Simulizi Mpya
Tidak ada notifikasi baru.

DINI YA SHETANI (15)

Mtunzi: Aziz Hashim

SEHEMU YA KUMI NA TANO
TULIPOISHIA...
Kwa bahati nzuri, yule jogoo aliendelea kudonoa punje nyingine, alipofika ya saba akapigapiga mabawa yake kisha akawika. Mganga akaupunga ule usinga hewani kisha akamkamata yule jogoo na kumshika kama alivyokuwa amemshika mwanzo, akanigeukia na kunitazama.

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Akatingisha kichwa kuonesha kukubali huku akiachia tabasamu hafifu.

“Huo ndiyo uanaume, hongera sana,” alisema huku akinipa mkono, akanishika na kuniongoza kurudi ndani.

Tulipoingia ndani, wale watu walishangilia kwa nguvu mpaka wengine wakawa wanasimama, tukapitiliza mpaka kule mbele. Kabla ya kufanya kitu kingine chochote, nilipitiliza mpaka pembeni ya kitanda alichokuwa amelala baba.

Cha ajabu, safari hii baba alikuwa ametulia kimya huku macho yake akiwa ameyafumba. Nilijaribu kumtingisha lakini hakutingishika, nikamtazama mama aliyekuwa amekaa upande wa pili wa kitanda, nikamuona amejiinamia huku machozi yakimtoka. Nilishindwa kuelewa kilichokuwa kinaendelea.

Baada ya hapo, sherehe kubwa ilifanyika pale kwa mganga, nikafanyiwa matambiko mengi huku nikinyweshwa dawa za kienyeji na kupewa hirizi. Kwa kuwa umri wangu

ulikuwa mdogo, mganga alishauri kuwa tukirudi nyumbani, mzee Mwalyego ambaye alikuwa akisaidiana na baba kwenye kazi za kanisa ndiyo ashike nafasi ya uchungaji lakini maelezo yote atakuwa anayapata kutoka kwangu.

Na yeye akafanyiwa tambiko na kupewa dawa huku mganga akimsisitiza kuwa hatakuwa na mamlaka ya kufanya jambo lolote bila kupata idhini kutoka kwangu.

Nikaambiwa sitakiwi kukaa mbali na kanisa na lazima kila kwenye ibada niwepo, tena nikae nyuma ya madhabahu. Tulikaa kule kwa mganga kwa siku tatu huku nikiwa sijui hatima ya baba.

Siku ya nne, mganga akatuelekeza kuwa turudi Tanzania ila tumuache baba kulekule ili aendelee kutibiwa. Kwa kauli le, nilitambua kuwa baba hawezi kupona tena na huo ndiyo mwisho wake, machozi yakawa yananitoka huku mama naye akilia muda wote. Mganga akatuambia kuwa tunapaswa kurudi kule kwake baada ya mwezi mmoja huku akituhakikishia kuwa tutamkuta baba ameshapona kabisa.

Tukaianza safari ya kurudi nyumbani huku njia nzima baba mkubwa akimlaumu mdogo wake (baba) kwa kuiingiza familia yake kwenye janga kubwa kama lile. Safari iliendelea kwa kutumia gari tulilokuja nalo huku njia nzima nikifikiria yale mambo niliyokutana nayo kule kwa mganga.

“Ningejua mambo yenyewe ndiyo haya wala nisingekuja huku,” niliwaza wakati gari likizidi kuchanja mbuga. Njia nzima hakuna aliyemsemesha mwenzake, tukasafiri mpaka tulipofika Kasumulu, kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi.

Nilikuwa natetemeka kuliko kawaida kwani nilijua tulichokuwa tunakifanya hakikuwa kinakubalika kwa wanadaamu wala mbele za Mungu. Mzee Mwalyego akapanda kwenye madhabahu na mimi nikakaa kwenye kiti maalum, upande wa nyuma na misa ikaanza.

SASA ENDELEA…

Nilikuwa na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wangu kwani hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kubebeshwa dawa za kienyeji na kuingia nazo kanisani bila uwepo wa baba. Muda wote nilikuwa natetemeka kwani sikuwa na uhakika kuwa misa itaisha salama bila kushtukiwa.

Kwa bahati nzuri, mambo yalienda vizuri. Mzee Mwalyego alipowatangazia waumini kuwa hali ya baba siyo nzuri na kwamba amesafirishwa kwenda nje ya nchi kutibiwa, niliwasikia watu wengi wakimuonea huruma sana. Baadhi ya waumini hasa wanawake walisikika wakilia.

Baada ya misa kuisha, ulifika muda wa kutoa sadaka. Siku hiyo kuliwekwa vikapu viwili, kimoja kikiwa ni kwa ajili ya sadaka na kingine kwa ajili ya mchango wa matibabu ya baba. Watu walitoa sadaka na mchango huo kwa wingi mpaka vikapu vyote viwili vikajaa.

Baada ya hapo, waumini walianza kutoka, wengi wakamfuata mama na wakawa wanampa pole kwa kuuguza. Baada ya watu wote kutoka kanisani, mimi na mzee

Mwalyego ndiyo tulikuwa wa mwisho. Kama kawaida, nilibeba vikapu vya sadaka na kutoka hadi nje, tukaelekea mahali gari tulilokuja nalo lilipokuwa limeegeshwa.

“Safi sana, unafaa kijana,” mzee Mwalyego aliniambia huku akinipigapiga mgongoni, mama na ndugu zangu wengine wakaja kwenye gari na safari ya kurudi nyumbani

ikaanza. Njia nzima sikutaka kuzungumza chochote mpaka tulipofika nyumbani. Nilishusha vikapu vya sadaka na kuingia navyo ndani, nikapitiliza mpaka chumbani.

“Mbona leo umepooza sana,” mama aliniuliza baada ya kuona sipo sawa, sikumjibu kitu zaidi ya kujiinamia, akanisogelea na kuanza kuniuliza kwa upole.

“Mama najihisi mkosefu sana mbele za Mungu kwa haya tunayoyafanya,” nilisema huku nikiwa nimeinama.

“Najua jinsi unavyojisikia mwanangu, utazoea tu na kila kitu kitakuwa sawa,” mama aliniambia huku akiwa amenikumbatia. Licha ya kunipa moyo, bado nafsi yangu ilikuwa nzito sana kukubaliana na hali ile. Baada ya muda, tulitoka sebuleni na kuanza kuhesabu sadaka tukisaidiana na mzee Mwalyego.

Tulipomaliza, mama alichukua kiasi na kumpa mzee Mwalyego kisha nyingine akaenda kuzihifadhi chumbani kwenye sanduku la chuma. Siku hiyo nilishinda nikiwa kama mgonjwa, kutwa nzima nilikuwa nikiijutia nafsi yangu kwa kitendo tulichokifanya siku hiyo kanisani.

Kwa jinsi nilivyokuwa najisikia, nilienda kulala mapema lakini usingizi haukunipitia haraka. Niliwaza mambo mengi sana usiku huo, nikamkumbuka Firyaal na yote tuliyoyafanya pamoja. Kuna wakati wazo la kuondoka nyumbani lilinijia lakini nilipofikiria nitamuachia nani majukumu ya kuongoza kanisa, nilijikuta nikikwama.

Hata hivyo, niliamua kupiga moyo konde na kuweka dhamira kuwa ni lazima niende Dar es Salaam. Kesho yake kulipokucha, niliamka nikiwa na wazo jipya. Nilitaka kusafiri mpaka Dar es Salaam ambako nilipanga kukaa siku kadhaa kisha kurejea kabla Jumapili haijafika.

Nikaanza kuwaza nitamdanganya vipi mama kwani katika hali ya kawaida, asingeweza kuniruhusu kirahisi. Baada ya kunywa chai, nilijaribu kuzungumza na mama ambapo kama nilivyohisi awali, hakuwa mwepesi kuniruhusu. Nilipomweleza kuwa nitakaa siku tatu tu, alinikubalia lakini akanisisitiza kuwa nihakikishe narudi kabla ya Jumapili.

Nilifurahi sana ndani ya moyo wangu kwani nilijua kwa mara nyingine naenda kuonana na Firyaal, kipenzi cha moyo wangu. Nilianza kufanya maandalizi ya hapa na pale, kesho yake asubuhi na mapema ndugu zangu wakanisindikiza mpaka stendi. Mama alinipa zawadi nyingi za kumpelekea baba mkubwa pamoja na familia yake.

Saa kumi na mbili na nusu za asubuhi nikapanda basi na safari ya kwenda Dar es Salaam ikaanza. Akilini mwangu nilikuwa namuwaza Firyaal kwani nilimkumbuka kuliko kawaida. Safari haikuwa nyepesi, tulisafiri kwa saa nyingi barabarani, ilipofika saa kumi na mbili za jioni, tuliwasili Dar es Salaam.

Sikutaka kwenda nyumbani kwa baba mkubwa, Kimara Kona, akili yangu ilikuwa ikimuwaza Firyaal tu hivyo nilishukia Mbezi. Nikatafuta bodaboda na kumuelekeza

dereva sehemu ya kunipeleka. Sikuwa na uhakika kama nitapakumbuka nyumbani kwa Firyaal kwani nilifika mara moja tu, tena nikiwa kwenye gari. Kwa bahati nzuri, yule dereva alikuwa mwenyeji mitaa ya Mbezi, akanipeleka mpaka kwenye mtaa aliokuwa anaishi Firyaal.

Kwa mbali niiliona nyumba yake, nikaikumbuka vizuri na kumwambia dereva wa bodaboda asimame. Nilimlipa hela yake kisha nikaanza kutembea harakaharaka kuelekea kwenye geti la nyumba ya Firyaal. Moyoni nilikuwa na furaha isiyo na kifani hata kabla ya kumuona Firyaal.

Nilipofika getini, nilibonyeza kitufe cha kengele na kusubiri kwa muda, nikaanza kusikia vishindo vya mtu akija kufungua mlango. Mlango ulipofunguliwa, nilikutana

uso kwa uso na Firyaal ambaye kwa jinsi nilivyomtazama, niliona kama amezidi kuwa mzuri. Kwanza alipigwa na butwaa kuniona kwani ni kama hakutegemea kama ningekuwa pale muda ule, akanirukia mwilini mzimamzima huku akipiga kelele kwa furaha.

Nami sikujivunga, nikajikakamua na kumpokea kifuani kwangu, akanimwagia mvua ya mabusu mfululizo huku akiniambia jinsi alivyokuwa amenikumbuka. Sikupata hata muda wa kupumua, akanishika mkono na kunipeleka moja kwa moja mpaka ndani.

Tulipofika sebuleni, alinisukumia kwenye sofa kubwa kisha na yeye akaja juu yangu. Tukagusanisha ndimi zetu huku mikono yake laini ikipita sehemu mbalimbali za mwili

wangu. Mapigo ya moyo wangu yalianza kubadilika na kuanza kwenda kasi, hata upumuaji wangu nao ulibadilika.

Firyaal naye alikuwa kama mimi, alikuwa akipumua harakaharaka huku akionesha dhahiri alivyokuwa amenikumbuka. Tuliendelea kupashana miili joto huku kila mmoja akiwa kimya, kilichosikika ilikuwa ni miguno ya raha tu.

“Naomba nikaoge kwanza nipunguze uchovu,” nilimwambia Firyaal, akaniangalia na macho yake mazuri kisha akainuka na kunishika mkono, akanipeleka moja kwa moja

mpaka chumbani na kuanza kunivua nguo moja baada ya nyingine. Alipomaliza alinifunga taulo na na yeye akavua zake na kujifunga upande wa kanga, akanishika mkono na kunipeleka bafuni ambapo alianza kuniogesha kama mtoto.

MWISHO

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
65 Dini ya Shetani Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni