DOKTA SIUMWI HUKO (11)

0
Mtunzi: ___

SEHEMU YA KUMI NA KWANZA
ILIPOISHIA...
Mimba zao zote zilikuwa za miezi 7 kila Mtu Sulee alikonda sana
alishindwa kula Hakuwa na Furaha kabisa Moyoni mwake
alimchukia kabisa dk kisarawe
kwaku sababisha Ndoa yake
kuvunjika :
“Monica nina siri kubwa sana
kuhusu Sulee”

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
“siri gani hiyo Shangazi…

Ila wewe inaonekana haujatulia
kabisa unaweza ukamwambia”
“Shangazi wewe ndiyo nguzo
yangu katika maisha yangu yote kwa sasa siwezi kumwambia kabisa shangazi naumia
sana kumwona sulee akiwa katika
hari ile”
“Hata mimi najuwa
sana kutoa mimba nikosa sana
lakini je ukimsababishia
nidhambi pia?”
“shangazi mh hapo sijuwi
ila ni dhambi siyo kubwa”
“huna uwakika Monica”
“ndiyo”
“basi kuna jambo ambalo
nataka itoke ikitoka
Nahuakika sulee mwanangu atakuwa na Afya njema”

“sasa shangazi ni jambo gani hilo
nijuwe maana mimi na wewe ni walezi wake sasa kila siku
hari yake ina zidi kuyumba
ona anavyo pungua hata kama na H I V. Ni miezi michache sana
hawezi kuwa ana dhohofika
kiasi hiki huyu hata mawazo
yana changia”
“ngoja kesho takwambia”
“shangazi sawa”
“acha niende kazini
badae”
“kazi njema Mama”
“leo unaniita mama”
“yah kuanzia leo
takuita mama nasiyo shangazi
naomba ukubali”
“sawa maana wanangu wote
wapo makwao hapa sina
mtu wakunipa mahaba ya kuniita mama nita furahi sana”
****

Baada ya siku moja:
“Monica”
“Naam sulee”
“hivi imekuwaje wewe huna ukimwi na mimi ninao”
“kwa nini wauliza hivyo”
“nawaza sana sijuwi
kwa nini maana wote tumetembea na mtu mmoja
Dokta kisarawe mwenye
ukimwi”
“hata mimi sijuwi
ila punguza mawazo mpezi angu
una niliza sana napo kuona”
“hapana Monica najuta sana
Mume wangu tulikuwa tukipendana sana sana ujinga wangu umeniponza nilifanya vile
kuokoa ndoa yangu kumbe ndiyo
nilikuwa naipoteza jamani
hiii hiii mmh”
“nyamaza wangu
usilie Sulee”
“ina uma sana”
“jikaze sulee angalia upo katika
hari mbaya siyo vizuri kulia lia
kila mara”

Hari ya Sulee ilikuwa mbaya sana
Monica alitoka inje nakumwita dereva ili wampe msaada :
“dereva sulee kadondoka
hari yake mbaya sana twende tukampe msaada”
Monica dereva pamoja na mlinzi
waliingia ndani nakumkuta
sulee damu zikimtoka
kwa wingi ukeni”
“jamani jamani nisaidieni
kumchukua kumpakiza kwenye gari tumpeleke hospital”
walimchukuwa
nakumwingiza katika gari nakumpeleka hospital
kwa matibabu”
“shangazi sulee kazidiwa
sana na damu zinamtoka sana ukeni kapoteza fahamu”
“mko wapi sasa”
“tupo hospital kubwa hapa”
“ok nakuja”

Monica alishangaa sana
alipo kuwa akiongea na shangazi/Mama kwakuto jari sana
angekuwa mwingine ange piga kelele (uwii jamani mwanangu)
lakini ilikuwa tofauti kabisa”
“kutokana na kupanda kwa bp
kwa kiwango kikubwa sana
imesababisha mimba kutoka
sasa mlikuwa mkiishi vipi na
huyu hamkujuwa kama mama
mwenye mimba anatakiwa
usi muudhi wala kufanyishwa kazi ngumu”
“dokta hari ya mgonjwa
imebadilika ghafra sana”
“basi ni hivyo ila kuna vipimo
vingine bado havijaja subiri
sawa mgonjwa mleteeni ndizi laini na uji ok bado anawekewa damu”
“sawa daktar”
“Mama ila
hari yake inaendelea poa
ila mimba imetoka”
“yes”
“shangazi yes wakati kiumbe
kimetoka mbona sikuelewi”
“Monica ni story ndefu kidogo
Nihivi Mimi na doktar Tuli….

Tuli Ongea adanganye
kuwa sulee ana HIV ili
Mumewe amuache nilikuwa
sipendi Sulee akae na Mumewe
kwani alikuwa hana Hadhi ya kuwa na sulee kwakuwa
walipendana na kuwa na ndoa
sikuwa na jinsi ya kuwatenganisha kabisa niliamuwa iwe hivyo tulijuwa
sulee atakuwa katika
mawazo sana na kupandisha BP
itakayo sababisha kujifungua
kwa kupewa dawa ya kukisukuma kiumbe au kutoka mimba mpaka hapo safi atarudi katika hari yake ya kawaida”
“lakini shangazi ulivyo fanya siyo
vizuri kabisa unajuwa”
“nyie mmefanya vizuri au unaongea tu”
“hapana shangazi kuuwa na kumsariti mwenzako
dhambi hazi fanani shangazi”
“kwahiyo mimi ni muuwaji
eeh”

shangazi alifoka kwa hasira sana
mpaka Monica aka shtuka na kujiludi chini.
“sina mana hiyo shangazi
namaanisha kuwa”
“kuwa nini eeh”
“kuwa dhambi ni dhambi tu”
“umeona sasa mbona mimi namuokoa sulee awe na maisha safi wewe unataka kusema mimi
nina kosa wewe Moni nini”
“aah shangazi ila naona upo sahihi tu sijuwi na mimi nitoe hii mimba”
“hapana usitoe takusaidia kuilea sawa sulee nimehangaika nae
tangia mtoto wa miezi mi4 wazazi wake walikufa hivi unajuwa mimi siyo shangazi yake wa damu”
“sijuwi kabisa nilijuwa ni dada wa baba yake wewe”
“hapana baba yake alikuwa dereva tax alikuwa ana nibeba kutoka kazini mpaka nyumbani
tukawa kaka dada baba yake ni mtu wa kenya na mama yake ni mtu wa kenya nae walikutana hapa hapa dar wakawa wapenzi
mpaka waka owana na kumzaa
Sulee, walikufa kwa ajari ya gari
wakitokea Bagamoyo”
“ooh kumbe sasa sulee ana juwa kuhusu hilo”
“hapana kuhusu kufa ana juwa
kuhusu kama mimi siyo shangazi wa damu hajuwi naomba kuhusu suala hili usimwambie sawa”
“nimekuelewa”

baada ya miezi 3:
Sulee alikuwa fiti kama zamani
japo kuwa alikuwa hana furaha kabisa alijaribu kuwasiliana na Mumewe lakini haikuwa poa kwakuwa Sulee aliasirika
Mumewe na sulee mwenyewe walijuwa hivyo
isinge kuwa Rahisi kurudiana
kuwa wapenzi au wana ndoa.
Shangazi alikuwa akimletea
dawa ili ameze kama dozi
ya HIV kumbe zilikuwa za BP
kwakuwa alikuwa hazijuwi dawa
alikuwa akimeza tu Nae Monica
hari yake ilikuwa siyo zuri
kutokana na miezi9 kutimia
ghafra uchungu uka mshika
saa6 usiku ya juma tatu alikimbizwa hospital kufika tu nakulazwa kitandani alipiga kelele sana kuomba msaada kwakuwa uchungua aliusikia
manesi na madaktar walimchukuwa nakumpeleka
katika chumba cha kujifungulia
walimsaidia na kufanikiwa kuzaa
mtoto wa kike.

“hongera sana umejifungua
mtoto wa kike yupo salama”
“ooh asante Mungu”
“sasa wewe pumzika kwanza
sawa mama”
“sawa”
“jamani mzazi wenu
amejifunguwa salama mtoto wakike”
Sulee alifulahi sana kusikia hivyo
“Monica hongera sana mwenzangu fungu lako limekuja
kama wewe”
“sulee asante mwaya”
“sulee hongera sana”
“asante shangazi”
“mh hata mimi sijuwi
angekuwa wakike”
Swali hilo lilimfanya MONICA atoe
machozi
“Monica mbona una lia
acha uchuro badala ufurahi una lia”
“Monica nakumbuka mengi sana
siyo kwaajiri ya mtoto Mume wangu Sulee”
sule aliwaza sana nae alianza
kudondosha machozi kwa sababu
tatu moja ana, hiv mbili kaachika, tatu mimba imetoka:
“jamani mna lia na mimi nifanyeje eeh”
Aliuliza shangazi
bila kupewa jibu Monica na sulee walikumbatiana huku wakilia.
**

Maisha ya mume wa sule yalizidi kuwa magumu kifedha alitamani
kwenda kwa shangazi yake Sulee lakini aliona aibu kwenda kuomba
alivumilia lakini ilizidi sana
kuwa mbaya maana alizoeya
kupewa na shangazi
Nae mume wa monica
ali Rudi kijijini kutokana na maisha kuwa magumu aliingia katika madeni makubwa benk wakataifisha nyumba na gari
lake
**

Sulee kwa nini usiende kupima
tena ujuwe afya yako”
“mimi nasubiri kufa tu”
“hapana sulee nenda wewe
mimi hainiingii akirini eti mimi sina ukimwi na wewe unao
wakati mwanaume mmoja
tumetembea nae”
“inatokea hivyo monica”
“jaribu wewe nakushauri tu
uwenda Mumeo alifanya njama
tu kwa dokta ili akuambie una virusi ili akuache maana aibu tume wapa”
“mh ina wezekana eti lakini haku paswa kufanya hivyo.
 “sulee haina haja ya
kufikiria kwa sasa maji yamesha
mwagika kuyazoa haiwezekani kabisa sawa”
“sawa ngoja kesho niende kupima tema hospital kama 4 kwauwakika zaidi uwongo Monica”
“fanya hivyo mpenzi wangu maana unaweza kuishi kwa mawazo wenda huna tatizo hilo
wangu”
“asante Monica”
“ila usimwambie shangazi
kama unaenda kupima sawa”
“kwa nini Monica”
“hupaswi kuuliza kwa nini
fanya hivyo”
_________________­__­____________________­

Dokta kisalawe alimsimulia Adams
Historia yake ya maisha aliyokuwa akiishi Dar najinsi alivyo kuwa akiwa fanyia wanawake za watu:
“Nihivyo Adams nilikuwa nikifanya dhambi kabisa
na sasa nimeamua kuokoka
sitaki dhambi tena”
“Uwamuzi wako mzuri sana
nakupa hongera sana mke wa mtu ni sumu kali sana usipende kupenda au kufanya mapenzi/sex nao utakufa mapema sana, ona mimi sina mke lakini sijihusishi na Mapenzi mpenzi wangu mimi ni kazi/pesa KISARAWE”
“Kweli nakuamini ndugu yangu”
“basi akiri yako wekeza kwenye
kazi jifunze nacho fanya sawa
usiwe na tamaa katika Mari yangu
ukiiba tu nikigundua nakupoteza asee sikutishi nakupa ukweli
angalia ulio wakuta wako vipi”
“sawa Adams nakuahidi sita fanya hivyo”
“asante kama itakuwa kweli”
_________________­__­____________________­

Kisarawe alizidi kuomba Mungu
na kutubu Dhambi zake zote yeye alikuwa mtu wakufunga na kusari
Mpaka Adams alishangaa sana
kubadilika sana alikuwa mkimya
sana hakupenda kabisa ku share na wanawake” Kisarawe vipi
mbona uko hivyo siku hizi”
“kivipi Boss”
“Hapana niite Adams inatosha
kaka”
“ok Adams”
“naona unabadirika sana
mkimya hupendi kukaa na akina dada”
“Adams nimeamua kubadilika
kidogo sipendi kukaa nao nataka
nisahau kabisa matukio yangu ya zamani nikikaa nao nitakumbuka
yaliyo pita na kuanza upya”

“Hivi ulishakuwa na mke”
“kwa nini una uliza hivyo”
“namaana yangu”
“Hapana sikuwa na mke”
“ndomaana ulikuwa ukitembea
na wake za watu”
“kwa nini”
“Ulikuwa huoni uchungu
wa mke ungekuwa na mke
usinge fanya hivyo, tuachane
na hayo kesho Naenda Dar
kuna kampuni moja nimeongea nao kuhusu gari wana hitaji”
“sawa Adams kwahiyo
kuhusu mpango wa sua kuhusu
trekta zile kumi inakuwaje
wamefika milioni95 kila moja”
“ooh nilisaha wambie waongeze 20”
“sawa”
_________________­__­____________________­_

ADAMS akiwa maeneo ya mbezi
alihisi tumbo likimuuma
ndani ya gari yake alikuwa
na Dereva aliye mkodisha
kuendesha gari yake kutokana
na kuto zijua vizuri njia na msongamano wa magari
kama unavyo lijuwa jiji la dar
alikuwa akilala mika sana
dereva alishauri waende
hospital ya Amana
kupima/kupewa matibabu
dk10 walifika na kuchukuliwa
vipimo wakati wakiwa
katika chumba cha kupumzikia wagonjwa walikuwa wengi
wakisubiri majibu yao ya
vipimo walikuwa wakiangalia video iliyo kuwa ipo juu ya ukuta
wote wagonjwa walikuwa wakitazama juu katika video hiyo
lakini kwa Adams ilikuwa tofauti kidogo.
Macho yake yalikuwa kwa Binti
mrembo sana aliye kuwa kakaa upande wa kushoto kwake.

“kaka vipi mbona hivyo”
ilikuwa sauti ya dereva wake
iliyo muuliza:
“ona yule dada alivyo”
“aah kaka mbona kama hao wengi tu wapo hapa Dar tena wazuri kushinda huyo mgonjwa
pesa yako tu kama upo tayali niambie nikupeleke viwanja”
walikuwa wakinong’onezana
masikioni ili watu wengine wasisikie.
“hapana asee Roho yangu
imetua pale asee”
“sasa kaongee nae basi”
“poa subiri hapa hapa”

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)