Notifications
  • MY DIARY (50)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA HAMSINITULIPOISHIA...Nilimnongo’oneza kuwa atumie kinga ili nisimwambukize ukimwi akanijibu kwa sauti ya mahaba nisiwe na hofu yeye yupo tayari kufa kwa ajili ya penzi langu hivyo hawezi kutumia kinga kwa mke wake aliyemoa tena siku muhimu kama hiyo.Sikutaka kumbishia yeye ndo muaamuzi wa mwisho kuhusu afya yake hivyo nilimuacha aendelee kufanya yake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kumbe na…
  • MY DIARY (49)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TISATULIPOISHIA...Baada ya maneno ya kusilimu ambayo waliambiwa wayatamke kiongozi huyo alisema neno ya mwisho kabla hajashuka.” Kila alie na akili timamu, mwenye busara naa anaetaka haki, na kusimama pamoja na haki, basi akiangalia dunia ilivyo na jinsi inavyokwenda basi lazima kutakuwa na nguvu kuuu nayo ni mwenyezi mungu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Kuna vitu vingi sana…
  • MY DIARY (48)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NANETULIPOISHIA...Familia yangu haikukubali kabisa mimi kuolewa na rangi nyeusi hivyo walinitenga na kusema hawanitambui kuwa mimi ni ndugu yao.Lakini kutokana na mapenzi mazito niliyokuwa nayo kwa baba yake na Leah nilijikuta nipo tayari kwa lolote hivyo nikahama na kwenda kuishi Tanzania.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Katika miaka hiyo tuliyokaa nilibahatika kupata mtoto huyu…
  • MY DIARY (47)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SABATULIPOISHIA...Lakini ilifikia mahali ndoto hiyo inanijia hata mchana nikiwa nimekaa mahali tulivu.Ilikuwa inanipa taswira nzuri ya sehemu ambayo madini yalikuwepo.Basi nilianza mikakati ya kulitafuta eneo hilo na hiyo ni mara baada ya ushauri wa mpenzi wangu Candy hapo akimaaanisha yule dada aliyekuwa naye pale jukwaaani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Candy alinisihii sana…
  • MY DIARY (46)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA SITATULIPOISHIA...Nilikuwa kama niliyepigwa butwaa nisiamini nilichokuwa nakiona mbele yangu. Oooooh my God hold me on yalikuwa ni maneno yaliyonitoka kutoka kwenye uvungu wa moyo wangu mara baada ya kumuona James kwa uzuri zaidi na kuamini kuwa yule kweli alikuwa ni kaka yangu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilishindwa kuelewa nini kimetokea mpaka yeye kurudi katika hali yake ya…
  • MY DIARY (45)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TANOTULIPOISHIA...Ndio niliona hipo haja ya kuokoka na kuishi maisha ya utakatifu kwa maana nishaishi maisha yote ya kuwa mbali na mungu. Nakumbuka nilipokuwa mdogo kipindi hicho naujua mlango wa kanisani tuisahawahi kufundishwa kuwa mtetezi wa kweli wa maisha ya mwanadamu ni Mungu.Na siku zote alaaniwe mtu yule amtegemeaye mwanadamu.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Sio kazi ya…
  • MY DIARY (44)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA NNETULIPOISHIA...Yani alianza kutaka uhusiano na mimi tena uhusinao wa mapenzi.Mda wote alikuwa akiniganda kama luba.Na mimi nilikuwa mjanja sana maana nilijifanya sinywi pombe wala kuvuta sigara.Pia baada ya kugundua kuwa wahusika wengine walikuwa wanajiachia niliamua kujifanya mshauri wa mapenzi na mahusiano.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilikuwa nawasshauri sana mshiriki wa…
  • MY DIARY (43)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA TATUTULIPOISHIA...Wakati nabadilisha staili kwa kukichua kile kifaa na kukiweka vizuri huku nikibinya ile switch hili iongeze spidi Mark aliingia. Ni kweli nilimuona ila sasa sikuwa na jinsi ilibidi nimalizie furaha hiyo ya uwongo uwongo. Yaani wazungu jamani sijui walifikiria nini maana kile kifaa ukikiminya kwa juu kinakuwa kinajizungusha chenyewe.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (42)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MBILITULIPOISHIA...Uzalendo ulinishinda ikabidi nimuulize ni kwanini bado wanatumia njia hiyo ya kizamani kutunza kumbukumbu wakati siku hizi kuna kitu kinachoitwa Human Resource Informaion system ambapo kumbukumbu zote za wafanyakazi kama waliochishwa kazi, wagonjwa, walioenda likizo ,waliopandishwa vyeo na taarifa nyingine muhimu uhifadhiwa kwa kutumia komputa.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (41)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA AROBAINI NA MOJATULIPOISHIA...Mark anashangaazwa sana na mwanamke huyo lakini kwa kuwa shida yake ilikuwa ni hela anaamua kuachana nae na kuanza maisha mapya hapo jijiini Dar es salaamMaisha yanaendela lakini Mark amekuwa tajiri na mtu mwenye mafanikio sana kiuchumi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Pamoja na mafanikio hayo ni mtu ambaye mapenzi bado yalikuwa yakimuumiza siku hadi siku.Filamu…

MTU WA UFUKWENI (1)

Mwandishi: Andrew Mhina

SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa ni kama ndoto ya mchana! Ndoto yenye kila aina ya dalili ya kuondoka na kubakia na kumbukumbu ya muda mfupi sana kwa baadhi ya mabaki ya ndoto hiyo. Nilijaribu kufikicha macho yangu ili kuhakikisha yale yaliyoko mbele yangu!.. Bado vitu vyote vilikuwepo! Lile jumba la fahari lilikuwa limetulia mbele ya macho yangu, wakati bwawa la kuogelea likiwa karibu yangu mahali nilipokuwa nimeketi.

Mazingira ya mahali hapa ni mazuri ajabu! Majani mafupi yaliyokatwa kwa mashine maalumu, bustani nzuri za maua na miti ya kimvuli iliyokuwa ikitingishwa taratibu na upepo, vilitoa burudani ya pekee. Niliamka taratibu pale nilipokuwa na kusogelea banda la magari. Nilikuwa nataka tena kuamini kuwa mali hizi zote zilikuwa ni za kwangu. Magari matatu ya fahari yalikuwa yametulia mahali pake. Haikuwa ndoto wala wazimu kwa mimi kushangaa mali zangu mwenyewe!

Historia yangu ndiyo iliyonilazimisha kuangalia mambo haya kama ndoto ya mchana. Historia yangu inanifanya nisiamini japo ndio niko ndani ya ukweli wa yale ninayoona kuwa ni ndoto. Mara simu yangu ya mkononi inaita! Niliitoa mfukoni na kuiangalia nione ni nani alikuwa akipiga. Nikiwa kando ya banda la magari nilipokea simu ile, alikuwa ni Jobiso Baro, mmoja wa waandaaji wa filamu mashuhuri nchini mwetu. Muda mrefu sana alikuwa akinishawishi kucheza filamu ya matukio yaliyopita katika maisha yangu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

Nilisita kufanya hivyo mara nyingi, sio kwamba kulikuwa na ubaya kucheza sinema ya maisha yangu la hasha! Bali nilikosa mahali hasa pa kuanzia katika mikasa yangu niliyopitia. Nilikuwa natafuta namna ya kuanza kuielezea historia yangu, kusudi nisije nikaacha chochote cha muhimu kuwekwa kwenye sinema hiyo.

Muda nao ulikuwa umenibana sana kwa sababu nilikuwa na majukumu ya kusimamia makampuni yangu mapya, ambayo nilitakiwa kila wakati niwepo mahakamani, kusudi nishughulikie kubadilisha jina la umiliki kutoka mmiliki wa kwanza.

Kutafuta wakili binafsi nalo lilikuwa swala la muhimu, lakini ni nani wakili atakayefaa kusimama na mimi katika mwendo mzima wa maisha yangu na mali zangu? Maswali mengi na mambo mchanganyiko vilibebana ndani ya kichwa changu hata nikawa sina muda wa kutosha kutoa maamuzi sahihi kwa vyote. Wafanyakazi wangu wa ndani ninashukuru sana kwamba walikuwa wakinielewa, hasa nilipowaambia kuwa nataka utulivu wa kutosha. Walifanya kazi zao mapema na kuniachia nafasi ya utulivu katika eneo la bustani yangu, iliyopo karibu na bwawa hili la kuogelea.

Mahali hapa huwa ninapatumia kupumzikia, wakati nikitoka ofisini na kutafuta utulivu wa kipi kianze kati ya majukumu yangu mengi niliyokuwa nayo. Pamoja na kwamba umepita muda wa miezi mitatu tangu niwe mmiliki wa mali hizi, lakini kila siku kwangu niliona kama ni ndoto ndefu.

Ndoto iliyotawala katika usiku wote bila kubadilika! Ndoto iliyofanana sana na ukweli halisi! Ndoto labda iliyokuwa na mapitio yaliyofanania na yale ya mawazo ya Alinacha wa kitabu cha Alfu lela u lela au siku elfu na moja! Tofauti moja ya ndoto yangu na Alinacha ni kwamba mwenzangu alikuwa akiwaza na kupotelea katika mawazo yake ya kiutajiri na usultani.

Lakini kwangu ni kwamba ninaishi kabisa ndani ya ndoto hizo. Ndoto zenye vitu vinavyoshikika na amri zinazotekelezeka! Naam! Ndoto ya mchana lakini iliyodumu kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu! Nilifikia mahali pa kukata shauri kukubaliana na ukweli uliopo, kuwa hii sio ndoto bali ni jambo halisi limetokea. Sababu ya kuyafananisha maisha haya na ndoto ni kwamba sikutegemea kuwa iko siku nitafikia vilele hivi vya mafanikio.

Taratibu nilipeleka simu ile sikioni mwangu na kuanza kuitikia:“Haloo Jobiso!”….“Habari Mheshimiwa!” Alijibu Jobiso…kisha akaendelea “Nimetaka kukujulia hali tu, pia nina jambo la muhimu kidogo nikujulishe.” Alisema Jobiso sauti yake ikisikika kama mtu mwenye haraka. “Jambo gani Jobiso! Mbona unaonekana kama unataka kukimbia uko sawa?” Nilimwambia kwa mshangao.“Niko sawa mheshimiwa, lakini nilitaka kama una nafasi tuanze yale mahojiano kusudi niandaye vipande vya Sinema yako.”Alisema kwa utulivu.

“Mbona una haraka sana Jobiso! Bado sijawa tayari kutokana na mibanano ya mambo yangu. Sijaandaa chochote nitaanzia wapi?” Nilimjibu kwa msisitizo kidogo. “Mheshimiwa nimekuambia hivyo kwa sababu baada ya mwezi mmoja nitakuwa nchini marekani kwa masomo. Leo hii mkurugenzi wangu ametoa ofa kwa wafanya kazi wake bora kwenda masomoni, ili kupanua ujuzi zaidi.

Mimi nimetokea kutangazwa kuwa mmoja wa wafanyakazi bora.”Jobiso alielezea kwa hamasa kuonyesha jinsi alivyovutiwa na ofa aliyopewa ya kwenda nchini Marekani. “Hongera sana bwana mdogo! Nimekuelewa, lakini unadhani kuna haja ya kufanya haraka juu ya sinema yangu? Maana sioni kwamba hata nikikuhadithia itaweza kuchezwa kwa kipindi hicho kifupi.

Nilimwambia kwa utulivu lakini nikitia msisitizo kuwa kazi ile haikuhitaji haraka kiasi hicho. “Kaka niruhusu tu nije mengi tutaongelea huko. Ninajaribu kuangalia uwezekano wa kufanya jambo kwa wakati. Unakumbuka waswahili na ule msemo wao maarufu?” Aliuliza huku akijiandaa kuachia kicheko chake cha uzushi. “Ndio nakumbuka kuwa linalowezekana leo lisingoje kesho.” Nilimjibu.Basi naomba nije ili tuangalie ni wapi pa kuanzia.” Alisema kwa shauku baada ya kuijibu methali yake. Nilifikiri kidogo nini cha kufanya kutokana na kutokujiandaa vema juu ya hili, lakini niliafikiana naye aje nyumbani.

“Basi dogo unaweza kuja wakati huu maana mimi nipo tu nyumbani.” Nilimwambia na kukata simu, baada ya yeye kupokea ukaribisho huo kama mtu aliyeokota kipande cha almasi! Nilijisogeza katika ngazi za kupandia kuelekea katika mlango unaonipeleka hadi kwenye sebule kubwa nzuri,sebule iliyojaa kila aina ya vifaa vya thamani.

Kando ya sebule hiyo kuna chumba maalumu nilichokiteua kiwe ofisi yangu. Chumba hiki kimejengwa kwa aina yake. Ofisi yangu hii ina kila aina ya vifaa vya kielektroniki, vya kunasia sauti na kamera za kuchukulia matukio mbalimbali. Nimeamua kutumia chumba hiki kwa ajili ya mahojiano yangu na Jobiso Baro, juu ya maandalizi ya sinema yangu.

Ulikuwa ni usiku wa manane kukiwa na manyunyu ya mvua kiasi na upepo wa hapa na pale. Nyota zilikuwa zimefichwa na mawingu meusi yanayoashiria mvua kubwa kunyesha. kijiji cha Makuyuni kilikuwa kimya isipokuwa sauti za watu wachache waliokuwa wakikohoa ndani ya nyumba zao na kilio cha mtoto aliyekuwa aidha anataka kunyonya, au ni deko la kijinga tu,kwa baadhi ya watoto.

Hali ilikuwa tofauti katika nyumba moja. Ni katika nyumba aliyokuwa akiishi bwana Kimbe na mkewe bi Nacharo. Mke wa Kimbe alikuwa katika wakati mgumu sana wa kutaka kujifungua. Hali hii ilikuja sambamba na ugumu wa maisha. Hakukuwa na hata senti moja mifukoni mwa Kimbe. Hakuwa hata na rafiki mmoja wa kumwendea usiku huo, hii ni kutokana na madeni aliyokuwa nayo katika kijiji hicho.

Hali ilikuwa ni mbaya kwa ujumla kiasi cha kumfanya akose jinsi ya kufanya. Maumivu ya uzazi yalikuwa ni makubwa kwa mkewe kiasi cha kupiga kelele hafifu, akitarajia kupata msaada. Baada ya muda mrefu kupita bi. Nacharo alifanikiwa kujifungua peke yake akiwa chumbani kwake! Kwa ujuzi kidogo wa kidaktari kuhusu mambo ya uzazi, bwana Kimbe alifaulu kumzalisha mkewe. Hali hii ilileta unafuu kutokana na gharama za hospitali ambazo wasingeweza kuzimudu.

Walimshukuru Mungu kwa kuwapigania, lakini kukabaki jambo moja kubwa ambalo ni la lazima. Mama mtoto alihitaji chakula na mafuta ya kutosha kwa ajili ya uzazi. Hiyo ilimfanya Kimbe aende kusaka kibarua baada ya mapambazuka baada ya kumwandalia mkewe uji. Kwa ugumu wa aina yake maisha yaliendelea na mtoto aliendelea kukuwa japo kwa udhaifu sana. Mtoto huyu alikuwa wa Kiume ambaye walimwita Ramsoni. Ramsoni ni jina la rafiki yake bwana Kimbe waliyeonana nchini India wakati Kimbe akichukuwa kozi yake ya udaktari. Ramson na Kimbe walikuwa wanafunzi wote katika chuo hicho cha Udaktari.

Wote walikuwa wakichukuwa kozi moja katika kitengo cha mifupa na upasuaji. Walitokea kuelewana sana mpaka mwisho waliachana kwa masikitiko makubwa baada ya kumaliza kozi hiyo. Mwishowe waliishia kupeana anuani na kuahidiana kuandikiana barua. Waliachana uwanja wa ndege kila mmoja akipanda ndege ya kurudi kwao, Ramson alirudi kwao Uholanzi. Kimbe alikuwa daktari mzuri sana katika kitengo cha Moi katika hosptali kuu ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam. Kwa miaka mitatu mfululizo alifanya kazi hiyo kwa amani hadi siku aliyofukuzwa kazi yake, hii ilitokana na kusingiziwa kuchukuwa rushwa kwa mmoja wa wagonjwa wake.

Sheria ya hospitali hii ilikuwa kali sana juu ya wala rushwa, sababu hii ilimfanya Dr.Kimbe afukuzwe baada ya kupewa malipo yake ya NSSF. Malipo ambayo hayakukidhi mambo mengi, zaidi ya kujenga nyumba yake ndogo kijijini hapa. Shamba lake alilopewa na babu yake kwa upande wa mama yake, ndilo lililowasaidia kupata chakula kidogo.

Lakini kama balaa kwa upande wake mjomba wake alimnyang’anya shamba hilo,akitumia kisingizio kuwa hakuwa na haki ya kurithi shamba hilo, kwa kuwa yeye hana ukoo na upande huo wa ujombani. Hali hii ilimwacha mtupu wakati huo akiwa tayari ameoa mkewe huyo.Dr. Kimbe hakutaka kurudi kwa wazazi wake baada ya kufukuzwa kazi, kutokana na aibu juu ya kashfa yake hiyo na kuhofia hasira za baba yake kutokana na jinsi alivyomsomesha kwa gharama kubwa.

Babayake Dr.Kimbe alikuwa na fahari kubwa baada ya mwanaye kurudi kutoka nchini India akiwa na shahada ya udaktari kwa upande huo wa upasuaji. Sherehe zilizofanyika kijijini hapo kwa kumpokea mtoto wake vilimtofautisha na wakaazi wote wa kijiji chao. Baba yake Dr. Kimbe anaitwa mzee Kihedu ambaye aliishi katika kijiji cha Taabu yanini kilichopo nje kidogo ya mji wa Tanga katika njia kuu ya kuelekea nchini Kenya.

Watu wote kijijini hapo walimwonea wivu mzee Kihedu kwa kuwa na mtoto msomi na mwenye kazi yenye kipato kikubwa. Sherehe hiyo iliweka alama za wivu kwa baadhi yawanakijiji katika mioyo yao. Baada ya sherehe hiyo minong’ono ya masengenyo ilikuwa imetapakaa kila mahali katika kijiji hicho. Maneno kuwa mzee Kihedu na mkewe Bi. Namkunda walikuwa wakiringa yalikuwa ni mengi lakini hayakupatilizwa.

Mzee Kihedu alimtuliza mkewe asiyafuatilie maneno hayo kwani hayana maana. Wao walijua kuwa kumsomesha mtoto wao ulikuwa ni wajibu wao. Na kila mtu alipaswa kufanya hivyo kwa familia yake kwa ajili ya maendeleo yake. Hilo halikumtisha na alimtahadharisha mkewe kutofuatilia chochote juu ya maneno ya majirani zao kusudi wasijenge uhasama zaidi. Busara ya kunyamaza ilimfanya ashinde na kurudisha hali ya urafiki kwa wale waliojaribu kujitenga nao kutokana na wivu.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
53 featured Mtu wa Ufukweni Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni