?”

“Nataka ila nawewe mbona hutaki kunielewa?” aliuliza Gideon kwa sauti ya upole na yenye kubembeleza.

Kila alichokuwa akikizungumza Juliana, Gideon aliingizia maneno yake. Juliana alichukia, kila alipomwangalia mwanaume huyo, moyo wake ulishikwa na hasira kiasi kwamba alitamani hata kumpiga vibao.

Akasimama na kuondoka zake kwa hasira.

Gideon akabaki mahali hapohapo, akamwangalia Juliana jinsi alivyokuwa akiondoka, moyo wake ulimuuma mno, alitamani kumfuata, kumsimamisha na kumwambia amsikilize tena.

Hakukoma, haukuwa mwisho, akapiga moyo konde na kuamini kwamba kuna siku angeweza kumpata msichana huyo. Akawaambia marafiki zake, ugumu wake kumuingiza Juliana mkononi mwake.

Wenzake wakamwambia kwamba kwa staili aliyokuwa akienda asingeweza kumpata, ilimbidi atumie mbinu nyingine zaidi.

“Ipi?” aliuliza Gideon huku akiwa na shauku ya kutaka kufahamu.

“Jifanye kuwa malaika wa nuru!”

“Mmh! Kivipi?”

“Jifanye umezama katika wokovu! Yeye si ndiyo anataka maisha hayo! Fanya hivyo!” alisema Amos.

Hakuwa na jinsi, ulikuwa mtihani mkubwa kwake lakini alitakiwa kuhakikisha anaufanya na kufanikiwa na kumnasa msichana huyo mrembo.

Baada ya siku mbili, akamfuata msichana huyo kwa mara nyingine, alipoanza kuzungumza naye, Juliana alishangaa, hakuamini kama kweli maneno hayo yanatoka kwa mwanaume huyo.

Aliongea kiustaarabu sana, kila alipokuwa akizungumza, alilitaja jina la Yesu, alipobadilisha, basi alitamka jina la ibada tu. Juliana alihisi kama mwanaume huyo alikuwa akiigiza lakini kila alipomwangalia, alionekana kubadilika.

“Juliana! Naomba umsahau Gideon yule wa nyuma. Amekufa! Huyu ni Gideon mpya aliyezaliwa mara ya pili. Ningependa uje kushiriki ibada kanisani kwetu kama hutojali,” alisema Gideon huku akiachia tabasamu pana.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
53 featured Juliana Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni