Notifications
  • MY DIARY (3)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TATUTULIPOISHIA...Nazani sasa unanielewa ninaposema nilikuwa sina ndugu kwani baba yangu hakuwa na ndugu yeyeote zaidi ya marafiki ambao na wao kwa sasa ndio hao wameshagawana mali zote. Nimebaki mimi na dunia yangu hivyo basi nilimwomba rafiki yangu wa kufa na kuzikana kwa jina Joyce anisaidie kunisitiri nyumbani kwao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Likizo ilipoisha tulirusi shuleni na…
  • MY DIARY (2)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA PILITULIPOISHIA...Kwa ufupi japo sitaki kueleza historia yake ila kwa sasa ni shoga na teja. Baba yetu alitupenda sana na alihakikisha tunapata elimu nzuri na bora. Mimi na kaka yangu wote tulisoma International school ya hapo Moshi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baadaye kaka yangu alianza kuvuta bangi kitu ambacho kilimtia hofu baba yangu na kuamua kumpeleka kusoma nje ya nchi.Alikosea sana…
  • MY DIARY (1)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KWANZANilikuwa juu ya jukwaaa nikifanya vitu vyangu ili hali nikijua kabisa watu wote waliokuwa wakinitizama walikuwa wanaumia roho kutokana na mvuto wa umbo langu niliokuwa nao. Nilisikia mijibaba miwili ikiulizana hivi lile wowoo ni la kwake au ni la mchina? Mmoja wao akaropoka “wee kitu original hicho,kwani umemsaahau huyu binti tulishakutana nae kule Arusha mpaka tukambatiza jina la soda kubwa tena ya fanta yaani BAMBUCHA.?” Yeah nimekumbuka alidakia…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (18)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (17)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na Wafuasi wake…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (16)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea mlio ule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…

SITOISAHAU FACEBOOK (26)


SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Akamsalimia mama kwa kupiga magoti.Kabla ya kujibu mama akaanza kuvuta kumbukumbu. “Eliza….nimekosea!!!” alimkumbuka jina lake kwa usahihi.“Mjukuu wangu huyu, kumbe ni mwanafunzi wako.” Yule mkunga aliyekuwa amesimama akasema huku sasa akikaa.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Mwanafunzi yule akawa ameujenga urafiki kati yetu.Tukakaribishwa ndani!!!Baada ya utambulisho mama alianza kujielezea juu ya jambo lililotuleta. Alianzia mbali sana hadi akalifikia lengo letu.Mama yule kwanza, alishtushwa na taarifa hiyo kisha akasema kuwa hajui lolote kuhusu tukio hilo.“Kwa hiyo una uhakika kuwa nilizaa mtoto na akawa hai?” mama alimuuliza akiwa amemkazia macho. Mkunga akawahi kukwepesha macho yake, nikamsoma na kugundua anatudanganya.“Sikumbuki..ujue nimewazalisha akinamama wengi sana…hakika sikumbuki.” Alijitetea huku akiwa na hofu.

Aliusimamia uongo wake huo hadi pale nilipoamua kuyaingilia mazungumzo haya, hasira ilikuwa imeanza kunitawala.Nikarusha karata yangu!!!“Mama mimi nadhani nimpigie simu yule baba aliyeshuhudia tukio hili, najua nikimpigia atakuja na yule askari. Kwa hiyo tutaufahamu ukweli.”Yule mama akatowa yowe la hofu huku akizungumza kikabila cha kwao, hakika alitaharuki kusikia polisi.“Mwanangu…usipige simu subiri tunayazungumza haya yanaisha.”Uwanja ukawa wake akazungumza.Kama dada Suzi alivyosimuliwa na marehemu baba juu ya uwepo wangu katika familia ile ndivyo ilivyokuwa kwa nesi huyu ambaye mara kwa mara alitusihi tuyamalize kindugu.

“Na mama yangu ni yupi?” nilimuuliza ghafla akashangaa.“Sikuelewi unaniuliza mimi au?”“Ndio nakuuliza wewe…..mimi ni huyo mtoto azliyeibiwa.”Akakodoa macho yake kwa hofu. Nikaiskia hasira ikinichemka sana nikatamani kumrukia.“Kwakweli mimi sijui labda Gloria ndio atakuwa anafahamu.”“Gloria ndio nani?” mama alimuuliza.“Tulikuwa naye..huyo ndiye aliyenishawishi.

*Hatukupoteza muda, tulimpa nafasi kidogo ya kujiandaa tukaondoka kuelekea kwa huyo aliyemuita Gloria. Haikuwa safari ndefu sana, tulitumia taksi.Na yeye tulimkuta vilevile akiwa yupo katika uzee.Baada ya salamu mbili tatu. Moja kwa moja ikawa zamu ya yule nesi kumueleza mwenzake juu ya tukio la miaka zaidi ya ishirini iliyopita.Kama ilivyokuwa wakati tunamueleza na yeye alileta ujanja wa kutaka kumruka mwenzake lakini alipothibitishiwa kuwa akileta udanganyifu yupo shahidi na polisi pia. Naye akanywea!“Tunachohitaji kujua ni kitu kimoja tu!! Mama aliyeibiwa mtoto ni nani.” Nilikoroma kwa hasira. Suzi na mama wakawa wakimya.

“Ni Dina….Dina yule…..”“Dina ni nani na anakaa wapi.”“Dina ni kichaa…eeh! Mungu nisamehe mimi nisamehe…” alianza kulia yule mwanamke.” Hakuna aliyembembeleza.Neno lake la kuwa Dina ni kichaa liliniacha njia panda, ina maana mama yangu ni kichaa na anaitwsa Dina? Hapana haiwezi kuwa!!! Nilipinga kimya kimya.Baada ya kutulia tena akatueleza juu ya kichaa aliyepewa mimba miaka mingi iliyopita. Mimba iliyotaka kuchukua uhai wake kwa sababu ya kukosa matunzo. Ilikuwa kama bahati diwani wa kata hiyo ambaye alikuwa mwanamke alipata kukutana na kichaa huyu. Wakati huo mimba ilikuwa na miezi saba. Huruma ilimshika kutoka na na imani yake ya kiroho..”“Ooh!! Jesus jesus!!” Suzi alinong’ona huku akiwa kama anasali.

Akaendelea yule mama. “Basi akafika mwenyewe hospitali na kutoa amri ya mwanamke yule kusaidiwa. Hatua za haraka zikachukuliwa. Mwanamke akaanza kukamatwa kinguvu na kupelekwa kliniki. Baadaye akafungiwa kabisa bila kutoka hospitali. Hatimaye miezi tisa ikatimia akajifungua bila kufanyiwa upasuaji. Mtoto wa kike!!!!Wakati anajifungua mtoto huyu ndipo ilipatikana biashara hii ya kuiba mtoto. Hakika hali ilikuwa ngumu sana kiuchumi. Utawala wa serikali ya awamu ya kwanza ulikuwa umechachamaa sana hivyo kwa pesa tuliyotangaziwa na yule kijana ambaye simkumbuki jina mimi na mwenzangu hatukuweza kuikataa.Pia tuliamini kuwa yule kichaa asingeweza kumlea mtoto wake. Hivyo kwa huruma tukamchukua yule mtoto na kumuuza.”

Simulizi ile ilinisisimua sana!! Nilikuwa natetemeka kwa kila neno alilotamka yule mwanamama. Nilijihisi kama nusu mwanadamu nusu nimekufa!!Kimya kikatanda. Kila mmoja akiwaza lake. Mimi nikizidi kuamini maneno ya mzee yule wa Iringa. Kuwa lile halikuwa jina langu na wala haukuwa ukoo wangu.“Mama yangu yupo wapi?” hatimaye niliuliza.“Kwa kweli ni siku ya nne hivi sijamuona lakini huwa anapatikana stendi na majalalani.” Nikasisimka tena kusikia maneno haya. Mama yangu anaishi majalalani!!! Niliumia.

Hapakuwa na jipya tena kwa pale. Kwa kuwa huyu mama alikuwa anamtambua Dina ilimlazimu kuzunguka nasi siku nzima kumtafuta.Siku ya kwanza hatukufanikiwa kumuona.Siku ya pili majira ya mchana baada ya kuzunguka siku nzima bado kimya. Tukapewa taarifa za juu juu kuwa aliingia katika gari ya kwenda Mbeya.Huo ukawa mwanzo wa safari nyingine.

“Tulimshusha Uyole.” Kondakta alitueleza baada ya kufanikiwa kulipata lile gari alilosadikiwa kupanda mama yangu.Wakati huu nilikuwa mimi na mama pamoja na yule mkunga. Dada Suzi alirejea nyumbani kwa ajili ya kulea mtoto ambaye sasa kilio kilikuwa kinapungua na kidogo alikuwa ananyonya.Safari ya kwenda Mbeya ikafuata. Tukaweka kituo Uyole. Kama vile chokoraa tulianza kuzurura huku na huko bila mafanikio. Yule mkunga ndiye aliyekuwa anaulizia mara kwa mara maana ni yeye alikuwa anaujua muonekano wa huyo Dina.

Siku mbili Uyole bila mafanikio. Mama alikuwa amechoka dhahiri lakini asingeweza kusema, nadhani kwa kuwa aliamini nipo katika matatizo pia ni kama mwanaye wa kumzaa, maana hata titi lake nilikuwa nimenyonya.Siku ya nne inakuja habari nyingine kuwa Dina alionekana sokoni. Asubuhi na mapema tukafunga safari kuelekea Uyole sokoni.Tulisubiri kwa masaa kadhaa.Kelele za akina mama zilitushtua, walikuwa wanahangaika huku na huko kutaka kushuhudia jambo huku wengine wakiwa wanakimbia.“Yule pale Dina!!” mkunga alipiga kelele huku akitujelekezea kwa kidole.

Mwanamke mnene, akiwa na malapulapu mwilini alikuwa akiwaponda watoto na mawe. Huku akiwa na fimbo mkononi. Alikuwa anajongea eneo la soko. Jambo hilo liliwapagawisha akina mama na sasa walikuwa wanapiga kelele.Nilimtazama mwanamke huyu anayesadikiwa kuwa ni mama yangu. Mara ghafla nikajikuta nipo wima, nikakimbia mbio mbio. Umati ulikuwa unashangaa na hata mwalimu Nchimbi alibaki kunitazama tu asijue la kufanya.Macho yetu yalipogongana nikaona kitu!!Ni kama kioo mbele yangu na nilikuwa najitazama.Damu nzito kuliko maji!!!Sikuogopa mawe aliyoshikilia, mavazi yake machafu!!Nikamsogelea na kumkumbatia.

Maajabu!! Na yeye akanikumbatia huku akizungumza kabila nisilolielewa. Kimya kikuu kikatawala!!Hakuna aliyetusogelea.“Mama!!” nilinyanyua kinywa changu na kumuita!!“Su…Subira…..” aliniita kwa mshangao.Alipotaja jina hilo. Nikajikuta kama nasukumwa chini. Nikaanguka kama mzigo.Nikajikuta katika filamu ya ajabu huku mimi nikiwa wa ajabu zaidi.Nilikuwa napambana na mamia ya watu. Na sasa nilikuwa ana kwa ana na Dokta Davis. Alikuwa ananiogopa sana, nami sikuwa na huruma. Nikiwa na panga kubwa mkononi. Nilimkaribia na kumfyeka.Nikatazama maadui wengine wanaonikabiri na wao nikawatenda nilichomtenda Davis.

Likafuata pambano kuu la kupambana na joka la maajabu.Lilinisumbua lakini kila liliponijeruhi na mimi niliondoka na kipande kimoja cha mwili wake.Pambano lilikuwa kali hadi walipotokea viumbe weupe sana wakaniweka kando kisha wakalimaliza joka.Kisha wakakiteketeza kijiji kile cha maajabu. Lakini cha kushangaza mimi sikuungua kabisa.Moto ulipokwisha nikajikuta nimesimama peke yangu. Uchi wa mnyama. Nilikuwa nimechoka na nilikuwa natokwa jasho.Ule ujasiri niliokuwanao ukayoyoma na sasa nikawa naogopa.Mara ghafla…”Mamaaaaaa!!” nikapiga kelele kubwa na kutaka kukimbia.Nilipojaribu kufanya hivyo nikakabiliana na kamba ngumu zikiwa zimeifunga mikono yangu na miguu. Nilikuwa natokwa jasho sana.

Niliangaza huku na kule bila kupata majibu.Mara kundi la watu likafika pale chumbani.Wote walikuwa wakinishangaa. Nikamuona mwalimu Nchimbi.“Mama ni nini hiki…mbona nimefungwsa hivi.” Niliuliza huku nikiwa nashangaa.Mwanaume mmoja nisiyemtambua akaanza kunielezea juu ya vurugu nilizokuwa nafanya licha ya kupigwa sindano ya usingizi.“Ni ugonjwa wa kushangaza sana.”Alinielezea tukio zima la kuanguka baada ya kukumbatiana na kichaa ambaye alitoweka pia baada ya mimi kuanguka.“Mama yangu!!” niliwaza!! Kisha nikatabasamu na akili ikiwa imerejea sawia.

Nilipofunguliwa kamba niliwaelezea juu ya yote yaliyokuwa yananikabili katika maono yangu ya ajabu.“Nimeikamilisha kazi!!!” hatimaye nilitamka hayo.Tulikuwa hospitali ya mkoa ya Mbeya. Baada ya siku nne niliruhusiwa kuondoka. Niliambatana na mwalimu Nchimbi.“Naitwa Subira!!” nilimweleza mama.“Najua!!” aliniambia, nikashangaa.“Umejuaje.”“Ulisisitiza sana wakati ukiwa umepoteza fahamu zako.”Nilitabasamu naye akatabasamu.Mtoto wa dada Suzi alikuwa halii tena japo mkono wake ulibaki kuwa vile umejikunja.Amani ikautawala moyo wangu!!!

Taarifa pekee iliyoniumiza ni juu ya kifo cha mama yule kichaa aliyekufa baada ya kugongwa na gari.Japo nilipata nafasi ya kusikia neno moja tu kutgoka kwake lakini alikuwa amenisaidia mengi mno.Familia yangu ilimzika kwa heshima zote kama ndugu.Baada ya kuyaweka haya yote pembeni niliirejesha akili yangu jijini Mwanza.Mama alikopa pesa nikasafiri kurejea chuoni.Safari ilikuwa njema sana.Maria akawa mwenyeji wangu jijini Mwanza. Akanielezea juu ya yote yaliyotokea. Hapakuwa na lolote baya, zaidi ya maajabu ya kanisa fulani kudai limemtoa John msukule kutoka gamboshi.

Nilitabasamu na kukiri kuwa dini imegeuka biashara. Lakini sikumwelezea Maria juu ya yote tuliyoyapitia.“Jesca na Jenipher je?” nilimuulizia na kutegemea jibu la maajabu tena.“Kumbe mwenzangu na wao hawakufa..eti vilizikwa vinu badala ya watu!! Dunia ina mambo.” Alijibu.“Kwa hiyo bado wapo chuo.”“Hapana hawapo kwa sasa. Lakini Jesca yupo mtaani.’“Amakweli dunia ina mambo…” nilimuunga mkono.Maria hakujua lolote lile kuhusu yaliyonisibu mimi. Na alikuwa kama anayenifahamisha juu ya yaliyotokea huku akiamini kuwa ile ruhusa niliyoomba ndio iliyonifanya nitoweke ghafla.“mwenzangu na mimi siku moja sijui nikaota madudu gani. Wacha nipagawe..” Maria alinisimulia alichokiota na kilikuwa sawa na kilke kichotutokea msituni.Maria hakujua kama ni kweli alikuja kule msituni!!!

“Nilipiga kelele wewe nikamuita Mungu, mama na mizimu yote!!” aliendelea kusimulia.Baada ya mazungumzo hayo marefu. Niliingia kuoga.Baada ya kuoga nikiwa katika kutafuta nguo ya kubadilisha nikakutana na kadi ya benki. Nikaitazama huku nikiweka mbali kabisa tamaa.Nilipokuwa nimebadilisha nguo, nikaanzisha moto mdogo nyuma ya ny

umba na kuviteketeza baadhi ya vitu ambavyo nilihisi vitakuwa vinanikumbusha juu ya Dokta Davis.Nilitaka kuiteketeza kadi ya benki pia lakini nikakumbuka kuwa ilikuwa pia kwa ajili ya matumizi ya chuoni. Nikaghairi zoezi hilo.*Baada ya wiki moja nikapata fursa ya kukutana na John!! Nilikutana naye akiwa anaelekea kanisani.“Bwana asifiwe dada..Bela.” alinisalimia huku akionekana kutokumbuka lolote.Nikamjibu, tukabadilishana naye mawili matatu. Akaenda zake huku akinisihi kuwa akitoka kanisani atanitafuta.

Niliondoka pale nikiwa natabasamu na kujipongeza kwa vita ile kuu ambayo nimeibuka kuwa mshindi. Vita ambayo nimepoteza kipande kidogo tu cha nyama yangu lakini kwa ukombozi wa mamia ya watu..kutoka katika milki ya Shetani na chapa yake ya 666.Japo sikutaka tena kurejea katika mtandao huo lakini nilikiri kwa kila neno la lugha ninayoifahamu kuwa kamwe SITOISAHAU FACEBOOK.

MWISHO

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
53 Simulizi Sitoisahau Facebook
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni