SITOISAHAU FACEBOOK (22)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mwandishi: Emmy John Pearson
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Hilo halikuniumiza kichwa sana, maana niliamini naweza kusimama cha msingi nia yangu kutimia. Kilichoniumiza kichwa ni hawa wenzangu. Itakuwaje!!Nilimshukuru yule bwana. Akanipatia namba yake ya simu. Ni hapo nilimtambusa jina lake aliitwa Saidi.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Ukinipigia simu we niite Side boy.” Aliniambia wakati ananiaga.Alinipatia kiasi kingine cha pesa.Nilishukuru kwa kuzaliwa mwanamke maana bila hivyo sidhani kama ningepata msaada.Jioni ilipofika. Jesca hakuwa ameambulia lolote. Na Sam hadi wakati huo hakuwa amerejea. Tukajipa moyo kuwa huenda amefanikiwa kupata kibarua chochote huko alipo. Ikafika giza nab ado Sam hakuwa amerejea. Hofu ikaanza kutuingia na kuamini kuwa Sam anaweza kuwa aliongea Kiswahili na kugundulika kuwa ni mtanzania asiyekuwa na uhalali wa kuishi Zambia.
Hatukujua kuwa ni wapi tuanzie kumtafuta. Kama tukisema twende polisi na sisi tutakuwa matatani. Tatizo jipya!!Jesca na Jenipher wakawa wananisikiliza mimi.Kimya kikatanda!! Makundi mengine hayakujua nini kinaendelea.Nilijiuliza maswali mengi sana bila kupata majibu. Samson amefanya jambo gani la kitofauti hadi wakati huu hajarejea.Au amerejea tena katika kijiji cha Dokta Davis. Niliwaza peke yangu bila kumshirikisha mtu yeyote hisia zangu.Saa nne usiku nilikuwa nimepitiwa usingizi.
Nilisikia kama natikiswa nikadhani ni Jesca amejigeza lakini nilikuwa naendelea kubughuziwa. Japokwa nilikuwa nimelala chini niliutamani usingizi.Nilijikaza nikafumbua macho.Usingizi ukakatika palepale. Alikuwa ni Sam!!“Bella!! Bella!!” alinong’oneza. Nikamtazama usoni nikahisi kuna nhali ya tahadhari. Nikajipa utulivu wa lazima.Akanishika mkono akaninyanyua. Akanivuta pembeni kidogo.“Ulikuwa wapi Sam.”“Bwana Mkubwa!!.”“Kafanyaje…ndio nani?” nilitaharuki.“Sio mtu ni sehemu inaitwa hivyo.”“Pamekuwaje…”“Nimekutana na mtu!! Aah!! Nimemuona mtu….amepata madini.”Bado sikuweza kumuelewa Sam anamaana gani. Nikamuomba anielezee kwa kirefu.
Akanieleza juu ya mgodi wa Bwana Mkubwa ambao upon je kidogo ya mji wa Ndolla. Mgodi huu alipoutaja tu! Sikuwa na swali lolote. Nilikumbuka somo la Historia kidato cha pili hadi cha tatu. Mgodi huo ukanikumbusha madini hadimu ya Risasi (Copper) ambayo hupatikana kwa wingi katika nchi ya Zambia. Hasahasa Ndolla.Sam akaendelea kunielewesha. Na sasa akanigusia juu ya bwana ambaye amepata madini hayo siku hiyo.
“Kwa hiyo ulikuwa huko.”Akanijibu kwa kutikisa kichwa juu na chini akimaanisha kuwa ni kweli alienda ‘Bwana Mkubwa’.Samson alikuwa amekuja na habari ambayo mwanzoni nilikuwa ninapingana nayo lakini hatimaye kulingana na shida tuliyokuwanayo nikaamua kukubaliana naye. Wizi!Samson alinihakikishia huyo bwana ana pesa nyingi sana. Amefuatilia nyendo zake hadi alipofanikisha kuyauza yale madini.“Alinipa lifti kwenye gari yake. Nilijifanya sijui lolote lile. Aliponishusha mjini nikamfatilia na kumuona aliyauza.”“Sasa tunampata wapi?”
“Yupo anakunywa pombe sasa hivi. Ni hapo pekee pa kumkamatia.” Alinisisitiza.“Nzuri zaidi ni mtanzania…” alinisisimua kwa kauli hiyo. Nikamwomba Mungu huyo bwana asiwe na tabia za kitanzania bali awe mbongo.Nilitulia kwa dakika chache kisha nikamuamsha Jesca. Hakunisikia. Nikapekua huku na huko. Nikachukua mafuta. Nikaenda bafu za kulipia nikaoga. Nikajipaka mafuta. Nikavaa kanga moja.Samson akawa kioo changu akakiri kuwa kwa namna ile lazima anitamani.Samson akaniongoza hadi nikafika eneo la tukio.
Jirani na bwana huyu palikuwa na kiti kipweke ambacho hakikuwa na mlevi aliyekikalia. Nilikitoa upweke nikajiweka juu yake.Haraka akafika muhudumu wa kizambia, mweusi na mbaya kumtazama. Nikaagiza soda.Meza yangu haikuwa mbali sana na yule bwana ambaye Samson alinielekezea. Nilikunywa soda taratibu huku nikiisoma akili ya yule bwana aliyepata bahati ya kupata madini Bwana mkubwa.“Yaani wahudumu wengine nao….ona sasa.” Nilizungumza kwa hasira. Kama najiongelesha. Sauti ikamfikia mlengwa ambaye ni yule bwana anayekunywa pombe.
Akajileta mtegoni.Akasogeza kiti karibu nami.“Wewe ni mtanzania kumbe..ama unaibiaibia Kiswahili. Nimefurahi kukusikia ukisema Kiswahili.”Nikatabasamu, nikalegeza jicho kimaksudi.“Yeah! Mtanzania halisi…..na wewe je?”“Mimi ndio orijino kabisa.” Alijibu. Nikacheka tena.“Dah!! Miezi miwili sijarudi nyumbani aisee. Maisha haya.” Nililalamika.“Aaah! Mimi kila wiki huwa naenda aisee.”Maongezi yakawa maongezi. Kama bahati alinipendelea vile. Yule bwana alikuwa na tabia za kibongo. Akaniingizia mada za mapenzi.Sasa nane usiku tukawa tunatafuta chumba kwa ajili ya kutimiziana haja. Yeye akinitaka kimwili na mimi nikimtaka kipesa.
Alilipia chumba cha bei ghali sana. Nilimshuhudia wakati anauacha mkoba wake mapokezi. Nikagundua mchezo unataka kuharibika.Nikajipa moyo. Nikaenda hadi chumbani!!Hapakuwa na jipya huko. Mzee huyu mwenye matamanio. Alinivagaa na kuanza kunisumbua huku na huko. Sikuwa na hisia hata kidogo. Niliwaza pesa tu.Nilipomtazama umri wake nikagundua huyu hana lolote la kuweza kunishinda. Akili ya maajabu ikanivaa, nikajikuta nimevamiwa na wazo kuwa kama nisipokuwa makini naweza kutumika kimwili na nisipate chochote kile.
Nikaamua kutumia nafasi moja tu kusawazisha mambo haya!!!Pata potea!!“Mh!! Hauna kinga?” nilimuuliza baada ya kuwa nimempelekesha akalegea kabisa macho yake na nikajua kuwa alikuwa anahitaji mwili wangu.Ni hapa nilikuwa napahitaji.“Sina mpenzi wangu…njooo tu hivyo hivyo” akajibu. Nikamtukania mama yake kimoyomoyo kwa ujinga aliozaa.Nikasimama. Nikamtazama kwa jicho la kimapenzi huku moyo wa chuki ukimtusi. Ubongo unaohitaji pesa nao ukifanya kazi kwa bidii kubwa.
“Ngoja niende kuchukua mpenzi wangu, naogopa mimba mwenzako, ujue nimeolewa eeh!!” nilimlaghai. Akaingia mkenge. Nikachukua upande wangu wa kanga, nikashusha ngazi mpaka mapokezi.Nikamkuta mwanadada mweupe akiwa ameuchapa usingizi.“Nipatie mkoba wa mzee!!” nilimwambia huku nikiwa nimetega mkono!! Moyo ukiwa hauamini kama nitafanikiwa.“Mmm. Hapana mwambie aje mwenyewe dada, hajaturuhusu kumkabidhi yeyote zaidi yake.” Alinipinga yule dada kwa kingereza chake kibovu kisha akaendelea kuuchapa usingizi.
Nilitamani sana kumrukia nimkabe. Lakini alikuwa ametenganishwa na nondo. Nisingeweza hata kumgusa.Niliondoka pale nikiwa nimetaharuki sana, mpango ulikuwa unakaribia kushindikana sasa, na asubuhi inayofuata nilitakiwa kusafiri kuelekea Mbeya.Nikapanda hadi juu kule chumbani nikaufungua mlango kwa ghadhabu kubwa.Yule bwana akashtuka.“Ndio ujinga gani huu huku Zambia I hate such embarrassment!!” nililalamika.“Nini tena mamito.” Aliniita kimapenzi akiwa amelegea.“Yaani hadi kuchukua kinga I need to go with you!!”“He!! Wamekunyima?” aliponiuliza swali hilo, nikajikuta Napata nafasi ya mwisho.
“Fanya hivi naomba umpigie umwambie anipe!! No discussion!!” niliwaka, zile hasira za kutaka kuikosa pesa ile zilikuwa zimenipanda.Mbongo akachukua simu akainyanyua. Nikaomba mizimu yote asije akasemam maneno mengi kwenye simu.“Halo!! Chumba namba 12….mpe huyo dada nilichomuagiza…na muache mambo ya kipumbavu” akakoroma kwa kiingereza kilichonyooka. Kisha akakata simu kwa hasira.Sikusema neno!! Nikafungua mlango, nikatoka.Nikiwa nimeukunja uso kwa ghadhabu nikafika mapokezi. Yule dada usingizi ulikuwa umekatika!! Tukatazamana!!
Yeye anaogopa na mimi naogopa!!!Maskini yule dada bila kujua kwamba ameambiwa anipatie kinga. Akadhani yule mbongo amemaanisha ule mkoba. Akaniomba msamaha kwa kila namna kisha kwa ukarimu kabisa akanipatia ule mkoba. Ulikuwa mzito kiasi. Nilipotaka kuondoka yule dada aliyekuwa amejikita katika kutafuta anachojua yeye, aliniita, nikageuka na kumshangaa kidogo.“Unatakiwa kuweka sahihi.” Alinielezea kwa ukarimu. Nikaona kama huyu binti ana nia mbaya na mimi. Nikabaki wima najiuliza iwapo niende mbele ama nirudi. Tukatazamana kwa sekunde kadhaa. Nikaona isiwe tabu. Nikarejea nikachukua kalamu niweze kuweka sahihi. Mara nikasikia fujo za mlango kufunguliwa.
Nikaomba Mungu usiwe mlango wa yule jamaa mbongo. Kisha nikasikia hatua kubwa kubwa zikitambaa.“How long does it take to…to…..hell..” (Inachukua muda gani ku…ku…. ). Ilisikika sauti yenye kitetemeshi cha hasira. Alikuwa yule mbongo.Sasa badala ya kuweka sahihi nikabaki kulishikashika tu lile daftari na kalamu. Mkojo ukatoka safari yangu ya mbali na sasa ulikuwa unahitaji kutoka. Nikabana miguu yangu!! Mkoba mkononi.
Ninafumaniwa Isabela mimi!!Nikataka nikimbie!! Miguu ikawa mizito. Sikuwahi kufanya kitendo cha wizi hivyo lazima hali kama hii ingenitokea.ingenitokea.“Iam sorry boss..i have already given her (samahani mkuu..nimempatia tayari.)” yule dada wa mapokezi alijitetea kwa uoga.Mara vile vishindo vikasita.Yakafululiza matusi ya nguoni kutoka kwa yule mlevi wa kibongo.Hapo sasa nikaangusha saini yangu.Narudi vipi na ule mkoba sasa!! Nikajikaza nikaanza kuondoka.Nilipogeuka nikakutana na kosa ambalo nililitegemea. Yule dada wa mapokezi alikuwa amebonyea chini tena.
Asante! Nilimshukuru kwa kitendo hicho.Ghafla nikabadili uelekeo. Nikaelekea katika vyoo.Upande huu, nikaambaa na korido hadi nikaufikia mlango wa kutokea. Nikamuachia tabasamu mlinzi aliyekua kwa nje na yeye akatabasamu. Tabasamuu la kizee. Kisha nikatoweka. Nikapiga hatua kwa hatua hadi nikalifikia geti kuu la kutokea. Hapa nilitakiwa kuandika jina. Nikaandika jina lililokuja kichwani mwangu lakini sio jina sahihi.Geti likafunguliwa. Mimi na mkoba wangu. Nikatoka.
Nilipogeuka nyuma nikakutana na maneno mazuri ya kupendeza.The Savoy Hotel12 Buteko AvenueNdolaZambiaHaya hayakuwa yananihusu. Niligeuka na kutazama mbele. Nikaanza kutokomea. Nikashtuliwa kwa kuguswa begani.Nikageuka upesi nikaikuta amani ambayo nilikuwa naihitaji.Samson…jemedari wa kisukuma.Akanikumbatia kunipongeza. Lile joto lake likanikumbusha mengi. Nikapuuzia.Oparesheni ilikuwa imekamilika.
****Pesa zilikuwa kwa mafungu yanayolingana. Zilikuwa zinang’ara kuonyesha kwamba hazikuwa zimepitia mikono mingi.Ilikuwa saa kumi alfajiri. Sasa nikiwa pamoja na Samson tulipita katika vijiwe ambavyo wenzetu walikuwa wanalala. Wote wakaamshwa. Hatimaye tukawa na mkutaniko wa pamoja wa kwanza tangu tuwe katika ardhi ile.Niliwakumbusha juu ya ahadi yangu!! Sasa ilikuwa imetimia.Hakuna aliyekuwa anafahamu thamani ya kwacha ya Zambia katika shilingi ya kitanzania. Hilo halikutupatia shida. Nikawachukua wenzangu watano wa kwanza. Nikaliendea basi linalotoka Ndolla kuelekea Mbeya mjini.“Kwacha ngapi?” niliuliza.
USIKOSE SEHEMU IYOFUATA
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni