Notifications
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (17)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na Wafuasi wake…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (16)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea mlio ule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (11)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MOJATULIPOISHIA...“Orion,” Seidon akamwambia Amatagaimba huku akikimbia. Amatagaimba akasimama na kugeuka nyuma huku tayari akiwa na upanga wake mkononi, Seidon alizidi kukimbia bila kutazama nyuma. Amatagaimba alipigwa kikumbo kikali kabla hajautumia upanga wake, kwani kasi ya Yule farasi alishindwa kabisa kuidhibiti kwa upanga wake huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (10)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMITULIPOISHIA...akaeuka ghafla na kukaa upande wa Seidon tayari upanga wake ulikuwa umekwishaondoa kichwa cha Yule jamaa, vurugu ikazuka kati ya watu wale na akina Amatagaimba, mapigano makali yakazuka, kila walipowakata kata na panga zao wale watu walizidi kuwa wengi na makelele yao yalikuwa yakiwasumbua masikio ya Amatagaimba na Seidon.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (9)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA TISATULIPOISHIA...“Seidon, hapa kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon, akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon, unawaza nini?” akamuuliza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata tamaa,” Seidon alijibu.“Usikate tamaa, hakikisha unafika…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (8)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA NANETULIPOISHIA...Amata ga Imba alipoona giza hilo akajua kumekucha, akapiga mbinja kali na muda mfupi tu, farasi wale wawili walikuwa tayari wamefika, Seidon akarukia juu ya mmoja wapo na Amata vilevile kisha wakapiga mbio kuelekea upande wa kusini. Nyuma yao jeshi lilikuwa likija kwa kasi na farasi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Amatagaimba! Wanatufuata….” Seidon alipiga…

SITOISAHAU FACEBOOK (23)


SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Hakuna aliyekuwa anafahamu thamani ya kwacha ya Zambia katika shilingi ya kitanzania. Hilo halikutupatia shida. Nikawachukua wenzangu watano wa kwanza. Nikaliendea basi linalotoka Ndolla kuelekea Mbeya mjini.“Kwacha ngapi?” niliuliza.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Akanijibu. Nikalipia nafasi za watu watano.Wakaingia garini. Kiongozi wao akiwa JescaNikarejea na kuwachukua wengine. Hawa kiongozi wao akawa Jenipher.Kundi la nne nikalikabidhi kwa Samson.Kisha nikabakisha kundi lililosalia mikononi mwangu.John!! Akiwa ameambatana nami!! Nilichukua siti ya watu wawili. Nikamuweka John kisha nikambebesha mfuko fulani.Hakuruhusiwa mtu kukaa pale.Safari ikaanza huku maelekezo yota ya tunakutana vipi yakiwa kwa viongozi wa msafara.Hatimaye tukaiacha Ndolla majira ya saa kumi na mbili. Safari ya kurejea Tanzania.

*Pesa zilibaki nyingi sana. Hivyo tuliamini kabisa hakuna kitakachoharibika. Jesca alikuwa na akiba yake, Jenipher na Samson vilevile.(Mshikemshike )TUNDUMA, Mbeya.Mji ulikuwa umetulia sana. Hapakuwa na harakati za hapa na pale. Ilinishangaza sana kwa boda kama hii kuwa katika utulivu huu.Tulikuwa tukihangaika kutafuta mahali pa kulala. Nyumba za kulala jirani na kituo cha mabasi zilikuwa zimejaa. Hivyo ilitulazimu kidogo kuzunguka. Hatukupata mahali pa kulala kwa wingi tuliokuwa nao. Sasa tuliamua kuishi maisha yetu ya Zambia. Tukaamua kulala katika stendi ya mabasi.

Baada ya kufikia uamuzi huo. Sasa mwenye kutafuta chakula aliruhusiwa lakini pa kulala tulikuwa tumeamua kabisa ni hapo hapo stendi.Wanaume watatu waliamua kusindikizana kwenda kutafuta chakula.Mkuu wa msafara huo Jesca aliwapatia pesa wakatoweka kwa ahadi ya kurudi upesi.Ahadi ikavunjwa maradufu!! Hawakurudi.Hadi tuliposinzia. Haikuwa kama yaliyomkuta Samson kule Ndola. Hawa hawakurudi kabisa.Kesho yake. Tulipotoa taarifa polisi tulikutana na taarifa ya vifo vya watu watatu kwa kukatwa na mapanga.

Walikuwa wenzetu!! Lakini hatukukiri!! Hatukuhitaji kuwa karibu kabisa na polisi. Kwa kifupi hatukuwa tunajua hatma yetu. Hasahasa mimi ambaye nilikuwa na siri nzito.Baada ya taarifa hizo kutapakaa. Tukajua nini kinachoendelea ndani ya mji wa Tunduma. Majambazi wa ajabu walikuwa wameuvamia mji. Hawa walikuwa na hadhi ya kuitwa majambazi wastaarabu. Walibandika matangazo kabisa kuwa kama mwanaume anatembea usiku basi awe na tahadhari aidha simu ama kiasi cha pesa shilingi. Elfu hamsini lakini bila hilo wakikutana ama zao ama zake.

Kumbe ndicho kimewasibu wenzetu!! Nilisikitika kuzipoteza roho hizi.Asubuhi hiyo nilitaka kwenda kubadili pesa. Lakini bahati mbaya sikuwa na kitambulisho chochote. Nikaitupa kazi hiyo kwa Samson. Akazunguka mtaani kuzibadili baada ya kugundua kuwa Kwacha moja ni sawa na shilingi 0.3 ya kitanzania.Baada ya zoezi lile kukamilika na kupata pesa ya kutosha sasa kila mmoja alitakiwa kuubeba mzigo wake mwenyewe. Aliyesema kuwa anaishi Dar alipewa nauli aondoke zake, wa Arusha naye vilevile. Na pesa ya ziada kila mmoja alipewa.

“Muutangaze ushuhuda huu bila kuipunguza wala kuongeza neno!” niliwaambia wakati tunaagana. Kila mmoja alikuwa na furaha huku wakiniona mimi kama Mungu wao. Sikujali sana!!Safari ya Mwanza tukabaki watano. Mimi, Jesca, John, Jenipher na Samson.Siku ya safari kama ilivyo kawaida nikalipia siti ya watu wawili, Jesca na Jenipher wakakaa siti moja huku Samson akikaa peke yake.Alama ya John shingoni ilinikwaza sana. Nilitamani aweze kutuona. Lakini alikuwa anauona ulimwengu wake mwenyewe.Safari nzima ilikuwa tulivu sana. Nilikuwa natafakari mambo mengi sana. Nilitamani kwenda Makambako kwa mama lakini niliamini haukuwa wakati sahihi.

Nilihitaji nkujua kitu kuhusu Maria. Maana alinitokea kule porini siku ya kwanza kabisa na kamwe sikumuona tena.Nini kilimsibu? Nilijiuliza.Tulipita miji mbali mbali. Tukaipita Makambako, nikainama nikajifuta machozi, tukaiacha Mafinga, tukaingia Iringa mjini. Na hapa hatukusimama sana tukaendelea na safari.Sasa gari lilisimama!! Hatukushangaa sana. Tulidhani ni kwa madhumuni ya kuchimba dawa. Lakini hatukuiona dalili hiyo.Dereva akateremka. Akaangaza gari lake bila kuona tatizo.Akaangaza tena. Hakuna tatizo.,Msaidizi wake naye akashuka. Hakuna msaada!!

Wakashuka mafundi wakajaribu kugusa hapa na pale. Gari lilikuwa limezima.Walijaribu kufanya kila wanaloweza lakini hapakuwa na matumaini. Dakika zikaanza kwenda. Masaa yakaenda. Hatimaye jioni.Abiria wakashindwa kuvumilia. Wakatoa matusi mengi lakini haikusaidia. Gari halikuweza kuwaka.Duh! Leo tunalala njiani!! Nilimweleza John japo hakunisikia.John alichoweza kuona ni chakula na mengineyo lakini si watu!! Na watu halisi pia hawakuweza kumuona yeye.

Simu ilipigwa ili gari jingine liweze kuja kutuchukua. Basi lilifika likiwa na abiria wengine. Likazimishwa ili tuweze kubananishwa wote twende Dodoma. Abiria walilaani kitendo kile kwa lugha zote, huku wakilalamikia usalama wao.“Kama hutaki basi hili hapa lala utasafiri kesho!!.” Zilikuwa kauli ngumu kutoka kwa mpigadebe. Hakuna aliyependezwa na kauli hiyo. Wakati huu sikuweza kukaa na John badala yake tulikuwa tumesimama. Ni Jesca pekee aliyepata nafasi ya kukaa. Yalikuwa mateso.

Walipofanikiwa kutubananisha kama viroba. Dereva akisifiwa na wapambe wake akaingia garini aweze kuendesha tuondoke.Ikaanza tena kama utani, akachokonoa kwa mara ya kwanza likagoma, akajaribu mara ya pili bado hali ileile.Akajaribu tena na tena. Injini haikuweza kuwaka. Kila mmoja akawaza lake. Watu wakakimbilia kwenye imani za kishirikina.Lakini huyo mshirikina ni nani? Hakuna aliyejua.Abiria wakashuka. Kila mmoja akarejea kwenye basi alilokuwa amepanda awali. Hapakuwa na safari tena.

Usiku ukafika wanakijiji wakapika chakula na kutuuzia kwa bei mbaya sana. Hatukuwa na ujanja tukanunua.Saa nne usiku mambo yakananza kubadilika. Hali ya hewa ilibadilika na kuwa ya kushangaza hata wanakijiji walikiri kuwa hiyo haijawahi kutokea. Badala ya baridi kali la Iringa sasa lilitanda joto.Joto hilo ni kama lilimshtua John. John akasimama akataka kuondoka. Nikamzuia. Akawa anatumia nguvu!! Nikamzuia John, John akanitazama kwa jicho la hasira. Macho yake yakiwa mekundu sana.

John alikuwa ananiona? Nilijiuliza.Lile joto likazidi. Abiria wakashuka garini.Kuna kitu hapa!! Mapambano mapya!! Nikajisemea huku nikiendelea kumzuia John.John sasa akanizidi nguvu.Akanitoka. Akashuka chini. Nikajaribu kumkimbilia.Huko nikamkuta akiwa anafanya jambo la ajabu. John alikuwa anajarfibu kuisukuma gari kwa kuitikisa.Ajabu! Ikaanza kutikisika kweli. Mtikisiko ule ukawashtua wengi. Sasa vilio vikaanza kusikika. Kila mtu kuitetea nafsi yake.

Watu wakashuka upesi kwa kugombania mlango. Basi likaanguka.Lilipoanguka John akatazama mahali. Na mimi nikageuza jicho kutazama. Yalikuwa makaburiMakaburi yaliyo na historia ya kushangaza. Makaburi ambayo yalimtoa nishai mchina alipojaribu kupitisha umeme juu yake. Umeme ukagoma kuwaka.Haya yalikuwa makaburi ya Kiyeyeu.Yalikuwa yanafuka moshi wa dhahabu!!Vita!!

Mayowe yakatawala, akinamama wakiwa wamesahau watoto wao na wanaume nao wakiwasahau wake zao sasa kila mmoja alikuwa akiipigania nafsi yake. Sikuwa katika umoja na akina Jesca tena! Hapa sasa kila mwenye macho hakungoja kuambiwa tazama!!Makaburi yale mawili yaliendelea kufuka ule moshi wa rangi ya dhahabu.Wenyeji wa kijiji kile walikuwa katika taharuki kubwa sana huku wakizungumzia juu ya kukasirika kwa mizimu.Nani sasa aliyeikasirisha? Walijiuliza.

Vilio vilisikika tena kutokea gizani. Watu wakakimbilia huko. Waliporejea ilikuwa taarifa ya mama mmoja aliyekuwa anakimbia ameshambuliwa na kitu kisichofahamika na hatamaniki tena. Amekufa!!Hali ikatulia kwa muda. Akajitokeza mzee mmoja wa makamo akitembea kwa kutumia mkongojo.Huyu hakuogopeshwa hata kidogo na hali iliyokuwa inaendelea. Alisimama mbele ya kundi na kuanza kusema anachokifahamu, alielezea historia fupi ya makaburi ya Kiyeyeu na majanga yanayotokea iwapo wazee wale waliolala katika makaburi yale wakikerwa na jambo. Hapa sasa akafikia kusema kuwa kuna mtu mmoja katika msafara alikuwa ameikasilisha mizimu!!

Ni lazima abaki ili kuwanusuru wenzake. Kama akiendelea mbele basi litatokea balaa kubwa zaidi ya hili. Alizungumza kwa sauti ya juu na kila mmoja aliweza kusikia. Sauti yake na umri wake vilikuwa vitu viwili tofauti!!“Hivyo kama unajua una lolote la kuikera mizimu hii ni heri ubaki nyuma kuwanusuru wenzako.” Alizungumza kisha akatuachia mtihani wa kuamua aidha kujitokeza ama la!Maneno yake niliamini kabisa yalikuwa yanamlenga John. Nilijisikia uchungu sana, John alitakiwa kubaki nyuma. Yaani harakati zangu zote hizo zinaishia hapa!! Niliumia sana.

Niliangaza huku na huko. Sikumuona John!! Nilitaka kumuita lakini niliamini kuwa hawezi kunisikia.Kimya kilitawala akisubiriwa mtu huyo ambaye ameikera mizimu aweze kujitoa kundini. Hakuna aliyejitokeza.Mzee akaendelea kusubiri!! Bado hakujitokeza mtu yeyote.Kimya kilikatishwa na sauti ya mwanaume akipiga mayowe. Tukageuka nyuma kumtazama. Alikuwa amejishika shingo yake huku akipiga kelele. Mara damu zikaanza kumtoka puani, masikioni na mdomoni. Badala ya kumsaidia kila mtu akawa anamuogopa!!Hatimaye akaanguka na kutulia tuli! Alikuwa amekata roho!!Kina mama wakapiga kelele sana, wanaume wakabaki kushangaa.

Yule mzee wa kimila akaipaza tena sauti yake, “Kama asipojitokeza mtu huyu majanga yataongezeka. Mizimu inakasirika.”Sasa watu wakaanza kusemezana huku wakisisitizana kuwa mtu huyu ajitokeze ili mizimu itulie. Bado hakuweza kujitokeza mtu yeyote.Zikaanza kutolewa hirizi miilini mwa watu, lakini yule mzee wa kimila akapinga kuwa hizo ndio tatizo.Waliokuwa na dawa za kienyeji wakatoa. Bado haikuwa tiba.Kiza kinene kikatanda kama dalili ya mvua. Mwanga mkali ukamulika bila kutoa kelele. Watu watatu wakasalimia na ardhi.Ilikuwa radi!! Na walikuwa maiti tayari.

Roho ikaniuma sana, nikajiona mimi ndiye muhusika. Nikatamani John atokezee nimtangaze kuwa ndiye chanzo. Lakini John hakuwepo tena!!Vile vifo vya radi ya ghafla vilimshtua kidogo yule mzee.Mara akabadilika sura na kuwa kama aliyekasirika!!Akatoa amri ya watu kujipanga msitari. Amri ikasikilizwa. Wanaume na wanawake mstari mmoja, mistari ilipopangwa ndipo nilimuona John. Na yeye alikuwa amepanga mstari. Akaanza kupita na kufanya kile anachokijua mwenyewe. Alimfikia John, na yeye akamuona akamshika mkono. Ina maana John anaonekana? Nilijiuliza.Nikiwa katika hali ya mashaka ya kila kinachoendelea.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
53 Simulizi Sitoisahau Facebook
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni