Notifications
  • MWALIMU MKUU (3)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA TATUILIPOISHIA...chausiku alishangaa kuziona zile sale “JAMANI NANI KAKUPA MWANANGUU??!!”aliuliza chausiku kwa mshangao“Kaka juma”alijibu ramekiIKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“Oooh juma jamani mungu akubariki ooooh asante mungu”alitamka mama rameck uku akinua mikono juuRameck alizijalibu zile nguo hakika alipendeza sana adi mama ake alimfagilia kwa vigeregere “jamani juma mungu akuwekee…
  • MWALIMU MKUU (2)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA MBILIILIPOISHIA...“MUNGU WANGU YULE SI MZEE ALINANI???!!!”aliuliza chausiku kwa mshangao chausiku alimuangaria mzee alinani ambae amepoteza furaha yake ya kusomaMzee alinani alikuwa anakuja kuangaria bishala zake pale sokoni kwa kina chausiku.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Mzee alinani alistuka kumuona chausiku alikwepesha macho yake kwa aibu alitoka kwenye soko lile, chausiku alimpitia…
  • MWALIMU MKUU (1)
    Jina: MWALIMU MKUUMtunzi: __SEHEMU YA KWANZA“MAMA USIFE MAMA NITAISHI VP NA HII MIMBA MAMA”ilikuwa ni sauti ya mdada aitwae chausiku akimwambia mama ake asifee bado anamtegemea mama ake na mimba yakee“CHAUSIKU MWANANGU NAJUA MIMI NDIYO TEGEMEZI LAKOO NILIPAMBANA NA KILIMO ILI USOMEE LAKINI UMECHEZEA SHIRINGI CHOONI MWANANGU UMESHIKA MIMBA BADO MWAKA MMOJA TUU UMALIZE LAKINI NDO IVYO MWANANGU MIMBA NDO ISHAINGIA SINA BUDI KUKUFUKUZA INGALI UKO MOYONI MWANGU NAKUPENDA MWANANGU CHAUSIKUU ILA…
  • THE NIGHTMARE (9)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TISAILIPOISHIA...“mmenifananisha, mimi ndio kwanza naigia ofisini mida hii.” Aliongea yule afande na kuigia kituoni.“sasa aliyekuwa anatuhoji ni nani kama sio huyo?”Alijikuta anajiuliza mwenyewe swali lililompa utata mkubwa kichwani mwake.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wakati wakiwa hawajui hili wala lile, walishangaa kuona maaskari wakijazana pale na ambulance ikafika…
  • THE NIGHTMARE (8)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NANEILIPOISHIA...Walipofika feri, walipewa nahodha mwingine tofauti na yule aliyemuota na boti ilikuwa ndogo tu ya kawaida tofauti na ile aliyoiota.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Sharji alijikuta anapiga makelele baada ya kumuona Balqis akiwa amejaa damu mdomoni huku ametoa makucha yake akimfata kwa nia ya kumdhuru.“AAAAAAAAAAAGH”Sharji alipiga kelele na kukurupuka.…
  • THE NIGHTMARE (7)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SABAILIPOISHIA...“kha!!!!”Ulikua mshangao mkubwa kwa watu karibu wote baada ya kumuona Sharji akiwa na taulo akitoka chumbani kwa Balqis.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Wengine walicheka na kaka yake alionekana kutoifurahia hali ile.“sasa wewe unatutia wasi wasi bure, si ungesema tu kama unaenda kulala kwa huyu dada?” aliongea kaka yake na kukirudia kile chumba alichompangia…
  • THE NIGHTMARE (6)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA SITAILIPOISHIA...“toa loud speaker bwana.”Aliongea Balqis baada ya Sharji kubonyeza kitufe cha kupaza sauti.“kwanini hutaki nisikie maongezi yenu?” aliongea Karimu kwa sauti ya ukali kidogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...“kwani kuna ubaya mimi nikiongea private na mdogo wako?” alijibu Balqis baada ya kuisikia sauti ya Karimu.“hakuna ubaya.” Alijibu Karim kwa sauti ya…
  • THE NIGHTMARE (5)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA TANOILIPOISHIA...Alijikuta outomatic akijisemea kwa mshangao baada ya kumuona dada mmoja mrembo mwenye asili ya kiarabu akiingia mule ndani. Hakuvaa ushungi kama alivyowazoea kuwaona waarabu wengi ambao alikutana nao. Huyu alivaa suruali ya jeanz nyeusi na juu akiwa na kikoti chake cheusi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Kati kati kulikua na nguo Fulani nyeupe iliyonakshiwa…
  • THE NIGHTMARE (4)
    Jina: THE NIGHTMAREMtunzi: Hussein O MolitoSEHEMU YA NNEILIPOISHIA...Aliongea Khalidi na kuufungua mkanda wa suruali yake na kuanza kumtandika Karim.“unanipiga mimi?...utaona!”IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈ENDELEA...Aliongea Karim na kuondoka huku analia.*****************************Zilipita wiki mbili bila ya Karim kuonekana nyumbani kwao. Sabra alisikitika kidogo kutokana na kuwapenda sana watoto wake japokuwa huyo mtoto mkubwa hakuwa…
  • Fumanizi la Mchepuko Mwizi😂 | Comedy
    Mume amefuma viatu vya mchepuko wa mke wake mlangoni lakini akakosea kuingia ndani kabla aweke umakini kwenye hivyo viatu mwisho wa siku akaibiwa na vyake😂Hili tukio lazima lichukuchekeshe sana hata kama ulikuwa haujataka kuchekaItazame kisha nipe like na ukinipa maoni kwenye comment nitashukuru sanaUsisahau kubonyeza Subscribe kama haujajiunga na fungua #ChekanaZephiline kupata video zangu zote ambazo zipo mtandaoniNashukuru sana kwa wewe ambaye unanipa nguvu ya kuendelea kuwaletea kazi nzuri…

MTU WA UFUKWENI (3)

Mwandishi: Andrew Mhina

SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
“Sawa baba nawatakia usiku mwema baba na mama.” aliaga. “Asante na nyinyi pia.” Walijibu Mzee Kihedu na mkewe kwa pamoja. Walitoka Kimbe na mkewe na kuelekea kwenye nyumba yao iliyoko kama mita mia mbili kutoka Nyumbani kwa Mzee Kihedu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Mapambazuko ya siku hii yaliambatana na mvua za hapa na pale. Hali ya hewa ilikuwa hairuhusu kwenda kokote, lakini kutokana na kazi nyingi za muhimu ililazimu Dr. Kimbe atoke na mkewe kwa ajili ya kusimamia uchimbaji wa kisima. Baada ya hapo alipanga kwenda Mtimbwani kuwaangalia vibarua wa shambani, kama wamemaliza kazi yao. Ramson naye alipenda kuambatana na wazazi wake japo alitakiwa aende kwa babu kutokana na hali ya mvua. hawakutaka kumlazimisha kubaki kwa babu kutokana na msimamo wake.

Baada ya kufunga milango ya nyumba waliondoka na kuelekea taratibu njia iendayo shambani kwao. Mazungumzo ya hapa na pale yaliwafanya waingie barabarani kutaka kuvuka kwenda ng’ambo ya pili bila kuangalia. Mara walisikia sauti ya Ramsoni akiita “mamaaa babaaa gariiiiiiiiii!!!”… Wakati wanageuka ili kumwangalia Ramson walikumbana na gari na mizigo likiwa hatua tatu mbele yao.

Milio ya breki za gari hilo iliwachanganya wakashindwa kufanya lolote na mwishowe gari hilo liliwagonga vibaya! Dreva wa gari hilo alijaribu kwa bidii zake zote kuwakwepa lakini kwa sababu ilikuwa kwenye kona hakuweza kuwaona wakiwa mbali, bidii zake zote hazikufua dafu badala yakealiishia kuwagonga na gari ikaserereka na kugonga mnazi kisha likazima.

Dreva aliteremka kwenye gari na kumkuta mtoto amewakumbatia wazazi wake wakiwa wametapakaa damu na sehemu nyingine hazitazamiki. Kelele zile za gari na Sauti za hamaki viliwavuta watu wengi kijijini. Wapita njia na wanakijiji walikusanyika kwa haraka na kuja kushuhudia ajali ile mbaya.

Kwa haraka walimwondoa mtoto Ramson juu ya miili ya wazazi wake alikuwa analia kwa uchungu mkubwa. Mwanzoni walifikiri kuwa na yeye pia aliumia kwa jinsi alivyotapakaa damu lakini baadaye wakagundua kuwa alikuwa hajaguswa popote. Walimweka kando na kukusanya maiti zile na kuita gari ndogo kwa ajili ya kuzipeleka Hospitali ya mkoa. Mzee Kihedu na mkewe walipata taarifa ya ajali hiyo wakiwa njiani kuelekea kwenye shamba lao la minazi. Taarifa kuwa Kimbe na mkewe walikuwa wamepoteza maisha viliwachanganya akili na kuwatesa sana moyoni.

Ilikuwa ni halaiki ya watu katika msiba huo. Watu walikuwa wakikanyagana katika eneo la mazishi. Magari yalijaa katika maeneo mbalimbali, marafiki wengi walioko pande mbalimbali walihudhuria baada ya kupata taarifa za Msiba huo wa kusikitisha. Vilio vya maombolezo vililipuka mara tu baada ya kuyaona makaburi, yaliyochimbwa karibu karibu kwa ajili ya Kimbe na mkewe Bi Nacharo.

Ilisikitisha sana lakini kila mmoja alikubaliana na matokeo hayo kwa sababu kazi ya Mungu haina makosa siku zote.Mchungaji Tito alikuwa akitoa mahubiri kwa watu waliokuwa mazishini, kulionekana kukiwa na utulivu wa hali ya juu Isipokuwa vilio vya hapa na pale vya akina mama.

“Ndugu zangu ni kweli kabisa msiba huu umetupa huzuni nyingi sana, kwani umemgusa kila mmoja wetu. Bwana Kimbe na bi Nacharo walikuwa ni watu wema sana na wenye ushirikiano na kila mtu hapa kijijini. Lakini tukiangalia Maandiko Matakatifu yanasema kuwa, Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi sio nyingi. Nazo zimejaa taabu. Ukweli wa maneno haya unadhibitika kila siku, watu wanakufa. Hii inaonyesha kuwa dunia hii sio ya kutegemea sana. Sio mahali pa kuishi milele. Tukiangalia vizuri maandiko yanatuonyesha kuwa mbele yetu kuna njia mbili. Njia ya kwenda mbinguni na njia ya kwenda jehanum. Njia hizi zote zinategemea uchaguzi wa mtu mwenyewe. Ukichagua kwenda mbinguni utaishi katika maisha ya kumcha Mungu. Utajiepusha na mambo mabaya na kutenda mema kwa msaada wa Mungu.

Kwa hiyo kila mmoja ajue kuyatengeneza maisha yake kabla hajapatwa na mauti kama ndugu zetu hawa.” Alisema Mchungaji Tito katika mahubiri yake. watu wengi walikuwa wametulia kimya wakisikiliza hotuba hiyo. Mchungaji anawataka ndugu wa karibu wawasindikize marehemu, kwa kutupa mchanga kila mmoja kwa zamu katika makaburi yote mawili.

Alifanya hivyo ili kukomboa wakati kwani makaburi hayo yalichimbwa katika eneo moja. Baada ya zoezi hilo Mchungaji alichukuwa mchanga kiasi na kutupa ndani ya kaburi huku akisema maneno haya:“Umetoka mavumbini na mavumbini umerudi,Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake libarikiwe. kisha akafanya hivyo kwa kaburi la Bi Nacharo, mwishowe akamalizia kwa sala maalumu Hatimaye ibada ya mazishi iliishana watu walitawanyika.

Mzee Kihedu na mke wake pamoja na Mjukuu wao Ramson walibaki na majonzi makubwa sana. Kubembelezwa hakukufaa kitu kwani Kimbe kwao ndiye aliyekuwa kila kitu. Alikuwa ni mtoto wao wa Pekee ambaye walimtegemea kusimamia mali walizokuwa nazo. Lakini mwisho wa yote walikubaliana na ukweli kuwa Mungu amewapenda zaidi. Walijikusanya tena kuweza kuendelea na maisha ya kawaida. Hali ilikuwa tofauti kwa Ramson kwani vifo vya wazazi wake aliviona kwa macho yake mwenyewe. Mara kwa mara aliota hali hiyo na wakati mwingine ilimjia katika mawazo yake kana kwamba inatokea sasa hivi. Majonzi yake hayakuisha mapema maana alikumbuka kila saa upendo wa wazazi wake.

Babu yake na bibi yake walimfanya asiwaze kwa kumtendea mambo mazuri ya kumshangaza kila wakati,kusudi asahau msiba ule lakini haikusaidia sana. Alizidisha Utulivu kwa kutafakari kwa kina mambo yaliyomtokea. aliwapenda sana babu na bibi yake. Walichukuwa nafasi ya wazazi wake lakini bado pengo lao lilikuwa wazi kabisa siku zote.

Pamoja na yote hayo aliendelea vizuri na masomo yake ya Chekechea, mwaka uliofuata alitarajiwa kujiunga na darasa la kwanza katika Shule iliyokuwepo kijijini hapo. Alikuwa na akili katika masomo yake na pia alikuwa na kipaji maalumu cha kuchora akiwa katika umri huo mdogo. Babu na bibi yake walimfurahia sana. Waliishi naye kama mtoto wao na sio mjukuu. walikuwa wanamchukulia kama Kimbe wao aliyefariki ghafla kwa ajali.

Ilianza kama mzaha sana unaoumiza moyo. Mzaha wa kitoto uliofanywa na watoto wenyewe wakati wa michezo yao ya kitoto: “Mwizi”! hayo ni maneno yaliyotamkwa na mmoja wa vijana kwenye kundi moja lililojadili unadhifu wa Mmoja wao kijijini hapo. Kila wakati vijana hao waliumiza vichwa vyao kutafuta nini cha kufanya ili wamharibie kijana huyo mpole na mwenye bidii.

Mioyo yao iliuma kwa wivu juu ya maendeleo ya Kijana mwenzao. Hali ya uvivu ilishamiri kwa baadhi ya wakazi wa kijiji hicho. Wengi walipokea urithi kutoka kwa wazazi wao na babu zao mashamba makubwa ya Minazi. Kwa hiyo hawakuona haja sana ya kushughulika na kazi za mikono zaidi ya kuwa na vishamba vidogo tu vya kulima mazao ya kukithi mahitaji ya chakula.

Wengi walikuwa wakikaa tu vijiweni na wengine kwenye vilabu vya pombe ya mnazi na kucheza bao, huku wakingojea kuvuna nazi tu zinapokomaa. Tabia ya wazazi ikachukuliwa na watoto wao kizazi hadi kizazi mpaka ikazoeleka. Mazoea haya ya kukaa tu na kucheza kwa kutegemea kurithi mali za wazazi ambao nao walirithi toka kwa wazazi wao ilifanyika kama ugonjwa. Hali hii iliwakumba hata wale ambao hawana kitu cha maana cha kurithi pindi wazazi wao wanapoondoka katika dunia hii.

Ugonjwa huu wenye jina maarufu lijulikanalo kama “Uvivu” liliwafanya vijana wote wakae tu vijiweni bila kazi. Hali hii haikukemewa na wazazi wao kwa sababu nao pia walikuwa hivyo hivyo. Kutokana na kukaa bila kazi tabia nyingi huzaliwa. Tabia ya kukaa vijiweni zilizaa maovu mengi sana yakiwepo utumiaji wa bangi, hatimaye madawa mengine ya kulevya. Tabia hizi nazo zikazaa udokozi na hatimaye wizi wa mifugo, ubakaji na mambo mengine kama hayo. kwa ujumla vijana wengi wakawa na magenge ya siri.

Magenge yaliyosababisha maovu mbalimbali kijijini hapo na vijiji vya Jirani. Lakini katika kijiji hiki aliishi kijana mmoja aliyekuwa tofauti na wengine. Kijana huyu si mwingine ila ni Ramson Kimbe! Upole wake na uchapa kazi vilimfanya awe tofauti kwa kila kitu. Umaridadi wake katika mavazi na maendeleo yake katika masomo, pamoja na mafanikio ya familia yake, vilimfanya awe tofauti sana. Kijana huyu ambaye anaishi na babu na bibi yake alikuwa na msimamo wa maisha yake binafsi.

Hakuridhika na mali za babu yake, japo alijua kuwa yeye ndiye mrithi wa mali hizo. Kutoridhika kwake kulimfanya azidishe bidii kwa masomo yake na kazi za shambani. Japo alikuwa na umri mdogo lakini alijitahidi kufanya kazi mbalimbali akisaidiana na babu yake. Alikuwa na mashamba yake mwenyewe aliyoyasimamia kwa kuyalima na kuweka vibarua, kazi ambayo babu yake alimsaidia.

Akiwa darasa la tano alikuwa ni kinara kwa umaridadi shuleni kwao na katika masomo alikuwa akiongoza pia. Umaridadi wake na ufahamu mkubwa katika mambo mbalimbali, vilimfanya apendwe na waalimu na watu mbalimbali kijijini hapo. Sifa zake hizo zilimfanya pia kupata maadui wengi wakiwepo vijana wenzake na watu wazima, waliokuwa na husuda kutokana na maendeleo yake.

Mambo haya yote yakifanyika bila yeye kujua lolote. Maisha kwake yaliendelea kama kawaida. Aliendelea kupanda na kuwa zaidi ya jana kila siku kutokana na mafanikio yake. Hakutaka kukaa vigenge wala majungu, kutokana na tabia yake hii alikosa marafiki kabisa. Vijana wengi walikuwa wavivu sana na wenye tabia mbaya. Kila aliyejaribu kuwa rafiki yake alimshauri kufanya kazi kwa bidii, ili kutengeneza hali ya maendeleo kwake binafsi na kijiji chao. Alipenda sana kuangalia maisha yajayo na kwamba matayarisho ya maisha bora ya sasa na ya baadaye yanamhitaji mtu mwenyewe.

Bidii na ubunifu kwa kazi ni sehemu ya maendeleo hayo yanayotamaniwa na wengi. Sera zake hizo zikaonekana kama Hadithi za ajabu kwa vijana wa rika lake, kwani walijua majukumu yote kwa umri wao yanabebwa na wazazi wao. “Kujitwisha majukumu mazito ya kufikiria maisha ukiwa mdogo, ni kujibebesha mzigo usiokuhusu.” Hayo ni baadhi ya maneno ya marafiki za Ramson waliokuwa wakimshauri apunguze harakati zake za kuyasaka maisha bora. Umri wake ukilinganishwa na mambo aliyokuwa akiyafikiria waliona kuwa havikulingana kabisa na yeye.

Pia ukichukulia kuwa Babu yake mzee Kihedu alikuwa ni tajiri wa mashamba na mifugo. Mali zote alizokuwa nazo Mzee Kihedu zote zilikuwa za Ramson, kwakuwa Mzee huyo hakuwa na mtoto mwingine zaidi ya baba yake Ramson ambaye ni marehemu kwa sasa. Hata babu yake alikuwa akimshauri atulie na kuangalia masomo tu kwa kuwa kila kitu kipo sawa ila Ramson aliendelea na msimamo wake na bidii katika mashamba hasa kusimamia na kufanya kazi.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
53 Mtu wa Ufukweni Simulizi Z53
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni