Notifications
  • MY DIARY (3)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TATUTULIPOISHIA...Nazani sasa unanielewa ninaposema nilikuwa sina ndugu kwani baba yangu hakuwa na ndugu yeyeote zaidi ya marafiki ambao na wao kwa sasa ndio hao wameshagawana mali zote. Nimebaki mimi na dunia yangu hivyo basi nilimwomba rafiki yangu wa kufa na kuzikana kwa jina Joyce anisaidie kunisitiri nyumbani kwao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Likizo ilipoisha tulirusi shuleni na…
  • MY DIARY (2)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA PILITULIPOISHIA...Kwa ufupi japo sitaki kueleza historia yake ila kwa sasa ni shoga na teja. Baba yetu alitupenda sana na alihakikisha tunapata elimu nzuri na bora. Mimi na kaka yangu wote tulisoma International school ya hapo Moshi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baadaye kaka yangu alianza kuvuta bangi kitu ambacho kilimtia hofu baba yangu na kuamua kumpeleka kusoma nje ya nchi.Alikosea sana…
  • MY DIARY (1)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KWANZANilikuwa juu ya jukwaaa nikifanya vitu vyangu ili hali nikijua kabisa watu wote waliokuwa wakinitizama walikuwa wanaumia roho kutokana na mvuto wa umbo langu niliokuwa nao. Nilisikia mijibaba miwili ikiulizana hivi lile wowoo ni la kwake au ni la mchina? Mmoja wao akaropoka “wee kitu original hicho,kwani umemsaahau huyu binti tulishakutana nae kule Arusha mpaka tukambatiza jina la soda kubwa tena ya fanta yaani BAMBUCHA.?” Yeah nimekumbuka alidakia…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (18)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (17)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na Wafuasi wake…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (16)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea mlio ule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…

SITOISAHAU FACEBOOK (24)


SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Na yeye alikuwa amepanga mstari. Akaanza kupita na kufanya kile anachokijua mwenyewe. Alimfikia John, na yeye akamuona akamshika mkono. Ina maana John anaonekana? Nilijiuliza.Nikiwa katika hali ya mashaka ya kila kinachoendelea.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Mara yule mzee mkongwe alinifikia, alikuwa anatabasamu, mgongo wake uliopinda ulimfanya awe ameinama na kuwa mfupi sana!!“Shkamoo babu.” Nilimsalimia.“Marahaba mjukuu wangu.” Alinijibu kwa ukarimu sana.Kisha akanishika mkono.Alipofanya hivyo kwa wasafiri wengine hakutumia muda mrefu, lakini kwangu ni kama alitumia sekunde nyingi.“Unaitwa nani binti.”“Isabela!!”“Nani alikwambia unaitwa Isabela.” Aliniuliza huku akinitazama usoni.“Naitwa Isabela mzee.” Nilitaharuki kutokana na maswali ya mzee huyu.

“Hilo sio jina lako binti.”“Sio jina langu?”“Na litakugharimu sana na kuwaumikza wengine katika maisha yako.” Kauli nzito za mzee huyu zilinishangaza.Isabela sio jina langu? Ni miaka zaidi ya ishirini tangu nipewe jina hilo. Sasa leo ananiambia kuwa hilo sio jina langu? Maajabu haya.“Hautaendelea na safari hii…kuwaepusha wenzako na mabalaa yasiyowahusu.” Alininong’oneza. Nikahisi ubaridi ukinipenya mwilini, mapigo ya moyo yakapungua kasi. Nikakata tamaa.

Mimi tena? Sio John!! Maajabu haya.“Kama unao upendo waruhusu wenzako waende zao. Janga lako haliwahusu hata kidogo.” Alinisihi. Nikatikisa kichwa kukubali. Huku nikiamini kwa asilimia kadhaa kuwa tatizo ni John na yule mzee hajui kitu.Mzee akawatangazia watu kuwa tatizo limekwisha. Na kweli nilipokubali tu waondoke zao. Nilipogeuka makaburini. Ule ukungu haukuwepo tena.Abiria wakaingia katika basi lile la ziada lililokuja kutuchukua.Tofauti na mawazo yangu. Kuwa John atazuia basi lisiondoke baada ya yeye pia kuwa mmoja kati ya abiria. Haikuwa hivyo. Basi liliwaka vyema. Na kutoweka!!

Ilikuwa usiku mnene lakini kinyume na taratibu za usafiri Tanzania, basi lile lilisafiri usiku. Hayakusikika malalamiko ya kubanana tena. Kila mmoja alitaka kutoweka eneo lile. Hata madereva na makondakta wote walikuwa waoga.Nilibaki na yule babu!!! Akina Samson, Jesca, na Jenipher walitaka kubaki na mimi lakini kwa maneno ya yule babu kuwa mzigo wangu hauwahusu. Niliwaruhusu waende zao huku nikiwapatia pesa nyingine ya ziada.

“Nendeni mkautangaze ushuhuda huu popote pale. Msifiche hata moja lililotokea. Hata kama sitafika huko mtakapokuwa. Naamini sisi ni washindi.” Niliwaeleza. Wakalia kwa uchungu. Samson akagoma kabisa kuondoka lakini hatimaye alikubali kuondoka.Nilibaki na mzee yule tukizungumza. Alinieleza juu ya jina langu. Akadai kuwa hakuwa akijua nilikuwa naitwa nani lakini Isabela halikuwa jina langu.“Rejea nyumbani ukalitafute jina lako. Jina lako limepotea ama limefichwa. Na ukiendelea kuamini kuwa wewe ni Isabela basi maisha yako yatakuwa ya tabu sana. Utawatesa wenzako nawe utateseka sana.” Alinieleza yule babu.

“Unaweza kwenda kupumzika nyumbani kwangu. Kesho upatafute nyumbani kwenu. Ukalitafute jina lako.”Tuliongozana na yule mzee hadi nyumbani kwake. Hapo tulipokelewa na mbwa wengi sana waliomlaki bwana huyu kwa furaha.Wahehe na mbwa!! Niliwaza.Nililala katika mkeka. Ni kama nililala kwa sekunde kadhaa hatimaye pakapambazuka.Mzee akaniamsha, akanisihi sana nihakikishe Napata jina langu halisi na hapo nitaendelea na maisha yangu vizuri.“Jina langu ni nani?” nilijiuliza kwa sauti akanisikia.“|Hata mimi silijui lakini ni lazima ulipate ili kuzikwepa laana za ukoo wako. Fuatilia historia yako vyema mwanzo hadi mwisho. Historia ya kweli ipo kwa mama…kamuulize mama yako. Wewe ni nani? Lakini nakukumbusha kuwa wewe sio Isabela

”Mzee alinisindikiza hadi njia ya mabasi.“Usizungumze na mtu yeyote, kwa usalama wako na abiria wenzako.” Alifanya kunisemesha kwa sauti hafifu. Nikamsikia na kumwelewa.Basi likapita. Nikapanda!! Mzee alinilipia nauli huku akichukua fursa ya kuzungumza na kondakta.Safari ya kurejea Makambako. Safari ya kwenda kulitafuta jina langu. Jina lililopotea.Kaka aliyekuwa pembeni yangu alikuwa anaongea maneno mengi sana. Lakini sikuwa namjibu chochote.Hatimaye tukaifikia Makambako!! Nikashuka garini nikaikanyaga ardhi ya Makambako kwa huzuni sana!! Hatua kwa hatua nikaanza kuelekea nyumbani.

SIRI SIRINI
Mwanamke wa makamo ambaye sasa mvi zilikikaribia kichwa chake chote alikuwa anafagia uwanja. Alikuwa akiimba nyimbo anazozijua yeye huku akionekana kuzifurahia. Nilimtazama kwa makini. Nikatamani ningekuwa nimekuja kwa mazuri huenda ningemshtua kisha tukacheka wote. Lakini nilikuwa nimekuja kwa mengine magumu sana.Huyu alikuwa ni mwalimu Nchimbi. Mama yangu mzazi.Nikanyemelea. Akashtuka akageuka.

“Belaaa….Belaaa mwanangu.” Akautupa ufagio, akanikimbilia, akanikumbatia kwa nguvu. Joto lake likaupenya mwili wangu ulio dfhaifu. Nikaamini kuwa nilikuwa nimemkumbuka sana. Chozi likanitoka. Nikamkumbatia kwa nguvu zaidi.“Karibu mwanangu…mbaya wewe..yaani kimya kimya au uliongea na Suzi..wabaya sana nyie.” Alilalamika nikajilazimisha kutabasamu.Tuliingia ndani. Tukafanya mazungumzo ya hapa na pale. Hadi tulipokatishwa na nyimbo nyingine kutoka kwa mlevi. Huyu alikuwa baba yangu mzazi. Asubuhi sana alikuwa anatokea kilabuni.Sijui alilala huko? Nilimuuliza mama./“Hamna sema ameamkia huko.”

“We Helena wewe…Aaah!! Suzy..ina maana haunioni uje kunipokea…si ku hizi hamsalimii watu!!” alizungumza kilevi. Macho yake hayakumwezesha kujua iwapo mimi ni Isabela.Akapita akiacha nyuma harufu ya pombe kali. Akaingia chumbani.Baada ya kelele za hapa na pale akasikika akikoroma!!!Nilijikaza sana na sasa nikaamua kumueleza mama kilichonileta pale nyumbani.“Mama hivi hili jina la Isabela ni nani alinitungia.”“Mbona wauliza hivyo mwanangu.”“Nipe jibu mama..ama ukoo wangu ni upi.”“We mtoto umekuwaje lakini.”“Nijibu mama.”“Mbona kila kitu kipo wazi..ukoo wako ni huu wa baba yako, na jina hilo ni mimi na baba yako tulikupatia.” Alinijibu.

Niliondoka sebuleni nikaenda chumba cha wasichana nikajinyoosha. Nikapitiwa na na usingizi.Nilikuja kushtuka nikiwa na njaa kali.Nikaliendea jiko.Nikajihudumia vilivyokuwepo, kisha nikareje chumbani. Majibu ya mama yalikuwa hayajaniridhisha hata kidogo.Nitamuuliza baba pia!! Huenda kuna kitu anajua.Kwa nini aliniita Isabela.Nikasinzia huku nikiwa nimejiahidi hivyo kichwani mwangu.Asubuhi na mapema nilikuwa wa kwanza kuamka. Nilihitaji kumuwahi baba akiwa katika akili zake vyema kabisa.Kabla hajalewa!!Niliwahi na kujifanya naosha vyombo.

Hatimaye nikasikia mlango wa chumbani unafunguliwa. Baba akatoka.“Aaah!! Bela mwanangu…lini tena umetuvamia wewe…umemaliza mitihani lakini.”“Nimemaliza..shkamoo baba….”`aliijibu salamu. Tukabadilishana mawazo na hatimaye kama kawaida yake akaniomba pesa.“baba kabla ya hilo…nahitaji kukuuliza kitu.”Alinisikiliza kwa makini, nikamueleza kile nilichomueleza mama. Baba alionekana kushtushwa na habari hiyo. Alijaribu kujiweka sawa lakini nilikuwa nimemsoma.

“Fanya hivi…nipatie hiyo pesa nikirejea tutaongea ni stori ndefu kidogo..si unataka kujua maana ya Isabela na kwanini tulikuita hivyo..nifanyie kwanza nienda kupata supu kidogo.” Alijaribu kukwepesha mada. Niliheshimu maamuzi yake. Nikaingia ndani nikarejea na pesa kidogo nikampatia. Akatoweka. Moyoni nilipata matumaini makubwa sana!! Niliyaamini yale maneno ya yule mzee.Sasa mimi ni nani kama sio Isabela? Na kuna siri gani inazunguka hapa. Nilijiuliza. Wa kunijibu alikuwa ni baba.Nilisubiri sana. Hadi pale ilipokuja taarifa kuwa baba amekutwa mtaroni. Hana jedraha lakini haijafahamika bado kama anapumua ama amekufa!!

Hii ilikuwa ni habari ya kushtua sana.Mimi na mama tukakimbia kuelekea hospitali ambayo tulielezwa kuwa amelazwa.Bahati mbaya zilikuwa mbio za kuwahi upepo.Baba yangu hatukuwa naye tena!! Kifo cha utata. Hakuwa amelewa. Alikutwa na ile pesa niliyompa.Hakika mimi sio Isabela, na kuna siri mzee wangu amekufa nayo!! Nilizungumza na nafsi yangu.Jina langu ni nani sasa? Na kwa nini waliniita Isabela?Ulikuwa msiba wa mtu maskini hata utata ungegubika vipi bado angezikwa na kusahaulika. Ndivyo ilivyokuwa kwa baba yangu.Licha ya kifo chake kuwa na utata hapakuwa na la ziada alitakiwa kuzikwa.

Msiba huu ulivuta watu wengi kiasi kutokana na jina la mwalimu Nchimbi ambaye ni mama yangu. Mwalimu!! Hivyo wanafunzi walijaa sana.Historia fupi ya marehemu ilisomwa.“….marehemu ameacha mjane na watoto wanne..mmoja wa kiume na watatu wa kike….Sebastian John, Suzan John, na Helena John.” Alimaliza kutaja majina ya watoto wa marehemu.Sauti za kuguna zukatawala ghafla, watu wakawa wanaulizana hao watoto wanne mbona hawajatimia? Kina mama wakashindwa kumezea wakauliza palepale.

Ujumbe ukamfikia msomaji baada ya kijana mmoja kuagizwa.Msomaji akaanza kupekua hapa na pale. Kimya kikatanda!!!“Anaitwa Isabela John huyu hapa.” Shangazi yangu alipaza sauti akanitambulisha ili kuondoa ile sintofahamu. Nikanyoosha mkono juu. Watu wakageuka na kunitambua.Tendo lile la watu kugeuka kuniangalia likanifanya nipatwe na aibu kidogo. Inakuwaje mimi jina langu linasahaulika?Sikuuliza!!! Nikauchuna.“Kwa hiyo mtoto wa nne ni Isabela John….samahani sana kwa mkanganyiko huu.” Aliomba radhi yule msomaji. Waungwana hawakulalamika.

Alipotaka kuendelea kusoma yanayoendelea katika risala hiyo akawa anatawaliwa na kigugumizi. Hali hii sasa ikaanza kuwakera watu. Lakini kabla hili halijapita akaanza kupiga chafya.“Samahani!” akaomba radhi tena.Haikukoma, ikaongezeka chafya ya pili, mara ya tatu ya nne, chjafya mfululizo. Akaachia lile karatasi lililoandikwa risala. Hali ikaonekana dhahiri kuwa si nzuri!!Akajikunja kunja huku akionekana kuzitafuta pumzi zake. Mwili ukakosa muhimili akaanguka chini.Wale waliokuwa na ghadhabu sasa ikawalazimu wakimbilie kutoa msaada. Msoma risala akatulia akiwa amejishika kifuani. Akafanana na ile maiti ya baba iliyopo katika jeneza.Baadhi ya wanaume wakamchukua garini.

Tuliosalia tukaendelea na taratibu nyingine, hatimaye tukazika. Watu walikuwa wanajiuliza kimemsibu nini yule bwana. Hakuna hata mmoja aliyeweza kutoa majibu hata mimi pia nilikuwa katika sintofahamu.Siku iliyofuata asubuhi na mapema la mgambo likalia. Msoma risala alikuwa amepoteza maisha!!!**Suala la baba kuondoka na siri kubwa aliyotakiwa kunieleza lilikuwa ni jambo lililoutafuna sana mwili wangu. Nilikuwa najiuliza bila kufikia muafaka.Maisha yaliendelea. Chuo kilikuwa kimefungwa jijini mwanza na nilikuwa nina kumbukumbu kuwa niliomba ruhusa maalumu kabla ya mitihani haijaanza. Hivyo nilitakiwa sasa kufuatilia iwapo mtihani umekaribia ama la.

Nilitafakari nani wa kumuuliza. Nikamkumbuka Maria. Nilijilazimisha kuamini kuwa yale ya mimi kumuona katika pori nchini Zambia zilikuwa ni ndoto tu.Nikajaribu kuvuta kumbukumbu za wapi nimewahi kuhifadhi namba yake sikupata jawabu. Hilo nalo likawa tatizo.Nikafikia uamuzi wa kwenda katika huduma za internet café sio mbali sana kutoka nyumbani kwetu. Wakati huo sikuwa na nywele kichwani hivyo nilikuwa nimejitanda ushungi.Nilifika kwa wakati muafaka nikapata nafasi, nikatazama yaliyonipeleka kisha nikalipia huduma ile.

Wakati nasimama niweze kutoka nikagonganisha macho yangu na mtu ambaye niliamini kuwa haikuwa mara yetu ya kwanza kuonana. Alikuwa ni msichana mnene. Nikavuta kumbukumbu lakini sikulipata jina lake.“Mambo…” nilimsalimia, akatabasamu kisha akanijibu.“Ujue nilidhani nakufananisha. Nilikuangalia wakati unaingia ujue nikahisi nimekufananisha.”“Na mimi hivyo hivyo!!” nilimuunga mkono.

Tukasogea nje na kupiga stori za hapa na pale.Wakati wa kuagana ndipo tukakumbuka kuulizana majina. “Naitwa Isabela.” “Mh!! Isabela!! Ulibadilisha jina ama..maana nakumbuka walikuwa wanakuita nani vilee.” Alijaribu kuvuta kumbukumbu. Mimi nikawa namtazama tu! Nilibadilishaje jina sasa mimi.“Hata sijabadili mbona.” Nilimwelewesha. Akazidi kupinga.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
53 Simulizi Sitoisahau Facebook
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni